Arafat
JF-Expert Member
- Nov 17, 2009
- 2,581
- 758
Katibu wa NEC Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma akimnyamazisha Asha Likalangala alipoangua kilio baada ya kuingiwa na maneno ya Katibu wa CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alipokuwa akihutubia katika mkutano wa hadhara Kilwa Masoko.
Nape akipokea kadi ya aliyekuwa katibu wa CUF kata ya Njinjo Kilwa Mohamed Likalangala katika mkutano wa hadhara Kilwa Kivinje.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akishauriana jambo na Katibu wa NEC Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma kwenye mkutano Kilwa Kivinje mkoani Lindi.
Nape akishauriana jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Ali Mtopa katika mkutano uliofanyika Kilwa Masoko, mkoani humo.
Nape akisakata muziki na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Ali Mtopa katika mkutano wa Kilwa Masoko.
Nape akisakata muziki na vijana wasanii wa Kilwa Masoko.
Nape na Asha Abdallah Juma wakisindikizwa na umati wa wakazi wa Kilwa Kivinje baada ya mkutano wa hadhara.
Wana CCM Kilwa Kivinje wakimshangilia Nape wakati akiondoka mara baada ya kumalizika mkutano wa hadhara.(Picha na Bashiri Nkoromo).
Labda Nape anafaa kuchukuwa nafasi ya Mkama? ndani ya CCM! au hizi ni safari tu kujitengenezea fedha za Posho! Maana CCM wana wazimu wa Posho.