TANZIA: Mwanasiasa maarufu, Richard Tambwe Hizza afariki Dunia. CHADEMA yatuma salamu za rambirambi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
tambwe1.jpg

Mwanachama wa CHADEMA, Richard Tambwe hiza amefariki dunia usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake. Mwili wake umepelekwa Hospitali ya Temeke Dar Es Salaam asubuhi hii. Hadi jana saa tano usiku alikuwa kwenye Kikao cha CHADEMA.

Marehemu Tambwe Hizza amefariki akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa pumu na amefariki akiwa ni mmoja wa waratibu wa kampeni za chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) katika jimbo la Kinindoni

Hizza anafahamika sana kwa siasa zake akiwa CUF, Baadae alihamia CCM na kuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda wa CCM na 2015 aliamua kuondoka CCM na kuhamia CHADEMA. Mwaka 2014 alisema angegombania Urais kupitia cha mapinduzi kwani ana uwezo, akili, elimu na afya ya kumuwezesha kuwa Rais wa tano wa Tanzania.

Jana alishiriki kampeni za kumnadi Salum Mwalimu Tandale mapema jioni kabla ya Vikao vya chama..


-----
CHADEMA watuma salamu za Rambirambi

hizaaaa.jpg
 
TANZIA:Mwanasiasa maarufu na wa siku nyingi Tambwe Hizza amefariki leo alfajiri nyumbani kwake jijini Dar es salaam.Marehemu Tambwe Hizza amefariki akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa pumu na amefariki akiwa ni mmoja wa waratibu wa kampeni za chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) katika jimbo la Kinindoni:Taarifa hizi zimethibitishwa na Mstahiki Meya wa Ubungo@Boniface Jacob
[HASHTAG]#DARMPYABLOGUPDATES[/HASHTAG]
 
Aisee mbona ghafla sana, au watu wasiojulikana wamebadili njia ya kutumaliza?, RIP
Unamfahamu vizuri marehemu? Muulize maalim seif na Rafiki kipenzi wa Marehemu Yusufu Makamba! RIP kada wa Cuf baadaye CCM na sasa kabla ya mauti CDM
 
View attachment 692398

Mwanachama wa CHADEMA, Richard Tambwe hiza amefariki dunia usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake.

Mwili wake umepelekwa Hospitali ya Temeke Dar Es Salaam asubuhi hii.

Hadi jana saa tano usiku alikuwa kwenye Kikao cha CHADEMA.

Jana alishiriki kampeni za kumnadi Salum Mwalimu Tandale mapema jioni kabla ya Vikao vya chama..

Hizza anafamika sana kwa siasa zake akiwa CUF, Baadae alihamia CCM na kuwa katibu wa propaganda na 2015 alimua kuondoka CCM na kuja CHADEMA. Mwaka 2014 alisema angegombania Urais kupitia cha mapinduzi kwani uwezo, akili, elimu na afya ya kumuwezesha kuwa Rais wa tano wa Tanzania.
So sad...
 
Back
Top Bottom