Mahesabu
JF-Expert Member
- Jan 27, 2008
- 6,016
- 3,973
Thursday, 14 April 2011
* Lengo kudhibiti matumizi ya fedha
* Mukama: Mabadiliko si kujipodoa
* January: Kuvaa magwanda si ujemadari
* Nape ataka wapinzani kufungasha virago
Joseph Damas na Theodos Mgomba, Dodoma
UTARATIBU wa kumpata mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2015 ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), umebadilishwa.
Hatua hiyo ni sehemu ya mageuzi makubwa yanayoendelea kufanywa ndani ya Chama. Mabadiliko hayo yanalenga kudhibiti wagombea wenye matumizi makubwa ya fedha kwa nia ya kununua kura za wajumbe wa vikao vya uchujaji na uteuzi wa majina.
CCM pia imetangaza kubadili utaratibu wa uteuzi wa wagombea ubunge na udiwani, ambapo sasa watachujwa kwanza ili kuwapata watatu, ambao watapigiwa kura ya maoni na wanachama.
Hayo yalielezwa jana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa, alipohutubia wana-CCM na kuitambulisha sekretarieti mpya ya Chama kwenye viwanja vya Nyerere Square, mjini hapa.
Alisema katika kuhakikisha hilo linatekelezwa kwa mafanikio, Chama kitarekebisha kanuni juu ya watendaji na viongozi wanaogombea nafasi za kisiasa, ambazo wao pia wanahusika katika vikao vya maamuzi ya juu.
Msekwa alisema mbio za urais katika uchaguzi wa mwaka 2015 zimekuwa zikiwaumiza vichwa kutokana na makundi yanayojipanga kuwania kuwagawa wanachama na kuathiri umoja na mshikamano.
"Kiini cha tatizo hili ni utaratibu wa kupata wagombea wa CCM unaotumika sasa, hivyo tumeamua kuubadilisha ili kudhibiti matumizi ya fedha," alisema.
Kuhusu suala la rushwa na ufisadi, Msekwa alisema limekuwa mzigo mkubwa kwa CCM licha ya juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na serikali.
Alisema Chama kimejipanga kuhakikisha kinafanya mageuzi makubwa ili kuondoa muonekano huo na kuwa ni Chama kinachopambana na rushwa kwa vitendo.
"Taswira ya Chama imeathiriwa mbele ya umma na migogoro ya viongozi kutokana na makundi yaliyopo. Tumebebeshwa mzigo kuwa tunakumbatia mafisadi," alisema.
Msekwa alisema CCM imepoteza sifa ya awali ya kuwa Chama kinachojali maslahi ya wanyonge, na sasa kinabebeshwa mzigo wa kuwa Chama cha matajiri.
Alisema mageuzi hayo makubwa yatadhihirisha kuwa CCM ni chama cha wanyonge na kwamba, hakikumbatii wala rushwa na mafisadi.
Kuhusu viongozi ndani ya CCM wanaotuhumiwa kwa ufisadi, Msekwa alisema wametakiwa kupima uzito na kuchukua hatua wenyewe.
Msekwa alisema Chama kina viongozi wengi, hivyo wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi na rushwa watajulishwa kwa barua na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama ili wajitambue na kuchukua hatua ya kujivua uongozi kwa maslahi ya Chama.
Hata hivyo, alisisitiza iwapo wahusika watashindwa kuwajibika, Chama kitawatimua na hilo litafanyika wakati wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kinachotarajiwa kuketi miezi mitatu ijayo.
Kwa upande wake, Mukama alisema Chama ni imara na kimeweza kufanya mabadiliko makubwa bila nchi kutikisika.
Alisema hilo linaonyesha ukomavu wa kisiasa ndani ya Chama tofauti na vingine, ambapo hata akijiuzulu kiongozi mmoja mambo hubadilika na vyama hivyo kuyumba.
"Mabadiliko haya si nguvu ya soda, ni endelevu na Chama kimekusudia hilo kwa lengo mahsusi. Si mabadiliko ya kujipodoa kwamba kesho ukikosa vipodozi unarudia sura yako ya zamani," alisema Mukama.
Mukama alisema CCM imedhamiria kurudisha imani ya wananchi kwa Chama, kwa kuwa uongozi hauwezi kuganda kama barafu na ndiyo maana hilo limefanyika.
Naye Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, aliwataka wapinzani kuanza kufungasha virago. Alisema amerejea nyumbani kwa kishindo.
Alisema serikali ilimuazima kwa kipindi cha miezi minane, lakini sasa amerejea akiwa na nguvu mpya na moto aliouanzisha utaendelea kushika kasi mikoa yote.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, January Makamba, alisema hotuba zake hazitakuwa na vifungu vya Biblia wala Kurani kwa kuwa kazi zake kikatiba ni kufuatilia hali ya siasa nchini.
Amesema jukumu lake lingine ni kufuatilia vyama vya siasa na kwamba, kazi hiyo anaimudu na kuwataka wana-CCM wasiwe na shaka hata kidogo.
"Kazi ya kuwabomoa wapinzani ni rahisi kwangu, nitaifanya kisayansi na wala msiwaone wamevaa magwanda mkaona ni majemedari... wale ni wapesi. Hakuna sababu ya kuwaiga kwa kuwashawishi vijana wa vyuo vikuu kuzomea.
"Jukumu letu ni kuwaeleza wanafunzi wasikileze hoja na baadae kujibu," alisema.
CHANZO: Gazeti la Uhuru