CCM yaanza kuchukua hatua, timu ya wataalamu yaitishwa

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Zikiwa zimebaki siku 11 za kampeni, CCM imeanza kuchukua hatua muhimu za kuelekea kupata ushindi. Tayari timu ya wataalamu imeitishwa bila kutishwa ili kusafisha njia ya ushindi. Wataalamu hao wanatokea kada mbalimbali za kimaisha kama sheria, utaalamu wa kompyuta, utaalamu wa kisiasa/kipropaganda, usalama na kadhalika. Pia,wamealikwa wasomi ili kuchangia mawazo.

Timu husika itakuwa na wajibu wa kuyapatia majibu mambo yote yaliyojitokeza katika kampeni ili CCM iweze kupeta pamoja na uwepo wa upepo huo. Wataalamu hao watasafisha CCM,kusawajisha na kufifisha upinzani na kukipatia chama chetu kura za ushindi wa kishindo katika namna za kitaaalamu. Wataalamu hao tayari wameshatumiwa nauli na kauli ili wasikioneshe chama jeuri na kiburi. Unatakiwa ushauri.

Kila litakalojiri, vutizi au la, mtalijua.Tumejipanga.....mwaka huu wataisoma!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Kujua mbinu za adui yako ni hatua moja ya ushindi

Tatizo msiba unawaaribia ratiba.
35B za walimu hazina madhara, polisi pamoja na kuwalipa wiki iliyopita bado wameshikilia msimamo
Mbinu moja tuu imebaki ni kufanya namna Lowasa aanguke jukwaani ili aonekane mgonjwa!
Mlipo tupo!
 
Kujua mbinu za adui yako ni hatua moja ya ushindi

Tatizo msiba unawaaribia ratiba
35B za walimu hazina madhara, polisi pamoja na kuwalipa wiki iliyopita bado wameshikilia msimamo
Mbinu moja tuu imebaki ni kufanya namna Lowasa aanguke jukwaani ili aonekane mgonjwa!
Mlipo tupo!

Watanzania tupo tayari kumchagua hata akiwa hospitalini kalazwa tutampa kura zetu kuliko kuichagua ccm
 
Watakimbia sana laki tunamuamini jk kwa kuiangusha ccm ili swahiba wake ashinde usiogope tuko na pandikizi la lowassa ndani ya ccm ni kikwete.

swissme
 
Inatakiwa vichwa vipya sio vile vile vya kina nape, makamba.... Angalia kampeni zenu nguvu mnazotumia. "pumzi imekata"
 
...nyie watu mnaendelea kuliwa pesa zenu za wizi tu.Eti mtaalamu wa sheria?!, atawasaidia nini wakati nilishaamua kura yangu kwa lowassa siku nyingi, au mnataka mkakate rufaa kwa nini nimempigia lowassa....
kweli kazi mnayo mwaka huu.!!
 
VUTA-NKUVUTE hizo mbinu za ushindi wa kitaalam maana yake nini?

Kwa hiyo sisi wananchi hatuna haja ya kwenda kupiga kura na zitapigwa kitaalam?

Hebu tufafanulie kidogo
 
Last edited by a moderator:
Mzee Tupatupa hizo mbinu za ushindi wa kitaalam maana yake nini?

Kwa hiyo sisi wananchi hatuna haja ya kwenda kupiga kura na zitapigwa kitaalam?

Hebu tufafanulie kidogo

Utajua hapahapa JF. Usiwe na haraka ukakosa baraka

Mzee Tupatupa
 
Si mlisema mtashinda hata kwa bao la mkono sasa labda mmekusanya kundi la wataalam wa bao la mkono aka pu----l---i---za:wink:
 
Utajua hapahapa JF. Usiwe na haraka ukakosa baraka

Mzee Tupatupa

Dalili zote za ccm kutaka kulazimisha matokeo ziko wazi. Ila watambue safari hii hakuna atakayekubali kuletewa mshindi wa mfukoni ambaye watakauwa wanamuongoza wapendavyo. Tumeamua tunataka mabadiliko ya mabadiliko ya kwanza ni pamoja na kuitoa ccm madarakani kwanza.
 
Tatizo mtooa mada, watu c kama tunampenda Lowassa, ila tumeichoka sana CCM! kwani wewe huna akili? huoni? mbna cwaelewi nyie mnaosema magufuli mchaa kazi? kwani atatawala kama anavyotawala ndani ya familia yake? acheni upuuzi na mcfurah kulipwa kwa kuiaisha ccm!
 
Siasa ni sayansi ambayo inafanywa kwa mikakati na si kwa mbwembwe na katika mchezo kubadilisha mbinu ni jambo zuri sana inapobidi
 
Zikiwa zimebaki siku 11 za kampeni, CCM imeanza kuchukua hatua muhimu za kuelekea kupata ushindi. Tayari timu ya wataalamu imeitishwa bila kutishwa ili kusafisha njia ya ushindi. Wataalamu hao wanatokea kada mbalimbali za kimaisha kama sheria, utaalamu wa kompyuta, utaalamu wa kisiasa/kipropaganda, usalama na kadhalika. Pia,wamealikwa wasomi ili kuchangia mawazo.

Timu husika itakuwa na wajibu wa kuyapatia majibu mambo yote yaliyojitokeza katika kampeni ili CCM iweze kupeta pamoja na uwepo wa upepo huo. Wataalamu hao watasafisha CCM,kusawajisha na kufifisha upinzani na kukipatia chama chetu kura za ushindi wa kishindo katika namna za kitaaalamu. Wataalamu hao tayari wameshatumiwa nauli na kauli ili wasikioneshe chama jeuri na kiburi. Unatakiwa ushauri.

Kila litakalojiri, vutizi au la, mtalijua.Tumejipanga.....mwaka huu wataisoma!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Jana umeona hiyo timu ya ufundi illivyo na akili finyu - Membe(Lindi), Mkapa(masasi) na Pinda(Sumbawanga) - CCM (chama cha Makabila)

By the way CCM haitarudi tena na sababu kubwa ni hii: Sita na chama chake waliwadharau maaskofu na kuwaaambia waraka wao ni wa kipuuzi na hawana utukufu! maaskofu wakaandika hivi Mithali 29:1 "Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafla, wala hapati dawa".

Hakuna dawa tena ya kuitibu CCM na wakilazimisha watikuwa wako kwenye matatizo makubwa kuliko hayo ya kushindwa!!
 
too late,
hilo jopo lifanye tathmini ya uchaguzi wa 2020 kwenye harakati za kujaribu kuirudisha CCM madarakani.
 
Back
Top Bottom