CCM ya Nape ni nadharia

Nape anatumwa na chama kusema,lakini bado chama kinashindwa kumwambia kitu gani muhhim cha kusema,kwa sababu chama hakina zuri la kulisemea na watu wa kuelezwa,kwa hiyo anajikuta anatumia calories nyiiingi kweli mtoto wa mzee Nauye

- Rome haikujengwa kwa siku moja, Nape ndio kwanza ameingia apewe nafasi kwanza ndio ahukumiwe!

Willie @ NYC, USA.
 
William, suppose wewe ndo ungepewa nafasi ya NAPE, ungebadilisha nini? Mimi namwona Nape jasiri sana. Pamoja na kujua kwamba kwa kuwa mkweli atajiweka mahali pabaya bado amediriki kusema. Lakini tugeuke nyuma tujikumbushe majibu ya Mukama dhidi ya kauli ya Nape ya kuwafukuza mafisadi ndani ya siku 90? Maana Nape alikuwa kifua mbele kutangaza siku tisini akijua alionao ndani ya chama wanamuunga mkono. Lakini Mukama alipoulizwa akasema kikao hakikutamka siku tisini. Vaa viatu vya Nape, useme katika majibu kama hayo unafanyaje? Twende mbele zaidi, Nape aliutangazia umma kwamba barua za kuwaondoa mafisadi zinaandaliwa, lakini walipoulizwa msekwa na mukama wote walikanusha kuhusu kuwepo kwa barua. hii ina maanisha nini? Nafikiri kama alivyosema Msema hovyo hapo juu, jamaa keshaachwa solemba. Na tuombe Mungu wasimuue. Maana CCM hawashindwi kitu.

- CCM inaongozwa na Mwenyekiti aliyewahi kusema kwamba kila analosema Nape lina baraka zake kwa 100%, that is all what counts katika siasa za taifa kama za Nape!

Willie @ NYC, USA.
 
Kwa hiyo ushauri wako ni upi, nilitegemea useme fanya 1, 2, 3.......kumbe ni kelele za majukwaani tu.... sema baba sema tupo nyuma yako.

- Kama kawaida yako umeanza tena za kutaka thread ifungwe? Unasema mimi niandike unavyotegemea wewe ndio JF policy hiyo?

- Na who are you mpaka niandike unavyotegemea wewe? Sasa sikuandika unavyotegemea wewe then what?

Willie @ NYC, USA.
 
- Rome haikujengwa kwa siku moja, Nape ndio kwanza ameingia apewe nafasi kwanza ndio ahukumiwe!

Willie @ NYC, USA.
W.J. Malecela,
Nape ni samaki mdogo sana ndani ya bahari hii ya UCCM, kama ungeelewa sababu alopewa nafasi hiyo wala usingefika kote huku. Wameshindwa waloshindwa, kajipendekeza wamembebesha mzigo kama punda, sasa hivi anachapwa bakora tu kufuata wanakotaka kwenda. Na kweli maneno yako Punda hana hatia wala hana akili ya kubeba mzigo na kuufikisha unakotakiwa ila uzito anaoweza kuubeba binadamu hauwezi...
Ukinielewa hapo tumemaliza!
 
- Nape simama hapo hapo, CCM inahitaji mapinduzi makubwa sana kutoka within na somebody had to start somewhere, so far so good it is only a matter of time CCM nzima itabadilika, na hasa kwenye uchaguzi wa 2015 ambapo CCM ni lazima ibadilike maana hakuna choice nyingine isipokwua kubadilika tu!- Bravo Nape! CCM inakuhitaji zaidi kuliko wakati wowote huko nyuma!Willie @ NYC, USA.
Humtakii mazuli wengi wamenyosha mikono huyo nisawa nasisimzi atakwapolojo za mende kadondosha kabati nape hawezi kuisafisha ccm kunawatu wapo ndani ya ccm hawapo kuendesha chama ila chama kinaendesha maisha yao sidhani kama ataeleweka vinginevyo atapotezywa
 
The CCM nominee will win 2015 Presidency, InshaAllah. Part of it is because of Nape's current efforts. It is what it is. The rest is just noise. Part of it is because Chadema as the main opposition is not a serious political party. Wananchi won't give presidency to a party with potential Ministers that includes Joseph Mbilinyi and GodBless Lema. And a Prime Minister as cunning and incompetent as Freeman Mbowe. Homeboy discovered public service after failing in life.
 
Mkuu kwa post yako hii sidhani kama umemsadia Nape. Najua wewe ni mwana-CCM, but you gonna have to be objective na mzigo aliobebeshwa Kijana mwenzetu Nape. Asije akashindwa, halafu uwe wa kwanza kusepa. Na hili tayari linajidhihirisha hata kwa wabunge vijana wa CCM. Sidhani kama nimesikia wakimuunga mkono in public. Whether wanafanya hivyo in private, I don't know.

Mkuu unapingana na ambacho Nape anakiamini unless labda awe amebadilika hivi karibuni. Wakati wewe unaangalia zaidi maslahi ya chama, Nape alishasema huko nyuma kuwa kwake yeye siasa ni utumishi kwa umma na katika hilo anaamini katika uzalendo kwa nchi kwanza, chama baadaye. "Tunakuwa na nchi kwanza tunayotaka kuijenga, ndipo tunaunda chama cha kujenga nchi tunayoitaka, kwa hiyo uzalendo kwa nchi unapaswa kuvuka mipaka ya itikadi zetu," anasema Nape.

Nakubaliana na hoja ya Mkumbo. Nape alipata misukosuko kwenye uchaguzi wa UVCCM, akavuliwa uanachama wa UVCCM pale alipojaribu kukemea ufisadi na baadaye kuangushwa hata kwenye kura za maoni za ubunge. There is no doubt kuwa matatizo ya ndani ya UVCCM yanaakisi yale ya CCM yenyewe. Kwamba ndani ya CCM kuna watu ambao nje wanaonekana kwamba wanafanya kazi ya kuendeleza nchi, lakini ukweli ni kwamba wanaendeleza maslahi yao binafsi. What Nape is trying to do now is exactly what he tried in UVCCM but failed miserably.

Well, utaniambia CCM imejivua gamba and it is "only in matter of time CCM nzima itabadilika". Lakini hutaki kufanya analysis hao walengwa (victims) nao wemejihami vipi. Unafikiri kuwa "CCM nzima itabadilika" in "matter of time" just like that. Hutaki kuumiza kichwa. Unafikiria kuwa tarehe 11 mwezi huu utaamka na kukuta "CCM nzima imebadilika". Never never underestimate the determination of quiet man.

Nape may be energetic and intelligent, but senior politicians in the party may hinder what he wants to achieve. Nakushauri ukasome kitabu kilichoandikwa na marehemu Patrick Ng'ara (RIP) kiitwacho KIKOMO. Kinaonesha jinsi mpelelezi alivyopata shida kupambana na majambazi ambao walikuwa na nafasi nyeti ndani ya serikali.

- The question ni kwamba Nape amefikaje alipo sasa baada ya kupigwa vita vya ajabu na hata kutaka kufukuzwa UV-CCM, unasema Seniors sasa walikuwa wapi alipopewa hii nafasi kama wana nguvu sana ndani ya CCM ya kumkwamisha huko mbele? Kwa nini hawakumkwamisha asipewe kama kweli wana hizo nguvu unazozisema?

- CCM ni lazima ibadilike tu, ingekua haiwezi kubadilika Nape asingeshika hiyo nafasi wala kupewa, kwenye uchaguzi wa 2015 CCM lazima itaweka a strong Candidate ambaye tayari anakubalika sana sasa hivi, tizama matokeo ya NEC ya CCM, utamuona tatizo lipo Chadema, watamuweka nani?

- Ningekuwa wewe ningekosa sana usingizi na kutaka kujua nani atasimama Chadema maana so far hakuna?

Willie @ NYC, USA.
 
The CCM nominee will win 2015 Presidency, InshaAllah. Part of it is because of Nape's current efforts. It is what it is. The rest is just noise. Part of it is because Chadema as the main opposition is not a serious political party. Wananchi won't give presidency to a party with potential Ministers that includes Joseph Mbilinyi and GodBless Lema. And a Prime Minister as cunning and incompetent as Freeman Mbowe. Homeboy discovered public service after failing in life.

Hapo kwenye red unajaribu kulinganisha kati ya worse and the worst to the effect that the the voters have got no option but to vote for the worse instead of the worst?
 
W.J. Malecela,
Nape ni samaki mdogo sana ndani ya bahari hii ya UCCM, kama ungeelewa sababu alopewa nafasi hiyo wala usingefika kote huku. Wameshindwa waloshindwa, kajipendekeza wamembebesha mzigo kama punda, sasa hivi anachapwa bakora tu kufuata wanakotaka kwenda. Na kweli maneno yako Punda hana hatia wala hana akili ya kubeba mzigo na kuufikisha unakotakiwa ila uzito anaoweza kuubeba binadamu hauwezi...
Ukinielewa hapo tumemaliza!

- Bob huu ni mtizamo wako na ni kawaida kwenye Demokrasia, mtizamo wangu ni kwamba CCM ilibidi tukubali kwamba times have changed na tulihitaji kubadilika, mimi mtizamo wangu ni kwamba Nape akishajiweka sawa ndani ya CCM ni a very strong force of change na CCM iko njiani kubadilika ndio maana akapewa hiyo nafasi, CCM under Nape ikishindwa kubadilika ninaahidi kurudisha kadi yangu wa kwanza!

- Nape is doing a great job na yupo right on the track na mabadiliko yanayotakiwa!, kwa kuanza kuwaondoa makatibu wengi wa wilaya mabadiliko kwenye chama cha siasa huanzia chini kwenda juu!

Willie @ NYC, USA.
 
- Nape simama hapo hapo, CCM inahitaji mapinduzi makubwa sana kutoka within na somebody had to start somewhere, so far so good it is only a matter of time CCM nzima itabadilika, na hasa kwenye uchaguzi wa 2015 ambapo CCM ni lazima ibadilike maana hakuna choice nyingine isipokwua kubadilika tu!

- Bravo Nape! CCM inakuhitaji zaidi kuliko wakati wowote huko nyuma!

Willie @ NYC, USA.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama! sijui kama unamaanisha kweli au unatani, maana sioni dhamira ya Mwenyekiti, Mkamu mwenyekiti, katibu, NEC yote na Mbaya zaidi Organs za Chama kam UVCCM, Wazee na UWT vyote havujui na havionyeshi kama vina juwa hata chorus ya wimbo anaoimba Nape peke yake kama mpiga kinanda wa lango la soko.
 
Humtakii mazuli wengi wamenyosha mikono huyo nisawa nasisimzi atakwapolojo za mende kadondosha kabati nape hawezi kuisafisha ccm kunawatu wapo ndani ya ccm hawapo kuendesha chama ila chama kinaendesha maisha yao sidhani kama ataeleweka vinginevyo atapotezywa

- Ni mtizamo mmoja kati ya mitizamo mingi sana kuhusu Nape, symbolically kwa kumpa nafasi Nape, CCM imekubali kwamba ni wakati wa Vijana kushika usukani, kwa mara ya kwanza Nape ameitoa Chadema kwenye agenda ya ufisadi na sasa Chadema wanaonekana kwa mara ya kwanza kuanza kuwa Creative na hatimaye kuanza tena kuwa useful kwa taifa, kama walivyokuwa zamani!

Willie @ NYC, USA.
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama! sijui kama unamaanisha kweli au unatani, maana sioni dhamira ya Mwenyekiti, Mkamu mwenyekiti, katibu, NEC yote na Mbaya zaidi Organs za Chama kam UVCCM, Wazee na UWT vyote havujui na havionyeshi kama vina juwa hata chorus ya wimbo anaoimba Nape peke yake kama mpiga kinanda wa lango la soko.

- Kwani Nape amepitia wapi kufika hapo si humo kwenye unaowasema, mbona hawakumzuia?

Willie @ NYC, USA.
 
- The question ni kwamba Nape amefikaje alipo sasa baada ya kupigwa vita vya ajabu na hata kutaka kufukuzwa UV-CCM, unasema Seniors sasa walikuwa wapi alipopewa hii nafasi kama wana nguvu sana ndani ya CCM ya kumkwamisha huko mbele? Kwa nini hawakumkwamisha asipewe kama kweli wana hizo nguvu unazozisema?

Sio ndio hapo sasa Mkuu. Mtu kavuliwa na kufukuzwa hata uanachama wa UVCCM kwa kuvunja sheria za chama, then hapo hapo kapewa ukuu wa wilaya, kabla ya kupewa tena madaraka CCM. How does CCM work? Wewe unaonaje hili?

- CCM ni lazima ibadilike tu, ingekua haiwezi kubadilika Nape asingeshika hiyo nafasi wala kupewa, kwenye uchaguzi wa 2015 CCM lazima itaweka a strong Candidate ambaye tayari anakubalika sana sasa hivi, tizama matokeo ya NEC ya CCM, utamuona tatizo lipo Chadema, watamuweka nani?

Kwa nini tuandikie wino wakati mate yapo? Nona wewe unaangalia zaidi 2015.

- Ningekuwa wewe ningekosa sana usingizi na kutaka kujua nani atasimama Chadema maana so far hakuna?

Mkuu kumbe na wewe ni mmoja ya wale ambao wakipingwa unawa categorise kama Chadema? Mkuu acha kufanya assumptions. Wengine tuko kitaifa hapa, sio kichama.
 
Sio ndio hapo sasa Mkuu. Mtu kavuliwa na kufukuzwa hata uanachama wa UVCCM kwa kuvunja sheria za chama, then hapo hapo kapewa ukuu wa wilaya, kabla ya kupewa tena madaraka CCM. How does CCM work? Wewe unaonaje hili?

Kwa nini tuandikie wino wakati mate yapo?

.

- National politics huchezwa tofauti na michezo yote mingine Duniani, ndio mana leo Mama Clinton ni Waziri wa Obama, Nape hakuvuliwa wala kufukuzwa uanachama kwa sababu NEC walikataa, ni NEC tu ndio wana mamlaka ya kufanya hivyo hawakufanya kwa hiyo ni hoja batili!

- Sijui kama nimesema wewe ni mwanachama wa Chadema, nimesema hivi ningekwua wewe ningekosa usingizi kuhusu nani atagombea urais 2015 on Chadema's ticket maana hawana so far!, unasema kwa kusema hivi nimekuita mwanachama wa Chadema? Is that right?

Willie @ NYC, USA.
 
Nape yupo hapo alipo aatumiwa tu.

Katika siasa CCM imejiona inapoteza mvuto kwa vijana. Kumuweka Nape ni katika kuwapaka vijana mafuta kwa mgongo wa chupa kuwa mabadiliko wanayotaka yanaweza kufanyika.......

Lakini ukweli Sioni nia na dhamiiri ya dhati ya CCM kuyafanya inayofanya bali ni shinikizo. CCM hawana option inabidi wacheze double standards. Wazuge wnashughulikia UFISADI ili wnanchi warudishe matumaini na wakati huo huku wanawapoza mafisadi kuwa wasiwe na wasi wasi Hakuna kibaya kitakacho wapata.

MKapa yeye aligoma kabisa kusikiliza. Huyu JK yeye kaamua kukubali lakini anamuua kudeal na ufisadi kwa maigizo ya kina MRAMBA YONA LIYUMBA etc. Seikali inamshtaki mtu kesho mwenyeiti chake anaruhusu agombee ubunge. Hiyo ndio sanaaa

CCM inataka kureform sio kwa sababu viongozi wake wanaona infaa kufanya reform . NO CCM wna reform sababu mazingira YANAWALAZIMISHA KUREFORM.
 
- Nape simama hapo hapo, CCM inahitaji mapinduzi makubwa sana kutoka within na somebody had to start somewhere, so far so good it is only a matter of time CCM nzima itabadilika, na hasa kwenye uchaguzi wa 2015 ambapo CCM ni lazima ibadilike maana hakuna choice nyingine isipokwua kubadilika tu!

- Bravo Nape! CCM inakuhitaji zaidi kuliko wakati wowote huko nyuma!

Willie @ NYC, USA.

Mkuu salama lakini hapo.Nakuja sasa tunaonane nitakaa hapo siku 3 tu
back to maelezo yako mzee nakujua sana wewe ni mkongwe hapa unataka mfanye changes karibia na uchaguzi kwa kuwaonyesha watanzania kwamba mnaweza ? Hii ni hadaa sasa mkuu .Nakuamini miaka yote hapa JF unasimamia Utaifa kwanza leo unasemaje maneno ya kufanya changes last minutes ili kupata kura mkuu ? Au umeamua nawe kuwa mgumu kama wao .Nakujua wewe ni CCM lakini ni CCM wa Tanzania kwanza chama nyuma leo hapa inakuwaje ? Nape kwangu namuona mtupu huyu si msaada na hana uchungu na Nchi hata mara moja .Nape ana mavyeo lukuki na mengine hata hawezi kuwatumikia wananchi bado aitwe mpambanaji ? Hapana huyu bado sana .
 
- CCM inaongozwa na Mwenyekiti aliyewahi kusema kwamba kila analosema Nape lina baraka zake kwa 100%, that is all what counts katika siasa za taifa kama za Nape!

Willie @ NYC, USA.
Mwenyekiti yupi unayemwongelea? As far as I know mwenyekiti mwenyewe ni mnafiki wa kutupwa. Yeye kashindwa kumkamata na kumshitaki Rostam kutokana na kashfa ya Kagoda, despite kwamba ni raisi wa nchi mwenye mamlaka ya mwisho juu ya chochote kile. Sasa Nape anatoa wapi hilo lungu la kumfukuzia Rostam, ambaye ndiye mfadhili mkuu wa CCM? Na zaidi sana, Rostam huyo ndiye aliyemweka Kikwete pale alipo? Huo ubavu wa kumvukuza aliyeshikilia ngazi wakati wewe bado upo juu unautoa wapi?
 
Aliyemtuma NAPE ambaye ni rais KIKWETE yeye mwenyewe ni FISADI,mikataba yote ya ulaghai anahusika,sasa hapo ni kuwatadanganya watanzania wakati KIKWETE si msafi,kwa upande wa NAPE ni mtu anayetumiwa bila kujijua baada ya wahusika waliomtuma kumuona ni mtu asiye makini kwa hiyo ni rahisi kumwambia alopoke lolote lile.
 
Back
Top Bottom