CCM ya Nape ni nadharia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM ya Nape ni nadharia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kitila Mkumbo, Jul 3, 2011.

 1. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #1
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Niliwahi kuandika haya hapa chini kwenye moja ya magazeti hapa nchini. Japokuwa malengo yalikuwa tofauti kidogo kipindi hicho, maudhui yake bado yanasimama. Nape ameanza kupambana na CCM muda kidogo na naona style yake haijabadilika, jambo linalomfanya aonekana 'odd out'. Wakati ule alishindwa kusimama sijui sasa tunapoelekea zile siku zao 90 kama ataweza. Kwa sasa, kama ningeandika tena hii makala, ningebadilisha tu neno Nchimbi na kuweka Lowasa na/au Chenge. Jikumbushe kama mie nilivyojikumbusha...
  ************************************************************************************************************

  CCM ya Nape ni nadharia; ya Nchimbi ndiyo iliyopo

  Kitila Mkumbo
  Nimefuatilia, kama ilivyo kwa watanzania wengine, ‘mgogoro' wa kifikra na mtazamo kati ya aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa UVCCM, Nape Nnauye, na Mwenyekiti anayemaliza muda wake katika umoja huo, Emmanuel Nchimbi. Hata hivyo nikiri mapema kabisa kuwa sielewi mantiki ya mgogoro huu na hatimaye mjadala uliofuatia na unaoendelea. Nisichoelewa hasa ni msingi wa dhamira ya Nape katika hoja yake ya kupinga mkataba wa mradi wa ujenzi wa jengo la makao makuu ya UVCCM, ambayo imevutia hisia za watu wengi, ndani na nje ya CCM.
  Najiuliza maswali mawili. Mosi, je, Nape ameibua hoja ya kupinga mkataba ‘haramu' wa mradi wa ujenzi wa jengo la UVCCM kama karata na turufu ya kumwezesha kushinda kiti cha uenyekiti wa umoja huo? Pili, je, ni kweli kwamba Nape ni miongoni mwa wana CCM wachache "waliokoka" na kujiunga na kundi kubwa la wananchi wanaochukizwa na kukerwa na mwenendo wa ufisadi miongoni mwa viongozi waandamizi wa CCM na serikali yake? Kama msingi wa hoja ya Nape ni ule wa kwanza, wa kutumia hoja yake kama turufu ya kuvuta hisia za wana UVCCM wenzake ili wamchague kuwa mwenyekiti wao, ni wazi kuwa amekwishashindwa kabla hajaanza. Kwa msingi huu, anachojaribu kufanya Nape ni kuvunja misingi mama ya kanuni za ushindani ndani ya CCM. Nape anataka achaguliwe kwa misingi ya hoja za kimantiki, uadilifu, ustaraabu, ukweli, uwazi, uhuru na kujitegemea katika kufikiri, na, zaidi ya yote, kutanguliza utaifa dhidi ya uchama na ukada. Yote hii ni misingi mizuri, lakini sio misingi ya CCM na ndipo upofu wa Nape ulipo. Kwa hoja zake, Nape anajaribu kuweka mlo safi katikati ya jalala la taka. Hautanoga na wala hataufaidi mlo huo, na zaidi ya yote anajiweka katika mazingira hatari ya kuambukizwa vijidudu hatari vitakavyompelekea augue ugonjwa hatari wa matumbo!
  Anachofanya Nape ni kupingana na misingi ya kanuni za msingi za kutafuta madaraka ndani ya CCM, ambazo, kwa uchache kabisa, ni pamoja na ubabaishaji, uzandiki, ujanjaujanja, njia za mkato, unafiki, ghiliba, kujipendekeza, kuiba wajumbe na kuwaficha, na muhimu zaidi kuliko zote, kutanguliza ukada na uchama dhidi ya uwezo wa kiuongozi na kiutendaji na uzalendo kwa nchi. Hii ndio CCM ambayo Nape anajaribu kuibomoa na ambayo Nchimbi na wenzake akina Makamba wanaipigania. Kwa hiyo utaona kwamba CCM ambayo Nape anajaribu kuipigania haipo, ni ndharia; iliyopo ni ile CCM ambayo Nchimbi na Makamba wanajaribu kuilinda kwa mafanikio makubwa.
  Niliwahi kuwa mwanachama na kada wa CCM kwa muda kidogo na nilijaribu kugombea nyadhifa kadhaa katika UVCCM, na,kwa bahati nzuri, nilishindwa zote! Kwa uzoefu nilioupata ni kwamba hushindi uchaguzi ndani ya CCM kwa kuwa na uwezo au kwa kujenga hoja za kimantiki zinazoweka maslahi ya nchi mbele. Unashinda uchaguzi ndani ya CCM kwa kujifanya wewe ni kada kuliko mmwingine yeyote, kwa ujanjaujanja, kwa kujipendekeza na kujipitishapitisha kwa baadhi ya wakubwa wanaoingia kwenye vikao muhimu vya CCM, kurubuni wajumbe wa vikao, ikiwemo kuwaficha wajumbe wa vikao hivyo. Ukitaka kushindwa kirahisi katika uchaguzi wa CCM uonyeshe uwezo na utangulize mambo ya taifa mbele badala ya ukada. Kama kuna kiongozi wa CCM aliyeshinda uchaguzi ndani ya chama hicho kwa kujenga hoja za kutetea maslahi ya taifa dhidi ya ukada awe wa kwanza kujibu makala hii.
  Nape, na wana CCM wengine makini, wanajua vizuri sana kwamba ingekuwa ni swala la uwezo na kutanguliza maslahi ya taifa, Rais Kikwete asingewashinda Salim Ahmed Salim, Mark Mwandosya, na hata Frederick Sumaye. Pamoja na mambo mengine, sifa kubwa iliyomfanya Rais Kikwete awashinde wenzake katika kinyang'anyiro cha kugombea urais ni ukada wake wa muda mrefu katika CCM. Kwa hiyo katika CCM ukada ndio sifa mama na kigezo muhimu cha kuweza kuchaguliwa. Ndio kusema Nape anapojaribu kutanguliza utaifa, tena kwa kuzomea ufisadi ambayo ni nguzo muhimu ya kuwepo kwa CCM, kama turufu ya kutaka achaguliwe kuwa mwenyekiti wa UVCCM anajaribu kukata mbuyu kwa uwembe. Hataweza; atajikata mwenyewe na kuuacha mbuyu umesimama kidete.
  Pengine tumpe Nape ile wazungu wanaita "the benefit of doubt". Kwamba Nape ni miongoni mwa wana CCM wachache waliokoka hivi karibuni, na ameamua kujitoa mwili na roho katika kujiunga na majemadari wa vita dhidi ya ufisadi. Kuokoka kupo sio tu katika siasa na dini, lakini pia katika nyanja nyingine za maisha ya kijamii. Lakini unapoamua kuokoka lazima ujue na uzingatie misingi ya wokovu, vinginevyo utaanguka tena. Kuokaka kisiasa na kidini kunahitaji ujasiri wa kukubali kusutwa na kuacha mazoea. Ili ukamilishe wokovu lazima ukubali kubadilika kimwili na kiroho.
  Ninachokiona hapa ni kwamba Nape amekwisha kutoka CCM kiroho, kiakili na kisaikolojia lakini bado amebaki kimwili. Hili ni tatizo linalowakumba wana CCM wengi. Ninaamini kuna wana CCM wengi waliokwisha kukihama chama chao kiroho, kiakili na kisaikolojia, lakini wameendelea kubaki huko kimwili kwa kukosa ujasiri au kwa sababu zingine, ikwemo kuamini kwamba ipo siku CCM itadilika. Nikiri kuwa mimi ni mojawapo ambaye ilinichukua takribani miaka mitano kuhama CCM kimwili. Nilikuwa nimeachana na CCM kiroho, kiakili na kisaikolojia tangu mwaka 2000, lakini ilinichukua miaka mitano hadi 2005 nilipoamua kujitoa hadi mwili na kujiunga na CHADEMA.
  Binafsi nilijitoa CCM baada ya kujiridhisha bila shaka kuwa CCM imefikia hatua ya usugu, na haiwezekani kubadilika. Ni hatua ambayo vyama dada kama KANU, ZANU-PF na UNIP vilipitia, na ambayo ni wananchi pekee wenye uwezo wa kuibadilisha. Kama kweli tumechoshwa na madhira ya CCM, ikiwemo ufisadi, inabidi tufike mahala tukubali kuachana na CCM. Kuendelea kuibakisha CCM madarakani ni kukubaliana kwamba, pamoja na kwamba tumeumia kama nchi, bado tunaweza kuendelea kuwavumilia CCM, hatujaumia vya kutosha. Kufikiri kwamba CCM inaweza kubadilika ni njia nzuri ya kujiridhisha kisaikolojia baada ya kushindwa kuitoa madarakani, lakini haisaidii kubadili hali ya mambo katika nchi yetu.
  Kwa hiyo Nape ana mambo mawili ya kuchagua. Mosi, anaweza akaendelea kubaki CCM kimwili na kuisaliti dhamira yake ya ndani na akaendelea kupiga kelele za ufisadi, ambazo zitazidi kumtenga na wenzake ambao "hawajaokoka" katika CCM, na hivyo kuendelea kuonekana kituko! Pili, anaweza akavaa ujasiri na akatoa mwili wake katika CCM na kujiunga na majemadari wengine walioamua kupigania maslahi ya nchi hii badala ya ukada na uchama. Tumemuonya, uamuzi ni wake.
  kitilam@yahoo.com
  0754 301 908
   
 2. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #2
  Jul 3, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nafikiri baada ya kususiwa na wenzake ndani ya CCM, Nape atahama rasimii chama kama si kuwa likondoo mbele ya wakubwa wake walioziba masikio na kuvaa miwani ya mbao, wakijifanya hawasikii wala hawaoni matatizo ya watanzania.

  Ni kweli kwamba Nape amejaribu sana kufanya tofauti na wanaCCM wengine. Angalau ameonyesha nia ya dhati ya kuuondoa au kuupinga mfumo mbovu na wa ufisadi uliomo ndani ya CHAMA chake. Hata alipokuwa akiwapa mafisadi siku tisini, aliamini kabisa kwamba walio nyuma yake watamuunga mkono. Lakini kwa hali ilyopo ni kama amebaki peke yake asiye na mbele wala nyuma. Wale aliodhani watamtetea na kuongea yale aliyokuwa anasema yeye, wamejitenga naye.

  Hivi sasa ameanza kutapa tapa kwamba ati hakutoa muda kamili wa kuwaondoa. Unaweza kwenda mbele au kurudishwa nyuma, lakini Nape jiangalie sana, juhudi zako za kumsafisha nguruwe zinaweza kukaharibia maisha yako. As i can see you are still young unahitaji kuandaa future yako nzuri. Lakini kupambana au kujaribu kuusafisha mfumo uliokwisha oza tayari, ni kupoteza muda na kuhatarisha maisha yako.
   
 3. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Binafsi namwonea huruma sana Nape ana kazi ngumu sana kuiwajibisha CCM ambayo bosi wake mkuu ndiye Rais wa nchi na ndiye baba wa huo ufisadi. Sijui atafanya lipi?
   
 4. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Nape is a guy who is in the wrong place at the wrong time in front of the wrong people. And, we all know that wrong place at the wrong time ruins young life.
   
 5. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Move yake nzuri ilikuwa ni ile ya CCJ, pale angepigana vita vya ukweli lakini ndani ya CCM hawezi na kamwe hataweza kutengeneza chama anachokitaka chenye katiba na sera kama za CCJ

  Nape ushauri wa bure,
  wewe ni kijana na ni mtu muhimu sana katika ukombozi wa Taifa hili, uozo mwingi umeuona na unajua chanzo chake na unajua solution zake, acha mambo ya asili (chama cha Baba), ingia kwenye mapambano ya kweli, siasa unayoifanya sasa haiwezi kumwokoa mtanZania aliyeko kijijini,wala mijini, toka ndani ya CCM ili ufanye siasa ya kweli kwa faida ya watanzania wenzio,
   
 6. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #6
  Jul 3, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,642
  Likes Received: 1,915
  Trophy Points: 280
  - Nape simama hapo hapo, CCM inahitaji mapinduzi makubwa sana kutoka within na somebody had to start somewhere, so far so good it is only a matter of time CCM nzima itabadilika, na hasa kwenye uchaguzi wa 2015 ambapo CCM ni lazima ibadilike maana hakuna choice nyingine isipokwua kubadilika tu!

  - Bravo Nape! CCM inakuhitaji zaidi kuliko wakati wowote huko nyuma!


  Willie @ NYC, USA.
   
 7. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,857
  Likes Received: 11,977
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo ushauri wako ni upi, nilitegemea useme fanya 1, 2, 3.......kumbe ni kelele za majukwaani tu.... sema baba sema tupo nyuma yako.
   
 8. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #8
  Jul 3, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Kuna kipindi niliikumbuka sana hii makala,nikaitafuta nikaisoma tena.

  Kaka yangu Nape, pengine hakujua ukubwa wa tataizo analopigana nalo na pia CCM ilikuwa imetafsiri tu kwamba kwa kuwa Nape alikuwa anapinga mambo mengi na kutafsiriwa na wenzake ndani ya chama kama vile mtu anayekichafua chama chake,wakaona ni bora wampe nafasi ya kukisafisha chama kile kile at the same time awe anavutia vijana wengi.Hii ya kwanza kwa kiasi fulani amejitahidi lakini huku tunakoelekea inabidi awe makjini asije akajikuta anatetea kile kile alichokuwa anapingana nacho.

  Hali ya kisiasa iliyopo ndani ya chama inabidi awe makini na asimamie kidete kile anachoamini hata kama ni kwa gharama ya kufukuzwa ndani ya chama chake.Ana kazi ambayo ni nzito sana kwake ya kutafsiri ideology ya chama iendane na matendo na kuvuta loyality ya wafuasi wake hasa kipindi hiki ambacho chama kinakabiliwa na upinzani wa ndani na tishio lingine kubwa zaidi upinzani wa nje.

  Hali iliyopo ni tete,safari ya urais na kushika dola 2015 kwa CCM imefungwa speed governer na makundi ya ufisadi ndani ya chama,makundi na au safu za madaraka(Mbio za urais) 2015.Kwa mantiki hiyo chama kinatakiwa sasa kivuke katika mtiani huu kwa kuwafukuza watuhumiwa wote wa ufisadi,again hapa sasa ndipo tutakapowazika kabla ya 2015.Kwa jinsi CCM walivyo desparate sasa inabidi wamuangukie Membe na magufuli(ambaye watanzania hawajamjua vizuri alivyo msanii) kwa sababu watataka kucheza na hisia za watu na uwezekano wa kumuweka candidate ambaye ni popular kwa wapiga kura na atakayetoa upinzani kwa mgombea wa Chadema.Hapa pia nako ni mtihani,hao wanaoitwa mapacha watatu watamwaga mboga na wataihujumu CCM beyond recovery.So nape hapa una kazi,hapa ndipo unapotakiwa kuonyesha unachosimamia na hapa ndipo utakapoonyesha nguvu na uwezo wako wa uenezi wa Itikadi ya chama chako

  By now ulitakiwa uwe umeshaonyesha uwezo na kuchora a very principled line kuwa kama chama hakitakuwa tayari kufanya kazi katika line ya ideology and values za chama chako basi hiyo kazi utaachana nayo ili wewe usije ukaingia katika historia ya kuangusha chama chako CCM kitakaposhindwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.Wasije wakakugeuza J.J Kamotho wa KANU ya 2002 Kenya.He came into terms with a tragic reality After December,2002 General election

  So you need to take precautions by abandon the usual way of doing business in your party and other political institutions.Rather than stand up against the obvious abuse of responsibility by those in power, many leaders in our political Institutions openly frolic with political champions for the sake of cheap publicity, political influence and their share in the taxpayers' money. As such, they are publically condoning this greed and power-mongering by their very attitude, abandoning the role of torch-bearers in the political landscape in particular and to the Nation in General

  It is one thing to make promises and be clueless about how to go about redeeming them; it is another to show you actually lack the spirit and will to want to redeem them in the first place. How do you hope to tackle corruption if you seek help from corrupt people to get into office in the first place?

  I wish him luck. He probably can't be any worse than the rest but it is now so glaring that he is not any better, either. Let his supporters spare me the pain of reading any more propaganda. The game is over; I now see him for who he is. For me, he has just lost the little edge he had, that that Dr.kitila call "benefit of doubt."

  Now Nape, inorder to bolister your movement,you need to be a lawyer, pyschologist and a smooth talker rolled in one but aiming on taking a tough stance at the end.
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Honestly mje mumsaidie msiishie kukaa nyuma ya keybod,nappe hana sapot na hao wanaomtuma hawana nia ya dhat zaid ya kumsukumia mzgo nape,umeona hata mzee John sasa hivi ameamua kuacha kuwa tingatinga,unadhan kuna mtu aliyewah kushika nafas kama ya nape akaimudu?,unamkumbuka Mapuri?what next?alifichwa China,Nape is intelligent but hajui anaongea nini?na kwa nani,kwa sababu hana cha kukiongea,sema mwenyewe utaiongelea nin sisiem kwa sasa?????
   
 10. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #10
  Jul 3, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,001
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  nape anakazi kubwa sana, uamuzi ni wake.
   
 11. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280

  CCM haiwezi kubadilika kwaq sababu wote ni wachafu, na wale wanaoonekana ni wasafi wanafunikwa ama wanatolewa kafara, Nape ametolewa kafara, wamempa kazi ya kukisaficha chama ambacho hakisafishiki,
  kumwambia Nape abaki ndani ya CCM ni kumwaribia malengo yake kisiasa kama anayo, CCM inatype zake lakini sio Nape, nape anajaribu kuforce na kukitengeneza chama kwa dream zake lakini anakutana na vikwazo vingi tu, angalia sasa Mukama kesha mkana na siku zake tisini alizotoa zimebakia nne tu
   
 12. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  William, suppose wewe ndo ungepewa nafasi ya NAPE, ungebadilisha nini? Mimi namwona Nape jasiri sana. Pamoja na kujua kwamba kwa kuwa mkweli atajiweka mahali pabaya bado amediriki kusema. Lakini tugeuke nyuma tujikumbushe majibu ya Mukama dhidi ya kauli ya Nape ya kuwafukuza mafisadi ndani ya siku 90? Maana Nape alikuwa kifua mbele kutangaza siku tisini akijua alionao ndani ya chama wanamuunga mkono. Lakini Mukama alipoulizwa akasema kikao hakikutamka siku tisini. Vaa viatu vya Nape, useme katika majibu kama hayo unafanyaje? Twende mbele zaidi, Nape aliutangazia umma kwamba barua za kuwaondoa mafisadi zinaandaliwa, lakini walipoulizwa msekwa na mukama wote walikanusha kuhusu kuwepo kwa barua. hii ina maanisha nini? Nafikiri kama alivyosema Msema hovyo hapo juu, jamaa keshaachwa solemba. Na tuombe Mungu wasimuue. Maana CCM hawashindwi kitu.
   
 13. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #13
  Jul 3, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,216
  Likes Received: 3,777
  Trophy Points: 280
  Sijaelewa unamshauri au una mshangilia?
   
 14. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2011
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi Nape amelifanyia nini Taifa hili au ameonyesha msimamo gani kwenye masuala mazito yenye maslahi kwa Taifa, ukiachilia mbali kupinga kwake ujenzi haramu wa makao makuu ya UVCCM tena ktk kipindi alichokuwa anafukuzia uenyekiti wa UVCCM, mpaka tumuone ni "mlokole" wa kisiasa?
   
 15. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #15
  Jul 3, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,642
  Likes Received: 1,915
  Trophy Points: 280
  - Ndugu yangu Ben, saafi sana ninajaribu kuisoma na kuitafakari sana hizi hoja zako, zimetulia sana!, ninatisoma tena kabla ya kuongeza chochote!

  Willie @ NYC, USA.
   
 16. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #16
  Jul 3, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Naamini kwa sasa nape ana siku chini ya saba kuamua moja, kutetea sera ya kujivua gamba au na yeye awe gamba la kungo'lewa
   
 17. F

  FJM JF-Expert Member

  #17
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mpaka sasa nimeshindwa kuelewa kama Nape anasema anayosema kwa sababu anasimamia kitu fulani au ametumwa kusema hayo kama sehemu ya ajira? Nadhani wako wengi wanapata shida juu ya huyu Ndugu Nape.
   
 18. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #18
  Jul 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nape anatumwa na chama kusema,lakini bado chama kinashindwa kumwambia kitu gani muhhim cha kusema,kwa sababu chama hakina zuri la kulisemea na watu wa kuelezwa,kwa hiyo anajikuta anatumia calories nyiiingi kweli mtoto wa mzee Nauye
   
 19. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #19
  Jul 3, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwa post yako hii sidhani kama umemsadia Nape. Najua wewe ni mwana-CCM, but you gonna have to be objective na mzigo aliobebeshwa Kijana mwenzetu Nape. Asije akashindwa, halafu uwe wa kwanza kusepa. Na hili tayari linajidhihirisha hata kwa wabunge vijana wa CCM. Sidhani kama nimesikia wakimuunga mkono in public. Whether wanafanya hivyo in private, I don't know.

  Mkuu unapingana na ambacho Nape anakiamini unless labda awe amebadilika hivi karibuni. Wakati wewe unaangalia zaidi maslahi ya chama, Nape alishasema huko nyuma kuwa kwake yeye siasa ni utumishi kwa umma na katika hilo anaamini katika uzalendo kwa nchi kwanza, chama baadaye. "Tunakuwa na nchi kwanza tunayotaka kuijenga, ndipo tunaunda chama cha kujenga nchi tunayoitaka, kwa hiyo uzalendo kwa nchi unapaswa kuvuka mipaka ya itikadi zetu," anasema Nape.

  Nakubaliana na hoja ya Mkumbo. Nape alipata misukosuko kwenye uchaguzi wa UVCCM, akavuliwa uanachama wa UVCCM pale alipojaribu kukemea ufisadi na baadaye kuangushwa hata kwenye kura za maoni za ubunge. There is no doubt kuwa matatizo ya ndani ya UVCCM yanaakisi yale ya CCM yenyewe. Kwamba ndani ya CCM kuna watu ambao nje wanaonekana kwamba wanafanya kazi ya kuendeleza nchi, lakini ukweli ni kwamba wanaendeleza maslahi yao binafsi. What Nape is trying to do now is exactly what he tried in UVCCM but failed miserably.

  Well, utaniambia CCM imejivua gamba and it is "only in matter of time CCM nzima itabadilika". Lakini hutaki kufanya analysis hao walengwa (victims) nao wemejihami vipi. Unafikiri kuwa "CCM nzima itabadilika" in "matter of time" just like that. Hutaki kuumiza kichwa. Unafikiria kuwa tarehe 11 mwezi huu utaamka na kukuta "CCM nzima imebadilika". Never never underestimate the determination of quiet man.

  Nape may be energetic and intelligent, but senior politicians in the party may hinder what he wants to achieve. Nakushauri ukasome kitabu kilichoandikwa na marehemu Patrick Ng'ara (RIP) kiitwacho KIKOMO. Kinaonesha jinsi mpelelezi alivyopata shida kupambana na majambazi ambao walikuwa na nafasi nyeti ndani ya serikali.
   
 20. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #20
  Jul 3, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,642
  Likes Received: 1,915
  Trophy Points: 280
  - What counts here ni kwamba unakubali kwamba Nape ni msafi, ndio maana tunasema atatusaidia sana CCM na siku Nape akishindwa nitarudisha rasmi kadi yangu ya CCM.


  Willie @ NYC, USA.
   
Loading...