CCM wekezeni kwenye akili acheni kutumia mitulinga

CCM wekezeni kwenye akili acheni kutumia mitulinga

Wanasaikolojia husema binadamu (siyo mtu) dhaifu hujaribu kuficha udhaifu wake kwa kufanya mambo yake kwa kutegemea mitulinga.

CCM imekuwa inaongoza nchi hii Kwa zaidi ya miaka 33 sasa tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe hapa nchini.

Lakini Katika jambo ambalo CCM wameshindwa kabisa kulitafutia ufumbuzi ni suala la ajira (siyo kazi) na ujira Bora Kwa watanzania.

Miaka nenda miaka rudi kwa zaidi ya miongo mitatu sasa CCM haijui ifanye nini kuongeza ajira na kuweka uhakika wa ajira kwa watanzania huku ujira kwa watanzania ukiwa mzuri na wa uhakika.

Hali hii inatokana na CCM kuwaza kuwa ajira ni kazi na kuwa kila kazi ni ajira. Upotofu huu umefanya ajira kisiwe kipaumbele cha CCM.

Viongozi kadhaa utawasikia wakisema kuwa "kama maisha ya mjini yamekushinda rudi kijijini ukalime". Yaani zama hizi kweli kulima kwa jembe la mkono inakuwaje ni chanzo cha ajira!?

Ukisikiliza jinsi CCM inavyowaona wamachinga, bodaboda au wapiga debe kuwa ni ajira rasmi, ndipo unapojua kuwa CCM inaona ajira ni kazi za kutoka jasho pekee!

CCM wekezeni kwenye matumizi ya akili ili kuongeza ajira kwa watanzania.
20250211_191743.jpg
 
Kama haya ndio mawazo yaliyojaa kwenye kichwa chako basi mtageuzwa geuzwa sana na wanasiasa.
Maana mmechagua mtu mmoja ndio awe anafikiri kwa niaba yenu.na ninavyokuona hata kesho lisu akisema, tutashiriki uchaguzi utashangilia tena kama unavoshangilia kampeni ya sasa,nyumbu daima nyumbu!
Kwa nini abadili mtizamo?
 
Kama waliweza kusema marehemu lowasa ni fisadi alipokuwa ccm ila alipojiunga nao wakasema ni mtu safi kabisa.unaweza kuwa na uhakika kiasi gani kuwa hawawezi kubadilika mda wowote?
Kwanza ili hoja yako ijadiliwe hebu elezea ilikuwaje CHADEMA walisema kuwa Lowassa fisadi!?
 
Kuna mahali nimeandika kuwa sikumbuki? Nataka kujua jee uelewa wetu ni mmoja ni kwa nini CHADEMA tulisema Lowassa ni fisadi.
Sio tu walisema fisadi.pia chadema walisema lowasa anatakiwa kuwa jela na kuzomewa. Lakini alipojiunga nao ghafla! walimshangilia na kumuimba kuwa ni mwanamabadiliko.
 
Sio tu walisema fisadi.pia chadema walisema lowasa anatakiwa kuwa jela na kuzomewa. Lakini alipojiunga nao ghafla! walimshangilia na kumuimba kuwa ni mwanamabadiliko.
Sasa wewe husemi ni kwa nini CHADEMA tulisema Lowassa ni fisadi. Kama hujui basi huwezi kujua ni kwa nini tukakubali awe mgombea wetu.
 
Sasa wewe husemi ni kwa nini CHADEMA tulisema Lowassa ni fisadi. Kama hujui basi huwezi kujua ni kwa nini tukakubali awe mgombea wetu.
Si tu mlisema fisadi,hadi Richmond mlisema ni yake na ina jina la mtoto wake na mahali alipotokea.
Na hata aliposema atagombea urais 2015 kupitia ccm bado mlimpiga vita hata kabla chama chama chake hakijapitisha mgombea rasmi.chadema walianza kusema lowasa ameanza kampeni kabla ya muda,lowasa alikataliwa hadi na mwl. Nyerere.,ni mzee na ni mgonjwa,hastahili hata kuendelea kuitwa mstaafu,anatakiwa kuzomewa n.k

Lakini alipojiunga na chadema tu ghafla,akawa sio fisadi,akawa msafi,akawa mpango wa mungu.
Mtu pekee ambaye alisimamia msimamo ni dr slaa peke yake.ambaye ujio wa lowasa chadema aliufananisha na kuweka kinyesi sebuleni.

Hawakuishia hapo. chadema wakaenda hadi kinyume na katiba ya chama Chao. kumruhusu mwanachama ambaye hajafikia vigezo kugombea nafasi ya juu kabisa ya uongozi.

Watu vigeugeu hivi unawezaje kuamini kuwa hawazi badilika muda wowote?
 
Kama haya ndio mawazo yaliyojaa kwenye kichwa chako basi mtageuzwa geuzwa sana na wanasiasa.
Maana mmechagua mtu mmoja ndio awe anafikiri kwa niaba yenu.na ninavyokuona hata kesho lisu akisema, tutashiriki uchaguzi utashangilia tena kama unavoshangilia kampeni ya sasa,nyumbu daima nyumbu!
Chawa kama chawa et el
 
Back
Top Bottom