CCM Wapongezwe kwa Kuiogopa CHADEMA, Wasibezwe!

FACTSFIRST

Senior Member
Dec 6, 2019
191
290
Tangu mwaka 2010 Chadema kilipokuwa chama kikuu rasmi cha upinzani nchini, siasa za Tanzania hazijawahi kubaki za kawaida! Kwa wenye kumbukumbu nzuri, tangu mwaka 2010 chama kilipoanza kuongozwa na Freeman Mbowe, CHADEMA kimekuwa chama pekee cha upinzani nchini kinachokua mfululizo (both institutionally and statistically) bila kudorora. Kutoka kuwa chama cha tata au cha nne kwa umaarufu mwaka 1995 uchaguzi wa kwanza ulipofanyika nchini, CHADEMA kimekuwa kikijengeka mwaka hadi mwaka, huku uimara wake ukiongezeka toka mijini hadi vijijini na kuweka mizizi ya wananchama maeneo yote nchini kama ilivyofanya CCM ndani miaka zaidi ya 50 ya kuwepo kwake.

Hili limedhirhirishwa wazi na idadi ya wananchama wanaojipambanua kuwa wana CHADEMA, hasa kupitia chaguzi mbalimbali ambapo mikutano ya hadhara, mikutano ya ndani ya wananchama, idadi ya viongozi ndani ya chama (ngazi zote mijini na vijijini), idadi ya madiwani, wabunge, na hata kura za urais ambazo zimekuwa zikipanda toka uchaguzi mmoja hadi unaofuata. Idadi ya Halmashauri za miji na wilaya zilizowahi kushikwa na CHADEMA kupitia wingi wa madiwani na wabunge, kama vile Mwanza, Arusha, Iringa, Mbeya, Kinondoni, na kwingneko, vinadhihirisha kukubalika kwa chama hiki pande zote nchini kiasi cha kuwa tishio kubwa kwa CCM na serikali yake (kiasi cha serikali kulazimika kutunga sheria mpya ya kodi za halmshauri ili kuhakikisha mapato makubwa toka halmashauri ziliziokuwa chini ya CHADEMA mwaka 2015 hazipati mapato ya kutekeleza mipango ya chama hicho kama walivyokuwa wameahidi kwenye ilani yao).

Hata kwa vipimo vyote vya kitaasisi, CHADEMA kimejipambanua kuwa chama halisi (authentic organized political party) chenye maono, nia, na focus ya kweli ya kuongoza nchi. Kwa wanaojua yanachofanyika nyuma ya pazia, CHADEMA kimekuwa kikishinda uchaguzi kiti cha uras tangu 2010 (Dr Slaa dhidi ya Kikwete) na 2015 (Lowassa dhidi ya Magufuli). Sote tunajua mioyoni mwetu kuwa Tume ya Taifa kwa muundo wake wa sasa haiwezi kutangaza mgombea wa Upinzani kushinda, kwa hiyo usiniulize kwa nini CHADEMA hawako ikulu!

Ukweli kuhusu nguvu na kuimalika kwa CHADEMA kuliitisha zaidi CCM katika uchaguzi Mkuu wa 2015 ambapo CHADEMA kilionekana kupigiwa kura na zaidi ya watanzania millioni 6 (japo kura halisi inasemekana zilikuwa zaidi ya milioni 7.8). Baada ya kuvuka kwa mbinde 2015, CCM na Magufuli (aliyekuja kuwa rais na mwenykiti mpya wa CCM) waliambiwa ukweli mchungu juu ya kuimarika kwa CHADEMA na kuonywa kuwa wasipokuja na mikakati thabiti, wajiandae kukabidhi nchi kwa CHADEMA ifikapo Oktoba 2020. Kupitia taarifa hiyo (iliyothibitishwa na takwimu za kuongezeka kwa kura za CHADEMA na ubunge na urais) rais Magufuli alitaharuki na kujua kwamba akifanya mchezo hatauweza moto wa chama hiki chenye kila aina ya viashiria vya kuiondoa CCM madarakani.

Ndipo Magufuli akaja na mikakati katili ya kuua CHADEMA (siyo upinzani) kwa nguvu zote (hata kama mikakati hiyo inavunja katiba ya nchi na sheria za vyama vya siasa). Kwa haraka haraka Magufuli akaamua kuzuwia vyama vya siasa (isipokuwa CCM) kufanya shughuli za kisiasa kwa mujibu wa katiba. Magufuli akapiga marufuku mikutano yote ya hadhara ya siasa na vikao vyote vya ndani. Lengo likiwa kuizuwia CHADEMA isiendelee kujitanua na kuimarika. Alipoona hiyo haitoshi, akaja na vitisho juu ya viongozi wa CHADEMA waliokuwa wakiukosoa utawala wake. Kunusurika kuuawa kwa mwanasiasa machachari na Mnadhimu wa kambi ya Upinzani bingeni, Tundu Atipas Lissu, ilikuwa ni desperate attempt ya ku silence CHADEMA by force. Hii ilifutiwa na kamata kamata na kufunguliwa kesi kwa viongozi wote wa CHADEMA nchi nzima. Alipoona hiyo haileti madhara, Magufuli kaja na mkakati wa kununua viongozi (wabunge, madiwani, wenyeviti) wa CHADEMA kwa kisingizio cha kuunga mkono juhudi. Alipoona CHADEMA bado haiyumbi akaiamuru serikali kumshughulikia binafsi kiongozi mkuu aliyeifikisha CHADEMA hapa ilipo. Mali za Mbowe, yakiwemo majengo, vifaa na mashamba yakaharibiwa kikatili bila chembe ya utu. Alipoona na hiyo haimhakikishii kuingia uchaguzi mkuu 2020 bila CHADEMA, sasa kaja na TAKUKURU kuchunguza madai ya wanachama waliohama CHADEMA baada ya kuCCM (kuChukua Chao Mapema). Kwa tunaojua historia ya vyama tawala vinavyoelekea mwisho, natabiri kwamba CCM na serikali yake watailazimisha ofisi ya Msajiri wa vyama kutafuta kila aina ya visingizio ili kuifuta kabisa CHADEMA hii inayotishia uhai wake isishiriki kabisa uchaguzi mkuu 2020. Hofu ya kufa si chezo!

Sasa hebu tuwe wakweli hapa, hivi hata kama ungekuwa wewe ndiyo CCM (hii iliyochoka, isiyo na mikakati, chini ya wachovu kama kina PolePole) na Magufuli (huyu mwoga wa chaguzi zenye ushindani maisha yake yote) usingeiopa kweli CHADEMA hii na kuanza kufanya kila linalowezekana kuhakikisha unaiua kabla ya uchaguzi mkuu 2020? Mie nadhani hizi ni hatua sahihi za kujihami zinazochuliwa na kila mtu anayenusa kifo chake. Kwa hito tusiwabeze CCM kwa hili, historia ya CHADEMA inatisha mno!! Tuwapongeze CCM kwa hatua zote wanazochukua dhidi ya CHADEMA (hata kama ni za kijambazi, kuvunja sheria, na woga wa kupita kiasi). Kwani wafanye nini zaidi kuizuwia CHADEMA inayotisha hivi?
 
Mleta uzi hili bandiko lako liko sahihi kwa 100%. Na sasa tunategemea hujuma za wazi kabisa katika uchaguzi huu ili kuhakikisha cdm inakufa. Uzuri wapiga kura wa cdm hawajayumba wala hawayumbi.
 
Kweli umesema kabisa.Lakini sasa wao watumie siasa za kistaarabu sio kutaka kuhatarisha usalama wa nchi.Ndio maana aliachana na ccm asilia ana kutaguta machotara ili waendeshe siasa ngeni hapa nchini.Lakini octoba tutabanana nao.wakirusha chupa sisi tunarusha nondo.
 
Mkuu kwanza hongera kwa uchambuzi mzuri. Pili hongera kwa kuusema ukweli wa kile kinachopita huko CCM. Huu ni ukweli mchungu kila mwananchi anaujua. Hata CCM wenye akili kidogo wanashanga vitendo vya mwenyekiti wao. Kama ni kifo kimeshafika ccm haichomoki.
 
Mleta uzi hili bandiko lako liko sahihi kwa 100%. Na sasa tunategemea hujuma za wazi kabisa katika uchaguzi huu ili kuhakikisha cdm inakufa. Uzuri wapiga kura wa cdm hawajayumba wala hawayumbi.
Mleta uzi amefafanua concept ya Causal-effect
 
IMG_20200601_173955.jpg
 
Chama kimebaki na wafagiaji ofisi tu wengine wote wamekimbia
Mleta uzi hili bandiko lako liko sahihi kwa 100%. Na sasa tunategemea hujuma za wazi kabisa katika uchaguzi huu ili kuhakikisha cdm inakufa. Uzuri wapiga kura wa cdm hawajayumba wala hawayumbi.
 
Jpm alimtuma lowasa awambie kuwa yeye hataniwi
Kweli umesema kabisa.Lakini sasa wao watumie siasa za kistaarabu sio kutaka kuhatarisha usalama wa nchi.Ndio maana aliachana na ccm asilia ana kutaguta machotara ili waendeshe siasa ngeni hapa nchini.Lakini octoba tutabanana nao.wakirusha chupa sisi tunarusha nondo.
 
Back
Top Bottom