CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu

CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu

Mimi Mwaka huu Wananchi wa Tanzania wakichagua tena CCM, ctokuwa na mda wa kuyaongelea maovu ya ccm maana wananchi wenyewe watakuwa wameridhika na hali hii na umaskini wao.
Kwangu mimi niliebaatika angalau kupata elimu ya Chuo, nina kazi yangu, watoto wangu na mke wangu wanaweza kupata kiendacho kinywani, naweza kuendesha gari yangu, natibiwa kwa kadi ya bima nk.
Namwambia mwananchi mlala hoi jinsi UKAWA utakavyowasaidia
1. Elimu bure adi vyuo vikuu
2. Bei ya vifaa vya ujenzi kushuka na atimae kila mtanzania kuondokana na nyumba za nyasi na tembe.
3. Matibabu bure kwa wazee
4. Serikali ya majimbo( Itakayoleta chachu ya maendeleo majimboni"county" na cyo kodi zote kujenga Dar na zinazobaki kuliwa.
5.na zingine nyingi.
Kwayo mimi na wezangu wengu humu hamtafaidika sana kama mwananchi
Wa kawaida.
Mfano: kuna watu humu wanaweka kazi zao rehani kuwatetea kazi ambazo wengine unaona tayari wana maisha angalau wana nyumba wanaendesha magari yao,
Lakini bado wananchi wanapinga hawasikii.
Ndugu zangu Inatosha, tujitoe kimasomasonmwaka huu tuwaambie wananchi kama hawatasikia kwa Kupewa kanga na vitisheti!!!!!!
Mtanishangaa kuanzia 2016.

Kuongea mbona rahisi sana ,ata mie ninaweza kukwambia CCM ikishindwa mwezi 10 kila raia atapewa mshahara wa million 10.Mdomo haulipiwi.Tatizi linakuja ni jinsi gani utafanya hayo?na ndio maana Dr Slaa kakimbia mdahalo maana mbele ya guru ka uchumi Prof Lipumba asingeweza kutetea hayo.

Katika upinzani kuna kichwa kimoja tu, Le Proffesseur Ibrahim Haruna Lipumba
 
Mm nipo bukoba, ya mwanza cjui, cement aina zote, simba, twiga, tembo n.k
 
Hoja ya mleta mada imejengwa katika Premises za uwongo na hivyo conclusion yake ni ya uwongo

Exchange rate mwaka 2005 ilikuwa above shilingi 1000 na si shilingi 650 kwa dola.

kwa logic hiyo hiyo ya mleta mada, kama bajeti ilikuwa shilingi Trillion saba mwaka 2005 kwa exchange rate ya shilling 1200 kwa dola moja mwaka huo, basi hiyo ni sawa na jumla ya dollar billion 5.3

kwa mwaka huu ambapo bajeti ni shilling trillion 22 na kwa kwa exchange rate ya shilling 2250 kwa dola moja mwaka huu basi ni sawa na jumla ya dola bilioni 9.78

Sasa ni Jukumu la Wapenda Ukweli kujionea wenyewe dola bilion 5.3 na dola bilioni 9.78 ipi kubwa?

Kiufupi Bajeti almost imedouble in 10 years, na hilo ni jambo la kuipa Kudos Serikali iliyoko Madarakani
sawa! Ila hebu weka na inflation rate kati ya 2005 na2015 ili tuone purchasing power ya mwaka huo na mwaka huu,yaonekana wewe pia ni mpenda namba,unafurahia wingi wa digits bila kujua stabillity yake,kweli tuna mipesa mingi isiyo na thamani!! Unafurahia hilo?
 
Ujinga wawatanzania bado umetufikisha hapa
 
CCM WANAPENDA NAMBA LAKINI HAWAJUI HESABU.!

Na Malisa GJ,

Leo tuongee uchumi kidogo.

Kuna watu wanapenda namba lakini hawajui hesabu. Kama na wewe ni mmoja wao tafadhali usisome makala hii.

Wabunge wengi na mawaziri wa chama cha mapinduzi ni wagonjwa wa namba. Wanapenda namba lakini hawajui hesabu. Ukitaka wakushangilie we ongeza tarakimu tu kwenye namba. Wanapenda namba lakini hawajui hesabu.!

Kama ulikua unamlipa mtumishi mshahara wa laki 5 mwaka jana mwaka huu mlipe laki 7. Atashangilia na kukushukuru. Kumbe hajui upande wa pili gharama za maisha zimeifanya hiyo laki 7 iwe sawa na laki moja ya mwaka jana. Yeye atakushukuru tu, kwa sababu anapenda namba lakini hajui hesabu.!

Naona wengi hamjanielewa. Ni hivi kuna faida gani kulipwa mshahara wa milioni mbili halafu ukauziwa sukari kilo moja sh.3000/=??? Si bora ulipwe laki 5 sukari uuziwe sh.500/= kwa kilo. Kama unapenda namba lakini hawajui hesabu huwezi kunielewa.

Twende kwenye historia kidogo. Mwaka 2005 wakati Rais Mkapa anaondoka madarakani bajeti ya serikali ilikua Trilioni 7. Mwaka huu ni Trilioni 22. Wanaopenda namba lakini hawajui hesabu wameshaanza kuhangilia eti "bajeti imekua".. huu ni ujinga wa kiwango cha Phd.!

Ukweli ni kwamba bajeti haijakua ila imezidi kuporomoka. Lets calculate together.

Ni hivi. Mwaka 2005 bajeti ilikua Trilioni 7 na thamani ya dola moja ilikuwa sawa na Sh.650. So ukichukua Trilioni 7 ukigawanya kwa Sh.650/= utapata 10,769,230, yani Dola milioni kumi na laki 7.

Mwaka huu bajeti ni Trilioni 22. Na thamani ya dola ni Sh.2250. Ukichukua Trilioni 22 ukigawanya kwa Sh.2250/= utapata 9,777,777 yani dola milioni 9 na laki 7.

Hii ina maana kuwa bajeti ya mwaka huu (dola milioni 9) ni ndogo kuliko bajeti ya mwaka 2005 (dola milioni 10).

Maana yake ni kwamba kwa miaka 10 yote tumepiga hatua 9 mbele tukarudi nyuma hatua 10. Wanaopenda namba lakini hawajui hesabu hawawezi kunielewa.!

Haiwezekani bajeti ya mwaka 2005 iwe kubwa zaidi kuliko bajeti ya mwaka huu wakati mwaka huu mahitaji mi makubwa zaidi kuliko ya 2005. Watumishi ni wengi zaidi, miradi ya maendeleo ni mingi zaidi na hata population ni kubwa zaidi. So tulitegemea bajeti ya mwaka huu iwe kubwa zaidi. Kubwa maradufu kuliko ya mwaka 2005. Lakini cha ajabu imekua ndogo kuliko ya 2005. Halafu wabunge wa CCM wanaopenda namba bila kujua hesabu wanashangilia eti bajeti imepanda.

Tafsiri hii ya bajeti ina maanisha kuwa kwa miaka 10 ya utawala wa Kikwete tumeshindwa kwenda mbele japo hatua moja. Badala yake tumerudi nyuma kwa hatua moja (10-9).

Kwa lugha rahisi ni kuwa maisha ya leo yamekuwa magumu zaidi (in one decimal place) kulinganisha na maisha ya miaka 10 iliyopita.

Yani mtumishi aliyekuwa analipwa mshahara wa laki 3 mwaka 2005 aliishi maisha mazuri kuliko mtumishi anayelipwa milioni moja leo.

Unajua kwanini? Mwaka 2005 sukari kilo moja ilikua Sh.500. Kwa hiyo kwa mshahara wa laki 3 ulikua una uwezo wa kununua kilo 600 za sukari kwa mwezi. Leo sukari kilo moja ni sh.2200/= kwa hiyo kwa mshahara wa milioni moja unaweza kununua kilo 454 tu za sukari. Hapa tunasema purchasing power ya shilingi imeporomoka mara dufu. Wanapenda namba lakini hawajui hesabu hawawezi kunielewa.!

Mwaka 2005 mfuko mmoja wa cement uliuzwa Sh.4500/= hadi 5000/=. Kwa maana hiyo mtumishi aliyelipwa mshahara wa laki 3 aliweza kununua mifuko 66 ya cement. Leo cement mfuko mmoja ni sh.20,000/= hadi 25,000/=. So mtumishi anayelipwa milioni moja ana uwezo wa kununua mifuko 40 tu ya cement.

Mfumuko wa bei kuanzia mwaka 2005 hadi sasa ni wa kiwango cha asilimia mia nne (400/%). Maana yake ni kwamba bidhaa zimepanda mara 4 ya bei yake just for ten years.

Nyama iliyokua inauzwa kilo moja sh.1000/= sasa hivi inauzwa 4000/= hadi 6000/=. Mchele uliokua ukiuzwa Sh.350/= kwa kilo moja saivi ni 1500/=. Nauli ya daladala iliyokua sh.100 saivi ni 400/=. Mafuta ya taa lita ilikua sh.350/= saivi ni karibia sh.2000/=

Kimsingi kila bidhaa imepanda bei mara 4 au zaidi ya bei yake ya mwaka 2005. Tafsiri yake ni kwamba mfumiko wa bei (inflation rate) ni ya kiwango cha zaidi ya 400% (Hyper Inflation)

Katika uchumi inflation yoyote inayoanzia tripple digit na kuendelea ni "Hyper Inflation". Yani ni mfumuko wa bei wa kiwango kibaya zaidi unaoweza kuathiri uchumi wa nchi kabisa.

Nchi inapaswa kuwa na mfumuko wa bei wa kawaida (moderate inflation) ambao ni single digit. Yani mfumuko ukiwa wa kuanzia asilimia moja (1%) hadi tisa (9%) hiyo ni moderate inflation na haina athari kubwa kiuchumi.

Lakini sisi tuna asalimia 400 za mfumuko wa bei. Hii ni hatari sana. Very soon tutawakaribia Zimbabwe au Somalia kuanza kutembea na hela kwenye matoroli. Hata wao walianza hivihivi.!

Thamani ya shilingi inaporomoka kila siku na watu wanashangilia. Huu ni uzwazwa wa kiwango cha Phd.

Jiulize embe lililokua likiuzwa sh.50 pale sokoni Buguruni leo linauzwa sh.500 hadi 1000. Mara 20 zaidi. So kwa mtindo huu ukitaka kujua bei ya embe miaka 10 ijayo chukua bei ya sasa (sh.1000/=) halafu zidisha mara 20. Utapata Sh.20,000/=.

Kwa hiyo tukipata Rais kama Kikwete miaka 10 ijayo tutanunua embe moja kwa sh.20,000/=.. walahi.! itabidi tuwe na noti ya shilingi laki moja.

Kama embe limepanda bei mara 20 tangu mwaka 2005 hadi 2015, tutegemee lipande tena mara 20 kuanzia 2015 hadi 2025. This means mwaka 2025 bei ya embe itakua elfu 20. Ukitaka kununua embe kumi unaenda na laki mbili. Sasa sijui wale wafanya biashara wa embe wanaonunua kwa fuso watalipa bei gani?

Bila shaka watalipa mabilioni kadhaa kwa fuso moja. Yani unaenda kwa mkulima na fuso lako limejaa hela (noti). Mkulima anapakua hela akimaliza anapakia maembe. Huko ndiko serikali ya CCM inakotaka kutufikisha.

Nisiongee sn maana napata tu hasira bure na huenda hata hamnielewi.
 
Mkuu maelezo yako na mifano uliyotoa ni rahisi mno kueleweka, hata kama kuna mwenye PhD ya ujinga ataelewa tu. Safi sana umetendea haki uzi wako!
 
Kuna watu wanapenda namba lakini hawajui hesabu. Kama na wewe ni mmoja wao tafadhali usisome makala hii.

Wabunge wengi na mawaziri wa chama cha mapinduzi ni wagonjwa wa namba. Wanapenda namba lakini hawajui hesabu. Ukitaka wakushangilie we ongeza tarakimu tu kwenye namba. Wanapenda namba lakini hawajui hesabu.!

Kama ulikua unamlipa mtumishi mshahara wa laki 5 mwaka jana mwaka huu mlipe laki 7. Atashangilia na kukushukuru. Kumbe hajui upande wa pili gharama za maisha zimeifanya hiyo laki 7 iwe sawa na laki moja ya mwaka jana. Yeye atakushukuru tu, kwa sababu anapenda namba lakini hajui hesabu.!

Naona wengi hamjanielewa. Ni hivi kuna faida gani kulipwa mshahara wa milioni mbili halafu ukauziwa sukari kilo moja sh.3000/=??? Si bora ulipwe laki 5 sukari uuziwe sh.500/= kwa kilo. Kama unapenda namba lakini hujui hesabu huwezi kunielewa.

Twende kwenye historia kidogo. Mwaka 2005 wakati Rais Mkapa anaondoka madarakani bajeti ya serikali ilikua Trilioni 7. Mwaka huu ni Trilioni 22. Wanaopenda namba lakini hawajui hesabu wameshaanza kuhangilia eti "bajeti imekua".. huu ni ujinga wa kiwango cha Phd.!

Ukweli ni kwamba bajeti haijakua ila imezidi kuporomoka. Lets calculate together.

Ni hivi. Mwaka 2005 bajeti ilikua Trilioni 7 na thamani ya dola moja ilikuwa sawa na Sh.650. So ukichukua Trilioni 7 ukigawanya kwa Sh.650/= utapata 10,769,230, yani Dola milioni kumi na laki 7.

Mwaka huu bajeti ni Trilioni 22. Na thamani ya dola ni Sh.2250. Ukichukua Trilioni 22 ukigawanya kwa Sh.2250/= utapata 9,777,777 yani dola milioni 9 na laki 7.

Hii ina maana kuwa bajeti ya mwaka huu (dola milioni 9) ni ndogo kuliko bajeti ya mwaka 2005 (dola milioni 10).

Maana yake ni kwamba kwa miaka 10 yote tumepiga hatua 9 mbele tukarudi nyuma hatua 10. Wanaopenda namba lakini hawajui hesabu hawawezi kunielewa.!

Haiwezekani bajeti ya mwaka 2005 iwe kubwa zaidi kuliko bajeti ya mwaka huu wakati mwaka huu mahitaji mi makubwa zaidi kuliko ya 2005. Watumishi ni wengi zaidi, miradi ya maendeleo ni mingi zaidi na hata population ni kubwa zaidi. So tulitegemea bajeti ya mwaka huu iwe kubwa zaidi. Kubwa maradufu kuliko ya mwaka 2005. Lakini cha ajabu imekua ndogo kuliko ya 2005. Halafu wabunge wa CCM wanaopenda namba bila kujua hesabu wanashangilia eti bajeti imepanda.

Tafsiri hii ya bajeti ina maanisha kuwa kwa miaka 10 ya utawala wa Kikwete tumeshindwa kwenda mbele japo hatua moja. Badala yake tumerudi nyuma kwa hatua moja (10-9).

Kwa lugha rahisi ni kuwa maisha ya leo yamekuwa magumu zaidi (in one decimal place) kulinganisha na maisha ya miaka 10 iliyopita.

Yani mtumishi aliyekuwa analipwa mshahara wa laki 3 mwaka 2005 aliishi maisha mazuri kuliko mtumishi anayelipwa milioni moja leo.

Unajua kwanini? Mwaka 2005 sukari kilo moja ilikua Sh.500. Kwa hiyo kwa mshahara wa laki 3 ulikua una uwezo wa kununua kilo 600 za sukari kwa mwezi. Leo sukari kilo moja ni sh.2200/= kwa hiyo kwa mshahara wa milioni moja unaweza kununua kilo 454 tu za sukari. Hapa tunasema purchasing power ya shilingi imeporomoka mara dufu. Wanapenda namba lakini hawajui hesabu hawawezi kunielewa.!

Mwaka 2005 mfuko mmoja wa cement uliuzwa Sh.4500/= hadi 5000/=. Kwa maana hiyo mtumishi aliyelipwa mshahara wa laki 3 aliweza kununua mifuko 66 ya cement. Leo cement mfuko mmoja ni sh.20,000/= hadi 25,000/=. So mtumishi anayelipwa milioni moja ana uwezo wa kununua mifuko 40 tu ya cement.
Mfumuko wa bei kuanzia mwaka 2005 hadi sasa ni wa kiwango cha asilimia mia nne (400/%). Maana yake ni kwamba bidhaa zimepanda mara 4 ya bei yake just for ten years.

Nyama iliyokua inauzwa kilo moja sh.1000/= sasa hivi inauzwa 40000/= hadi 6000/=. Mchele uliokua ukiuzwa Sh.350/= kwa kilo moja saivi ni 1500/=. Nauli ya daladala iliyokua sh.100 saivi ni 400/=. Mafuta ya taa lita ilikua sh.350/= saivi ni karibia sh.2000/=

Kimsingi kila bidhaa imepanda bei mara 4 au zaidi ya bei yake ya mwaka 2005. Tafsiri yake ni kwamba mfumiko wa bei (inflation rate) ni ya kiwango cha zaidi ya 400% (Hyper Inflation)

Katika uchumi inflation yoyote inayoanzia tripple digit na kuendelea ni "Hyper Inflation".
 
Kama ulikuwa unamlipa mtumishi mshahara laki tano mwaka jana mwaka huu mlipe laki 7. Atashangilia na kukushukuru. Naona wengi hamtaelewa ni hivi kuna faida gani mtu kulipwa milioni mbili huku sukar unauziwa 30000? Si bora ulipwe laki 5 sukari uuziwe sh.500 kwa kilo.

KAMA UNAPENDA NAMBA ILA HUJUI HESABU HUWEZI UKANIELEWA.
 
Mkuu hapa unajichanganya mwenyewe haiwezekani mtu asishangilie namba wakati huko dukani tayari hesabu zimeshapanda (kumbuka hata kama wewe ndo mwenye nafasi ya kudhibiti kushuka kwa shilingi au mfumuko wa bei kwanza nitakudai ongezeko la mshahara halafu nakwambia hebu dhibiti kushuka kwa shilingi, ukifanikiwa ndo utakuwa na jukumu la kuendelea kunilipa kwa kiwango kipya au cha zamani kwasababu utakuwa na hoja tayari)
 
Umecopy halafu haujsmalizia kucopy vizuri,na kweli hawatakuelewa
 
Mkuu hapa unajichanganya mwenyewe haiwezekani mtu asishangilie namba wakati huko dukani tayari hesabu zimeshapanda (kumbuka hata kama wewe ndo mwenye nafasi ya kudhibiti kushuka kwa shilingi au mfumuko wa bei kwanza nitakudai ongezeko la mshahara halafu nakwambia hebu dhibiti kushuka kwa shilingi, ukifanikiwa ndo utakuwa na jukumu la kuendelea kunilipa kwa kiwango kipya au cha zamani kwasababu utakuwa na hoja tayari)

mkuu mi nadhan wangetibu tatizo la kuporomoka kwa uchumi kwa sababu miaka kumi ilyopita sukar ni ilikua mia 5 kwa kilo leo ni zaid ya mara nne na hii ni kipind cha miaka kumi,je ?baada ya miaka kumi tena sukr itakua sh. ngpi ?tupo karibu kubeba viroba vyenye makartas ya pesa
 
Fundishaneni kwanza huko Ufipa ili muache kununua magari chakavu kwa bei za kutupwa. Muache kugeuza chama cha siasa kuwa SACCOS ya kukopeshana mihela.

Una akili nzito sana mganga njaa wewe
 
mkuu mi nadhan wangetibu tatizo la kuporomoka kwa uchumi kwa sababu miaka kumi ilyopita sukar ni ilikua mia 5 kwa kilo leo ni zaid ya mara nne na hii ni kipind cha miaka kumi,je ?baada ya miaka kumi tena sukr itakua sh. ngpi ?tupo karibu kubeba viroba vyenye makartas ya pesa
kutokuzalisha + mahitaji ya dollah ni makubwa kwa ajili ya manunuzi ya nje + uchaguzi mkuu (watu wanaficha hela kwa hofu) = mfumuko wa bei & shilingi kukosa thamani
 
sawa! Ila hebu weka na inflation rate kati ya 2005 na2015 ili tuone purchasing power ya mwaka huo na mwaka huu,yaonekana wewe pia ni mpenda namba,unafurahia wingi wa digits bila kujua stabillity yake,kweli tuna mipesa mingi isiyo na thamani!! Unafurahia hilo?

Hoja ya Purchasing power na Inflation ingekuwa na mashiko kama bajeti ya mwaka 2005 ingeendelea kubaki ile ile hadi mwaka huu wa 2015.

Hata hivyo kudouble kwa bajeti kunasaidia kupunguza kwa kiwango kikubwa athari za mambo hayo.

Ifahamike hata dola yenyewe purchasing power yake inabadirika with time

Dola moja ya mwaka 1964 siyo sawa na dola moja ya mwaka 2005

Na dola moja ya mwaka 2005 siyo sawa na dola moja ya mwaka 2015

Mleta mada ametudanganya katika namba zake toka awali na hivyo conclusions zake ni feki
 
umejitahidi kutoa hoja ila kwny bei ya bidhaa umeongeza chumvi sana mfano bei ya saruji 20k-25k sijui ni wapi uko mfano Dar 11400, MBY 13900, Arusha 12600. Pia bei ya bidhaaa mbalimbali pamoja na kiwango cha ubadilishaji sarafu ya mwaka 2005 sidhani km ni sahihi.

Mwisho niungane nawe kusema awamu ya 4 imeprove FAILURE

mkuu, hajazidisha bei, nakumbuka mwaka 2013 kata ya Kisorya wilaya ya Bunda mkoa wa Mara saruji(cement) ilikuwa 21,000/=,sijaulizia hivi karibuni lakini kwa bei ndiyo hali ilivyokuwa.
 
Safi sana Malisa.... siasa zitaliangamiza hili taifa... kila kitu wanakifanyia mzaha!!! Sarafu yetu itaporomoka mpaka basi hatua madhubut zcpochukuliwa
 
Back
Top Bottom