CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu

CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu

Mambumbu yako mengi sana kuliko!
Sasa waziri wa fedha, wabunge hamja wahi kuliongelea hili, inamaana. Hata nyie Kumbe mnapenda namba na kukokotoa hamjui!!!!hongera Rais wetu.
 
Gharama ya kuliendesha Bunge ni kubwa kuliko thamani ya kazi wanayofanya.
 
Nimeipenda sana hii makala, imekaa uchi kwa kila mtu kuelewa na kuona, japo pia ina contradictions chache:- Soma mpaka mwisho ujiongeze kidogo

Wabunge wengi na mawaziri wa chama cha mapinduzi ni wagonjwa wa namba. Wanapenda namba lakini hawajui hesabu. Ukitaka wakushangilie we ongeza tarakimu tu kwenye namba. Wanapenda namba lakini hawajui hesabu.!
Kama ulikua unamlipa mtumishi mshahara wa laki 5 mwaka jana mwaka huu mlipe laki 7. Atashangilia na kukushukuru. Kumbe hajui upande wa pili gharama za maisha zimeifanya hiyo laki 7 iwe sawa na laki moja ya mwaka jana. Yeye atakushukuru tu, kwa sababu anapenda namba lakini hajui hesabu.!Naona wengi hamjanielewa. Ni hivi kuna faida gani kulipwa mshahara wa milioni mbili halafu ukauziwa sukari kilo moja sh.3000/=??? Si bora ulipwe laki 5 sukari uuziwe sh.500/= kwa kilo. Kama unapenda namba lakini hawajui hesabu huwezi kunielewa.

Twende kwenye historia kidogo. Mwaka 2005 wakati Rais Mkapa anaondoka madarakani bajeti ya serikali ilikua Trilioni 7. Mwaka huu ni Trilioni 22. Wanaopenda namba lakini hawajui hesabu wameshaanza kuhangilia eti "bajeti imekua".. huu ni ujinga wa kiwango cha Phd.! Ukweli ni kwamba bajeti haijakua ila imezidi kuporomoka.Lets calculate together.Ni hivi. Mwaka 2005 bajeti ilikua Trilioni 7 na thamani ya dola moja ilikuwa sawa na Sh.650. So ukichukua Trilioni 7 ukigawanya kwa Sh.650/= utapata 10,769,230, yani Dola milioni kumi na laki 7.Mwaka huu bajeti ni Trilioni 22. Na thamani ya dola ni Sh.2250. Ukichukua Trilioni 22 ukigawanya kwa Sh.2250/= utapata 9,777,777 yani dola milioni 9 na laki 7. Hii ina maana kuwa bajeti ya mwaka huu (dola milioni 9) ni ndogo kuliko bajeti ya mwaka 2005 (dola milioni 10).

Maana yake ni kwamba kwa miaka 10 yote tumepiga hatua 9 mbele tukarudi nyuma hatua 10. Wanaopenda namba lakini hawajui hesabu hawawezi kunielewa.! Haiwezekani bajeti ya mwaka 2005 iwe kubwa zaidi kuliko bajeti ya mwaka huu wakati mwaka huu mahitaji mi makubwa zaidi kuliko ya 2005. Watumishi ni wengi zaidi, miradi ya maendeleo ni mingi zaidi na hata population ni kubwa zaidi. So tulitegemea bajeti ya mwaka huu iwe kubwa zaidi. Kubwa maradufu kuliko ya mwaka 2005. Lakini cha ajabu imekua ndogo kuliko ya 2005. Halafu wabunge wa CCM wanaopenda namba bila kujua hesabu wanashangilia eti bajeti imepanda.Tafsiri hii ya bajeti ina maanisha kuwa kwa miaka 10 ya utawala wa Kikwete tumeshindwa kwenda mbele japo hatua moja. Badala yake tumerudi nyuma kwa hatua moja (10-9). Kwa lugha rahisi ni kuwa maisha ya leo yamekuwa magumu zaidi (in one decimal place) kulinganisha na maisha ya miaka 10 iliyopita.

Yani mtumishi aliyekuwa analipwa mshahara wa laki 3 mwaka 2005 aliishi maisha mazuri kuliko mtumishi anayelipwa milioni moja leo. Unajua kwanini? Mwaka 2005 sukari kilo moja ilikua Sh.500. Kwa hiyo kwa mshahara wa laki 3 ulikua una uwezo wa kununua kilo 600 za sukari kwa mwezi. Leo sukari kilo moja ni sh.2200/= kwa hiyo kwa mshahara wa milioni moja unaweza kununua kilo 454 tu za sukari. Hapa tunasema purchasing power ya shilingi imeporomoka mara dufu. Wanapenda namba lakini hawajui hesabu hawawezi kunielewa.!Mwaka 2005 mfuko mmoja wa cement uliuzwa Sh.4500/= hadi 5000/=.
Kwa maana hiyo mtumishi aliyelipwa mshahara wa laki 3 aliweza kununua mifuko 66 ya cement. Leo cement mfuko mmoja ni sh.20,000/= hadi 25,000/=. So mtumishi anayelipwa milioni moja ana uwezo wa kununua mifuko 40 tu ya cement.Mfumuko wa bei kuanzia mwaka 2005 hadi sasa ni wa kiwango cha asilimia mia nne (400/%). Maana yake ni kwamba bidhaa zimepanda mara 4 ya bei yake just for ten years.

Nyama iliyokua inauzwa kilo moja sh.1000/= sasa hivi inauzwa 40000/= hadi 6000/=. Mchele uliokua ukiuzwa Sh.350/= kwa kilo moja saivi ni 1500/=. Nauli ya daladala iliyokua sh.100 saivi ni 400/=. Mafuta ya taa lita ilikua sh.350/= saivi ni karibia sh.2000/=Kimsingi kila bidhaa imepanda bei mara 4 au zaidi ya bei yake ya mwaka 2005. Tafsiri yake ni kwamba mfumiko wa bei (inflation rate) ni ya kiwango cha zaidi ya 400% (Hyper Inflation)Katika uchumi inflation yoyote inayoanzia tripple digit na kuendelea ni "Hyper Inflation". Yani ni mfumuko wa bei wa kiwango kibaya zaidi unaoweza kuathiri uchumi wa nchi kabisa. Nchi inapaswa kuwa na mfumuko wa bei wa kawaida (moderate inflation) ambao ni single digit. Yani mfumuko ukiwa wa kuanzia asilimia moja (1%) hadi tisa (9%) hiyo ni moderate inflation na haina athari kubwa kiuchumi.Lakini sisi tuna asalimia 400 za mfumuko wa bei. Hii ni hatari sana.

Very soon tutawakaribia Zimbabwe au Somalia kuanza kutembea na hela kwenye matoroli. Hata wao walianza hivihivi.!Thamani ya shilingi inaporomoka kila siku na watu wanashangilia. Huu ni uzwazwa wa kiwango cha Phd.
Jiulize embe lililokua likiuzwa sh.50 pale sokoni Buguruni leo linauzwa sh.500 hadi 1000. Mara 20 zaidi. So kwa mtindo huu ukitaka kujua bei ya embe miaka 10 ijayo chukua bei ya sasa (sh.1000/=) halafu zidisha mara 20. Utapata Sh.20,000/=.Kwa hiyo tukipata Rais kama Kikwete miaka 10 ijayo tutanunua embe moja kwa sh.20,000/=.. walahi.! itabidi tuwe na noti ya shilingi laki moja.Kama embe limepanda bei mara 20 tangu mwaka 2005 hadi 2015, tutegemee lipande tena mara 20 kuanzia 2015 hadi 2025. This means mwaka 2025 bei ya embe itakua elfu 20.

Ukitaka kununua embe kumi unaenda na laki mbili. Sasa sijui wale wafanya biashara wa embe wanaonunua kwa fuso watalipa bei gani?Bila shaka watalipa mabilioni kadhaa kwa fuso moja. Yani unaenda kwa mkulima na fuso lako limejaa hela (noti). Mkulima anapakua hela akimaliza anapakia maembe. Huko ndiko serikali ya CCM inakotaka kutufikisha.Nisiongee sana maana napata tu hasira bure na huenda hata hamnielewi. Of course Kuna inflation rate lakin bado hatujafkia kweny hyper inflation bhna yan 400%ujue ni digit 3 tatu iyo mbna tungekua zaid ya Zimbabwe Tz bado tupo kweny digit 2 na si tatu na was na elimu ya uyo jamaa.

Makala hii nimeitoa kwenye blog ya Josephat Lukanza, lakini mwandishi halisi ni Dr. Gideon (Nipashe)

Huyu Dr kaiba hii kazi, mwandishi halisi ni Kamanda Malisa Godlisten...na mpaka sasa atashitakiwa na kutakiwa kulipa kiasi cha Tzs 100M
 
Nilimsifia sana Dr. Gideoni, kumbe kaiba kazi za watu? Pumbavu zake....., mwizi na muongo kama CCM
 
Mwaka wa serikali 2014/15 mshahara ulkuwa 30000sh
Ambao ni sawa na dolla 176 ambapo dola ilkuwa inasimamia 1700sh

Lkn leo utaongezewa itafika 350000 ambao ni sawa na dollar 159 ambapo tumefanya dollar kuwa2200

Je itabakhapo hapo bila kupanda?

Na ss tutaendelea kufurahia ujinga hadi lini?
 
Mushi92

Ni kitendawili kigumu sana kwa wengi. Kuna ambao hata hawaelewi kama shilingi haitamaniki mbele ya dola!

Safari bado ni ndefu sana kufika kule tuendako!!
 
Last edited by a moderator:
Kupanda kwa dola kumevuruga sana uchumi wetu hasa kwenye welfare za vitu...
Na mbaya zaidi hatuna substitute industries za kuzalisha hata hizo basic needs tunazo-import...
 
Hizo hesabu ni wachache watakao kuelewa watanzania wangekuwa waelewa wangelalamikia mfumuko wa bei ushuke na siyo kuomba serikali wawaongezee mshahara
 
Khaa!! Huku kwetu maneromango hatutumii dola kabisa na maisha yanaenda tu :wacko:

pole sana mkuu kutoitumia au ishika dola hakukukwepeshi na garama za ongezeko lake .

ww subilia tuu uone laki yako uliyokuwa unaweza kuitumia wiki 3 nne inavyoisha faster ndani ya wiki 1. nahakuna cha maana ambacho utakuwa umefanyia.
 
Hizo hesabu ni wachache watakao kuelewa watanzania wangekuwa waelewa wangelalamikia mfumuko wa bei ushuke na siyo kuomba serikali wawaongezee mshahara

Kweli kabisa mkuu,mimi nipo huku kijijini yaani maisha yamepanda bei hadi tunahisi kuchanganyikiwa.Lakini cha ajabu mwananchi wa kawaida hajui nini sababu na hata ukimweleza sababu hakuelewi,yeye ni kukifagilia chama tawala,kweli wa-tz bado sana ngoja tukipate cha mtema kuni hadi tutakapo kuwa na akili.
 
Mimi ninawaambia tunakoelekea Shilingi yetu itakuwa sawa na ile ya Uganda au kuwa chini yake,sasa huwa ninashangaa sana wanaposema eti Nchi yetu ipo kwenye orodha ya nchi
Uchumi wake unakua kwa kasi.Siku zote Mungu huwa hamfichi mnafiki,Kushuka kwa thamani ya shilingi yetu na Maisha magumu ya Wa-tz ni kielelezo tosha kuwa Wa-tz tunahadaiwa kwa takwimu feki.
 
J. F. Kennedy"dont ask what your country can do for you, just ask yourself what you can do for your country".
Watanzania tusiwe wajinga kufikiria tukaishia kulalamika bila kuchukua hatua zozote. Kabla mleta post haujaja kujambajamba apa jukwaani jiulize je wewe umechangia nini kwenye uchumi wa nchi yako? Shillingi yetu inashuka kutokana na watu kupenda kununua bidhaa toka nje badala ya kusaidia na kununua bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini ndio maana viwanda vya ndani vinakosa nguvu matokeo yake ndio ayo dollar kupanda zidi ya shillingi yetu na sio hiyo tu tukiendelea kulalamika ushishangae hata hela ya kagame itakuwa juu siku moja kuliko hela yetu
 
J. F. Kennedy"dont ask what your country can do for you, just ask yourself what you can do for your country".
Watanzania tusiwe wajinga kufikiria tukaishia kulalamika bila kuchukua hatua zozote. Kabla mleta post haujaja kujambajamba apa jukwaani jiulize je wewe umechangia nini kwenye uchumi wa nchi yako? Shillingi yetu inashuka kutokana na watu kupenda kununua bidhaa toka nje badala ya kusaidia na kununua bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini ndio maana viwanda vya ndani vinakosa nguvu matokeo yake ndio ayo dollar kupanda zidi ya shillingi yetu na sio hiyo tu tukiendelea kulalamika ushishangae hata hela ya kagame itakuwa juu siku moja kuliko hela yetu

Brain washed. . . . . . .Hebu taja hizo bidhaa unazoita za ndani zinazoweza endesha maisha ya mtanzania wa kawaida bila kununua za nje
 
Back
Top Bottom