CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu

CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu

I say huyu jamaa amefanya uchambuzi sahihi kwa cc wajuzi wa namba
 
Kuna watu wanapenda namba lakini hawajui hesabu. Kama na wewe ni mmoja wao tafadhali usisome makala hii.-

Wabunge wengi na mawaziri wa chama cha mapinduzi ni wagonjwa wa namba. Wanapenda namba lakini hawajui hesabu. Ukitaka wakushangilie we ongeza tarakimu tu kwenye namba. Wanapenda namba lakini hawajui hesabu.!

Kama ulikua unamlipa mtumishi mshahara wa laki 5 mwaka jana mwaka huu mlipe laki 7. Atashangilia na kukushukuru. Kumbe hajui upande wa pili gharama za maisha zimeifanya hiyo laki 7 iwe sawa na laki moja ya mwaka jana. Yeye atakushukuru tu, kwa sababu anapenda namba lakini hajui hesabu.!

Naona wengi hamjanielewa. Ni hivi kuna faida gani kulipwa mshahara wa milioni mbili halafu ukauziwa sukari kilo moja sh.3000/=??? Si bora ulipwe laki 5 sukari uuziwe sh.500/= kwa kilo. Kama unapenda namba lakini hujui hesabu huwezi kunielewa.

Twende kwenye historia kidogo. Mwaka 2005 wakati Rais Mkapa anaondoka madarakani bajeti ya serikali ilikua Trilioni 7. Mwaka huu ni Trilioni 22. Wanaopenda namba lakini hawajui hesabu wameshaanza kuhangilia eti "bajeti imekua".. huu ni ujinga wa kiwango cha Phd.!

Ukweli ni kwamba bajeti haijakua ila imezidi kuporomoka. Lets calculate together.

Ni hivi. Mwaka 2005 bajeti ilikua Trilioni 7 na thamani ya dola moja ilikuwa sawa na Sh.650. So ukichukua Trilioni 7 ukigawanya kwa Sh.650/= utapata 10,769,230, yani Dola milioni kumi na laki 7.

Mwaka huu bajeti ni Trilioni 22. Na thamani ya dola ni Sh.2250. Ukichukua Trilioni 22 ukigawanya kwa Sh.2250/= utapata 9,777,777 yani dola milioni 9 na laki 7.

Hii ina maana kuwa bajeti ya mwaka huu (dola milioni 9) ni ndogo kuliko bajeti ya mwaka 2005 (dola milioni 10).

Maana yake ni kwamba kwa miaka 10 yote tumepiga hatua 9 mbele tukarudi nyuma hatua 10. Wanaopenda namba lakini hawajui hesabu hawawezi kunielewa.!

Haiwezekani bajeti ya mwaka 2005 iwe kubwa zaidi kuliko bajeti ya mwaka huu wakati mwaka huu mahitaji mi makubwa zaidi kuliko ya 2005. Watumishi ni wengi zaidi, miradi ya maendeleo ni mingi zaidi na hata population ni kubwa zaidi. So tulitegemea bajeti ya mwaka huu iwe kubwa zaidi. Kubwa maradufu kuliko ya mwaka 2005. Lakini cha ajabu imekua ndogo kuliko ya 2005. Halafu wabunge wa CCM wanaopenda namba bila kujua hesabu wanashangilia eti bajeti imepanda.

Tafsiri hii ya bajeti ina maanisha kuwa kwa miaka 10 ya utawala wa Kikwete tumeshindwa kwenda mbele japo hatua moja. Badala yake tumerudi nyuma kwa hatua moja (10-9).

Kwa lugha rahisi ni kuwa maisha ya leo yamekuwa magumu zaidi (in one decimal place) kulinganisha na maisha ya miaka 10 iliyopita.

Yani mtumishi aliyekuwa analipwa mshahara wa laki 3 mwaka 2005 aliishi maisha mazuri kuliko mtumishi anayelipwa milioni moja leo.

Unajua kwanini? Mwaka 2005 sukari kilo moja ilikua Sh.500. Kwa hiyo kwa mshahara wa laki 3 ulikua una uwezo wa kununua kilo 600 za sukari kwa mwezi. Leo sukari kilo moja ni sh.2200/= kwa hiyo kwa mshahara wa milioni moja unaweza kununua kilo 454 tu za sukari. Hapa tunasema purchasing power ya shilingi imeporomoka mara dufu. Wanapenda namba lakini hawajui hesabu hawawezi kunielewa.!

Mwaka 2005 mfuko mmoja wa cement uliuzwa Sh.4500/= hadi 5000/=. Kwa maana hiyo mtumishi aliyelipwa mshahara wa laki 3 aliweza kununua mifuko 66 ya cement. Leo cement mfuko mmoja ni sh.20,000/= hadi 25,000/=. So mtumishi anayelipwa milioni moja ana uwezo wa kununua mifuko 40 tu ya cement.-
Mfumuko wa bei kuanzia mwaka 2005 hadi sasa ni wa kiwango cha asilimia mia nne (400/%). Maana yake ni kwamba bidhaa zimepanda mara 4 ya bei yake just for ten years.

Nyama iliyokua inauzwa kilo moja sh.1000/= sasa hivi inauzwa 40000/= hadi 6000/=. Mchele uliokua ukiuzwa Sh.350/= kwa kilo moja saivi ni 1500/=. Nauli ya daladala iliyokua sh.100 saivi ni 400/=. Mafuta ya taa lita ilikua sh.350/= saivi ni karibia sh.2000/=

Kimsingi kila bidhaa imepanda bei mara 4 au zaidi ya bei yake ya mwaka 2005. Tafsiri yake ni kwamba mfumiko wa bei (inflation rate) ni ya kiwango cha zaidi ya 400% (Hyper Inflation)

Katika uchumi inflation yoyote inayoanzia tripple digit na kuendelea ni "Hyper Inflation". Yani ni mfumuko wa bei wa kiwango kibaya zaidi unaoweza kuathiri uchumi wa nchi kabisa.

Nchi inapaswa kuwa na mfumuko wa bei wa kawaida (moderate inflation) ambao ni single digit. Yani mfumuko ukiwa wa kuanzia asilimia moja (1%) hadi tisa (9%) hiyo ni moderate inflation na haina athari kubwa kiuchumi.

Lakini sisi tuna asalimia 400 za mfumuko wa bei. Hii ni hatari sana. Very soon tutawakaribia Zimbabwe au Somalia kuanza kutembea na hela kwenye matoroli. Hata wao walianza hivihivi.!

Thamani ya shilingi inaporomoka kila siku na watu wanashangilia. Huu ni uzwazwa wa kiwango cha Phd.-

Jiulize embe lililokua likiuzwa sh.50 pale sokoni Buguruni leo linauzwa sh.500 hadi 1000. Mara 20 zaidi. So kwa mtindo huu ukitaka kujua bei ya embe miaka 10 ijayo chukua bei ya sasa (sh.1000/=) halafu zidisha mara 20. Utapata Sh.20,000/=.-

Kwa hiyo tukipata Rais kama Kikwete miaka 10 ijayo tutanunua embe moja kwa sh.20,000/=.. walahi.! itabidi tuwe na noti ya shilingi laki moja.

Kama embe limepanda bei mara 20 tangu mwaka 2005 hadi 2015, tutegemee lipande tena mara 20 kuanzia 2015 hadi 2025. This means mwaka 2025 bei ya embe itakua elfu 20. Ukitaka kununua embe kumi unaenda na laki mbili. Sasa sijui wale wafanya biashara wa embe wanaonunua kwa fuso watalipa bei gani?-

Bila shaka watalipa mabilioni kadhaa kwa fuso moja. Yani unaenda kwa mkulima na fuso lako limejaa hela (noti). Mkulima anapakua hela akimaliza anapakia maembe. Huko ndiko serikali ya CCM inakotaka kutufikisha.

Nisiongee sn maana napata tu hasira bure na huenda hata hamnielewi.-
 
Umeanza vibaya ila umemaliza vzur , panic mode ilikua juu Ila imeshuka taratibu , nimekuelewa sana
 
Mimi Mwaka huu Wananchi wa Tanzania wakichagua tena CCM, ctokuwa na mda wa kuyaongelea maovu ya ccm maana wananchi wenyewe watakuwa wameridhika na hali hii na umaskini wao.
Kwangu mimi niliebaatika angalau kupata elimu ya Chuo, nina kazi yangu, watoto wangu na mke wangu wanaweza kupata kiendacho kinywani, naweza kuendesha gari yangu, natibiwa kwa kadi ya bima nk.
Namwambia mwananchi mlala hoi jinsi UKAWA utakavyowasaidia
1. Elimu bure adi vyuo vikuu
2. Bei ya vifaa vya ujenzi kushuka na atimae kila mtanzania kuondokana na nyumba za nyasi na tembe.
3. Matibabu bure kwa wazee
4. Serikali ya majimbo( Itakayoleta chachu ya maendeleo majimboni"county" na cyo kodi zote kujenga Dar na zinazobaki kuliwa.
5.na zingine nyingi.
Kwayo mimi na wezangu wengu humu hamtafaidika sana kama mwananchi
Wa kawaida.
Mfano: kuna watu humu wanaweka kazi zao rehani kuwatetea kazi ambazo wengine unaona tayari wana maisha angalau wana nyumba wanaendesha magari yao,
Lakini bado wananchi wanapinga hawasikii.
Ndugu zangu Inatosha, tujitoe kimasomasonmwaka huu tuwaambie wananchi kama hawatasikia kwa Kupewa kanga na vitisheti!!!!!!
Mtanishangaa kuanzia 2016.
 
Ukiacha changa la exchange rate na kujumuisha kulikopitiliza. Ujumbe wako ni mzuri
 
Hivi wanaoandaa bajeti si wachumi..?
Malisa kwa kweli imenichukua muda kukuelewa na sasa nimekuelewa Jana pale nje ya Hospitali ya BURUHANI Nilimkuta muuza machungwa nikatamani kula nilipomuuliza Bei Akanijibu shilingi 500 chungwa moja.CCM Kwanini hamuoni hali hii kwani ahitawasumbua wasiokuwa wanaCCM BALI KILA Mwanachi ona leo kila Mtanzania anaezaliwa anadaiwa zaidi ya sh 800,000.2025 tutadaiwa kiasi gani?
 
Hoja ya mleta mada imejengwa katika Premises za uwongo na hivyo conclusion yake ni ya uwongo

Exchange rate mwaka 2005 ilikuwa above shilingi 1000 na si shilingi 650 kwa dola.

kwa logic hiyo hiyo ya mleta mada, kama bajeti ilikuwa shilingi Trillion saba mwaka 2005 kwa exchange rate ya shilling 1200 kwa dola moja mwaka huo, basi hiyo ni sawa na jumla ya dollar billion 5.3

kwa mwaka huu ambapo bajeti ni shilling trillion 22 na kwa kwa exchange rate ya shilling 2250 kwa dola moja mwaka huu basi ni sawa na jumla ya dola bilioni 9.78

Sasa ni Jukumu la Wapenda Ukweli kujionea wenyewe dola bilion 5.3 na dola bilioni 9.78 ipi kubwa?

Kiufupi Bajeti almost imedouble in 10 years, na hilo ni jambo la kuipa Kudos Serikali iliyoko Madarakani
 
Kibaya zaidi hawa wachumi wetu wa 'grade A' na 'pass' wamekopa pesa nyingi zaidi ya mara 50 ya mwaka 2005 huku idadi ya watu nayo ikiongezeka zaidi ya 2005.

Tukubali ccm hawaelewi lakini na sisi wananchi ni wajinga zaidi yao unless we prove differently by October 2015!
 
nenda kadanganye wapumbavu wenzako. mwaka 2005 wakati mkapa akiondoka madarakani US dola 1 ilikuwa sawa na Ths 1200.
acha kupotosha watu kuwa dola 1 ilikuwa Tsh. 650. again kadanganye wapumbavu wenzako. sijui umekula maharage ya wapi wewe.
Weye mpuuzi Dolla ilikuwa haijafika elfu moja sote tupo mujini hapa,,,acha kupotoshaa kiushabiki wa kijinga na kitoto huyu bwana kwenye bango awali kasema 950 which very true 110%
 
JLwlrukiJrgAAAABJRU5ErkJggg==

XE.com - USD/TZS Chart
Maelezo yote yamekosa maana kwa sababu msingi wa data ni uongo. Exchange rate ya tarehe 01/06/2005 ione hapo juu ni TSH 1,122/=.Hakuwkuwahi kuwa na exchange rate chini ya 1000 ni karibu mara mbili ya TSH 650 aliyoitumia kukokotoa.

Nasikitika kuwa mleta mada pia anapenda namba lakini hajui hesabu.Data hizi zinapatikana kirahisi sana,kama aliweza kuandika maelezo yote hayo alishindwa vip crosscheck msingi wa hoja yake ambao ni exchange rate?
 
umejitahidi kutoa hoja ila kwny bei ya bidhaa umeongeza chumvi sana mfano bei ya saruji 20k-25k sijui ni wapi uko mfano Dar 11400, MBY 13900, Arusha 12600. Pia bei ya bidhaaa mbalimbali pamoja na kiwango cha ubadilishaji sarafu ya mwaka 2005 sidhani km ni sahihi.

Mwisho niungane nawe kusema awamu ya 4 imeprove FAILURE

Kagera bei ya cement hajakosea, alafu hiyo ndo bei ya serikali hasa kwa wakandarasi, kwenye BOQ
 
Kagera bei ya cement hajakosea, alafu hiyo ndo bei ya serikali hasa kwa wakandarasi, kwenye BOQ

Usichanganye, tunazungumzia bei za wananchi wa kawaida.Achana na hizo zenye 10%.

Bei ya cement Kagera leo hii ni sh ngapi?
 
Malisa amesema 2005 dolla moja ilikuwa sawa na 950 siyo 650.

Naona na wewe pia unapenda namba lakin hujui hesabu.

Ni kweli kaibandika pale ya 950 ambayo nayo ni ya uongo, lakini hajakokotoa kwa 950 bali kakokotoa kwa 650.

Kakokotoa kwa 65p kwa sababu alijua kuwa kama angekokotoa ata kwa 950 basi hoja aliyotaka kuijenga ingepungua nguvu.

Kama unajua hesabu ungeona pale japo kataja 950 lakinu kakokotoa kwa 650.

Ila nimeipenda hii ya watu kupenda namba lakini hawajui hesabu.Nakupongeza kwa hili tu la msemo huu.Sio kwa mengine.
 
Usichanganye, tunazungumzia bei za wananchi wa kawaida.Achana na hizo zenye 10%.

Bei ya cement Kagera leo hii ni sh ngapi?

Bukoba mjini 20,000/- ,ukienda wilayani kama karagwe ni 25,000/-
 
nenda kadanganye wapumbavu wenzako. mwaka 2005 wakati mkapa akiondoka madarakani US dola 1 ilikuwa sawa na Ths 1200.
acha kupotosha watu kuwa dola 1 ilikuwa Tsh. 650. again kadanganye wapumbavu wenzako. sijui umekula maharage ya wapi wewe.

Naona wasiofikiri wamekurupuka na kuanza kumpongeza moja kwa moja.

Ata hawajishughulishi ata walau kugoogle.Ndio maana nina shaka sana na hivi vyama vya upinzani maana vimejaa watu wakurupukaji na wasiojishughulisha kufikiri.
 
Back
Top Bottom