zema21
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 619
- 257
Wakuu, nimekuwa najiuliza sana juu ya hili, Tanzania imekuwa ikizalisha wasomi toka enzi za ukoloni, lakini cha ajabu ni kwamba mpaka leo hii Nchi yetu hii haizalishi chochote, mpaka vijiti vya kuchokonolea meno tunavi import toka uchina. Hivi hawa wasomi wetu wana matatizo gani! Wanafundishwa nin huko vyuoni?
Barabara zetu, majengo makubwa mijini,tafiti mbalimbali utasikia ni kampuni za kigeni zinaongoza watanzania hawana nafasi!? Wazee wetu walitusaidia kuua viwanda nchi nzima.
Sasa mi nashindwa kuelewa japo wazee hao hao wanaishia kulalamika kuwa eti elimu ya sasa haiwasaidii wahitimu kuwa wabunifu wakiwalaumu vijana eti wajiajiri, lakini wazee hao hao hawana lolote manake hawajawahi kufanya ubunifu wowote, hata wale waliofeli form four walikuwawa na uhakika wa ajira, asilimia tisini na na tisa kati yao ni waajiriwa wa serikali.