CCM wamhusisha Karume na Uamsho

CCM wamhusisha Karume na Uamsho

Mheshimiwa Amani karume anataka wazibar wanaotaka serikali tatu nao wasikilizwe. - nakubaliana naye 100%. Hotuba ya Amani karume ya jana ambayo ninaamini iliwakera wanaccm wengi, japokuwa hakukuwa na aliyeweza kukanusha hadharani hotuba hiyo kutokana na ugumu wa mazingira ya siasa za Zanzibar, nitafafanua.

Karume alisema, namnukuu, Kuhusu katiba mpya watanzania wote na wazanzibar pia wasikilizwe na watoe maoni yao hata yale tusiyoyapenda. Akaendelea, kuhusu Muungano wapo wanaotaka serikali mbili - wasikilizwe, wapo wanaotaka muungano wa mkataba wa serikali mbili- wasikilizwe na wapo wanaotaka serikali tatu -- wote wasikilizwe. Aliposema muungano wa mkataba kelele zilianza, aliposema serikali tatu kelele ziliongezeka. Wapiga kelele hawakuwa na ujasiri wa kumzomea lakini walionekana kupiga kelele za kutokubaliana naye - kwa kuwa hawakufanya hivyo kwa wasemaji wengine ni dalili za wazi kwamba aliwakera wengi.

Japokuwa magazeti ya leo hayakuandika kwa upana habari hiyo, hotuba ile imefungua ukurasa mpya kuelekea serikali tatu ambayo ni Sera ya Chadema na CUF - muungano wa serikali mbili sasa ni njia panda.

Kabla ya kufikia hoja hiyo, Amani Karume aliwakubusha wajumbe kuhusu Chama cha ASP, akawaonesha wajumbe kadi yake ya uanachama wa ASP na kuwasomea malengo ya ASP yaliyoko ktk kadi ikiwepo kupigania mustakabali wa wazanzibar. Indirectly, anataka Zanzibar yake.

Ukiunganisha dots ktk hotuba ya Mh Amani karume utagundua kwamba anataka wazanzibar wasikilizwe na kama wanataka serikali tatu nao wasikilizwe. maana yake wakichagua serikali 3 waruhusiwe kama ilivyokuwa kwa serikali ya umoja wa Kitaifa waliyoichagua wenyewe.

Ukiinganisha hotuba ya jana na kitendo chake kusimamia uundaji wa serikali ya umoja wa kitaitaifa akishirikiana na Maalim Seif ili kuwaunganisha wazanzibar - utagundua kuwa Karume anataka Zanzibar huru - kwa maoni yangu at least.

Katika hotuba yake ya Jana, alizungumzia watu kutishana Zanzibar na kuipinga jambo hilo. Na kusema mtu akiwa na maoni tofauti anapewa jina lile ( Hakulitaja ila alimaanisha uamsho). Hii ina maana kwamba Amani karume anawatetea kwa kwa namna isiyo ya moja kwa moja (Indirectly) viongozi wanaotaka muundo tofauti wa Muungano wa sasa (waziri aliyetimuliwa na Shain?). Na ukiunganisha dots hapa anazunguzia kauli kwamba wanaotaka muundo wa serikali ambao hauendani na sera ya ccm wajiondoe ccm- yeye anataka wazanzibar wasikilizwe siyo wanaccm. Na hataki wanaccm kufukuzwa hata kama ni kiongozi kwa kutoa maoni tofauti.
Na kwa maana hiyo, kwa kumsikiliza mantiki ya Amani Karume anawatetea pia wanaUAMSHO ambao ndio wanainijinia muungano wa Mkataba, serikali tatu au kuuvunja kabisa - nao wasikilizwe.

Ifahamike, Uamsho ni kundi la wazanzibar wasiotaka Muungano. Karume kaongea vizuri kabisa kwa niaba yao- kawatetea.
Kwa lugha nyingine, uamsho jana ulitoa hotuba yao ndani ya mkutano mkuu wa CCM wakiwakiliwalishwa na Mwanachama wao - kimtazamo, mkiti mstaafu wa ccm - AMANI KARUME.

Ikumbukwe, CUF wanahusishwa na UAMSHO. Na wakati huo huo injinia wa kuinganisha CUF wanaohusishwa na UAMSHO ni karume huyu huyu aliwatetea UAMSHO jana akitaka wasikilizwe.

Na ikumbukwe pia kuwa , Maalim Seif wa CUF inayohusishwa na Uamsho ambaye ni katibu mkuu wa CUF, alishawahi kupendekeza kwamba Karume wa ccm aliyetetea hoja ya UAMSHO jana aongezewe Muda wa Urais Zanzibar hata baada ya mwaka 2010- karumu na Maalim Seif Hawakufanikiwa.

Nahitimisha kwa kusema, japokuwa Karume alipinga vurugu na uvunjifu wa Amani Zanzibar na kusema kwamba wahalifu washtakiwe, ni wazi kwamba hakubaliani na wazanzibar kulazimishiwa Muungano kwa staili ya sera ya ccm na kutaka wazanzibar wapewe uhuru wao wa kuchagua. Na wakichagua serikali tatu ambayo ni mhogo mchungu kwa ccm na iwe hivyo na wakichagua kuuvunjwa kwa muungano kama wanavyotaka wanauamsho na iwe hivyo.

Na kwa mantiki hiyo, tusitarajie kwamba uamsho utaisha Zanzibar kirahisi na tusitarajie Muungano wa staili ya ccm utaendelea kulazimishwa Zanzibar - Hapana - naktaaa. Uamsho ni mtazamo kuhusu Mustakabali wa Zanzibar kwa macho ya baadhi ya wazanzibar, muafaka kuhusu Muungano kwa mtazamo wao - karume yumo.

Kwa hiyo, hoja ya uamsho ya kubadilisha muundo wa Muungano ingalipo na ndo kwanza inapata wanachama wenye status kubwa - KARUME akiwemo. Hapa tulipofika, njia ya ccm kukwepa at least Serikali tatu ambayo pia ndiyo sera ya Chadema imefika mwisho.
 
Tuhuma hizi zimeenea sana Znz na baadhi ya maeneo ya bara wakisema ni moja ya maagano ya serikali ya umoja wa kitaifa kati ya Karume na maalim Seif ya hatimaye kuvunja muungano. Maalim Seif anasemekana na yeye ni Uamsho.

Uamsho walianza kipindi cha Karume kwa lengo hilo. Agenda kuu ikiwa waache waznz wapumue.
 
Dah, ni hatari. Sasa hapa mambo yameanza kuwa wazi kabisa, wale watu wakubwa waheshimikao nao wamo enh...
 
Sioni Tatizo KArume kuwa UAMSHO!.
by the way nimependa hoja yake..UAMSHO wana haki ya kutoa maoni ,wasivunje tu taratibu.
viva UAMSHO
 
Mkuu nng007
Karume ni uamsho mtupu amemtumia sana shemeji Mansoor Himid kuleta vurugu ndania ya chama; Dr. Shein hakuwa na jinsi na alitumia madaraka yake kumuondoa Himid kwenye uwaziri; tamaa yake ya madaraka imemponza; aling`ang`ania madaraka ya umakamu kwa kuwakingia kifua uamsho; tunamuomba ajondoe kabisa kwenye ajiunge na uamsho rasmi!

Chama
Gongo la mboto DSM

CC
Barubaru Ritz
 
Last edited by a moderator:
Nafikiri baadhi yetu tunasukumwa na matamanio yetu kuliko kujenga hoja,ukiisoma habari hii vizuri na ukilinganisha na hotuba ya karume utagundua kuwa habari hii imeongezewa maneno mengi ambayo karume hakuyasema na nafikiri imefanyika hivyo ili kutii kiu ya mwandishi,ningefurahi sana kama mwandishi angeandika kile ambacho karume alikisema peke yake na wadau watoe mitazamo yao kutokana na hutoba husika.
 
Haya anayofanya yatamgharimu yy na kizazi chake, hata hao Uhamsho wakifanikiwa malengo yao yy na wote wenye asili ya bara watasakamwa waondoke, hatakuwa na amani ataitwa mlowezi.
Hata bara atapitilizwa hadi kwa Joyce Banda,huko ndiko atakoendeleza UAMUSHO
 
Dah, kumbe uamsho ni CCM hao hao??
No wonder na Ponda anaweza kuwa na mkono wa mtu

Hizi nguvu wanazipata wapi??
Kama ni kweli Shame on Karume!
 
Hilo halina ubishi kuna post yangu nililigusia hilo...stay soon mtabaini ukweli.
 
This guy thinks outside the box, uwezo wa hali ya juu ambao wana CCM wengi hawana, kama angalikuwa rais kipind kile cha Dr Salmin Amoor,yumkini mauaji yale ya January 27 yasingalitokea, hawa uamsho mnaowapigia kelele sasa hivi ipo siku mtawatafuta mkae nao meza moja kwa mazungumzo kama vile mlivyompuuzia sharif hamad na mkawa mnamwibia kura kila uchaguz, uvumilivu ulipomshinda na kuanzisha vuguvugu lisiloisha mlimtafuta na kumpa cheo...
Viongozi visionary wapenda mageuzi yanayoendana na wakati always hupewa majina ya ajabu afrika, Muungano haubebeki, ipo siku utavunjika kwa gharama kubwa, heri hawa jamaa wa UAMSHO wasikilizwe mapema na suluhu ipatikane.
 
napenda kutofautiana na wengi juu ya mada hii,na mojakwa moja niungane na rais mstaafu Dr.Aman Karume,kuwa alichoomaanisha ni kila mtu kupata fursa ya kutoa maoni yake kwa tume ya mabadiriko ya katiba mpya,muungano hauna hati miliki kwa wenye mawazo ya serikali mbili tu,akitokea mtu wa msimamo tofauti huitwa uamsho au anayetetea watu wote watoe mawazo yao binafsi kama alivyofanya karume hubambikwa na wana ccm kuwa mtetezi wa uamsho,hizi jamani ni fikra mgando kwa wana ccm,wenzangu.alichosema karume ni sahihi na watu wengine wote mashuhuri kama yeye waseme hivyo waziwazi bila chembe ya unafiki ndani yake.
 
Kila mtu anahaki yakutoa maoni yake na kusikilizwa kikatiba, si busara kuzomea hapo unamnyima uhuru mtu kusikilizwa na unavunja haki yake kikatiba.:A S angry:
 
nyongeza ni kwamba karume anatakiwa akumbukwe katika historia ya siasa za zanzibar maana ndiye aliyebuni namna ya kuifanya zanzibar ikalike kwa maana ya amani na usalama,kaukutana na maalimu seif Hamad kuunda serikali ya umoja wa kitaifa(SUK)na sasa zanzibar imetulia na hii ndio faida ya kiongozi kuwa mbunifu,japo kuna baadhi ya viongozi wenzake wapenda sfa hasa watokao bara kuwa ndio waliofanikisha mtengamano huo.karume anastahili tuzo kubwa kwa hili.
yaani the honoural doctarate for conflict resolution &Arbitration.
 
About 75 percent of zanzibaris THEY ARE SEEMED dont like uion.why kiwete and his army colaborate with few zanzibaris oppresing and giving bad name all people who dare to say "WE A TAYAD BAI THIS UNION"there fore,all togeza we have to say,no union.
 
Hapa naona watu wanachuki tu na wengine wanafik. Karume ni kiongozi anaependwa na wazanzibari hana haja ya kuoendwa na wanafik wana CCM!
Akina mkapa na wenzake imewauma sana kuona Karume analeta mseto zanzibar, na bado, karibuni CCM zanzibar itapata aibu!
Kila anaeterea zanzibar huitwa uamsho, tushazoea hayo! Kwaiyo nyie watanzania BARA kaeni mpige majungu yeye yake yana muendea, ungekua unajua maisha yake yanavomiendea ungejua hasa kama hana time na CCM zaidi ya kuwapotezea mda, amekwisha wasaliti zamani wanafik, amezinduka mapemaaaaa!!

Karume oyeeee!! Ameleta maendeleo zanzibar ndicho kinachowauma maadui wa zanzibar kama Mkapa na wenzake!
 
Change is inevitable,unavoidable kabisa! Progressives will prevail. Zanzibar shall not die.
 
[h=1]
karume.jpg
[/h] RAIS Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mh Aman Karume


Na Julius Magodi na Habel Chidawali, Dodoma
Posted Jumatano,Novemba14 2012 saa 21:31 PMKwa ufupi
Dalili za Rais Karume kuzomewa zilianza baada ya baadhi ya wajumbe kutoka Mkoa wa Mjini Magharibi kuanza kutaja neno ‘Uamsho’ kila alipokuwa akizungumzia matatizo yaliyopo Zanzibar.




RAIS Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Aman Karume juzi usiku alizomewa na baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku wakimwita kwamba ni mmoja wa wanakundi la Uamsho.

Uamsho ni kundi ambalo katika siku za hivi karibuni limekuwa likihusishwa na vurugu ambazo zimekuwa zikitokea Tanzania Visiwani, ambazo zimesababisha watu kadhaa kukamatwa na kufikishwa mahakamani.

Rais Karume alikutana na zahama hiyo wakati akitoa hotuba ya kuwaaga wanaCCM baada ya kumaliza ngwe yake ya utumishi ndani ya chama hicho akiwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.

Dalili za Rais Karume kuzomewa zilianza baada ya baadhi ya wajumbe kutoka Mkoa wa Mjini Magharibi kuanza kutaja neno ‘Uamsho’ kila alipokuwa akizungumzia matatizo yaliyopo Zanzibar.

Hali ilikuwa mbaya zaidi pale alipokuwa akizungumzia vurugu za kidini ambazo ziliikumba Zanzibar hivi karibuni zikiongozwa na kikundi cha Uamsho.

Karume alisema kuwa kikundi cha Uamsho kina haki ya kutoa maoni yake kuhusu muungano, lakini hakipaswi kufanya vurugu kama ambavyo kimekuwa kikifanya.

Wakati akiendelea kuzungumzia suala hilo, kelele nyingi zilienea katoka kwa wajumbe wa mikoa ya Zanzibar ambao walikuwa wakipaza sauti, “ Uamsho huyo….Uamsho huyo… Uamsho huyo….”

Hali hiyo ilimfanya wakati mwingine kukatiza hotuba yake na kulazimisha kuwatuliza watu hao kwa kusema “CCM oyeee….CCM…..oyeee…Mapinduziii….”
Hata hivyo, baada ya kelele hizo kuendelea Karume alionekana kuhamaki na kuwaambia wajumbe hao kwamba amechoka kusikia akiitwa jina hilo la Uamsho.

“Nimechoka kusikia naitwa jina hilo ati,” alisema Karume na kuongeza:
“Hivi wengine wana vichwa vya samaki kwa nini mnapiga kelele wakati mimi ninapozungumza, si mniache nizungumze mambo ambayo ni muhimu zaidi kwa masilahi ya chama chetu.”

Hata hivyo, licha ya kutafuta namna ya kuwatuliza wanachama hao kwa maneno mengi na historia ya maisha yake tangu alipojiunga na Chama cha ASP mwaka 1970, bado hakukuwa na utulivu na safari hii kelele zilianza kwa pande zote za wajumbe.

Kwa upande wa wajumbe wa Bara, baadhi yao walikuwa wakipiga kelele za kumtaka kumaliza hotuba yake ambayo walisema ilishachukua muda mrefu huku wakisema hakuna cha ajabu alichokuwa akizungumza.

Mara baada ya kumaliza hotuba yake, Karume alihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Redio Deutche Welle ya Ujerumani, na alisisitiza kuwa Uamsho wana haki ya kutoa maoni yao kuhusu muungano, lakini hawaruhusiwi kuvunja sheria.

Aliwataka wanachama wa kikundi hicho kujenga hoja, kwani alisema wengine wana hoja za msingi, lakini wasitumie vitisho.

Karume alistaafu uongozi wa CCM katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti (Tanzania Visiwani) na nafasi yake ilichukuliwa na Rais wa sasa wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein.

Tofauti na utamaduni ambao CCM kimeujenga kwa viongozi wake wakuu, Karume aliendelea kuwa makamu mwenyekiti hata baada ya kustaafu urais wa Zanzibar, hivyo kumlazimisha Dk Shein kusubiri hadi juzi kuchukua nafasi hiyo.

Kwa kawaida, viongozi wa ngazi ya Rais wa Muungano na Zanzibar, baada ya kuondoka katika nafasi zao za uongozi wa nchi, pia huachia madaraka ndani ya chama na kumwachia Rais mpya.

Chanzo Mwananchi
 
Back
Top Bottom