CCM Wameishika CHADEMA PABAYA...

Wapendwa wana JF, nimesikia mara nyinyi CHADEMA wakihusishwa na Udini, Ukanda, Dhuluma na sasa Ufisadi. Inaniumiza sana, maana nina imani sana na CDM, lakini kama hizo hoja ni za kweli……....mmmmm.
Jana nilikuwa na mkongwe wa siasa na mwanazuoni maarufu sana hapa Tanzania, katika zungumza yake alisema na ninamnukuu "CHADEMA is a gang of criminals, am just deeply sorry for Dr. Slaa, Zitto Kabwe and my great comrade Prof. Baregu……You know, CDM is not a political party rather…..a group of frustrated and disparate individuals under the umbrella of politics….". Ukweli niliumia sana kimoyomoyo na nikaamua kutoka mahala pale. Kwa hiyo nimeona ni vema nijaribu kujua zaidi juu ya CDM.
Kwa yeyote mwenye takwimu au ufahamu naomba anisaidie kujua yafuatayo:
1. Uwiano wa waislamu kwa wakristo miongoni mwa wabunge wa CDM
2. Uwiano wa waislamu kwa wakristo miongoni mwa wajumbe wa Halmashauri Kuu na Sekretariat ya CDM
3. Kati ya wabunge wote wa CDM ni wabunge wangapi wa CDM wanatoka Kanda ya Kaskazini hususani mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara+ na Singida?
4. Je ni kweli Mh. Mbowe kawauzia CDM magari 3 yaliyotumika kwa TSh 480,000,000?
5. Kama ni kweli, ni magari mangapi, aina gani (kama ni Fuso truck, je ni 4ton au 10ton) na ya mwaka gani?
6. CHADEMA ati wamewadhulumu watu wengi waliojitoa kupiga kampeni kwa matarajiyo ya kurudishiwa japo kidogo walichotumia, hii ni kweli? Mfano ni yule M/kiti wa CDM aliyekimbilia CCM majuzi...na wengine wengi wanalalamika....
1.Hoja ya Uislamu na ukristo ilishajibiwa mara nyingi hapa jamvini. Hata hivyo kama wananchi wamempigia kura mbunge wa CDM sio kwa sababu ya ukristo au uislamu wake ni kwa sababu ya kukubalika kwake. Labda tuzungumzie viti maalum.
Hata hivyo wabunge wa Majimboni baadhi yao ni kama wafuatao
Mnyika (Ubungo-Mkristo), Zitto (Kigoma-Muislamu), Ndesamburo (Moshi-Mkristo), Selasini (Rombo-Mkristo), Lema (Arusha-Mkristo), Said Arfi (Mpanda- Muislamu), Mustaafa Akunaay (Mbulu-Muislamu) n.k.
Upande wa viti maalum ambako ndiko kunakoweza kuzua maswali angalia hapa: Mhonga said (Kigoma-Muislamu), Paulina Gekul (Manyara- Mkristo), Chiku Abwao (Iringa-Muislam), Sabrina Sungura (Kigoma-Muislamu),Raya Ibrahimu Khamis (Pemba- Muislamu), Mariam Salum Msabaha (Unguja-Muislam), Rose Kamili -Manyara (Muislamu), Leticia Nyerere -Mwanza (Mkristo), Lucy Owenya, Grace Kiwelu Kilimanjaro (Mkristo), Conjesta Rwamlaza -Kagera (Mkristo). Christowaja Mtinda- Singida (Mkristo) na Esther Matiko Mara ( Mkristo) kwa kuwa taja wachahce tu kati ya wabunge 23 wa Majimbo na 25 wa viti Maalum. Sijui tatizo hapa liko wapi?
2. Hivi Singida nayo ipo kaskazini? Huu ugonjwa kuwachukia kaskazini tuwaachie CCM waliosema Lowassa na Sumaye hawatakuwa Maraisi wa Tanzania kwa kuwa ni zamu ya watu wa Pwani

3. Kwenye Katiba hakuna Halmashauri Kuu kama CCM ila kuna Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu. Wajumbe wengi katika vyombo hivyo huingia kwa nafasi zao au kwa kuchaguliwa. Mfano Wenyeviti wote wa wilaya wa CDM ni wajumbe wa Baraza Kuu. Wenyeviti na makatibu wa Majimbo ni wajumbe wa Mkutano Mkuu akiwemo huyu anayeandika hapa. Mwenyekiti, Katibu mkuu, Makamu wenyeviti na Manaibu Katibu (Bara Na visiwani), Wenyeviti wa Mabazara na Wajumbe wa kuchaguliwa pamoja na wachache wa kuteuliwa huunda Kamati Kuu. Sijui huyo Mwanazuoni wako anaijua katiba ya CDM au ndio Dr Bana?

4. Hoja ya magari fuatilia tamko la la Kamati Kuu na Baraza Kuu na majibu ya marando na Komu kwa Nape Nnauye. Si busara kurudia rudia kitu hichohicho.

5.CDM sio CCM kwamba wakati wa uchaguzi ndio wa kunnemeka na kukwapua. Kama kuna mtu alipoteza mali zake kwa ajili ya CDM (mimi nikiwemo) hakuna sababu ya kulaumu CDM bali mfumo uliopo unaotulazimisha tupiganie nchi mara ya pili. Sisi wengine huwa inafika muda familia zetu zinakosa hata chai lakini hatuwezi kulalamika.

6. Sekretariet nenda kwenye website ya CDM utaona kila kitu. Mwmabie na huyo mwanazuoni asiwe mvivu wa kusoma awe mdadisi sio kuleta uzushi mitaani huku akijua kuwa kuna watu kama wewe wanaohitaji kupewa facts na sio jungu.
7. Mwisho lakni kwa Uzito Mpe ujumbe huyo Mwanazuoni kama ni Dokta au profesa, ni afadhali asingesoma kuliko kusoma na kuwa na fikra mgando kama hizo. Akuambie nini maana ya Politicala party kama CDM sio kimojawapo. Amshauri na JK kuwa hicho kikundi cha msimu kitamng'oa sipokuwa makini.
Ujumbe : AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZA KWAKO (JK)
 
Mie nilikuwepo bunda wote waliochukuwa kadi za ccm ni wana ccm tayari nawajuwa. Huyo mzee si alikuwa mwenyekiti wa kitongoji kupitia ccm kipindi fulani hivi, na kama kweli mwandishi ulikuwepo weka picha acha unafiki na story za kutunga.

Ndiyo mie niko bunda hapa ukanda wa benki kule kwenye mkutano walikuwepo wazee tu, na hata kama waliorudisha kadi ni idadi unayotaja wewe, kwenye mkutano watu wengi saizi hiyo hawakuwepo labda mkutano mzima walikuwa wanrudisha kadi acha uongo.

Pia mie ni mwana ccm acha kutuharibia chama hivi kama chama hakina mvuto kwa sasa why mseme uongo na kesho story kama hii utaikuta gazeti la mzalendo, uhuru na habari leo huo ni ujinga na upuuzi ndiyo maana hamuuzi, mwambie Nape , huyo mukama wako na chiligati waende chuo chochote tanzania ambapo kuna vijana wasomi hata mwalimu nyerere university kigamboni uone kama hawajazomewa achani ujinga na unafiki chama kwa sasa hakikubaliki lazima tubadilike, hao wazee wanaotudanganya kuwa chama kipo they will be dying soon.

"Nape mtetezi wa CCM na mwanzilishi wa CCJ"

Kwa UNAFIKI NA UONGO HUU unataka kutudhihirishia kuwa unaogopa kusema ukweli kuwa sio mwana ccm au?
 
2011429113945309140_20.jpg
 
Kama ccm inaweza kuwakusanya watu na kuwalipa ili waende kwenye mikutano yao, itashindwaje kuwalipa wa 230 ili wawape kadi zao? CDM hatutishwi na propaganda za ccm kwenye gazeti la uhuru! Tunatishwa na maisha magumu yanayowakumba watz kwa sababu ccm na serikali yake imeshindwa kupanga mikakati ya kutekeleza sera yake ya MAISHA BORA KWA KILA MTZ
 
Ni makundi hayo hayo mawili yenye red pamoja na la watoto ambalo hapa mtunzi wa riwaya hii hakupenda kuwataja kwa sababu za kimaudhui, ambayo mara zote yamekua yaking'ara katika tunzi za CCM hasa zile zinazochapishwa na shirika la uchapishaji la UHURU. It's no coincidence kwamba hata kwenye vita wanaoathirika sana ni akina mama, wazee na watoto. (no offence):A S 39:
Monday, 16 May 2011

* Akomba wanachama wake 239
* Chiligati: Mamluki CCM kudhibitiwa

Na Ghati Msamba, Bunda
Gazeti la Uhuru

Wanachama hao wapya wa CCM wamesema wameridhishwa na kasi ya maendeleo na utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kuondoa kero za wananchi. Mukama akiwa katika siku ya kwanza ya ziara wilayani Bunda, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kata ya Kibara, wananchi hao walitangaza kujiengua CHADEMA na kujiunga na CCM. Katika mkutano huo, Mukama alisema CCM ndicho Chama pekee kinachoweza kusimamia rasilimali na kubadilisha maisha ya wananchi. Aliwaasa Watanzania kutokubali kurubuniwa na kuwasikiliza watu wanaopotosha ukweli kuhusu dhana ya CCM kujivua gamba kwa kuwatosa watuhumiwa wa ufisadi.

Katibu Mkuu alisema CCM ni taasisi kubwa, hivyo haiwezi kufa kirahisi kama wanavyoota wapinzani, hususan CHADEMA kwa kuwa ina viongozi wenye maadili ya uongozi. “Miaka 34 ya CCM ni mingi, hivyo ni lazima viongozi wabadilike na ndiyo dhana ya kujivua gamba ili kuleta mageuzi, kwani kwa kufanya hivyo ni kuonyesha ukomavu na umakini,” alisema.

Alitumia fursa hiyo kuwataka wakuu wa wilaya mkoani Mara kusimamia kikamilifu fedha za miradi ya maendeleo ya wananchi zinazotengwa na serikali kwa halmashauri.

Katika mkutano huo, wazee wa Bunda wakiwakilishwa na Raphael Gurinja, walimuomba Mukama kurudi wilayani humo ili kusafisha siasa chafu na sumu iliyoenezwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa. Alisema Dk. Slaa amekuwa akieneza siasa chafu zenye mwelekeo wa kuvuruga amani nchini, hivyo kumuomba Mukama amfundishe siasa.

“Dk. Slaa anaeneza chuki wakati wenzake wanamwaga sera, sasa inabidi afundishwe jinsi ya kuhubiri sera na si siasa chafu,” alisema Gurinja. Akikabidhi kadi kwa wanachama wapya, Mukama alisema wamechukua uamuzi sahihi kurejea CCM, kwani vyama vya upinzani havina sera. “Nawapongeza kwa uamuzi wa kujiunga na CCM. Kitendo hiki kimewaziba midomo wale wanaodai eti Chama hiki kinakufa, karibuni nyumbani,” alisema.

Mukama pia alikabidhi kadi kwa wanachama wapya 175 wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na kuwataka kuimarisha jumuia hiyo kikamilifu.

Katibu Mkuu Mukama yuko katika ziara ya siku nane mkoani Mara, ambapo pamoja na mambo mengine atahimiza uhai wa Chama. Mamluki CCM kudhibitiwa CCM imesema itahifadhi majina na kumbukumbu za wanachama wake nchini kwa kutumia mfumo wa kompyuta.

Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mageuzi ndani ya Chama, ambapo imewaagiza makatibu kukusanya kumbukumbu kutoka kwenye matawi na kuzipeleka makao makuu ya CCM, mjini Dodoma, ambako zitahifadhiwa. Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Chiligati, alisema hayo wakati akihitimisha ziara ya wajumbe wa sekretarieti mpya ya CCM.

Alisema utaratibu huo unatakiwa kukamilika kabla ya uchaguzi mkuu wa CCM na jumuia zake utakaofanyika mwakani. Chiligati ametoa miezi mitatu kwa makatibu kuwa wamewasilisha kumbukumbu na majina ya wanachama makao makuu kwenye Kitengo cha Oganaizesheni kinachosimamia uratibu wa masuala ya uchaguzi, uhai wa Chama na jumuia zake.

Alisema makatibu watapeleka wanachama hai kwa kulipa ada na wale ambao hawajalipa watatakiwa kutuma makao makuu kila yanapotokea mabadiliko, yakiwemo ya wanachama wapya, wanaoacha uanachama au kufariki dunia. Chiligati alisema utaratibu huo unalenga kukomesha uwepo wa wanachama mamluki na wa msimu wa uchaguzi, ambao hawana faida kwa uhai wa Chama.

Ziara ya wajumbe wa sekretarieti ya CCM iliyofanyika kwa siku sita katika maeneo mbalimbali mkoani Singida, iliwahusisha Chiligati, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Mwingulu Nchemba na Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Asha Juma Abdallah.
 
Pambaf kabisa!!
Huyu mwandishi amepewa rushwa msh***********nnzi mkubwa.
Wewe utuambie wanachama 239 wamejiunga CCM toka CHADEMA bila ya kutuwekea picha zao kweeli inaingia akilini???Maana kama kuna 239 wametoka CHADEMA kuingia CCM basi mkutano huo ulikuwa umefurika kweli kweli. Weka picha za ukweli na zisiwe za kuchakachua kama mlivokuwa mnachomekea mwaka jana kwenye Kampeni. Yaani picha ya watu 20 unaiungaunga ionekana ni watu wengi!!!

Wewe huoni mikutano ya CDM inaambatana na idadi ya watu waliofurika kwenye mikutano??
 
tatizo sisi hatuangalii logic habari imeanza na mwandishi kusema wamekomba watu mia mbili na usee na dheni akaendelea kusema maombi ya watu wa bunda na kumalizia na jumuia ya wanawake kuchukua kadi.ukiangalia kwa makini hakuna palipoandikwa mchanganua wa watu kurudisha kadi au mchanganua wa ni nani kutoka wapi ndiye aliyerudisha,hii habari imekaa kisiasa zaidi na kishabiki kwanza ameandikwa na uhuru gazeti ambolo halinunuliwi
 
Yaani nimeishiwa na nguvu baada ya kusoma ujinga huo. Hivi niwaulize CCM ni nani katika nchi hii hawajui ninyi kuwa mmeishiwa sera, na hamna cha kusema kwa sasa. Nani ambaye hajui kuwa maisha kwa sasa yamebana kwa sababu ya sera na ujinga wa ccm wa kugawa mali asili za nchi kwa mabwana zao? Hatudanganyiki katu na uongo wenu na magazeti yenu ya kijinga hayo. Hata habali za wazi mnachakachua...! kweli mmezidi. Hivi nani? nchi hii asiemjua DR.Slaa na CHADEMA kwa umakini wake toka akiwa Bungeni akitetea wanyonge wa nchi hii. 279 hao ni wanachama wa CCM wanajifurahisha tu. Mtu mwenye akili hawezi kufanya ujinga wa kuchukua kadi za kifisadi.
 
Mie nilikuwepo bunda wote waliochukuwa kadi za ccm ni wana ccm tayari nawajuwa. Huyo mzee si alikuwa mwenyekiti wa kitongoji kupitia ccm kipindi fulani hivi, na kama kweli mwandishi ulikuwepo weka picha acha unafiki na story za kutunga.

Ndiyo mie niko bunda hapa ukanda wa benki kule kwenye mkutano walikuwepo wazee tu, na hata kama waliorudisha kadi ni idadi unayotaja wewe, kwenye mkutano watu wengi saizi hiyo hawakuwepo labda mkutano mzima walikuwa wanrudisha kadi acha uongo.

Pia mie ni mwana ccm acha kutuharibia chama hivi kama chama hakina mvuto kwa sasa why mseme uongo na kesho story kama hii utaikuta gazeti la mzalendo, uhuru na habari leo huo ni ujinga na upuuzi ndiyo maana hamuuzi, mwambie Nape , huyo mukama wako na chiligati waende chuo chochote tanzania ambapo kuna vijana wasomi hata mwalimu nyerere university kigamboni uone kama hawajazomewa achani ujinga na unafiki chama kwa sasa hakikubaliki lazima tubadilike, hao wazee wanaotudanganya kuwa chama kipo they will be dying soon.

"Nape mtetezi wa CCM na mwanzilishi wa CCJ"

Umesema vyema .Nilitaka kushangaa sana kwamba Mukama apate watu wa Bunda kiasi hicho . Je Mkama anajua kuongea ? Unajua walidhani kwa kumweka Mukama basi Mara itaunga mkono CCM bado wana kazi kubwa mno ngojea uone muda unasogea kutafuta mgombea Urais utajua mengi.
 
Jitengenezee utamaduni wa kuifikiri.
Dini za watu na makabila yao si kigezo cha kuchagua viongozi.(Kama unafikiri ni vigezo basi we ndio mdini na mkabila).
Kama umeambiwa jambo na mtu jaribu na wewe kumhoji,kama ni vema kujua idadi ya waislamu na wakristo chadema je kwa vyama vingine?
 
Source gazeti la uhuru.Mnatoa nakala ngapi kwa siku?coverage yenu ya mauzo ikoje?

Tumeshawazoea wasanii, ninyi any way watu wa leo hawaambiwi tazama.

Josephine,

I like your response.
The situation on the ground is not a fairy tale, is it? It is funny the way Chama cha mapinduzi fellows attack those who tell them the truth in black and white

I think some people should be careful about what they wish for. JK and CCM is not a "a good leader or political institution" . In reality , and looking at the big picture , JK and his Blind followers are a very important members of the majority in leadership i.e Mukama is the voice of the selfish and self-serving majority who have gotten us where we are today. These people are hellbent on self-preservation at any cost perhaps to include the disintegration of Tanzania . We saw how a very wicked cabal , with an evil spokesman in Nape and Mukama, recently held Tanzania hostage through imparting tribalism and religion ideology without considerations for our unity as a Nation.

Many actions, has proven beyond doubt that they are only capable of providing the type of weak , unprincipled , indecisive, profligate, insensitive and "more of the same" leadership that will hasten Tanzania's demise.

Those who think CCM can achieve anything are simply ignorant of the situation on the ground in Tanzania
 
Wewe ninani mpaka hata uwesemee. Acha wajitetee wenyewe. Hawa watu wanautajiri wa kupindukia wewe hapa kula yako ni shida ila tu unaendeshwa na hisia kuwatetea. I gess you are crazy. Nani alijua kuwa Rostam anatuibia miaka nenda miaka rudi? Nani alikuwa anajua kwa akina patele & Co wanatuibia? Nani alijua hata Rais wetu mstaafu anatuibia (pamoja na kujiita Mr claen). What about Manji? Chenge Je?
Mimi naungana na hawa wanaosema kuwa ni mafisadi akina Mbowe et al. Juzi ni nimeona thread haka ikieleza jinsi Mbowe alivyochomekea dili la Mil 180 kwa ajili ya kofia, fulata etc kule China baada ya yule mze sabodo kutoa Mil 100.
Huo usafi wa mbowe ni upi?
What abou slaa (na mamilioni ya chadema as salary huku akiwa amesahau alichokuwa akihubiri bungeni)
Na zito (hummer mil 200 katika ubunge wa miaka 5), Na Ndesa..... malizia mwenyewe kwani iko wazi.
Kuna uwezekano hata rais aliyepo madarakani akawa balaa, ngoja muda wake uishe, we will see.
Hebu waTZ tuache ushabiki wakijinga.
 
1.Hoja ya Uislamu na ukristo ilishajibiwa mara nyingi hapa jamvini. Hata hivyo kama wananchi wamempigia kura mbunge wa CDM sio kwa sababu ya ukristo au uislamu wake ni kwa sababu ya kukubalika kwake. Labda tuzungumzie viti maalum.
Hata hivyo wabunge wa Majimboni baadhi yao ni kama wafuatao
Mnyika (Ubungo-Mkristo), Zitto (Kigoma-Muislamu), Ndesamburo (Moshi-Mkristo), Selasini (Rombo-Mkristo), Lema (Arusha-Mkristo), Said Arfi (Mpanda- Muislamu), Mustaafa Akunaay (Mbulu-Muislamu) n.k.
Upande wa viti maalum ambako ndiko kunakoweza kuzua maswali angalia hapa: Mhonga said (Kigoma-Muislamu), Paulina Gekul (Manyara- Mkristo), Chiku Abwao (Iringa-Muislam), Sabrina Sungura (Kigoma-Muislamu),Raya Ibrahimu Khamis (Pemba- Muislamu), Mariam Salum Msabaha (Unguja-Muislam), Rose Kamili -Manyara (Muislamu), Leticia Nyerere -Mwanza (Mkristo), Lucy Owenya, Grace Kiwelu Kilimanjaro (Mkristo), Conjesta Rwamlaza -Kagera (Mkristo). Christowaja Mtinda- Singida (Mkristo) na Esther Matiko Mara ( Mkristo) kwa kuwa taja wachahce tu kati ya wabunge 23 wa Majimbo na 25 wa viti Maalum. Sijui tatizo hapa liko wapi?
2. Hivi Singida nayo ipo kaskazini? Huu ugonjwa kuwachukia kaskazini tuwaachie CCM waliosema Lowassa na Sumaye hawatakuwa Maraisi wa Tanzania kwa kuwa ni zamu ya watu wa Pwani

3. Kwenye Katiba hakuna Halmashauri Kuu kama CCM ila kuna Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu. Wajumbe wengi katika vyombo hivyo huingia kwa nafasi zao au kwa kuchaguliwa. Mfano Wenyeviti wote wa wilaya wa CDM ni wajumbe wa Baraza Kuu. Wenyeviti na makatibu wa Majimbo ni wajumbe wa Mkutano Mkuu akiwemo huyu anayeandika hapa. Mwenyekiti, Katibu mkuu, Makamu wenyeviti na Manaibu Katibu (Bara Na visiwani), Wenyeviti wa Mabazara na Wajumbe wa kuchaguliwa pamoja na wachache wa kuteuliwa huunda Kamati Kuu. Sijui huyo Mwanazuoni wako anaijua katiba ya CDM au ndio Dr Bana?

4. Hoja ya magari fuatilia tamko la la Kamati Kuu na Baraza Kuu na majibu ya marando na Komu kwa Nape Nnauye. Si busara kurudia rudia kitu hichohicho.

5.CDM sio CCM kwamba wakati wa uchaguzi ndio wa kunnemeka na kukwapua. Kama kuna mtu alipoteza mali zake kwa ajili ya CDM (mimi nikiwemo) hakuna sababu ya kulaumu CDM bali mfumo uliopo unaotulazimisha tupiganie nchi mara ya pili. Sisi wengine huwa inafika muda familia zetu zinakosa hata chai lakini hatuwezi kulalamika.

6. Sekretariet nenda kwenye website ya CDM utaona kila kitu. Mwmabie na huyo mwanazuoni asiwe mvivu wa kusoma awe mdadisi sio kuleta uzushi mitaani huku akijua kuwa kuna watu kama wewe wanaohitaji kupewa facts na sio jungu.
7. Mwisho lakni kwa Uzito Mpe ujumbe huyo Mwanazuoni kama ni Dokta au profesa, ni afadhali asingesoma kuliko kusoma na kuwa na fikra mgando kama hizo. Akuambie nini maana ya Politicala party kama CDM sio kimojawapo. Amshauri na JK kuwa hicho kikundi cha msimu kitamng'oa sipokuwa makini.
Ujumbe : AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZA KWAKO (JK)
Naona unajitahidi mpaka kuongezea majina ili kujustify. Suala linabaki palepale kuwa chadema kina udini, haijalishi hayo uliyoainisha hapo juu. You need to change, Period. Otherwise you are finnished. Siunajua wale wale watu wa vibarakashea. Huwa hawarubuniwi ovyoovyo. shauri yako kana kutayazingatia haya.
 
Soma hili andiko la mh. lwaitama

Mimi nadhani ndugu zangu wanahabari tunasaidia kupindisha hoja juu ya dhana ya ufisadi...Kuwa na mshahara mkubwa au kuwa na kipato kikubwa ulichopata kwa makubaliano na waajiri wako au kwa juhudi zako halali au za ndugu zako si ufisadi...Kutembelea gari la kifahari ulilopewa au kuazimwa au kununua kwa kipato halali chako au ndugu yako... ilo pekee alikufanyanyi mtu kuwa fisadi...Ufisadi, kwa maana yenye mashiko kisiasa, ni kushiriki kwenye vitendo vya kupata kipato cha siri kama malipo kwa kutumia cheo chako serikalini au katika chama tawala kufanikisha malengo yakujitajirisha kinyume cha sheria ya mtu au kakundi ka watu..Sasa ndugu yangu Nape kusema eti Dr. Slaa naye ni fisadi maana yake ni nini kimantiki? Kama Dr. Slaa ni fisadi basi kwa vile tu Chadema wamempa mshahara mkubwa kwa cheo chake cha ukatibu wa chama taifa ( ambayo si sawa na kuwa mbunge wa jimbo moja!!!!) sasa CCM wanajivua gamba kwa nini yalabi? Kama hiyo ndiyo dhana ya ufisadi ya ndugu yangu Nape basi haina maana kusambabisha uwezekano wa mifarakano ndani ya CCM kwa kutaka mafisadi wake wajiuzuru....Wanyime tu mishahara mikubwa!!!!!Eti?!!!..

Maana sasa kumbe ufisadi ni kupokea milioni 7 au hata 10 kwa kazi ya chama chako cha kisiasa kitaifa eti vile uliwai kusema wabunge wajimbo moja la watu wasiozidi milioni moja wasipate mshahara "mkubwa" wa milioni 7????!!! Hii inamantiki kweli??!!! Kashfa ya EPA, rada, Richmond...makashfa yenye harufu ya rushwa kubwa kubwa ya watu wenye madaraka makubwa makubwa serikalini, sasa yanalinganishwa na eti Dr. Slaa kulipwa mshahara wa milioni 7 au hata 10 kwa kazi ya ukatibu wa chama kitaifa chenye Wabunge na Madiwani na wafuasi kibao nchi nzima????!!!...Kweli kabisa hiyo ndiyo dhana ya ufisadi ya ndugu yangu Nape???

Huyu ndiye Nape anayetaka mimi na wewe tumwamini kuwa anakisaidia chama cha wakulima na wafanyakazi cha CCM kijivue gamba??? Gamba la nini kama si matajiri wanaoajiri mamia ya wafanyakazi na hivyo ni wanyonyaji lakini wameteka chama cha wakulima na wafanyakazi badal ya kuanzisha chama chao cha liberal democratic union au republican??? Gamba la nini kama si wafanya biashara wakubwa wakubwa wenye kutuhumiwa ufisadi kama ule wa EPA, Richmondi na Rada??? ...Kumbe ndugu yangu Nape tafsiri yake ya ufisadi ni kule kuwa na mshara wa milioni 7 au hata 10...Ina maana Maximo aliye kuwa kocha wa TFF na Gavana wa Benki Kuu ni fisadi vile waanapokea/walipokea mshahara mkubwa tulio wapangia sie? Kweli ndugu huyu Nape anataka tumwamini kuwa ni mpambanaji dhidi ya ufisadi? Kwa nini tusiamini kuwa lengo la uteuzi wake ni kupotosha umma juu ya dhana mzima ya ufisadi ili baadaye kusiwepo hata mmoja hatayeondoka CCM kwa kutajwa kuwa fisadi??? Yaani ufisadi ndani ya CCM utaondoka kwa kuzunguka nchi nzima tukishutumu ufisadi wa Dr. Slaa wa Chadema??!!!Maana sasa CCM itakachoitaji kufanya ni kuchapisha nakala za malipo ya mishahara ya wote wanaotuhumiwa kuwa mafisadi, eti? Hapo kweli sasa mafisadi watabaki akina Dr. Slaa na Gavana wa Benki Kuu, na Mkurugenzi Mkuu wa TRA, siyo?Tuache utani bwana!!!!Nape? Unatukatisha tamaa sisi CCM wafu!!! Tulidhani kumekucha kumbe bado giza totoro?!!
Wakatabahu,
Mwalimu Lwaitama
 
Naona unajitahidi mpaka kuongezea majina ili kujustify. Suala linabaki palepale kuwa chadema kina udini, haijalishi hayo uliyoainisha hapo juu. You need to change, Period. Otherwise you are finnished. Siunajua wale wale watu wa vibarakashea. Huwa hawarubuniwi ovyoovyo. shauri yako kana kutayazingatia haya.
Tatizo liko wapi? Hapo kwa Rose Kamili ni nimekosea sawa, huyo Chikiu ana tatizo gani
 
Wapendwa wana JF, nimesikia mara nyinyi CHADEMA wakihusishwa na Udini, Ukanda, Dhuluma na sasa Ufisadi. Inaniumiza sana, maana nina imani sana na CDM, lakini kama hizo hoja ni za kweli……....mmmmm.
Jana nilikuwa na mkongwe wa siasa na mwanazuoni maarufu sana hapa Tanzania, katika zungumza yake alisema na ninamnukuu "CHADEMA is a gang of criminals, am just deeply sorry for Dr. Slaa, Zitto Kabwe and my great comrade Prof. Baregu……You know, CDM is not a political party rather…..a group of frustrated and desparate individuals under the umbrella of politics….". Ukweli niliumia sana kimoyomoyo na nikaamua kutoka mahala pale. Kwa hiyo nimeona ni vema nijaribu kujua zaidi juu ya CDM.
Kwa yeyote mwenye takwimu au ufahamu naomba anisaidie kujua yafuatayo:
1. Uwiano wa waislamu kwa wakristo miongoni mwa wabunge wa CDM
2. Uwiano wa waislamu kwa wakristo miongoni mwa wajumbe wa Halmashauri Kuu na Sekretariat ya CDM
3. Kati ya wabunge wote wa CDM ni wabunge wangapi wa CDM wanatoka Kanda ya Kaskazini hususani mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara+ na Singida?
4. Je ni kweli Mh. Mbowe kawauzia CDM magari 3 yaliyotumika kwa TSh 480,000,000?
5. Kama ni kweli, ni magari mangapi, aina gani (kama ni Fuso truck, je ni 4ton au 10ton) na ya mwaka gani?
6. CHADEMA ati wamewadhulumu watu wengi waliojitoa kupiga kampeni kwa matarajiyo ya kurudishiwa japo kidogo walichotumia, hii ni kweli? Mfano ni yule M/kiti wa CDM - Mbeya Mjini aliyekimbilia CCM majuzi...na wengine wengi wanalalamika....

Hii ni topic ya kipumbavu kwa siku ya leo! I dont see any point here to discuss
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom