CCM wameanza kuisoma namba kabla ya UKAWA

CCM wameanza kuisoma namba kabla ya UKAWA

Haaa haaa wadau bado wanagonga mvinyo kwenye mahekalu ya duniani uko wanatunga sheria waje vipi,nashauri mzee wangu aanze pole pole abakie na pumzi maana naona vita itakua ndefu na ngumu hawa wenye Tz yao wanajulikana kwa counter attack.
 
na bado yule mwizi mkubwa aliyerejeshewa fedha za EPA na wezi wenzake na pia kuhifadhi majina ya wauza unga, lazima aje atoe maelezo ya kutosha kuhusu wizi na utapeli wake kwa taifa la tanzania. pia wale vibaka wenzake aliowateua mpaka siku ya mwisho ya kukaa ofisini, wataondolewa kwenye nyadhifa zao. huwezi kumteulia mtu mizigo huku ukijua siku zako za uongozi zinakaribia ukingoni!

mkuu mimi kwamakufuli na ccm sion jipiya kwa sababu najua hii ni amri ya wakubwa zake kina mkapa na jk. kaambiwa afanye kidogo kuwaridhisha wananch mutulize hasira maana washajua kimenuka hawapendwi.na pia ili waendelee kuficha madudu yao yale makubwa.kama maccm humu ndani yanabisha hili.tusubiri kama atagusa yale matatizo yetu makubwa.mutakumbuka tunayo mikataba lukuki inayotuingizia hasara kila kubwa kila siku.mfano gass na petroli madin makaa ya mawe na nk akiweza kuigusa hii ikawa na maslahi kwetu hapo ndipo muniambie anafanya kazi nitakubali lakin hii ya kubana matumiz huku akiachia wazungu kuendelea kushindilia matumbo yao na kukuza uchumi wa nch zao huku wakijilimbikizia akiba ya kizazi chao kijacho kupitia raslimali zetu huku sisi tukibanwa matumbo yetu kwa kodi hapana hamujanishawishi kumkubali huyu jamaa
 
Nikupe angalizo tu...Rais ni watu wote na sio wa chama.Na sidhan kama yupo kwa hilo lengo unalolisema hapo juu..Epuka sana uchochezi,kila mtu atawajibika kwa nafasi yake kama ni Mtumishi wa serikali hii haijalishi ana itikadi ipi.ila usitamke kitu ambacho hujakisikia kutoka kwake coz kinaweza kukuletea madhara.kumbuka kuna watu wana Tabia ya kucopy vitu huku na kuanza kuvisambaza
Hujasikia kama bodi ya hospitali ya Muhimbili imevunjwa?
 
Hujasikia kama bodi ya hospitali ya Muhimbili imevunjwa?

Najua ndio bt nimekuwa worried na statement kuwa kaambiwa bandari kuna UKAWA n.k...ujue mtu anaweza kushikilia kitu kidogo kikamuweka mtu matatani..ni mtazamo wangu tu mkuu
 
Safari za nje zimesitishwa watoto na ndugu za wanufaika ambao ni wana CCM wanalia,

Rweyemamu ameambiwa afungashe virago ikulu atakuwa anaiona ikulu kwenye TV ameanza kuisoma,

Ruge tenda za matamasha ya ikulu zimeyeyuka alikuwa anaingia ikulu kama choo cha stand sasa ameanza kuisoma,

Posho za wabunge nje ya vikao zimefyekwa wataisoma,

Reshuffle la maDC linakuja...humo mwote hakuna UKAWA hata mmoja wataisoma,

Hadi sasa wanaCCM ndio walioanza kulia hata kabla ya UKAWA.

Waliokuwa wanadhani ni UKAWA pekee wataisoma namba walikuwa wanaota,

Magufuli bado anaendelea kufagia nyumba yake mliozoea kula vya kunyonga sasa mtaisoma, hakuna cha vimemo na bado.

Mkuu Quinine umefanya haraka kumkubali huyu jamaa, tunahitaji kumtathmini kama anamwelekeo wa kuirudisha Tanzania tunayoitaka............
 
magufuli aliomba urais ili awatumikie watanzania wala sio ccm wala ukawa ndio maana hata mimi ingawa sio ccm nilimpigia kura tatizo lenu nyinyi ukawa mbowe anawadanganya sana kuwa amefungua kesi lowasa atakuwa rais inabidi utambue kuwa ulikosea kushabikia ukawa na mafisadi
 
Safari za nje zimesitishwa watoto na ndugu za wanufaika ambao ni wana CCM wanalia,

Rweyemamu ameambiwa afungashe virago ikulu atakuwa anaiona ikulu kwenye TV ameanza kuisoma,

Ruge tenda za matamasha ya ikulu zimeyeyuka alikuwa anaingia ikulu kama choo cha stand sasa ameanza kuisoma,

Posho za wabunge nje ya vikao zimefyekwa wataisoma,

Reshuffle la maDC linakuja...humo mwote hakuna UKAWA hata mmoja wataisoma,

Hadi sasa wanaCCM ndio walioanza kulia hata kabla ya UKAWA.

Waliokuwa wanadhani ni UKAWA pekee wataisoma namba walikuwa wanaota,

Magufuli bado anaendelea kufagia nyumba yake mliozoea kula vya kunyonga sasa mtaisoma, hakuna cha vimemo na bado.

Kwanini watumishi wa umma unawaita ccm?
Nadhani kati ya watu mil 8 waliomchagua Magufuli hawazidi 20% ambao ni watumishi wa umma, lkn miongoni !mwa watumishi hao, si zaidi ya 2% walikuwa wananufaika na ikulu!
Lakini swali kwako bwana quinine, hivi ulitaka ukawa waingie ili upate manufaa binafsi, kwa njia ya upendeleo?
 
hapo hakuna chochote,wanasubiri mheshimiwa pombe amalize honeymoon yake ya urais ili na yeye aanze kuisoma namba mtu mmoja hawezi kupambana na system iliyomuweka tunadanganyana tu,ccm ni ileile,mawaziri ni walewale,mwanasheri mkuu wa serikali ni yuleyule kilaza.nothing new

amka na fanya kazi acha kubishana na ukweli uliza wizara alizofanya kazi kila mwenye akili timamu ana appreciate sasa wewe endelea kujidanganya #HapaKaziTu
 
Kwanini watumishi wa umma unawaita ccm?
Nadhani kati ya watu mil 8 waliomchagua Magufuli hawazidi 20% ambao ni watumishi wa umma, lkn miongoni !mwa watumishi hao, si zaidi ya 2% walikuwa wananufaika na ikulu!
Lakini swali kwako bwana quinine, hivi ulitaka ukawa waingie ili upate manufaa binafsi, kwa njia ya upendeleo?
Hakuna sehemu niliyosema UKAWA wakiingia nitanufaika ni CCM hao hao walikuwa wakitamba Magufuli akiingia UKAWA wataisoma namba kinyume wao ndio wamekuwa wa kwanza kuisoma.
 
Watanyooka tu. Sema naogopa ya kolimba. Chama cha ki lucifer sana kile
 
Kwa Magufuli lazima wote turudi kwenye square one, watoto wa Masaki waliokuwa wanakesha mitandaoni kukejeli watu lazima joto limeanza kuwafikia.

RAIS WA AWAMU YA TANO AVUNJA REKODI. AMEUSHANGAZA ULIMWANGU KWA KUENDESHA KIKAO NA MAKATIBU WAKUU WA WIZARA ZOTE KWA GARAMA YA T.SH. 20000.

KAMANDA JPM AMESEMA HAKUNA HAJA YA KUTUMIA MILIONI MIA TATU KWA KIKAO KIMOJA KAMA ILIVYOKUWA IMEZOELEKA. AIDHA AMEONGEZA KWA KUSEMA VIKAO NI SEHEMU YA MAJUKUMU YAO YA KILA SIKU HIVYO HAKUNA SABABU YA KUWALIPA POSHO WALA KUTUMIA GARAMA ZISIZO NA ULAZIMA.

MH. JPM AMEONGEZA KWAKUSEMA NI MARUFUKU KUTUMIA GARAMA KUBWA KWENYE VIKAO VYA MAOFISINI. KIKAO HICHO KILIKUWA NA MAJI KILIMANJARO DAZANI TATU KILA DAZANI NI TSH. 4500 JUMLA NI 13500. NA KARANGA ZA TSH. 6500.

Watanyooka tu awamu hii.
 
Safari za nje zimesitishwa watoto na ndugu za wanufaika ambao ni wana CCM wanalia,

Rweyemamu ameambiwa afungashe virago ikulu atakuwa anaiona ikulu kwenye TV ameanza kuisoma,

Ruge tenda za matamasha ya ikulu zimeyeyuka alikuwa anaingia ikulu kama choo cha stand sasa ameanza kuisoma,

Posho za wabunge nje ya vikao zimefyekwa wataisoma,

Reshuffle la maDC linakuja...humo mwote hakuna UKAWA hata mmoja wataisoma,

Hadi sasa wanaCCM ndio walioanza kulia hata kabla ya UKAWA.

Waliokuwa wanadhani ni UKAWA pekee wataisoma namba walikuwa wanaota,

Magufuli bado anaendelea kufagia nyumba yake mliozoea kula vya kunyonga sasa mtaisoma, hakuna cha vimemo na bado.
Pia angejitahidi kujenga sehemu ya kufia viongozi pale muhimbili ili kupunguza gharama za viongozi kwenda kufia India. Tuna poteza mabilioni ya shilingi kwa kulipia gharama za safari za watu kwenda kufia India wakati watanzania masikini wanafia kwenye vi zahanati na Hospitali chafu. Waingizwe madaktari bingwa wachache na tuwe na vifaa na vipimo bora vya kutolea huduma zote za matibabu kuanzia kwa Rais hadi watu wa chini. Huduma zote zifanyike hapa hapa nchini.
 
Kwanini watumishi wa umma unawaita ccm?
Nadhani kati ya watu mil 8 waliomchagua Magufuli hawazidi 20% ambao ni watumishi wa umma, lkn miongoni !mwa watumishi hao, si zaidi ya 2% walikuwa wananufaika na ikulu!
Lakini swali kwako bwana quinine, hivi ulitaka ukawa waingie ili upate manufaa binafsi, kwa njia ya upendeleo?
Hahaaa . mkuu unataka kuhalalisha kwamba Magufuli kachaguliwa kweli na watu milioni 8 au unaleta jokes? Jana nasikia kaenda Muhimbili. Leo mwambieni aende pale Kigamboni kuna Jahazi la kwenda Bagamoyo kwa wakwere linatusumbua kuwaka wakati lilinunuliwa kwa zaidi ya bilion 8. Akawashughulikie waliyo fanya manunuzi ili tujue hii # Hapa kazi TU ina maana ya kweli.
 
Akitoka hapo anaenda kwa waliochukua chao mapema,ranchi na ng'ombe wetu watarudishwa,mashamba(nyika)huko Mvomero,nayo yapo mbioni kurudishwa kwa wananchi,tenda za car park jijini Dar nazo karibu zitaota mbaya,matajiri ''wauza juice'' muda wa kulipakodi ili tupate elimu bure sasa umefika,ndoto za kumiliki vitalu vya gesi kwa ubweche ndio hizoo zimeyeyuka,hakika huu ni mtego wa panya wanaingia waliokuwemo na wasio kuwemo,Tinga mbaya,teh teh,Tinga mbaya wewe teh teh.

Mimi bado nipo napiga nyimbo za sifa kwa Mungu maana kwa hakika hakuna fisadi aliyekanyaga jumba letu takatifu na Tanzania njema ni lazima.......

Glory honor and majesty belongs to you my living and mighty God kwa hakika wewe ni mtakatifu!
 
Watanyooka tu. Sema naogopa ya kolimba. Chama cha ki lucifer sana kile

God is still in His throne usiogope, anaulinzi wa Mungu usio na mashaka kwani anaitenda kazi ya Mungu ya kuwatetea wanyonge!
 
hapo hakuna chochote,wanasubiri mheshimiwa pombe amalize honeymoon yake ya urais ili na yeye aanze kuisoma namba mtu mmoja hawezi kupambana na system iliyomuweka tunadanganyana tu,ccm ni ileile,mawaziri ni walewale,mwanasheri mkuu wa serikali ni yuleyule kilaza.nothing new

Sahihisho....system tena ya CCM haikumweka Magufuli....acha waisome tu na magari yao yaendayo kasi kama vipi watumie kufugia kuku
 
Kwanini watumishi wa umma unawaita ccm?
Nadhani kati ya watu mil 8 waliomchagua Magufuli hawazidi 20% ambao ni watumishi wa umma, lkn miongoni !mwa watumishi hao, si zaidi ya 2% walikuwa wananufaika na ikulu!
Lakini swali kwako bwana quinine, hivi ulitaka ukawa waingie ili upate manufaa binafsi, kwa njia ya upendeleo?

Yale anayofanya Magufuli ndo vyama vya upinzani walikuwa wanataka wafanye , na ccm hawakutaka kabisa kutoa nafasi kwa upinzani kwa kuogopa kubanwa.

Sasa mh. Magufuli ana tembea kama ccm lakini anatenda kama Ukawa. Ndiyo maana bw. Quinine anasema ccm wamekuwa wa kwanza kuisoma namba.
 
Wenye akili tulimuona Magufuli hayuko upande wao,

Wizara 8 kufyekwa wana CCM wengi ndio wanaolia, nasikia Hosea wa Takukuru naye nje ni wana CCM tu wanaolia, kilio cha vigogo ni kicheko kwa walala hoi.
 
Yale anayofanya Magufuli ndo vyama vya upinzani walikuwa wanataka wafanye , na ccm hawakutaka kabisa kutoa nafasi kwa upinzani kwa kuogopa kubanwa.

Sasa mh. Magufuli ana tembea kama ccm lakini anatenda kama Ukawa. Ndiyo maana bw. Quinine anasema ccm wamekuwa wa kwanza kuisoma namba.

Nakwakusema hivi inaonyesha UKAWA mmemkubali Dr.Magufuli
 
Back
Top Bottom