Uchaguzi 2020 Kura za maoni CCM-Rorya huenda ukawa ni wa ukabila/utarafa dhidi ya rushwa

OBWERE

Member
Jan 14, 2011
46
8
*KURA ZA MAONI CCM-RORYA: HUENDA UKAWA NI WA UKABILA/UTARAFA DHIDI YA RUSHWA*

na Mwl. Chacha Matete
Idara ya Elimu ya Ufundi - MUST

Moja ya ahadi za mwana TANU ambazo mwana CCM anapaswa azifahamu ni ahadi namba nne (5) inayosema *rushwa ni adui wa haki, sitopokea wala kutoa rushwa*. Hii ahadi imenikumbusha ilee CCM ya Mwl JK Nyerere ambayo Mhe JPM amejitahidi sana kuirudisha. Sasa hivi hali ya rushwa kidogo inaridhisha tofauti na miaka mitano iliopita, angalau watu wanaogopa kupokea au kutoa rushwa.

Tofauti na utaratibu wa zamani wa kumpata mgombea wa ubunge au udiwani ndani ya CCM ambao wanachama wote kuanzia ngazi ya shina walipiga kura za maoni, sasa hivi ni viongozi wa kuanzia ngazi ya tawi na kata ndiyo watahusika. Mabadiliko yaliofanywa na CCM yamelenga kupunguza kama sio kuondoa mianya ya rushwa iliokuwa imeota mizizi na kuwapunguzia gharama watia nia, hii imewapa fursa hata wasio na kipato kikubwa kutia nia maana inakuhitaji kuwa na nauli yako, hela ya kulipia fomu na kwa hiari yako pesa ya kuchangia chama shughuli za uchaguzi/maendeleo

Vijana wengi wameitikia wito wa mwenyekiti wa CCM kitaifa na kusisitizwa na mkuu wa mkoa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka ya kuwataka vijana kugombea badala ya kuwa wapambe na wapiga debe wa wagombea.

Jimbo la Rorya ni miongoni mwa majimbo yatakayoingia kwenye kinyang'anyiro hicho. Niliwahi kuandika kwenye makala yangu kuwa kuna tatizo kubwa sana la utarafa uliobeba sura ya ukabila na rushw a. Tarafa ya Suba na Nyancha zinazokaliwa zaidi na jamii zenye nasaba na kabila la wakurya wameunda umoja wao ujulikanayo kama suba 1&2, huku wenzao wa Girango na Luo-imbo wakiunda kile kinachoitwa G6 (Japo Luo-imbo kwa uchache wao wanajificha wasionekane kuwa ndani ya G6), nimepokea simu nyingi sana za wana Rorya wengi wakikubaliana nami na wengine wakikataa kutokuwepo ukabila kuibuka wakati huu. Yupo mchangiaji mmoja alinivutia kidogo hoja yake, yeye alinieleza kuwa *umoja wa tarafa ya Suba na Nyancha ni mbinu ya kutaka huruma (sympathy) tu ili na wao wapewe nafasi ya kuongoza jimbo la Rorya kwa kuwa hawana uwezo na fedha kuongoza*. Kwa kweli kama mwana Rorya kwa uzawa, kukulia na kusomea nikaingiwa na wasiwasi mkubwa sana, nikapata mawazo haya:

*A* Mpiga simu alishindwa kunithibitishia kuwa makundi haya hayapo na hakuna mpasuko huo. Naomba wanarorya wenzangu waelewe haya makundi yapo na kuna makundi sogozi yameundwa na yanajiita Suba 1&2, na lile la G6 na yanaratibu shughuli za uchaguzi nyuma ya pazia

*B*. Nimepatwa na wasiwasi na kauli yake ya kutokuwa na uwezo wa kuongoza na fedha wa watu kutoka tarafa ya Nyancha na suba, nikaona kuna mpasuko mwingine wa ubaguzi wa kuwaona wengine hawana uwezo na hivyo kuhitaji huruma tu wa
wengine kuongoza.

*C*. Mpiga simu ameshindwa kukanusha kuwa huenda kukaibuka hali ya rushwa kubwa kwenye kura za maoni kwa wale wanaojiita G6 dhidi ya Suba 1&2 ambao wanachukuliwa kutokuwa na uwezo kifedha.

Huenda wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya/jimbo wakasahau ile ahadi namba 4 ya mwana TANU ambayo mwana CCM anatakiwa aijue na kuifuata inayoongelea rushwa kama adui wa haki. Nitaeleza:

*A* Wajumbe wa mkutano mkuu wilaya watakaopiga kura wanakadiriwa kufika *900+*. Hii itawajumuisha
1. Mwenyekiti wa tawi
2. Katibu wa tawi
3. Katibu Mwenezi wa tawi
4. Mjumbe wa mkutano mkuu ngazi ya wilaya
- kutoka ngazi ya kata watakaopiga kura ni:
1. Mwenyekiti wa CCM kata
2. Katibu wa CCM kata
3. Katibu mwenezi kata
4. Mjumbe wa mkutano mkuu
- ukiongeza na wawakilishi wa makundi ya UVCCM, CWT, nk kwa kila kata inakadiriwa kuwa na wapiga kura *34* ukizidisha Mara kata *26* utapata wajumbe *884+*

Tarafa ya Nyancha na Suba watakuwa na wajumbe wengi *(554+)* kuliko Girango na Luoimbo *(340+)* ni kweli bila kificho wajumbe wengi kutoka tarafa ya Nyancha na Suba wanahitaji sana mbunge kutoka kwenye maeneo yao baada kuonekana kutengwa sana kimaendeleo kwa kipindi kirefu lakini ilivyoelezwa na yule mpiga simu hawana uwezo kifedha na hawawezi kushindana na G6 wenye uwezo kifedha, mbinu pekee iliobaki ni kuungana kwa itikadi ya utarafa/ukabila.Hii ni mbinu chafu na haikubaliki lakini kwa mtizamo wa wengi hawana jinsi bali ni kuungana tu dhidi ya wale wanaosemekana kuwa ni watesi wao (G6)

*B*. Kura za maoni zinaweza kuingiliwa sana na rushwa kuliko nyakati zote kuwahi kutokea kwa sababu:

1. Iwapo wajumbe wa mkutano mkuu kutoka suba 1&2 wataungana mbinu pekee iliobaki kuwasambaratisha ni kwa njia ya rushwa. Kwa njia yoyote kama atapitishwa mtia nia kutoka SUBA 1&2 dhidi ya wa G6 mbinu pekee ni kuwamaliza ni rushwa kwani kweli wamefanywa tegemezi kuomba rushwa *GONYA*

2. Tayari mhe mbunge anayemaliza muda wake ameshajinasibu kuwa yeye kiwango chake cha kutoa rushwa ni Tsh 100,000 kwa kila mjumbe ambayo itamuhitaji kuwa na kiasi cha *Tsh 88,400,000+* kuwaonga wajumbe wote.
Akiongea na wana CCM wa kata ya Nyamagaro, Mhe.LOA aliwajibu wale waliomtuhumu kuwa ameanza kuwaonga wajumbe wa kata za Nyamagaro, Nyamtinga na Kyangasaga kiasi cha Tsh 5000 kwa kila mjumbe.Mhe alisema yeye kutoa kiwango hicho cha sh 5000 ni kuwadhalilisha wajumbe kwani ni kiasi kidogo mnooo!!!!
- Hii inadhihirisha kuwa Mhe huyu akipitishwa na CC kuwa miongoni mwa wale tatu bora basi atategemea zaidi kuwaonga wajumbe. Kwa kiongozi mwenye ueledi na anaijua vyema ile ahadi No. 4 ya mwana CCM hakukuwa na haja ya kujibu tuhuma zilizoandikwa mitandaoni tu na pengine hazina ushahidi wowote.
*C*. Kuna dalili kuwa ilikugawana kura za Nyancha na Suba wadadisi wa siasa wa jimbo la Rorya wanasema inawezekana kupangwa kwa watia nia ambao hawana nia ya kugombea bali *kumpamba, kumsifia na kumpigia debe* wakati wa kuomba kura kwa wajumbe badala ya kujiombea kura. Hii imewahi kutokea kwenye uchaguzi wa 2010 na 2015 ambapo mtia nia mmoja ambaye kazi yake kubwa ilikuwa ni kumpamba na kumsifia LOA ambaye alikuwa mpinzani wake na kumuombea kura badala ya kujiombea. Kibaya zaidi mtia nia huyo alikuwa akipangiwa ratiba ya kuongea aidha kabla au baada ya LOA kuongea. Haikuhitaji kuwa na elimu kubwa kiwango cha PhD kugundua hili kuwa mtia nia huyo alipangwa na pengine alilipwa kuharibu kura za wengine hasa za Nyancha na Suba, hii inaweza kutokea tena.
*D*. Iwapo hakutakuwa na utaratibu mzuri wa kulipia gharama za nauli na chakula wajumbe wote na kuwahitaji wajumbe kujigharamia basi hii itakuwa fursa kubwa sana kwa kundi la G6 kwani wataitumia fursa hio kuwakirimu wajumbe kwa kuwalipia gharama hizo kwa ahadi ya kupigiwa kura

Kiujumla na bila kumumunya maneno kushinda chaguzi ndani ya Rorya ni mashindano ya fedha ambapo mshindi lazima apatikane kwa fedha na wananchi wamezoeshwa hivo na hili kundi, asiyetoa pesa anaonekana kama hayuko siriasi au kama mshamba fulani hivi, mfano:
- 2010 pale kijiji cha Bukama wapiga kura za maoni walipiga kelele wakati wagombea wakijinadi kuwa wao hawana masikio, wao wana matumbo, na wanasikilizia matumbo yao na sio masikio. Alipopanda jukwani Mhe LOA akasema bila uoga kuwa *kiingereza bila pesa ni kelele*
- 2015 Mtia nia ndg yangu Yesse Nyamisogoro (R.I.P) aliwahi kunichekesha kuwa alienda kijiji cha Kitembe na kutoa Tsh 360,000 lakini aliambulia kura 6 tu ikiwa na maana kuwa kila kura ilimgharimu Tsh 60,000, aliporudi kuwashukuru, wapiga kura wapatao 200 walimueleza kuwa kura zao zimefiamo (zipo ndani ya hizo kura sita), akabaki anashangaa alipateje kura sita?...kifupi kuna mtia nia alitoa zaidi.
- Juzi nimeipata hio kuwa kuna mtia nia amewatembelea wajumbe huko kata ya Ikoma na kitembe akakuta wajumbe wameshakula na kunywa na bili ni juu yake ameambiwa alipe!!!

*USHAURI WANGU*

*1* TAKUKURU wasilichukulie kwa wepesi kauli ya LOA ya kutoa Tsh 100,000 kwa kila mjumbe.TAKUKURU mkoa watusaidie sisi wananchi wanyonge kudhibiti mianya hii hasa kutokana na kwamba ameshaeleza wazi tena kwa umma. TAKUKURU wasijali pesa zake, cheo chake wala umaarufu wake, watutendee haki wapiga kura kwani tumeona taasisi hii mikoa mingine ikifanya kazi nzuri tena kwa ueledi mkubwa hivo hata hili hawatashindwa kulifanyia kazi.

*2* TAKUKURU watusaidie kudhibiti usafirishaji wa wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya maana hapo ndipo kuna rushwa kubwa sana, watia nia wasikodi na kuwalipia wajumbe usafiri na chakula.

*3*. Ningemuomba kaka yangu Mhe LOA akae pembeni (japo inaonekana anagombea tena) na asimuunge mkono mtia nia yeyote (japo inasemekana tayari ameweka mtu kutoka *LUOIMBO* ambaye asipopitishwa atamgharamia kwa hali na Mali ashinde). Heshima aliojijengea inatosha na kama ameharibu sehemu tutamsamehe na apewe mwingine nafasi arekebishe kwani uongozi ni kupokezana. Ajifunze kwa akina Dr William Shija, Njelu Kasaka, Stephen Wassira, John Samuel Marecela, Edward Oyombe, waliolazimisha kugombea hata baada ya kuchokwa wakapotea kabisaaaa. Hii itaisaidia jimbo kuondoa mgawanyiko wa ukabila na hali ya rushwa.

*3*. Niwaombe wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya watupatie wagombea makini, wenye dira, wanaokubalika na ambao hawana harufu ya rushwa na hawakutoa chochote, na atakae teuliwa na CC tutamchagua kwa uwezo wake ili aje atuoneshe kazi zake alizofanya akimaliza muda wake kwani tukimchagua kiongozi kwa kutoa rushwa hatutokuwa na uwezo wa kumuuliza kazi alizofanya kwani atatujibu kuwa alishatulipa, mtu kutoa million 88 sio mchezo ndugu zangu. Mhe LOA akasome kitabu cha Ellen Johnson Sirleaf kiitwacho *This Child will be Great: Memoirs of a Remarkable life by Africans' First Woman President* anasema *Leadership is not about which path you take, it's about the choice you make when the road diverge* najua anajua kusoma na kuelewa.

*4*. Ombi langu maalum kwa Rais wangu mpendwa na mwenyekiti wangu wa CCM ni kuwa jimbo letu la Rorya lina mpasuko mkubwa sana, inawezekana hawakuelezi vizuri wasaidizi wako hasa mwenyekiti wa CCM mkoa ambaye yuko kwenye kundi la G6 lakini najua una vyombo vyako vya usalama vyenye ueledi mkubwa na watakuandikia ripoti nzuri watakupa picha halisi ya jimbo letu lilivyo na hili limesababishwa na kundi la wafanyabiashara wachache wanaojiita G6. Iwapo Lameck Airo akigombea tena tunaomba sana tena sana mkate jina lake. Kwa sasa Mhe huyu hatufai tena kuwa muwakilishi akitia nia najua atashinda kura za maoni kwa sababu ya nguvu zake kiuchumi na sio kwamba anakubalika, ametusababishia rushwa kubwa sana jimboni, amesababisha mgawanyiko mkubwa utarafa, anawatumikisha madiwani kama wanae, mpaka sasa hivi Diwani wa kata ya Nyambori Mhe. Mamba amehamia nyumbani kwake Utegi ni mfanyakazi wa ndani, aliekuwa diwani wa Nyamtinga Mhe Komba alihamia kwake Tarime ili tu wamtumikie yeye na sio wananchi.

Mhe huyu anafanya vizuri sana kwenye biashara zake na mungu amempa kipawa hicho, mwache afanye biashara zake aajiri vijana wetu wanaomaliza elimu za juu, kwenye uwakilishi hawezi tena kwani yuko bize na biashara zake hata bungeni haudhurii na wala hajawahi kusimama kuchangia mada yoyote bungeni kwa kipindi cha miaka 10. Wenzetu wa upinzani watapata agenda nyingi sana ya kusema dhidi yake wakati wa kampeni hivyo CCM watapata upinzani mkubwa sana Rorya kwenye uchaguzi huu. Tupe mgombea mwingine mpya asie na doa wala kasoro hizo na tutalichukua hili jimbo mchana kweupeee.

*TUSIMAME TUIJENGE RORYA YETU*

Maoni
+255 752 761116
 
Waambieni wanaotoa rushwa wakumbuke kuna chujio jembamba la chama, la kuengua wachumia tumbo.
Chek sura za kazi! Hapa watoa rushwa wanapitaje?
Screenshot_20200704-131553.png
 
Mkuu Obwere! Salamu. Kwanza nakupa hongera kwa andiko lako. Ila naomba nikuulize hivi ni wapi Rorya kuna maendeleo? Ni wapi Girango au Luo Imbo penye maendeleo kuliko huko Nyancha au Suba?. Kwa uelewa wangu Rorya nzima ni hovyo ikiwa na wananchi fukara wa kutupwa. Jinsi ambavyo la Kairo amewazoeza watu kwa pesa ndiyo utamaduni wa chama chenu hicho. Unasema mwenyekiti wenu hataki Rushwa huku yeye akitumia mbinu mbovu dhidi ya wenzake huoni hana Integrity kama huyo LOA?
 
Lameck kashatangaza hagombei tena ila najua bado ana ushawishi ndani ya chama chenu hicho. Tatizo letu wasomi wa Rorya ni kujificha na kuibuka wakati wa uchaguzi. Maprofesa wengi kuanzia Monyo, huyo Nyamisogoro na wengine pamoja na wasomi wengine hawana mchango hata kwa familia zao achilia mbali Wilaya. Hiyo G6 siyo kikundi cha tarafa mkuu ni watu tu. Ila jimbo ambalo najua CDM wakijipanga vizuri wanachukua ni hiyo Rorya liko wazi mno kwa cdm mwaka huu.
 
Tukimwondoa Mbunge "Bubu" Lameck, hivi hii wilaya ya Rorya imeshawahi kuwa na Mkurugenzi au hata kuwa na Idara yoyote ya kusimamia mradi wowote wa Halmashauri kweli?
Ina maana hii Halmashauri ina Madiwani kweli?
Hawa Madiwani huwa wanapanga kitu gani kama kwa miaka yote toka Rorya ijitegemee hamna maendeleo yoyote?

Mbunge bila Madiwani wanaojielewa, Rorya bado UMASIKINI tuko nao sana.
 
*KURA ZA MAONI CCM-RORYA: HUENDA UKAWA NI WA UKABILA/UTARAFA DHIDI YA RUSHWA*

na Mwl. Chacha Matete
Idara ya Elimu ya Ufundi - MUST

Moja ya ahadi za mwana TANU ambazo mwana CCM anapaswa azifahamu ni ahadi namba nne (5) inayosema *rushwa ni adui wa haki, sitopokea wala kutoa rushwa*. Hii ahadi imenikumbusha ilee CCM ya Mwl JK Nyerere ambayo Mhe JPM amejitahidi sana kuirudisha. Sasa hivi hali ya rushwa kidogo inaridhisha tofauti na miaka mitano iliopita, angalau watu wanaogopa kupokea au kutoa rushwa.

Tofauti na utaratibu wa zamani wa kumpata mgombea wa ubunge au udiwani ndani ya CCM ambao wanachama wote kuanzia ngazi ya shina walipiga kura za maoni, sasa hivi ni viongozi wa kuanzia ngazi ya tawi na kata ndiyo watahusika. Mabadiliko yaliofanywa na CCM yamelenga kupunguza kama sio kuondoa mianya ya rushwa iliokuwa imeota mizizi na kuwapunguzia gharama watia nia, hii imewapa fursa hata wasio na kipato kikubwa kutia nia maana inakuhitaji kuwa na nauli yako, hela ya kulipia fomu na kwa hiari yako pesa ya kuchangia chama shughuli za uchaguzi/maendeleo

Vijana wengi wameitikia wito wa mwenyekiti wa CCM kitaifa na kusisitizwa na mkuu wa mkoa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka ya kuwataka vijana kugombea badala ya kuwa wapambe na wapiga debe wa wagombea.

Jimbo la Rorya ni miongoni mwa majimbo yatakayoingia kwenye kinyang'anyiro hicho. Niliwahi kuandika kwenye makala yangu kuwa kuna tatizo kubwa sana la utarafa uliobeba sura ya ukabila na rushw a. Tarafa ya Suba na Nyancha zinazokaliwa zaidi na jamii zenye nasaba na kabila la wakurya wameunda umoja wao ujulikanayo kama suba 1&2, huku wenzao wa Girango na Luo-imbo wakiunda kile kinachoitwa G6 (Japo Luo-imbo kwa uchache wao wanajificha wasionekane kuwa ndani ya G6), nimepokea simu nyingi sana za wana Rorya wengi wakikubaliana nami na wengine wakikataa kutokuwepo ukabila kuibuka wakati huu. Yupo mchangiaji mmoja alinivutia kidogo hoja yake, yeye alinieleza kuwa *umoja wa tarafa ya Suba na Nyancha ni mbinu ya kutaka huruma (sympathy) tu ili na wao wapewe nafasi ya kuongoza jimbo la Rorya kwa kuwa hawana uwezo na fedha kuongoza*. Kwa kweli kama mwana Rorya kwa uzawa, kukulia na kusomea nikaingiwa na wasiwasi mkubwa sana, nikapata mawazo haya:

*A* Mpiga simu alishindwa kunithibitishia kuwa makundi haya hayapo na hakuna mpasuko huo. Naomba wanarorya wenzangu waelewe haya makundi yapo na kuna makundi sogozi yameundwa na yanajiita Suba 1&2, na lile la G6 na yanaratibu shughuli za uchaguzi nyuma ya pazia

*B*. Nimepatwa na wasiwasi na kauli yake ya kutokuwa na uwezo wa kuongoza na fedha wa watu kutoka tarafa ya Nyancha na suba, nikaona kuna mpasuko mwingine wa ubaguzi wa kuwaona wengine hawana uwezo na hivyo kuhitaji huruma tu wa
wengine kuongoza.

*C*. Mpiga simu ameshindwa kukanusha kuwa huenda kukaibuka hali ya rushwa kubwa kwenye kura za maoni kwa wale wanaojiita G6 dhidi ya Suba 1&2 ambao wanachukuliwa kutokuwa na uwezo kifedha.

Huenda wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya/jimbo wakasahau ile ahadi namba 4 ya mwana TANU ambayo mwana CCM anatakiwa aijue na kuifuata inayoongelea rushwa kama adui wa haki. Nitaeleza:

*A* Wajumbe wa mkutano mkuu wilaya watakaopiga kura wanakadiriwa kufika *900+*. Hii itawajumuisha
1. Mwenyekiti wa tawi
2. Katibu wa tawi
3. Katibu Mwenezi wa tawi
4. Mjumbe wa mkutano mkuu ngazi ya wilaya
- kutoka ngazi ya kata watakaopiga kura ni:
1. Mwenyekiti wa CCM kata
2. Katibu wa CCM kata
3. Katibu mwenezi kata
4. Mjumbe wa mkutano mkuu
- ukiongeza na wawakilishi wa makundi ya UVCCM, CWT, nk kwa kila kata inakadiriwa kuwa na wapiga kura *34* ukizidisha Mara kata *26* utapata wajumbe *884+*

Tarafa ya Nyancha na Suba watakuwa na wajumbe wengi *(554+)* kuliko Girango na Luoimbo *(340+)* ni kweli bila kificho wajumbe wengi kutoka tarafa ya Nyancha na Suba wanahitaji sana mbunge kutoka kwenye maeneo yao baada kuonekana kutengwa sana kimaendeleo kwa kipindi kirefu lakini ilivyoelezwa na yule mpiga simu hawana uwezo kifedha na hawawezi kushindana na G6 wenye uwezo kifedha, mbinu pekee iliobaki ni kuungana kwa itikadi ya utarafa/ukabila.Hii ni mbinu chafu na haikubaliki lakini kwa mtizamo wa wengi hawana jinsi bali ni kuungana tu dhidi ya wale wanaosemekana kuwa ni watesi wao (G6)

*B*. Kura za maoni zinaweza kuingiliwa sana na rushwa kuliko nyakati zote kuwahi kutokea kwa sababu:

1. Iwapo wajumbe wa mkutano mkuu kutoka suba 1&2 wataungana mbinu pekee iliobaki kuwasambaratisha ni kwa njia ya rushwa. Kwa njia yoyote kama atapitishwa mtia nia kutoka SUBA 1&2 dhidi ya wa G6 mbinu pekee ni kuwamaliza ni rushwa kwani kweli wamefanywa tegemezi kuomba rushwa *GONYA*

2. Tayari mhe mbunge anayemaliza muda wake ameshajinasibu kuwa yeye kiwango chake cha kutoa rushwa ni Tsh 100,000 kwa kila mjumbe ambayo itamuhitaji kuwa na kiasi cha *Tsh 88,400,000+* kuwaonga wajumbe wote.
Akiongea na wana CCM wa kata ya Nyamagaro, Mhe.LOA aliwajibu wale waliomtuhumu kuwa ameanza kuwaonga wajumbe wa kata za Nyamagaro, Nyamtinga na Kyangasaga kiasi cha Tsh 5000 kwa kila mjumbe.Mhe alisema yeye kutoa kiwango hicho cha sh 5000 ni kuwadhalilisha wajumbe kwani ni kiasi kidogo mnooo!!!!
- Hii inadhihirisha kuwa Mhe huyu akipitishwa na CC kuwa miongoni mwa wale tatu bora basi atategemea zaidi kuwaonga wajumbe. Kwa kiongozi mwenye ueledi na anaijua vyema ile ahadi No. 4 ya mwana CCM hakukuwa na haja ya kujibu tuhuma zilizoandikwa mitandaoni tu na pengine hazina ushahidi wowote.
*C*. Kuna dalili kuwa ilikugawana kura za Nyancha na Suba wadadisi wa siasa wa jimbo la Rorya wanasema inawezekana kupangwa kwa watia nia ambao hawana nia ya kugombea bali *kumpamba, kumsifia na kumpigia debe* wakati wa kuomba kura kwa wajumbe badala ya kujiombea kura. Hii imewahi kutokea kwenye uchaguzi wa 2010 na 2015 ambapo mtia nia mmoja ambaye kazi yake kubwa ilikuwa ni kumpamba na kumsifia LOA ambaye alikuwa mpinzani wake na kumuombea kura badala ya kujiombea. Kibaya zaidi mtia nia huyo alikuwa akipangiwa ratiba ya kuongea aidha kabla au baada ya LOA kuongea. Haikuhitaji kuwa na elimu kubwa kiwango cha PhD kugundua hili kuwa mtia nia huyo alipangwa na pengine alilipwa kuharibu kura za wengine hasa za Nyancha na Suba, hii inaweza kutokea tena.
*D*. Iwapo hakutakuwa na utaratibu mzuri wa kulipia gharama za nauli na chakula wajumbe wote na kuwahitaji wajumbe kujigharamia basi hii itakuwa fursa kubwa sana kwa kundi la G6 kwani wataitumia fursa hio kuwakirimu wajumbe kwa kuwalipia gharama hizo kwa ahadi ya kupigiwa kura

Kiujumla na bila kumumunya maneno kushinda chaguzi ndani ya Rorya ni mashindano ya fedha ambapo mshindi lazima apatikane kwa fedha na wananchi wamezoeshwa hivo na hili kundi, asiyetoa pesa anaonekana kama hayuko siriasi au kama mshamba fulani hivi, mfano:
- 2010 pale kijiji cha Bukama wapiga kura za maoni walipiga kelele wakati wagombea wakijinadi kuwa wao hawana masikio, wao wana matumbo, na wanasikilizia matumbo yao na sio masikio. Alipopanda jukwani Mhe LOA akasema bila uoga kuwa *kiingereza bila pesa ni kelele*
- 2015 Mtia nia ndg yangu Yesse Nyamisogoro (R.I.P) aliwahi kunichekesha kuwa alienda kijiji cha Kitembe na kutoa Tsh 360,000 lakini aliambulia kura 6 tu ikiwa na maana kuwa kila kura ilimgharimu Tsh 60,000, aliporudi kuwashukuru, wapiga kura wapatao 200 walimueleza kuwa kura zao zimefiamo (zipo ndani ya hizo kura sita), akabaki anashangaa alipateje kura sita?...kifupi kuna mtia nia alitoa zaidi.
- Juzi nimeipata hio kuwa kuna mtia nia amewatembelea wajumbe huko kata ya Ikoma na kitembe akakuta wajumbe wameshakula na kunywa na bili ni juu yake ameambiwa alipe!!!

*USHAURI WANGU*

*1* TAKUKURU wasilichukulie kwa wepesi kauli ya LOA ya kutoa Tsh 100,000 kwa kila mjumbe.TAKUKURU mkoa watusaidie sisi wananchi wanyonge kudhibiti mianya hii hasa kutokana na kwamba ameshaeleza wazi tena kwa umma. TAKUKURU wasijali pesa zake, cheo chake wala umaarufu wake, watutendee haki wapiga kura kwani tumeona taasisi hii mikoa mingine ikifanya kazi nzuri tena kwa ueledi mkubwa hivo hata hili hawatashindwa kulifanyia kazi.

*2* TAKUKURU watusaidie kudhibiti usafirishaji wa wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya maana hapo ndipo kuna rushwa kubwa sana, watia nia wasikodi na kuwalipia wajumbe usafiri na chakula.

*3*. Ningemuomba kaka yangu Mhe LOA akae pembeni (japo inaonekana anagombea tena) na asimuunge mkono mtia nia yeyote (japo inasemekana tayari ameweka mtu kutoka *LUOIMBO* ambaye asipopitishwa atamgharamia kwa hali na Mali ashinde). Heshima aliojijengea inatosha na kama ameharibu sehemu tutamsamehe na apewe mwingine nafasi arekebishe kwani uongozi ni kupokezana. Ajifunze kwa akina Dr William Shija, Njelu Kasaka, Stephen Wassira, John Samuel Marecela, Edward Oyombe, waliolazimisha kugombea hata baada ya kuchokwa wakapotea kabisaaaa. Hii itaisaidia jimbo kuondoa mgawanyiko wa ukabila na hali ya rushwa.

*3*. Niwaombe wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya watupatie wagombea makini, wenye dira, wanaokubalika na ambao hawana harufu ya rushwa na hawakutoa chochote, na atakae teuliwa na CC tutamchagua kwa uwezo wake ili aje atuoneshe kazi zake alizofanya akimaliza muda wake kwani tukimchagua kiongozi kwa kutoa rushwa hatutokuwa na uwezo wa kumuuliza kazi alizofanya kwani atatujibu kuwa alishatulipa, mtu kutoa million 88 sio mchezo ndugu zangu. Mhe LOA akasome kitabu cha Ellen Johnson Sirleaf kiitwacho *This Child will be Great: Memoirs of a Remarkable life by Africans' First Woman President* anasema *Leadership is not about which path you take, it's about the choice you make when the road diverge* najua anajua kusoma na kuelewa.

*4*. Ombi langu maalum kwa Rais wangu mpendwa na mwenyekiti wangu wa CCM ni kuwa jimbo letu la Rorya lina mpasuko mkubwa sana, inawezekana hawakuelezi vizuri wasaidizi wako hasa mwenyekiti wa CCM mkoa ambaye yuko kwenye kundi la G6 lakini najua una vyombo vyako vya usalama vyenye ueledi mkubwa na watakuandikia ripoti nzuri watakupa picha halisi ya jimbo letu lilivyo na hili limesababishwa na kundi la wafanyabiashara wachache wanaojiita G6. Iwapo Lameck Airo akigombea tena tunaomba sana tena sana mkate jina lake. Kwa sasa Mhe huyu hatufai tena kuwa muwakilishi akitia nia najua atashinda kura za maoni kwa sababu ya nguvu zake kiuchumi na sio kwamba anakubalika, ametusababishia rushwa kubwa sana jimboni, amesababisha mgawanyiko mkubwa utarafa, anawatumikisha madiwani kama wanae, mpaka sasa hivi Diwani wa kata ya Nyambori Mhe. Mamba amehamia nyumbani kwake Utegi ni mfanyakazi wa ndani, aliekuwa diwani wa Nyamtinga Mhe Komba alihamia kwake Tarime ili tu wamtumikie yeye na sio wananchi.

Mhe huyu anafanya vizuri sana kwenye biashara zake na mungu amempa kipawa hicho, mwache afanye biashara zake aajiri vijana wetu wanaomaliza elimu za juu, kwenye uwakilishi hawezi tena kwani yuko bize na biashara zake hata bungeni haudhurii na wala hajawahi kusimama kuchangia mada yoyote bungeni kwa kipindi cha miaka 10. Wenzetu wa upinzani watapata agenda nyingi sana ya kusema dhidi yake wakati wa kampeni hivyo CCM watapata upinzani mkubwa sana Rorya kwenye uchaguzi huu. Tupe mgombea mwingine mpya asie na doa wala kasoro hizo na tutalichukua hili jimbo mchana kweupeee.

*TUSIMAME TUIJENGE RORYA YETU*

Maoni
+255 752 761116
Kama wana Rorya wapiga kura wana akili ya kujua huyu hatufai na huyu anatufaa, hilo swala la hela zake wala sio tatizo, ni kwamba kula hela yake na kura mpe anaefaa hata kama sio wa chama chako!!Tatizo ukiwa unapiigia kura chama!!
 
Wana Rorya na Mara kwa ujumla ni wapinzani wazuri, endeleeni namna hiyo na sio kuwa kondoo wa ccm kwa miaka 60 kama wengine.
 
Back
Top Bottom