kinepi_nepi
JF-Expert Member
- Aug 16, 2007
- 869
- 236
- Naomba kuwaaamsha usingizini wale wote ambao bado wamelala usingizini, people tupo vitani yaani kwenye vita vya Itikadi za vyama vyetu vya siasa, wenzetu huko Chadema walianza siku nyingi sisi CCM tulikuwa bado hatujaelewa hilo, lakini Inshallah sasa somo limeanza kueleweka, matusi hapana, viroja hapana, hoja tu jamani lakini ni lazima tusimamie na kutetea itikadi zetu, kama huwezi kusimama kutetea itikadi ya chama chako cha siasa sio sawa hata kuwa mwanachama wa CCM!!
- Simama juu uhesabiwe! People msidanganywe hakuna chama cha upinzani kinachotutakia mema CCM wote wanegependa kuona wanatushinda na CCM inakufa, sasa msijidanganye na siasa za kujifanya kukubalika kila upande ninawaona wanasiasa wengi wakijaribu kuwa kila upande poleni sana, CCM lazima tusimame imara na hakuna kuogopa!! Tusimamie itikadi yetu hata kama it means kufa na tufe lakini hatuwezi kukubali kushindwa kusimamia itikadi, kumbukeni kwamba:- "IN LIFE IF YOU DON'T STAND FOR SOMETHING, YOU WILL FALL FOR ANYTHING"
- KIDUMU CCM! KIDUMU CHAMA TAWALA!!
FMES - SAUTI YA UMEME!!
Kweli kabisa Le CCMiz
Ulichoandika kina make point
Ningefurahi sana kama CCM wangekubali kusimamia itikadi yao na kuitetea kwa nguvu zake zote.
Itikadi zenyewe ni hizi, rushwa, ufisadi, uzushi, uhujumu, nk.
Tukiangalia katiba ya CCM na matendo yake au ya viongozi wake wote ni kwamba hiki chama kimekufa. Field Marshall unawaonea wana CCM wanaoshindwa kutetea chama kwa sasa kwani hakuna cha kutetea, si unaona hata Mwenezi Nape hana cha kueneza sasa amebakia kusema watu washikishwe ukuta, mtu mzima hovyo, Lusinde naye siwezi kiyasema.
Ingebidi uanze kuitetea CCM kisera ili wengine wajue.
Sisi Chadema tunasema, elimu bure kwa wote mpaka sekondari, vifaa vya ujenzi bei nafuu ili kuondoa nyumba za tende, kuongeza mfumo wa ajira kwa kuwezesha wengi. Kumfumua mtaala wa eli ili iweze kuendana na karne ya sasa na kuweza kumsaidia mwanafunzi baada ya kumaliza shule.
Kuleta ushindani wa kimajimbo na kiuchumi
Kuhakikisha mali asili zetu zinawanufaisha watanzania
Kuwatumia wataalamu wa ndani ili kukuza uchumi, kupanua ajira, kuongeza ubunifu na kiwango.
Kuhakikisha rushwa inapigwa vita na sheria kufuatwa kwa kila takayepatikana ama ametoa ama kuchukua bila kuogopa cheo, jina wadhifa ama hali.
Mahakama kuwa huru huku majaji wote wakiwa wanaidhinishwa na bunge.
Kuhakikisha bunge linakuwa la kisasa badala ya sasa kuwa rubber stamp.
Kukifanya kilimo cha kisasa zaidi badala ya hiki cha powertilla.
Kinacho washinda wenzako ni jinsi ya kutetea Kagoda, EPA, DeepGreen, Richmond, ukizingatia fedha hizi nyingi ndizo zilizomzawadia Mkuu wa kaya uraisi. Sasa watetee sera gani??
Hongera lakini kwa kuona kuna haja ya kuwa na mashambulizi ya kifedha kuliko sasa tunaswaga muda mwingi kwenye non issues.