VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Uzee ni dhahabu na hujaa adabu. Uzee huambatana na uzoefu, utaalamu na misimamo isiyoyumba kama nyumba. Wazee tupo imara kama mnara. Vijana walijaribu kufuata mkumbo wa kuonesha misimamo yao hadharani, hatimaye wamesanda. Wamejisalimisha kwa Mwenyekiti.
Kama wamesema na kutenda waliyoyaamini, kwanini waombe msamaha? Msamaha wao si usaliti kwenye imani yao, maoni yao na maono yao? Kuomba msamaha kwa maoni, imani na maono ni dalili za uoga, kujikomba na kulitumikia tumbo kwa tambo. Vijana wamesanda!
Wazee tuko imara. Maoni yetu yapo hapa JamiiForums, Twitter, Facebook na kwingineko. Haturudi nyuma katika maoni, maono na imani zetu. Tumeshasema, imeshasikika. Ujumbe umeshafika. Tusilazimishane kuomba msamaha ili ionekane tulikosea tulichoongea. Msamaha haulazimishwi!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Singida, Tanzania)