CCM, tutawapuuza muda si mrefu, Hii kuwasema watu baada ya kuwakimbia si sawa

Aliyehusika na wizi wa Richmond mlipa wadhifa gani huko chadema?
Chadema ya leo ijiweke mbali kuongelea ufisadi kwa kuwa imegeuka kuwa chaka kuu la ufisadi na ujangili
Kwani wenye dola ya kuchunguza,kukamata na kufikisha mahakamani ni chadema? Zipo wapi tambo za mahakama ya mafisadi? Ccm ni pango la mafisadi na ndipo yanapohifadhiwa
 
Kwa miaka 50 ijayo CCM bado itaendelea kuongoza Tanzania...huku ikiendelea kuwa Chama adui kwa mafisadi na majangili ambao wanapata hifadhi chadema
Jinga lao hivi una matarajio ya kuishi na ccm yako miaka kumi ijayo?
 
Jilulize anaetajwatajwa kuhusika katika kuagiza vichwa vya treni vyenye utata ana wadhifa gani leo hii?

Leo wako kimya siujui wanasubiri siku ahame chama ndio waanze kumsimanga?

Mawaziri waliotajwa katika ripoti za kamati za madini kuna hata mmoja ameshatakiwa?

Leo hii Chenge ana wadhifa gani Bungeni?

Jiulize ni kweli mahakama ya mafisadi imekosa watu au ni watu wameinyama kazi mahakama hii?

Poleni sana wenye imani na hiki chama!

Zoezi la kifisadi la kugawana nyumba za serikali lilisimamiwa na mwenyekiti wa sasa wa CCM, ambaye pia ni Rais wa Tanzania. Mbona wako kimya? Au wanasubiri siku ahamie Chadema ndio waanze kumsimanga kwa kusimamia zoezi lile lililojaa jeuri na kibri kubwa kupata kutokea hapa nchini?
 
Hata magu akiondoka Leo watasema ni fisadi aliuza nyumba za siri Kali, meli ya bagamoyo itaibukia hapo
 
Maana tumejenga mahakama ya mafisadi na baada ya mwaka tukadai mahakama imekosa kesi, ila wanachama wakitikimbia tinadai ni majizi na mafisadi! Si ajabu Chenge, Ngereja na pamoja na Tibaijuka, nao tunasubiri siku wakitangaza kuachana na chama chetu ndipo tuanze kusema kuwa ni mafisadi!

Ushauri wangu kwa chama change

Tuchukue hatua madhubuti na sahaihi kwa wakati unaofaa, badala ya kushiriki nao kwa kila jambo then wakitukimbia ndipo tuanze kulalamika eti ni mafisadi! This is cheap propaganda na haina dhamira ya dhati.

Nawasilisha
 
Hivi bro ulioleta mada hii bado unajiuliza mpaka leo kama chama lawanu wako serious au la!!? Nadhani tayari una umri wa kujua hilo. Usitegemee miujiza hapo bro....
 
CCM ni chama Mfu....akijamba Mwekiti Watu wana Simama na Kupiga Vigelegele...
 
"Kwakuwa mmekuwa madarakani tangu kuanzishwa kwenu mwaka 1977, hamuwezi kusema kuna mahali kuna majizi mengi kuliko nyinyi kwakuwa mko wengi".

Hapa ni kama umekubaliana na hoja ya Nyalandu kwamba "CCM imeshindwa kuisimamia dola" au siyo Bw. Mselewa?
 
"Kwakuwa mmekuwa madarakani tangu kuanzishwa kwenu mwaka 1977, hamuwezi kusema kuna mahali kuna majizi mengi kuliko nyinyi kwakuwa mko wengi".

Hapa ni kama umekubaliana na hoja ya Nyalandu kwamba "CCM imeshindwa kuisimamia dola" au siyo Bw. Mselewa?
Wewe wasema!
 
tukiwapuuza kwa hilo ambalo angalau baadhi wanashughulikiwa, wanaopokea hao ambao tunawatumia kama kigezo cha kuipuuzia CCM wanapaswa kufutwa kabisa akilini mwa watanzania.
 
CCM NI MTAMBO WA KUZALISHA MAFISADI, WEZI NA MATAPELI WA NGAZI ZOTE......

CHADEMA NI MTAMBO WA KUSAFISHA MAFISADI NA MATAPELI WA AINA ZOTE....

ANACHOTAKIWA KUFANYA NI KUHAMA TU KUTOKA KWENYE MTAMBO WA MAFISADI NA KUJA UPANDE WA PILI AMBAPO ANAKUWA MSAFI KAMA THELUJI........

CHENGE NI FISADI AMBAYE CCM IMESHINDWA KUMSHUGHILIA LAKINI AKIHAMIA CHADEMA ANATANGAZWA KUWA MTAKATIFU.......

BADO NASHINDWA KUELEWA KUSHINDWA KUWASHUGHULIKIWA WEZI NA MAFISADI NDANI YA CCM KUNAMFANYAJE KUWA MSAFI AKIWA CHADEMA...!!!?

YOTE MAISHA......
 
Dogo hivi bado hata hawajakupa U-DC? Mbona wanaoingia kwenye chama wanateuliwa ... au nyinyi
wakubwa wanaona buku saba zinawatosha??? (by the way najua JPM anataka wasomi..kama vipi kamata diploma pale Open University). Otherwise utaua watoto kwa njaa...
Maana naona JPM anateua wanaoingia tuu..akina mama Mghwira, Kitila Mkumbo, Shonza..na nyinyi wapiga ramli mkiishia mitandaoni tuu....

Pambanane mkumbukwe!

Na wanao watetea wezi ambayo serikali dhalimu ya CCM imeshindwa kuyashughulikia na wao wanafanya hivyo wazawadiwe nini....!!!?
 
Siasa za hii nchi ndivyo zilivyo, zimeathiri hata maisha yetu ya kawaida.

Mfano, unakua na mwanamke miaka kadhaa, unamlisha, unamvisha na kila kitu, siku mkiachana utasikia oooh, kwanza ana kibamia, mara alikua ananipiga, mara alikua ananitesa na kuninyanyasa

Sasa miaka yote hiyo ungekua unateseka na kupigwa si ungekua umeondoka, vinginevyo ni kua ulikja unafurahia kipigo.

Wanasiasa wa nchi hii wametufanya sisi wananchi kuwa ni mazezeta
 
Jilulize anaetajwatajwa kuhusika katika kuagiza vichwa vya treni vyenye utata ana wadhifa gani leo hii?

Leo wako kimya siujui wanasubiri siku ahame chama ndio waanze kumsimanga?

Mawaziri waliotajwa katika ripoti za kamati za madini kuna hata mmoja ameshatakiwa?

Leo hii Chenge ana wadhifa gani Bungeni?

Jiulize ni kweli mahakama ya mafisadi imekosa watu au ni watu wameinyama kazi mahakama hii?

Poleni sana wenye imani na hiki chama!

Hebu nisaidie Hili ndugu yangu...!!!?


Kushindwa kwa CCM kuwashughulikia wezi walioko huko kwao.....kuna wafanya je hao wezi kuwa wasafi ndani ya CDM....!!!?
 
Nawaandikia viongozi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM). Nawaandikia kuwaambia kuwa siku si nyingi tutawapuuza kwa kila mnalolisema au kulitenda. Hii tabia ya kukaa na mafisadi na majizi kwenye chama chenu hadi wahame au waachane na siasa ndiyo muwanyooshee vidole na kuwasema si sawa.

Uzuri wenu CCM ndiyo mnaounda Serikali. Mna kila uwezo, kama kuna nia pia, ya kuwachunguza, kuwabaini na kuwashughulikia mafisadi na majizi yote yaliyopo kwenye chama chenu. Kwakuwa mmekuwa madarakani tangu kuanzishwa kwenu mwaka 1977, hamuwezi kusema kuna mahali kuna majizi mengi kuliko nyinyi kwakuwa mko wengi.

Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wenu wa Taifa wa CCM aliingia madarakani, pamoja na sera nyinginezo, na sera ya kupambana na kuyashughulikia mafisadi na majizi yote ya hapa Tanzania. Sera yake hiyo, ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa Mahakama ya Mafisadi, iliwavutia watanzania waliokuwa wamechoshwa na ufisadi na kumchagua Magufuli kwa wingi wao.

CCM mnapaswa kumsaidia Rais Magufuli kwa matendo katika vita dhidi ya mafisadi na majizi ya mali za umma. Msaidieni Rais kuwabaini, kuwachunguza na kuwashughulikia mafisadi wote waliopo CCM hivi sasa ili kama usafi uanzie ndani ya CCM. Kungoja hadi mwanasiasa ahame CCM na nyinyi kuanza kumsema kuwa ni fisadi na mwizi ni utapeli wa hali ya juu.

CCM, kuweni serious na mambo yenu. Kuaminika kwenu kunategemea na mnayoyasimamia na kuyafanya sasa. Pia, mnapaswa kujibu kichama mapigo yote ya wanaohama bila ya kuwategemea wasomi makada na watawala kuwajibu wanaoibua maswala ya kichama zaidi. Nasema tena, mafisadi na majizi yote yaliyopo CCM yashughulikiwe sasa. Au mseme wazi sasa kuwa ndani ya CCM hakuna mafisadi au majizi.

Msipowashughulikia sasa mafisadi na majizi hadi msubiri wahame au wajiuzulu, tutawapuuza na kuwaona matapeli, walaghai na watu wa propaganda. Muda wa kuwashughulikia mafisadi ma majizi ndani na nje ya CCM ni sasa katika kuunga mkono sera ya Rais wetu na mwenyekiti wenu Dr. John Pombe Magufuli.
Mwizi hawazi kujishughulikia mwenyewe!
 
Moja ya tukio ambalo limechukua nafasi kwenye media ni juu ya kuhama kwa Nyalandu toka CCM kwenda CHADEMA. Kuhama kwake Nyalandu kumeenda sambamba na kuachia ubunge na nafasi zote alizokuwa nazo ndani ya CCM.

Kutokana na kuhama kwake, upande alikotoka yaani CCM wameanza kumshambulia kuwa Nyalandu ni FISADI na majina mengi tu kama hayo.

Swali langu na ambalo kila Mtanzania mwenye akili ya kiasi au ya kawaida atauliza ni hili;

Kwa nini Nyalandu alipokuwa CCM hakuchukuliwa hatua kisheria kutokana na kile kinachoitwa ufisadi? Je, ndiyo tunaaminishwa kuwa CCM imejaa mafisadi ila wanashindwa kupelekwa mbele ya sheria kwa sababu za kulindana? Na kama mnalindana na kulinda mafisadi, hoja yenu ya uzalendo inapataje nguvu mbele yetu sisi Watanzania wenye akili kiasi na ya kawaida?

Swali lingine, kama kweli Nyalandu na wengine waliohama CCM na kwenda aidha CHADEMA na kwingineko ni MAFISADI, ugumu uko wapi kuwachukulia hatua watu hawa? Au ukihama CCM na kwenda CHADEMA na vyama vingine tayari unakuwa na immunity ya kutokushitakiwa?

Nimalizie kwa kusema hivi, ndugu zangu wa CCM, hoja ya MAFISADI kwa sasa haina nguvu. Ni hoja ambayo inawapaka matope nyie wenyewe. Njooni na hoja tofauti ili tuwaamini kwa maneno na matendo yenu. Na kama hamjagundua, ukweli ni kwamba CHADEMA kwa sasa imewafunika mara mbili ya miaka miwili iliyopita.

Ni mimi Mtanzania, Undecided au Floating Voter.

Wasalaam!
 
Back
Top Bottom