CCM, tutawapuuza muda si mrefu, Hii kuwasema watu baada ya kuwakimbia si sawa


Hebu ona na watu wao wajinga kama Le mutuz na Muro wanavyotengeneza mambo ya kijinga na kusambaza kwenye mitandao ili kuwaaminisha wajinga wenzao uhuni huu wa kishamba!
CCM ya Sizonje na Slowslow Chakubanga imepatwa na nini? Ndio maana Msomali kaikacha kiaina.
 
Bw. Petro, ufisadi na ubadhirifu ndio uhai wa CCM. Ni sawa sawa na damu kwa uhai wa binadamu au wanyama, bila rushwa/ufisadi/ubadhirifu CCM itakufa, narudia wakikosa hayo watakufa i.e. natural death.

Ndio maana rushwa, ufisadi na ubadhirifu viko kitaasisi zaidi kuliko kwa mtu mmoa mmoja CCM. Wanachofanya CCM ni kumzodoa/kumtisha tu (kwa vile lazima alishiriki alipokuwa ndani kama vile) yeyote anayeondoka kwao. Nakubaliana na CCM 100% kuwa hakuna msafi aliyeko CCM, ndio maana kila anayetoka wao huanza kumsemea machafu yake (ingawa sio vyote ni kweli). Huwa ni njia mojawapo ya kujihami kitaasisi ndio maana wao huanza kuwachafua ili kuwatisha wasije wakatoa siri zao.

Ila katika wote nataka sana Bw. Nyalandu asikae kimya tu, ningependa kumsikia majukwaani akijibu shutuma na kutuonyesha wananchi jinsi rushwa ya kimfumo na kitaasisi inavyofanyika na wanufaikaji wakuu ni akina nani.

Ndipo umma utakapojua maana halisi ya kauli ya aliyekuwa Waziri Mkuu awamu ya 4, Bw. Mizengo Pinda , kusema "......mafisadi wakishughulikiwa nchi itayumba....."
 
CCM wanatawala si kwa mazuri yao bali ni mabingwa wa kugangania kwenye usukani.
CCM ilikuwa na labda bado ni kimbilio au sehemu salama kama hutaki kukumbana na mkono wa sheria,au kuwa karibu na serikali ili mambo yako yanyoke haraka.
Lakini kwa sharti la kuwa utabakia "mwenzetu"ndio wao wanaita kukomaa kisiasa.
Ila usiwageuke,ukiwageuka umetangaza utovu wa maadili ya chama, watakushughulikia ipasavyo,na umaarufu wako uwe wa kisiasa,kibiashara utafutika kabisa.
Kuna wakati mwingine wanaweza kukuvua madaraka lakini usijifanye kuchonga mdomo,just keep quiet kuna uwezekano mkubwa wakakukumbuka na kukusamehe siku za mbeleni
CCM ni mseto wa tabia za wanachama wenye nia moja tu kutawala Tanzania kwa gharama yoyote.
 
CCM chama cha ovyo kabisa ubabe na udikteta ndo bado unawafanya waendelee kusurvive
 
Yale manunuzi ya madiwani Arusha bado ameniacha hoi, siamini kama CCM watatufikisha tunapotaka kufika kwa mwenda huu - kitendo cha kununuana madiwani then mnunuzi mkuu anapandishwa cheo waziwazi - aisee!!!

Nukuu:

"Ndugu watanzania, vita ya Rushwa ni ngumu mno; ngumu mno - niombeeni"
 
Aliyehusika na wizi wa Richmond mlipa wadhifa gani huko chadema?
Chadema ya leo ijiweke mbali kuongelea ufisadi kwa kuwa imegeuka kuwa chaka kuu la ufisadi na ujangili
Leo Wakina seth n'a ruge mmewabana lkn nakumbuka kuna kiongozi fulani wa Nchi mkubwa wakati ule alisema fedhazile Siyo za umma na ipo Siku huyo bwana mkubwa ataitwa Kama shahidi mahakamani na hapo kesi itakuwa imekwisha

Ova
 
Leo Wakina seth n'a ruge mmewabana lkn nakumbuka kuna kiongozi fulani wa Nchi mkubwa wakati ule alisema fedhazile Siyo za umma na ipo Siku huyo bwana mkubwa ataitwa Kama shahidi mahakamani na hapo kesi itakuwa imekwisha

Ova
Huyo kiongozi mkubwa wala hayuko mbali, msoga tu pale.
 
Nawaandikia viongozi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM). Nawaandikia kuwaambia kuwa siku si nyingi tutawapuuza kwa kila mnalolisema au kulitenda. Hii tabia ya kukaa na mafisadi na majizi kwenye chama chenu hadi wahame au waachane na siasa ndiyo muwanyooshee vidole na kuwasema si sawa.

Uzuri wenu CCM ndiyo mnaounda Serikali. Mna kila uwezo, kama kuna nia pia, ya kuwachunguza, kuwabaini na kuwashughulikia mafisadi na majizi yote yaliyopo kwenye chama chenu. Kwakuwa mmekuwa madarakani tangu kuanzishwa kwenu mwaka 1977, hamuwezi kusema kuna mahali kuna majizi mengi kuliko nyinyi kwakuwa mko wengi.

Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wenu wa Taifa wa CCM aliingia madarakani, pamoja na sera nyinginezo, na sera ya kupambana na kuyashughulikia mafisadi na majizi yote ya hapa Tanzania. Sera yake hiyo, ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa Mahakama ya Mafisadi, iliwavutia watanzania waliokuwa wamechoshwa na ufisadi na kumchagua Magufuli kwa wingi wao.

CCM mnapaswa kumsaidia Rais Magufuli kwa matendo katika vita dhidi ya mafisadi na majizi ya mali za umma. Msaidieni Rais kuwabaini, kuwachunguza na kuwashughulikia mafisadi wote waliopo CCM hivi sasa ili kama usafi uanzie ndani ya CCM. Kungoja hadi mwanasiasa ahame CCM na nyinyi kuanza kumsema kuwa ni fisadi na mwizi ni utapeli wa hali ya juu.

CCM, kuweni serious na mambo yenu. Kuaminika kwenu kunategemea na mnayoyasimamia na kuyafanya sasa. Pia, mnapaswa kujibu kichama mapigo yote ya wanaohama bila ya kuwategemea wasomi makada na watawala kuwajibu wanaoibua maswala ya kichama zaidi. Nasema tena, mafisadi na majizi yote yaliyopo CCM yashughulikiwe sasa. Au mseme wazi sasa kuwa ndani ya CCM hakuna mafisadi au majizi.

Msipowashughulikia sasa mafisadi na majizi hadi msubiri wahame au wajiuzulu, tutawapuuza na kuwaona matapeli, walaghai na watu wa propaganda. Muda wa kuwashughulikia mafisadi ma majizi ndani na nje ya CCM ni sasa katika kuunga mkono sera ya Rais wetu na mwenyekiti wenu Dr. John Pombe Magufuli.
Toka waseme wamefungua mahakama ya mafisadi hatujaona yeyote akipekekwa huku,tanroad imejaa ufisadi wa kutisha hatujawahi kusikia hata siku moja malaika akiwasema tanroad kwa ufisadi,kila mwaka ripoti ya CAG inataka ufisadi huko au huko kunaishi wasafi tu.
Yeye alikua kiongozi wao miaka 8 hakua anayaona au ndio funika kombe mwanaharamu apite
 
Nawaandikia viongozi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM). Nawaandikia kuwaambia kuwa siku si nyingi tutawapuuza kwa kila mnalolisema au kulitenda. Hii tabia ya kukaa na mafisadi na majizi kwenye chama chenu hadi wahame au waachane na siasa ndiyo muwanyooshee vidole na kuwasema si sawa.
Ungewaandikia hao wanaowapokea ungekuwa umetenda jambo jema sana
Kwetu sie ccm sio chama kinachostahili kutuongoza,lakini je hao ambao wanatakiwa kupewa dola wako strict kivipi?
 
Hatuwezi kunyamazia ufisadi na ujangili
Vipi tanroad miaka yote CAG anatoa ripoti ya ufisadi mbna hatujawahi kusikia amekamatwa mtu kutoka huku,au malaika hajui kma kuna tanroad kichaka cha rushwa,shubamiiit kumbafuuu zenu
 
Back
Top Bottom