iArmaniAdamson
JF-Expert Member
- Jun 15, 2015
- 944
- 289
Kwanza nianze kwa kusema, nimesikitishwa na kukosekana kwa watu makini wa kujaza nafasi sita zilizobaki kwenye wizara muhimu katika baraza hili la mawaziri.
Nina amini kabisa hata wengine wanaweza kukubaliana na mimi kwamba Rais Magufuli ni mtu makini kwenye kazi yake na kutopitishwa kwa watu kama Membe, Nyalandu, Asha Migiro, Tibaijuka, Chenge, Kagasheki ni kuonyesha kwamba kwa kiasi kikubwa ufanisi na 'makandokando' hayana nafasi kwenye serikali ya JPM.
Ila pia kurudi kwa watu kama Makamba na Muhongo ni kudhihirisha sio kila anayelaumiwa na kusemwa, "hafai", na ukweli daima husimama baadaye.
MSHITUKO mkubwa niliopata ni hasa kuhusiana na kukosekana kwa watu KAMILI 34 kwenye baraza la mawaziri hasa kwenye wizara muhimu sana ILHALI CCM tuna wabunge 277+... Mimi nimesikitika sana kwamba wana CCM hasa wateuliwa hawana uzoefu au weledi wa kujumlishwa kwenye kuongoza taifa to the extend that Rais ilibidi atoke nje ya wabunge wa CCM wateule kwenda kutafuta walioko nje ili waje kujazia.
Kwa kipindi kirefu niliamini kwamba walioweka CCM dosari ni watu wachache wasiozidi 20 (hasa wale waliokuwa kwenye uongozi hivi karibuni), sikujua tatizo ni kubwa sana kiasi hiki kama alivyotuonyesha Rais Magufuli.
Watu wote 277+ hata wale wasiofahamika hawafai? Hali ni mbaya ndani ya CCM.
SIKUJUA KAMA HALI NI MBAYA KIASI HIKI.