CCM tumefikaje hapa tulipo?

CCM tumefikaje hapa tulipo?

Kwa maelezo ya jaji warioba ...na Butiku leo ni "mtandao" ulionzishwa mwaka 1995 na kuamua kuasi utaratibu wa chama na kua na chama ndani ya chama mpaka ulipokuja kufarakana kwa maslahi yao serikalini. .wametuasa ni kuwaogopa wana mtandao kama ukoma kwani wanavunja utaratibu hivyo sio rahisi kwenda kusimamia utaratibu pindi watapo kuwa madarakani..na ni rushwa rushwa rushwa
 
- So hii ndio sababu wewe unajua CCM imefikaje hapa? hahahahaha Seriously?

Le Mutuz

Hadi Kingunge analia mwee ccm ilikuwa enzi zilee za Nyerere akiwa hai yaani naamini angalikuwa hai hata huo utitiri wa kuwa na wagombea 40kwenye chama moja tusingeona ila inasikitisha Baba kaondoka na ccm yake.
 
Mawazo mazuri lkn ccm hawataki hata kuusikia
 
Jamani hivi huyu mtu mnayemtetea sana mbona naona kama ana Parkinson's disease,Muacheni Ngoyai apumzike jamani,ni mgonjwa.
Mawazo mazuri lkn ccm hawataki hata kuusikia
 
"Don't trust a woman even if she's naked" James Hadley Chase
 
William tatizo kubwa ni watu ambao wana nia nzuri na kuheshimika kwenye jamii kufanya mambo mawili (1) kuapa kwamba hawawezi kuhama chama cha mapinduzi wa watakuwa huko milele (2) Kutokusema lolote wanapoona maovu. Haya mawili strategically yamewafanya wala rushwa kuto kumemewa, kuto kuogopa na wanajua hakuna atakaye hama!. CCM ni chama kisicho wa nithamu kila mtu anapeta. Lakini vilevile Raisi kikwete ameweka urafiki sana mbele zaidi ya chama
 
Mleta mada analaumu alipoangukia badala ya alipojikwaa-haya unayoyaona leo ni matokeo ya mlichokifanya kwa muda mrefu na hiki si kingine bali ni kumuona raisi ndio kila kitu na raisi kama mwenyekiti wa chama Taifa ni mungu mtu hastahili kukoselewa wala kuonywa.

Nyerere angekuwa hai angemsema na kumuonya hadharini na hakika angechukua hatua mapema hata pasipo yeye kupenda.

Baada ya kumlea Lowassa,sasa mnawajibika kulea mtoto wa Lowassa kama mjukuu na mjukuu huyu mkishindwa kumlea,hakika atakwenda kwa majirani zenu, si kulalamika tu, bali na kutoa siri zenu.

It is too late brother!
 
CCM imefikia hapa ilipo kwa kukubali kuongozwa na wezi, wahuni, wala rushwa, majangili, mafisadi akina Kikwete, Mkapa, Lowassa, Chenge, Tibaijuka, Ngeleja na wengi wengineo ndani ya chama hiki cha wahuni. Baba wa Taifa aliyaona haya katika siku zake za uhai na kuionya CCM lakini hakuna aliyemjali sasa yamekuwa kweli.
 
Sawa iwe vyovyote agenda yake ya moyoni ,unadhani aliyoyasema hayana mantiki?na unafikiri ni busara kumhukumu kama W.J.Malecela au ni vyema tuihukumu hoja aliyoileta jamvini kama mwanajamvi yaani tujifanye kama mtu tusiye mfahamu kabisa kama vile mimi na wewe ambapo mwanzo na mwisho wa kufahamiana kwetu ni hapa tu.

1. Kwani anahukumiwa au inaongelewa hoja kwa kumchukulia yeye kama mfano hai wa hoja anayoilalamikia leo??!!!
2. Ndio maana nimeuliza je yeye bado kiongozi??!! Kama ndio aachie ngazi kwanza sababu mfumo alioingilia madarakani ndio huu anaulalamikia leo, uhalisia uko wapi??!!!
3. Hatuwezi kujifanya hatumfahamu, wakati uhalisia ni kuwa tunafahamu na yeye ni mnufaika wa huu mfumo

Mantiki itapatikana kwa yeye kukubali ukweli kuwa mfumo huu sio sawa tangu yeye anakuwa kiongozi na hivyo aseme wazi kuwa tangu kipindi hiko mfumo haukuwa sahihi. . . . nje ya hapo anakuwa hana mamlaka ya kukemea sebuleni wakati anakumbatia hicho hicho akiwa chumbani . . . .NO
 
- Sio siri kwamba katika mchakato wa Wagombea Urais 42 wa CCM ulioisha hivi karibuni ni Wagombea 3 walio onyesha kukubalika zaidi na wana CCM wengine wa kwanza ni Lowassa, Membe na Mwigulu hili wala halina mjadala ni FACT na ni the TRUTH ya what we all saw with our eyes kutokana na Mikutano yao ya kutangaza nia mpaka mapokezi yao kila walipokwenda kutafuta Wadhamini. Now in a very serious tone kama Uchaguzi ungekuwa based na walipofikia so far Lowasa is a clear winner, it does not matter kama nampenda au simpendi na it does not matter kama namuunga mkono au simuungi mkono but this is a FACT ambayo Wananchi wote tumejionea kwa macho yetu.

- Now, ninasikitika sana kuona kwamba Tanzania tumefikia mahali kwamba huwezi kusema maneno kama yangu bila kutafuta uadui na watu na bila kuzushiwa majungu, na hivi karibuni nimeona Viongozi wengi wakuu wa CCM Taifa wakihaha kwenye majukwaa na hoja moja very interesting kwamba Kuna wagombea Urais ambao hawana maadili yanayokubalika na Chama hicho kukiwakilisha kwenye kugombea Urais kwa hiyo majina yao yatakatwa. Kinachonishangaza ni the fact kwamba hakuna mtu anayewahoji wala kuwauliza exactly what are they trying to tell us?

- Kwamba CCM inajua kwamba ina Viongozi wake wengi wakuu ambao hawana maadili ya kukidhi uongozi wa kitaifa wa Chama hicho lakini haijawahi kuwaadhibu wala kuwafukuza Chama hicho, now leo wanagombea nafasi ya kukiwakilisha chama hicho kwenye urais ndio CCM inaamka na kuanza kulalamika kwa Wananchi kwamba baadhi ya waliochukua fomu zao hawafai kwa sababu hawana maadili ya CCM? Na Wananchi mpaka Media imenyamaza kimya as if this theory is a perfect politics? REALLY?

- I mean kugombea Urais inatakiwa kuwa the simplest thing kwenye Taifa lolote linalofuata misingi ya KISHERIA na DEMOKRASIA binafsi nimebahatika kuishi kwenye Demokrasia ya kweli kwa miaka 30, now ninaambiwa na hapa Tanzania tunaishi kwa Demokrasia ile ile niliyoiona kwenye Demokrasia ya kweli, ninapata taabu sana kuelewa is it that there is something I am missing au ni Demokrasia tofauti, maana mtu una mke wako unaishi naye unakuja mtaani kulalamika kwamba hafai lakini the next thing ana Mimba yako wewe mwenyewe now next time ukisema mke wako hafai ninakusikilizaje? How do I trust anything you say anymore?

- Something is a miss na our Democracy, I am not a Lowasa's Fan but nikisema kama ninvyosema hapa ninakuwa nimepewa pesa na Lowasa na nikisema Membe anafaa zaidi ya Lowasa ninakuwa nimepewa pesa na Membe, halafu ni a serious uadui I mean what Democracy is this? Wananchi wote tumeona jinsi Lowasa anavyojaza Wananchi kwenye mbio zake za kutafuta Urais ni FACT now here comes other theories kwamba sitakiwi kusema hivi kwa sababu Lowasa anawanunua hawa wananchi, jamani how do I say that bila FACTS? Binafsi nimehusika sana kuisaidia Kamati ya Richmond nikiwa ninaishi nje tena kupitia hapa hapa JF ni kwa sababu I knew beter, nilikuwa ninajua kwamba Richmond hawakuwa na Ofisi Texas na iliyokuwepo ilikuwa ni ofisi ya magazeti sio Kampuni ya Umeme, so for that matter nilikuwa ninapigana nikiwa na FACTS and EVIDENCE. Now do I have evidence kwamba Lowasa amewanunua wote wanaomshabikia NO, je hao Wakuu wa CCM wanazo FACTS and EVIDENCE? Great watuwekee wazi tuzione ili watuwazima wenye akili timamua tuzichambue tuone ukweli, kwenye kesi ya Richmond tuliweka FACTS and EVIDENCE from here JF ambazo zilipelekea Lowasa mwenyewe kushindwa kupigana nazo mpaka akajiondoa Uwaziri Mkuu.

- Now my point here is CCM please tuonyesheni FACTS and EVIDENCE in the public kuhusu wale wote wanaonunua support kwenye huu urais na kama Lowassa ananunua Support pia tuwekeeni kama ilivyokuwa kwenye Richmond, ingawa CCM must get its acts together baada ya huu uchaguzi, ninajua for a FACT kwamba Rais wa sasa ametumia muda mwingi sana kushindana na maadui wake ndani ya CCM ambao hawakutaka awe Rais kutokana na tabia za CCM za kutokuwa wawazi mapema kabla ya uchaguzi wa Rais. Sasa hivi wananchi tunataka kutoana macho kisa wagombea na cha kusikitisha ni kwamba hatugombani kwa sababu ya record zao za kazi kwa Taifa hapana tunagombana kwa sababu tu ya kutofautiana kambi za Wagombea, matokeo yake kuna mpaka theories kwamba Jaji Ramadhani ndiye anayefaa maana hana makundi now ninajiuliza ni Mwanasiasa gani wa kweli Duniani ambaye hana kundi la wafuasi wake wanaomuunga mkono? Binafsi nimemsikia Jaji Ramadhani kwa mara ya kwanza alipochukua fomu tu sijawahi kusikia ameshika nafasi yoyote ya CCM kama chama ila sifa yake kubwa ambayo inaweza kuishia kumpa ushindi wa Urais CCM ni kwamba hafahamiki na hana makundi..hahahaha jamani kweli only in Tanzania.

- Wa-Tanzania tubadilike jamani Demokrasia is a good thing sio uadui na vita na unazi kama wa Yanga na Simba, hapa tunaongelea hatma ya Taifa, CCM must do something now ili mbele ya safari tuachane na mambo ya ubishi wa Yanga na Simba Wagombea wanachukua fomu za Urais ukweli unakuwa wazi based on their records za uongozi kama kuna Kiongozi wa CCM amekiuka maadili aadhibiwe au aufukuzwe Chama mapema na wananchi tujue sio kutufikisha kwenye this kind of tensions na uadui wa binafsi badala ya kupigania maendeleo ya Taifa kwanza. Tatatizo la CCM ni Process sio Wagombea, fix the process now please!!

MUNGU AIBARIKI TANZANIA

Le Mutuz Nation

Siku ingine chagua lugha moja ya kuwasilishia hoja zako.ila lowasa lazima akatwe maana hakuna jinsi
 
Yaani nyie watu mna matatizo sana
William anaharibu vibi amani kwa hoja yake hii
Unajua ninyi mijitu ya CCM mnaudhi sana

Huwezi elewa kama unasoma maandishi kama Juma na Roza. . . . .
Walewale. . . . unatetea upuuzi na kujidai unajua watu. . . . . . by the way una EVIDENCE na FACTS kuwa mimi ni CCM?!!!!
 
W.J.Malecela said:
CCM tumefikaje hapa tulipo?
Eti CCM tumefikaje hapa tulipo? Is this a joke? Yaani kuna mtu ndani ya CCM yuko kwenye msafara ingawa hajui msafara wenyewe unaelekea wapi? Au pengine ndivyo walivyo wengi ndani ya hicho chama...wapo wapo tu kwenye msafara bila kujua wanakwenda wapi. Sasa wanafika mwisho wa safari ndio wanashangaa wamefikafikaje walipo.

This is more than funny...this is serious. Kwamba kwa miaka 50 wameng'ang'ania usukani wakilikokota taifa bila dira. Ghafla kama vile wanazinduka usingizini na bila haya wanaanza kushangaa na kujiuliza ni wapi walipo na wamefikaje huko! Wanasahau kuwa hapo walipo pia ndipo walipolifikisha na taifa na wanatakiwa kuwajibika kwa hilo.

Kwa mwana CCM ambaye, pamoja na sisi wananchi kuwapigia kelele tukiwa na wasi wasi wa tunakoelekea, kuanza kuonesha mshangao wa namna tulivyofika tulipo ni ulaghai mtupu. Kejeli, dharau, mapigo na mateso tuliyoyapata kila tulipojaribu kukataa kuburuzwa hatutakaa tuyasahau kamwe na utetezi wowote ule hautoshi.

Kama ni kweli CCM wanashangaa tumefikaje tulipofika dawa ni moja tu, kuwaomba radhi wananchi na kuacha kung'ang'ania madaraka kwani uhalali, uwezo, nia na sababu hawana tena. Madhara yaliyosababishwa na uongozi wa miaka 50 bila dira ni makubwa na huu ndio mtihani mkubwa kwa timu mpya itakayokamata dola Oktoba.
 
Hakuna msafi ndio CCM wote corrupted "over"
 
Eti CCM tumefikaje hapa tulipo? Is this a joke? Yaani kuna mtu ndani ya CCM yuko kwenye msafara ingawa hajui msafara wenyewe unaelekea wapi? Au pengine ndivyo walivyo wengi ndani ya hicho chama...wapo wapo tu kwenye msafara bila kujua wanakwenda wapi. Sasa wanafika mwisho wa safari ndio wanashangaa wamefikafikaje walipo.

This is more than funny...this is serious. Kwamba kwa miaka 50 wameng'ang'ania usukani wakilikokota taifa bila dira. Ghafla kama vile wanazinduka usingizini na bila haya wanaanza kushangaa na kujiuliza ni wapi walipo na wamefikaje huko! Wanasahau kuwa hapo walipo pia ndipo walipolifikisha na taifa na wanatakiwa kuwajibika kwa hilo.

Kwa mwana CCM ambaye, pamoja na sisi wananchi kuwapigia kelele tukiwa na wasi wasi wa tunakoelekea, kuanza kuonesha mshangao wa namna tulivyofika tulipo ni ulaghai mtupu. Kejeli, dharau, mapigo na mateso tuliyoyapata kila tulipojaribu kukataa kuburuzwa hatutakaa tuyasahau kamwe na utetezi wowote ule hautoshi.

Kama ni kweli CCM wanashangaa tumefikaje tulipofika dawa ni moja tu, kuwaomba radhi wananchi na kuacha kung'ang'ania madaraka kwani uhalali, uwezo, nia na sababu hawana tena. Madhara yaliyosababishwa na uongozi wa miaka 50 bila dira ni makubwa na huu ndio mtihani mkubwa kwa timu mpya itakayokamata dola Oktoba.

Asante sana mkuu, Taifa limekuwa hivi sababu ya watu kama yeye. . . . .na bado kuna watu uumu hawaoni hatari ya uthubutu wa mtu kama mtoa mada kuja kujipambanua ati hajui nini kimetokea. . . .Kweli tukae kimya na kumuunga mkono??!!

HAPANA. . . . . . .
 
huyu le mutuz c lile baba zima lililopigwa picha likiparty katikati ya wajukuu zake kwenye after school bash, ila co issue namuuliza tu mpango wake wa kumngoa lusinde mtera bado anao?
 
Back
Top Bottom