CCM tumefikaje hapa tulipo?

CCM tumefikaje hapa tulipo?

Evidence na Facts ni zao la scientific procedure yenye objectivity isiyo na mashaka hakuna blah blah unapolenga objectivity. .. . . . .hili halina patchy work....yeye ni mmoja wa walionufaika na mfumo huu usiofuata facts na evidence ili aweze kuongelea hili lazima yeye akubali haya la sivyo mtu subjective hawezi kuwa na authority ya kuongelea mambo yanayohitaji objectivity!!!!!

Kwenye siasa acha waseme watakavyo ila kwenye intellectuallity kuna ethics.........sio sehemu kila mtu anasema atakacho no way.......there has to be REFLEXIVITY

Kwa hiyo una muweka group gani?
 
Ni hatari sana kama hata wewe unajifanya huoni rafu anazocheza Lowasa. Anacheza mchezo mchafu.huoni? Hebu vua miwani labda unaweza kuona. Lowasa atawadanganya baadhi ya watu tu kuwa yeye ndiye lakini hawezi kuwadanganya watu wote. Watu wanajuwa nguvu ya Lowassa nyuma yake kuna nini. Siamini kama wewe ni mtoto mdogo usiyetambuwa hili otherwise na wewe unajuwa unachokifanya.
 
Le Mburulaz, ushahidi wa rushwa ni mgumu sana, hata hivyo Ushahidi ulio wazi wa Richmond, Meremeta, EPA, Escrow, Matumizi makubwa serikalini nk, yanaonyesha CCM wote ni wezi na hawafai kupewa nchi.
 
Inaonekana wewe huijui katiba ya CCM. KUKATA MAJINA ni lazima, kwasababu ni takwa na kikatiba ya CCM. Ni Majina 5 tu ndio yanayotakiwa kupelekwa NEC. Hivyo lazima majina 33 yakatwe. 38-33=5.

BTW, kwanini humu support dada yako Dr. Mwele Malecela kwenye mbio za Urais wa CCM? Au kwakuwa wewe ni mtoto wa mchepuko?!
 
Matatizo ya ccm mmeyalea wenyewe. Imefikia hatua mtu anawambia wazi asiyemtaka ccm aondoke yeye.mnamwangalia tu.inakuwaje mtu anakuwa na nguvu kuliko Chama? Jibu rahisi ni kwamba mwenye fedha ndio mwenye Chama.mtajuwana wenyewe.
 
Wewe mwenyewe kiongozi Wa ccm umefanya nini upo kwenye jumuiya ya wazazi Je hata familia yako iko sawa tatizo ccm kila mtu anakisema chama sasa chama kimekuwa cha lawama hadi viongozi nmakisema chama chenu
 
Kwa wasiomjuwa Le Mutuz nawapa pole sana, anachokifanya ni kujiandaa kisaikolojia thread zake zimo humu akimkashifu Lowasa na pia akimtukana Kikwete kwa fake ID.

Le Mutuz ataungwa mkono na wageni humu JF na wavivu wa kufikiri tu, mtu yeyote makini ni lazima atampuuza mtu huyu.
Huongei kisomi!! Kila wakati tunajifunza kutoka kwa wajuao na wasiojua, hivyo tunabadilika hata na misimamo yetu. Ni vyema ukasoma andiko la mtu kiwakati. Hili andiko aliloliandika lina mantiki ndani yake. Kama yalopita hayakuwa na mantiki hiyo ni bora kwani JF imeweza kumbadili mtu angalau kwa sekunde chache. Ila kusema za ukweli anavyojibu watu katika sred hii ni yule aliye juu anajua.
 
Tatatizo la CCM ni Process sio Wagombea, fix the process now please!!

MUNGU AIBARIKI TANZANIA

Le Mutuz Nation
True dat jumlisha na leadership command ambayo aina control ya wanachama na viuongo vyake vya usaidizi kwenye kusimamia na kutunza heshima na maadili ya chama na wanachama.

Katika miaka kumi ya raisi lazima higher hierarchy ya chama na washauri wake kiwe kilikuwa kinajua kina kasoro gani na nguvu gani, na kutafuta au kujenga viongozi wenye sifa sahihi kuelekea uchaguzi unaokuja. Na wala aitaki siri mgombea huyo au kundi hilo la viongozi liwe tayari walishalinadi kwenye jamii kwa sifa zao za uongozi na uwezo, uthubutu na publicly demonstrated leadership skills.

Binafsi sijaona kiongozi yeyote bila ya kusemwa kuwa CCM imemjengea uwezo huo zaidi ya Mwigulu lakini sijaona mahala ambapo kapewa kufanya maamuzi ya chama atakacho kiendesha na isitoshe sioni public support ya viongozi wa ngazi ya juu kama ni mtu wetu hivi vitu avitaki siri kwa sababu unauza ubora wa product vyama vya siasa nchi za wenzetu sasa vinatumia marketing guru kwenye kuuza viongozi wao how much public support is important sasa leo ujui kati ya Lowassa CCM inayompinga na mgombea wao nani anakubalika mbele ya jamii.

Ndio matokeo yake watakwambia tumejifanyia tathmini ya chama na tumeone mapungufu ya lipo and then what mnaitaji conundrum ya watu 42 walio ndani na nje ya chama kuja kutatua hizo kasoro; hivi mtu ambae ajawahi kuwa ata mwenyekiti wa wilaya ataweza kweli kuwa mwenyekiti wa taifa hiyo experience ya ku-deal na ego za viongozi wa juu kaitoa wapi kwenye siasa. Chama cha mafia tu mkubwa anapotoka kinajua nani mwenye sifa za kuchukua uongozi hili kuendeleza utamaduni na adabu; sasa chama kinachoongoza watu karibu 50m akina watu wake wawili watatu ambao awaitaji mjadala wa mwisho kipindi hiki ilikuwa wanajipambanua binafsi kwa ubora wao.

CCM ndio kwanza inaangaika na hoja ya maadili yap ni process from the outset kuanzia kwenye succession planning and existing leadership control jamaa wamepishana mpaka unashangaa hiki kweli ni chama kimoja cha siasa, siku zote naamini hawa jamaa wanamengi ya kujifunza kutoka kwa Mbowe na Slaa jinsi ya ku-control party discipline. Juu ya mapungufu yake Mbowe ni natural born commander what he lacks is vision.
 
Huongei kisomi!! Kila wakati tunajifunza kutoka kwa wajuao na wasiojua, hivyo tunabadilika hata na misimamo yetu. Ni vyema ukasoma andiko la mtu kiwakati. Hili andiko aliloliandika lina mantiki ndani yake. Kama yalopita hayakuwa na mantiki hiyo ni bora kwani JF imeweza kumbadili mtu angalau kwa sekunde chache. Ila kusema za ukweli anavyojibu watu katika sred hii ni yule aliye juu anajua.

Wewe una usomi gani? Mjinga kabisa wewe, watu wa mikoani mna matatizo sana, hivi hili jina la Malecela limekutoa akili kabisa!! Hopeless kabisa.
 
Umeandika kama mwanafunzi wa fm 2.
 
-

- hivi karibuni nimeona Viongozi wengi wakuu wa CCM Taifa wakihaha kwenye majukwaa na hoja moja very interesting kwamba Kuna wagombea Urais ambao hawana maadili yanayokubalika na Chama hicho kukiwakilisha kwenye kugombea Urais kwa hiyo majina yao yatakatwa. Kinachonishangaza ni the fact kwamba hakuna mtu anayewahoji wala kuwauliza exactly what are they trying to tell us?

- Kwamba CCM inajua kwamba ina Viongozi wake wengi wakuu ambao hawana maadili ya kukidhi uongozi wa kitaifa wa Chama hicho lakini haijawahi kuwaadhibu wala kuwafukuza Chama hicho, now leo wanagombea nafasi ya kukiwakilisha chama hicho kwenye urais ndio CCM inaamka na kuanza kulalamika kwa Wananchi kwamba baadhi ya waliochukua fomu zao hawafai kwa sababu hawana maadili ya CCM? Na Wananchi mpaka Media imenyamaza kimya as if this theory is a perfect politics? REALLY?

- Now my point here is CCM please tuonyesheni FACTS and EVIDENCE in the public kuhusu wale wote wanaonunua support kwenye huu urais na kama Lowassa ananunua Support pia tuwekeeni kama ilivyokuwa kwenye Richmond, ingawa CCM must get its acts together baada ya huu uchaguzi,

- Wa-Tanzania tubadilike jamani Demokrasia is a good thing sio uadui na vita na unazi kama wa Yanga na Simba, hapa tunaongelea hatma ya Taifa, CCM must do something now ili mbele ya safari tuachane na mambo ya ubishi wa Yanga na Simba Wagombea wanachukua fomu za Urais ukweli unakuwa wazi based on their records za uongozi kama kuna Kiongozi wa CCM amekiuka maadili aadhibiwe au aufukuzwe Chama mapema na wananchi tujue sio kutufikisha kwenye this kind of tensions na uadui wa binafsi badala ya kupigania maendeleo ya Taifa kwanza. Tatatizo la CCM ni Process sio Wagombea, fix the process now please!!

MUNGU AIBARIKI TANZANIA

Le Mutuz Nation
malecela+px.jpg

Maneno aliyosema mwl. Nyerere kuwa IKULU sio pango la walanguzi usikimbilie kwenda IKULU ni mahali patakatifu mtu yeyote anayekimbilia IKULU bila kujiuliza mwogopeni hafai kuwa Rais. Maneno hayo ya mtu kukimbilia IKULU aliyarudia kuyasema Waziri mkuu mstafu mzee John Malecela.

Mzee john malecela amekitaka chama cha mapinduzi CCM kumchukulia hatua kali waziri wa zamani aliyefukuzwa na bunge la Tz Edward Lowassa kwa kitendo cha kugawa fedha nchi nzima kugawa Boda boda nchi nzima kugawa Tisheti nchi nzima zilizoandikwa kwa jina lake Lowassa.

Mzee malecela amesema mtu huyo hafai kuwa kiongozi hafai kuwa hata Balozi wa nyumba 10 anagawa fedha ili awe Rais ananunua urais kwa fedha pesa hizo atazirudisha kwa njia gani? Kwa nini asipumzike kama nilivyopumzika mimi na maswala ya urais mtu huyo hafai.

Mzee malecela amesema wapo baadhi ya wapambe wake wamekuwa wakisema Lowassa anataka urais ili atimize ndoto zake hata akipewa wiki mbili zinatosha kutimiza alichotamani kwa muda mrefu jiulizeni hapo kuna kitu gani nyuma ya pazia kilichojifich Pia mzee malecela amesema sizungumziii wizi wa Lowassa tuhuma zake maana kila mtu anajua Lowassa jinsi alivyo.

Mzee malecela amesema nawashangaa sana baadhi ya watu wanasema Lowassa mchapa kazi ana maamzi magumu sio kweli mimi namfahamu vzr sana Lowassa nilifanya naye kazi ofisini kwangu nikiwa waziri mkuu lkn nilishangaa sana kusikia Lowassa ameteuliwa kuwa waziri mkuu nilisema kijana huyo hatadumu kwa muda mrefu kwenye hiyo nafasi.

Mzee malecela amesema Watanzania waliona Lowassa alipokuwa waziri mkuu alianzisha njia tatu mkoa wa dar es Salaam ili kupunguza foleni bila kufuata sheria zilizowekwa watu wengi sana walikufu na wengine wameshakuwa vilewa wa miguu pia aliagiza jengo la golofa 10 lilipo masaki karibu na nyumbani kwake livunjwe.

Jengo hilo lilifunjwa na suma JKT. bila kufuata sheria matokeo yake serikali ilishindwa na kuamliwa na mahakama kumlipa mwenye Jengo hilo mamilioni ya pesa serikali ililipa hela za umma na aliyesababisha upotevu wa fedha za umma ameachwa yupo anadunda mitaani mambo mengi yalitokea kipindi akiwa waziri mkuu leo hii ndio awe mwenye maamzi magumu.

Mungu anamjua Rais aajaye chama kinamjua atakaye kuwa Rais pia serikali inajua urais wa nchi hautafutwi kwa namna hiyo ameongea mzee John Malecela waziri mkuu mstafu wa Tanzania.
 
MALECELA..jpg

Ndugu zangu waandishi wa habari, awali ya yote naomba niwasalimie na niwapongeze kwa kufika mwaka mpya 2014,pia naomba niwapongeze kwa kazi kubwa ambayo mmekuwa mkiifanya hasa kuhakikisha watanzania wanapata habari kwa kila jambo linaloendelea kila kona ya taifa letu la TanzaniaNdugu waandishi wa habari nimewaita hapa ili kuzungumza nanyi na mnisaidie kufikisha ujumbe kwa watanzania hasa kuhusu jambo hili ambalo limekuwa gumzo kwa watanzania wengi la mbio za urais 2015 kwa baadhi ya watu ndani ya chama changu cha mapinduzi (CCM),kilichonisukuma zaidi na kupata hamu ya kuongea nanyi ni baada ya kumsikia na kumuona kijana wetu ndani ya chama cha mapinduzi bwana paul makonda akiwa na ujasiri wa kukemea vitendo mambo haya yanayofanywa na baadhi ya viongozi bila uwoga wowote naomba tuchukue fursa hii kumpongeza sana kijana huyu.Nadiriki kusema nampongeza kijana huyu hasa kwa kauli zake nzito na za kijasiri kwa maslahi ya chama changu cha CCM ili chama kiendelee kupendwa na kuchaguliwa na watanzania.
Pia itakuwa si busara kama sitawapongeza vijana wangu katibu mkuu wa chama ndugu ABDULRAHMAN KINANA na NAPE NNAUYE kwa juhudi zao za dhati za kujenga chama na kuendelea kuwaeleza wananchi juu ya misingi bora ya chama cha mapinduzi (CCM)kwa kuwakemea viongozi wasiofaa bila kujali cheo na umaarufu wao ndani ya chama na serikali,nawaomba waendelee na juhudi zao hizo nami naziunga mkono juhudi zao na kama kuna watru wanaowabeza naomba wasijali kwani kukemea viongozi wasiofaa ndani ya chama na serikali ni msingi wa chama chochote kilichounda serikali.


Aidha nawaomba watanzania wenzangu wazalendo wasikubali kukatishwa tama na kikundi cha watu wachache wasio na mapenzi mema na taifa letu ambalo limekuwa mfano wa kuigwa kwa amani,upendo,utulivu na mshikamano urithi tulioachiwa na baba yetu wa taifa mwalimu julias kambarage nyerere ndani na nje ya mipaka ya bara letu la afrika.


Ndugu zangu waandishi wa habari naomba niwaambie kuwa msemaji wa UVCCM kijana wetu paul makonda namuunga mkono kwa kitendo chake cha ujasiri cha kumkemea ndugu EDWARD NGOYAI LOWASA bila uwoga kwa jinsi anavyokivuruga chama chetu kwa lengo la kutaka urais 2015 huku secretariet ya chama ikiwa imekaa kimya wakati inajua kuwa muda wa kuanza mbio hizi bado na kufanya hivi kwa sasa ni kukiuka misingi na katiba ya chama.hapa najiuliza kuwa ile misingi imara ya uongozi ndani ya chama chetu cha mapinduzi iko wapi?mpaka tumuachie mototo ndio akemee haya?je!hapa chama kiko wapi?


Ukweli ni kwamba wanachama wetu na vijana wamekuwa njia panda huku wakitamani kusikia tamko au karipio la chama juu ya suala hili la harakati za urais 2015 bila mafanikio.


Naomba niseme kuwa bila kuwa na karipio au tamko la chama, hawa wanaotumia pesa zao hadharani kwa lengo la kutafuta umaarufu na ushawishi kwa vijana ili kupata madaraka wanaharibu misingi yetu bora ya uongozi iliyowekwa na waasisi wetu ndani ya chama.


Kinachonisikitisha zaidi ni kuona juhudu za uongozi wa sasa wa chama ngazi ya juu ikiwa ni pamoja na sekretarieti inayoongozwa na katibu mkuu ABDULRAHMANI KINANA na katibu mwenezi NAPE NNAUYE za kutetea chama hiki zinatiwa mchanga.


Ninaomba juhudi hizi zisibezwe na watu wenye nia njema na chama.,ukweli ni kwamba vijana hawa wamekuwa na juhudi kubwa sana ya kujenga na kuimarisha chama chetu kwa wananchi kila pembe ya taifa letu kwa kukemea na kueleza misingi ya uongozi bora. swali:je! Chama hakioni haya mpaka vijana ndio waone?


Kwa hili ni lazima tubadilike ili kujenga chama chetu na naishauri secretariet ya chama lazima ichukue hatua mara moja,kijana huyu paul makonda asingesema haya yote kama hana uhakika wa ushahidi wa wa haya aliyoyasema na nampongeza sana.
[TABLE="width: 442"]
[TR]
[TD] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Mzee malecela akionesha moja ya vionjo vya safari[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Vijana na wanachama wengi wa CCM wamekuwa na hamu kwa muda mrefu ya kutaka kujua msimamo wa chama chao bila mafanikio na ndio sababu ya baadhi ya
wengine kupoteza mwelekeo.


Sisi tulikijenga chama hiki kwa taabu sana hapakuwa hata mtu mmoja aliyediriki kutumia fedha zake kutaka madaraka.nidhamu,busara na uchungu wa rasilimali za taifa hili kwa maslahi ya wananchi ndio vilituongoza kufuata misingi na maadili ya uongozi ndani ya chama na serikali,ndio maana tunaumia sana kuona chama sasa kinataka kutekwa na wenye fedha kwa uchu wa madaraka,mpaka tunashangaa na kujiuliza hizi pesa wanatoa wapi?na haya madaraka wanayotaka kwa kununua ni kwa maslahi ya nani?huku watanzania wakiendelea kuwa maskini.


Mfano hivi karibuni baadhi ya viongozi wa chama ngazi ya juu wamejibishana kwenye vyombo vya habari,vitendo hivi havina tija kwa chama na wala havileti umoja na mshikamano ambao umedumu ndani chama kwa muda mrefu.


Mwisho Ninaomba sekretarieti ichukue hatua haraka kama alivyoomba kijana wetu makonda na kweli kuchelewa kuchukua hatua jambo hili kumejionyesha wazi kwamba utaleta kutokuelewana ndani ya chama kusiko kuwa na lazima.
 
sasa mtu ambaye una facts zake za Richmond unamuonea aibu ya nini ? je uaminifu wake leo ukoje ? kwanini ? ndio maana mnaambiwa mmelipwa .
 
Back
Top Bottom