Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,115
- 35,124
Kwakuwa tumeanza kujibu hoja za Chadema basi tujibu zote ili tutoke kwenye wakati mgumu huu, maana wananchi kipindi hiki wanasikiliza wagombea wote na kupima hoja zao.
MOSI. Chadema kwa kupitia mgombea wao amekuja na hoja ya kutaka kufifisha kazi nzuri na kubwa iliyofanywa na serikali ya ccm katika miradi yote mikubwa ya kununua Ndege, Bwawa la Umeme na Treni ya SGR. Miradi hii yote ya maendeleo kwa kuwa haihakisi maendeleo ya watu ni bure tu. Kwani hata Wakoloni na Makaburu Africa Kusini wamefanya zaidi ya hayo yote, lakini kwa kushindwa kuwapa maendeleo watu wao walikataliwa na kupingwa. Chadema wakazungumzia mfano wa nchi ya Ethiopia wanayo yote hayo lakini wananchi wake wako tayari kufia kwenye Makontena au kwenye mitumbwi kwenda nchi nyingine kwa kuzamia kutafuta maendele. CCM tunatoa majibu mepesi tu. Hii hoja ijibiwe tusiahibike.
PILI. Chadema wamekuja na hoja ya kuwa na Majimbo kwa maana kuwa, kila sehemu (kwa maana ya mkoa na wilaya) waongozwe na viongozi waliochaguliwa na wananchi ili waweze kuwawajibisha. CCM tunajibu kwa hoja nyepesi kwamba wanataka kutugawa kwa kuwa tumechanganyika Makabila italeta ukabila. Tunasahau kwamba ua tunachagua Wabunge bila kujali hilo. Inahitajika hoja nzito kujibu hili sio jepesi kama hivyo.
TATU. Chadema wamezungumzia kuhusu wafanyakazi kutoongezwa kwa mishahara kwa kipindi chote cha miaka mitano na wanaahidi kuwalipa walicho kosa tena na riba. Sisi tunakuja na majibu mepesi kwamba tutaongeza, hii ni kama kumwambia mtoto usilie nitakununulia Pipi. Tutoe suluhisho la hili na jinsi tutakavyoaminika mbele ya wafanyakazi, la sivyo kura zao na wategemezi wao tutazikosa.
NNE . Chadema wametoa shutuma nzito kabisa kwamba Serikali ya ccm, imeua watu Kibiti, watu wameokotwa kwenye viroba baharini, watu wametekwa, watu wanafunguliwa Kesi kubwa kubwa bila hata hizo kesi kuendeshwa wanaozea magerezani mpaka ulipe Pesa ndiyo uachiwe na ufilisiwe. Pia mgombea wao Tundu Lissu anashutumu serikali kwamba ndiyo ilimpiga risasi na hamna hata mtu mmoja aliwahi kukamatwa, kunyimwa matibabu, kuvuliwa Ubunge na hila kama hizo. Haya yote hata hayajajibiwa au kukanushwa kabisa ina maana ni kweli serikali imeyafanya?. Kama tumeamua kujibu kila hoja hizi zisikae kimya bila kujibiwa.
TANO . Chadema wameelezea kwamba wafanya biashara wanafilisiwa na TRA kwa kukwapua pesa zao kwa njia ya Agency Notice kwenye Mabenki, na Biashara nyingi zimeumia na hiki tumekaa kimya. Je ukimya wetu ndiyo kukubali kwamba haya yanatendeka? Mimi ni kada tu sio mfanyabiashara je, kweli Wafanyabiashara wanafanyiwa hivyo? Au propaganda za Chadema? Tukikaa kimya tunawapa point bure kwa kuwa tunajibu hoja na hizi tuzijibu.
SITA. Chadema wanakuja na hoja ya kwamba NEC inawahujumu kwa mambo ya kishenzi hili tuliangalie maana kuna mambo mgombea wetu anavunja kabisa taratibu na NEC haisemi kitu lakini ikitokea kidogo Chadema wanajitokeza kujifanya wanafuatilia. Kwa hili niseme wazi NEC inaihujumu CCM kiaina. Ukimya wetu juu ya vitendo vya NEC unatugharimu mbele ya wananchi.
SABA . Chadema imekuja na hoja ya uwanja wa Ndege cha Chato. Kwa kweli Mgombea wetu jibu la kwamba nikifa sitazikwa nacho ni ya kuzalilisha nafasi aliyo nayo anayogombea ingawa hata Mjumbe wa nyumba kumi hasingeweza kujibu hivyo. Kweli tulishindwa hata kusema kwa ajili ya Utalii.
NANE. Chadema wamekuja na shutuma dhidi ya Rais kuwa amejimilikisha ardhi yenye ukubwa wa zaidi ya ekari 25000. Hili tukiliacha kulijibu vyema sasa litatugharimu sana, maana watu wameanza kuliamini hasa baada ya waziri wa ardhi kusema 'wakubwa' wamemilikishwa ardhi hizo kihalali.
Kabla hatuja ahidi nini tutafanya miaka mitano ijayo tuanze kwanza kuzijibu hizi hoja kwa kweli na uwazi ama sivyo tutakuwa na wakati mgumu kwa wapiga kura.
(Makala hii imeandikwa na Buzer Mpangale, mimi nimeinakili kutoka mtandao fulani na kuileta hapa JF)