binti ashura
Senior Member
- Jan 14, 2011
- 118
- 19
Ndugu zangu habarini za asubuhi!, mie nimekuwa nikifuatilia mwenendo mzima wa chama cha mapinduzi, nikaja gundua kuwa chama hiki sasa kinasimama kama kampuni ambalo lina wakurugenzi, na mameneja wakujitolea ambao ni wenyeviti kuanzia mikoani mpaka ngazi ya mtaa na mabarozi wa nyumba kumi (ingawa hiyo ya nyumba kumi ilishageuzwa siku nyingi mpaka sasa hakuna balozi anaesimamia nyumba kumi tu ila wanasimamia mpaka nyumba 70). mabalozi hao huwa wanathaminiwa wakati wa kampeni tu, ikipita hapo chama kinakuwa cha wakurugenzi tu. tena wale wenye hisa nyingi ndiyo wenye sauti kubwa (hii hainipi shida kwakuwa ni kawaida ya makampuni yote mwenye hisa nyingi ndiye mwenye sauti zaidi katika kampuni). kampuni lenyewe linaendeshwa kibepali wapo tayari watu wapate shida ilimradi wapate faida kubwa. ukiona umeanza kuipenda ccm ujue unaelekea kujengeka kuwa na moyo usiokuwa wa huruma kwako na hata kwa familia yako. naamini hata kama angefufuka leo Nyerere asinge jiunga na CCM. ninaushahidi wa kutosha kuwa asingejiunga CCM, tazama jana hata yule mzee ngombalemwilu ambaye alivaa na suti zile za kipindi kile cha ujamaa kuonyesha kuwa yeye ni mwanaujamaa safi, na alikuwa miongoni mwa waliohamishia taifa hili kwanye mfumo wa ubepari na Juzi tumemsikia akisema taifa lina shida ya viongozi (hapo si anashindwa tu kutoka). poleni sana wana ccm mnaoishi maisha ya unafiki, un..................., na uzandiki.