Wajumbe wa ngazi za chini licha ya kufanya yao na kuwapiga chini wahamiaji kutoka upinzani, kumbe waligeuzwa kuwa mabwege kwa kuwa viongozi wao walikuwa na yao mioyoni kwao. Wajumbe hawakujua kuwa biashara ilikwisha kufanyika na dau kupangwa.
CCM ya sasa si mali tena ya wanachama, bali ni mali ya Mwenyekiti Taifa. Kipaumbele kwa nafasi za uungozi na hata sifa za uwakilishi ni wahamiaji walionunuliwa kutoka upinzani, kujitenga kwa namna yoyote ile na timu Membe ama kufanya jitihada zenye kudhihirika za kutaka kuua upinzani, kutoa matusi kwa viongozi wa upinzani na juhudi za wazi ktk kudhoofisha upinzani hasa CDM.