CCM si baba yangu wala mama yangu - Sitta


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,095
Points
2,000
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,095 2,000
USAFI wa roho, mwili na kiakili aliouonyesha wazi, Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta, alipofanya mahojiano kwenye kipindi kimoja kinachorushwa na kituo maarufu cha televisheni hapa nchini unaonyesha maruweruwe.

Kwa wale waliobahatika kufuatilia kipindi hicho, Sitta atakuwa amewaachia Watanzania maswali mengi na hasa wasomi na wazalendo waliopaswa kumuona mtu mwenye sifa na tabia hizo akijiweka mbali na watu anaodai kuwa ni mafisadi wenye kutishia uhai wake na hasa wale wanaoendelea kumchafua kwa kuwa wanamiliki vyombo vya habari.

Kwa mtu kama Sitta na namna alivyoweza kujipambanua kwa kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya serikali na bado ni Waziri mwenye dhamana upande wa jumuiya ya Afrika mashariki, ameyasema mengi alipokuwa akihojiwa na kituo hicho akiwa na sura za aina mbili.

Kwanza naweza kusema, Mheshimiwa msomi, Samuel Sitta, kwa kuwa ni mwanasheria amejaribu sana kueleza yale yaliyomsibu katika maisha yake yote baada ya kuamua kujiingiza kwenye siasa bila kujua kuwa sheria na siasa ni vitu viwili tofauti kwenye siasa hakuna msumeno huko kuna maneno yanayogeuka kila siku kutokana na upepo wa kisiasa.

Kwa kutambua kuwa kaingia kwenye siasa, kwenye kundi la watu wanaoweza kujenga majungu, chuki, kutishana na ikiwezekana kabisa wengine wamepoteza maisha kwa ajili ya siasa na hatua hiyo ya kupotezeana uhai ndiyo inayotishia zaidi mlolongo wa wanasiasa wanaojipambanua kuwa ni wapambanaji.

Ili kuweza kutoa madukuduku yaliyosibu, Sitta kwa muda wote na hadi alipofikia uamuzi wa kutapika machache aliyokuwa nayo, ameweza kutumia sana mbinu za kisheria kuficha ukweli wa mambo mengi ya msingi ambayo ameyaacha moyoni kwake licha ya kudai kuwa kwa muda mrefu ameumizwa sana na wanasiasa wenzake lakini hawezi kutoka ndani ya kundi linalomtafuna.

Shaka na hofu ilisimama katika ndimi za Sitta, ulifika wakati alitaka kusema yote yaliyomsibu na pengine kuwataja wale wanaomkosesha furaha katika maisha yake kwa kumsakama na vitisho visivyo kwisha hadi anapofikia uamuzi wa kubadili kila wakati namba za simu zake ili kukwepa vitisho hapo anamaanisha kuwa kwa kiasi kikubwa anafaa uso wa hofu na shaka ya kuuawa.

Kwa kuwa Sitta ni binadamu kama walivyo wengine kwa namna moja au nyingine naweza kusema hakujua siasa zilivyo ndio maana anadiriki kujutia pengine uamuzi wake mbaya wa kujiingiza kwenye siasa chafu, siasa ambazo kwa kiasi kikubwa hazijaonyesha sana kuikomboa nchi masikini bali zimekuwa siasa za kukomoana.

Anadiriki kusema kuwa chama cha siasa alichojiunga nacho tangu ujana wake, akitokea TANU na kujikuta akiwa mmoja wa waasisi wa CCM pamoja na sifa hizo anakosa faraja na kukosa furaha maridhawa kwa kuwa haoni kukua kwa siasa bora kama huko nyuma alikotoka, sasa anashuhudia siasa chafu, za makundi na zilizobebwa na nguvu za wenye fedha.

Anasema kuwa CCM si baba yake wala mama yake na kwamba endapo utafika wakati ambao uvumilivu utamshinda ataamua kitu cha kufanya, hapo ndipo ninapoanza kuona ndoto anazoota na naanza kuona kuwa kiongozi huyu mzoefu wa siasa na sheria ametumwa kusema hayo au amejituma ?

Kama anaota au kajituma na kutamka wazi kuwa CCM si baba yake wala mama yake ni wazi kuwa kauli hiyo ya dhati kutoka kwenye moyo wa mtu makini, mwenye utu na akili timamu alipaswa kujua kuwa CCM sio baba yake wala mama yake miaka mingi na alipaswa kuchukua uamuzi wa kutengana na nguvu za mafisadi mapema.

Kama nguvu za mafisadi, sitta anazijua kuwa ndizo hizo hizo zilizomnyima nafasi ya kuendelea na uspika na akaukubali uwaziri itakuwaje awe ndani ya kundi hilo hilo analodai kuwa wamekuwa wanatumia nguvu za fedha kuingia kwenye siasa na kama anawafahamu hao na hakuweza kuwataja kuwa ndio wanaoongoza mfumo wa kisiasa na pengine ndio waasisi wa ufisadi itakuwaje awatumikie ?

Sasa acha niseme kuwa, Sitta anayo mengi moyoni mwake, amesema machache kwa kuwa hana ujasiri wa kulilia kifo huku akiwaona wenzake aliokuwa akiwafahamu kwa ujasiri wao wamekwisha kutangulia mbele ya haki, vitisho anavyo viogopa na kumfanya abadili kila wakati namba za simu ni ishara kwamba anaogopa kifo ambacho siku ikifika lazima kitamkamata, iwe kwa mambo ya siasa au kwa uweza wa Mungu.

Kama hayo yapo lazima wanasiasa wenye tabia kama za kina Sitta wanapaswa kuonyesha zaidi uzalendo wao katika nchi hii maskini kuliko kila mmoja akisema yake kuhusu hali ya kisiasa na nguvu za mafisadi jinsi zinavyoongoza nchi kama vile hakuna wasomi na watu makini wanaoweza kuthubutu kuleta mabadiliko makubwa ya kisiasa na kiuchumi.

Kila mwana siasa aliyeshika madaraka makubwa serikalini wamebaki kulalamika tu, huku wakijua kuwa CCM wanayoilalamikia kwa siasa chafu na msimamo wao wa kuvuana gamba bado hakutibu majeraha ya kisiasa wanayokumbana nayo kina Sitta na wenzake ambao wanadhani kuwa wanapigania wananchi kumbe wanajipigania wenyewe.

Kwa kuwa Tanzania ni nchi yenye mfumo wa vyama vingi vya siasa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alishawahi kusema katika uhai wake kuwa kiongozi mzuri atakayoweza kuiondoa CCM madarakani lazima atoke kwenye chama hicho na kujiunga na vyama vingine vya upinzani, kama si leo basi wakati ukifika itakuwa hivyo.

Mazingira hayo ndiyo yanayotia mashaka na kuonyesha mahali ulipo uadilifu wa viongozi wanaolalamika kwa kudhani kuwa CCM ni baba yao na mama yao, kumbe kwa upande mwingine wapo wanasiasa wanaothubutu kusema wazi kuwa chama hicho hakiwezi kulinganishwa na wazazi wa mtu, lazima sasa watu wajenge utashi wa kizalendo kuliko itikadi ya vyama vyao kunakowatafuna kila siku.

Kuthubutu kwa Sitta na kutamka wazi kuwa amekuwa akifuatwa na wanasiasa wenzake kutoka kambi ya upinzani wakimshawishi atoke kwenye chama hicho kwa kuwa hakiendani na msimamo wake lakini amekuwa akiwakatalia bado hapo kunatia mashaka kuwa anachokisema na kutaka kuwathibitishia wananchi si hoja ya kuondoka CCM isipokuwa ni hofu ya kifo anayotishiwa na mafisadi.

Ukweli unabaki pale pale kuwa Sitta ana kila sababu ya kutaka kuondoka na kujitenga na kundi la mafisadi na anajua fika kuwa moyoni mwake anapenda kujiunga na chama kipi kingine cha siasa lakini anaogopa kwa kuwa ndani ya CCM na serikali yake ana kinga kubwa juu ya usalama wake na familia yake kuliko kama atatoka nje na kuiacha CCM kwa kuwa idadi ya maadui zake itaongezeka na nguvu ya kinga itapungua.

Kama Sitta ni jasiri na ameweza kuthubutu kwa ujanja wa kisheria kusema mengi kwa mafumbo na pengine hakuweza kumsema wazi hata kiongozi wa nchi aliyempa uwaziri, alitumia muda huo kumsifia badala ya kuweka wazi dhamira yake hadharani kuwa kundi linalompotosha kiongozi wa n chi asiweze kufanya kazi zake vizuri ni hili.

Katika mahojiano hayo ambayo naamini watu wengi walikuwa na hamu ya kutaka kusikia mambo mengi na mapya yakitamkwa hakuweza kuondoa kiu ya wasikilizaji kwa muda wote, wapo waliomuona kuwa ni jasiri na wapo waliomuona kuwa ni mwoga na kwa namna yoyote ile naweza kusema kuwa kitendo cha kuendelea kulalamika kwenye chama ambacho dhahiri anaona kuwa kimekosa mwelekeo na yeye akabaki ndani hana uzalendo kabisa.

Hana uzalendo kwa kuwa angekuwa na dhamira ya kweli, uzalendo alionao angeutumia mapema, muda unazidi kwenda na hali ya chama chake inazidi kuwa mbaya na mashaka hayo aliyoonyesha angesema wazi kama ambavyo mmoja wa waasisi wa chama hicho alitamka wazi kuwa "CCM imekosa dira na mwelekeo" sijui mahali alipo huyo kada, kama yupo hai au katangulia mbele ya haki, basi Sitta asiongope kwa kuwa anajua fika kuwa kila mtu ipo siku atakufa tu.

Kifo cha ushujaa ni furaha kuliko kufa kifo cha dhambi na kwa kuwa Sitta amejipambanua kuwa haishi kwa nguvu za mafisadi, hakuupata uongozi wake kwa nguvu za fedha na amekuwa akiishi kwa mshahara wake na marupurupu mengine halali basi sasa anapaswa kuwapigania wananchi wote na si kuipigania CCM ambayo si baba yake wala mama yake, huo muda anaousubiri atawaambia nini Watanzania akiukosa ?

 
Last edited by a moderator:
Alfred Daud Pigangoma

Alfred Daud Pigangoma

Verified Member
Joined
Mar 30, 2009
Messages
1,792
Points
1,250
Alfred Daud Pigangoma

Alfred Daud Pigangoma

Verified Member
Joined Mar 30, 2009
1,792 1,250
Kinyang'io cha urais kitawaua!! Naona pro-6 umejipambanua kumpamba asiyepambika. Subiri wale vijana wanaoshinda pale Lumumba wakiwania posho za upambe waje ndo utajuta kwani mtu wao sio huyo uliyempigia malimba.
 
H

Honolulu

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Messages
5,649
Points
1,225
H

Honolulu

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2012
5,649 1,225
Unafiki mtupu!! Hakuna aliye safi ndani ya CCM!!!
 
N

Newcastle

Senior Member
Joined
Oct 11, 2012
Messages
142
Points
170
N

Newcastle

Senior Member
Joined Oct 11, 2012
142 170
6ta nyamaza umesahau ya Kolimba?au hamia ccj
 
Fpam

Fpam

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Messages
290
Points
0
Fpam

Fpam

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2011
290 0
huyu mzee 6 anazeeka vibaya ukiona mtu kadiri umri unavyoenda anakuwa manafiki na porojo nyingi kama yupo na wajukuu zake wake anawasimulia hadithi wakati anajua anaongelea hatima ya maisha ya watu ujue mwisho umefika

makaburi ya hawa watu yakuja kuchapwa sana viboko
 
Z

Zimamoto

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2012
Messages
464
Points
195
Z

Zimamoto

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2012
464 195
Tatizo la Sitta kila kukicha anapoteza ujasiri aliodhaniwa kuwa nao.
 
MANGUNGO

MANGUNGO

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Messages
1,538
Points
1,170
MANGUNGO

MANGUNGO

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2011
1,538 1,170
6 mnafiki,alianza kupambana na gazeti la Mwana Halisi,akaanza kuishusha hadhi chadema wapambanaji wa ufisadi wa ukweli,akaanza mapambano na Dr.Slaa lakini mwisho wa siku zote yule anaepambana na chadema au Dr.Slaa uishia shimoni kama Shekh YAYA
 
brasy coco

brasy coco

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2012
Messages
1,457
Points
2,000
brasy coco

brasy coco

JF-Expert Member
Joined Apr 25, 2012
1,457 2,000
Unafiki mtupu!! Hakuna aliye safi ndani ya CCM!!!
si kweli kabisa, katika Gamilia ya watu wabaya yupo aliye mzuri ila uwezi kumuona 7bu amezungukwa na wabaya hata akisena ya kweli utasema mnafiki, kwa kujua hilo ndomana Nyerere akasema Kiongozi atakayeitoa CCm madarakani atatoka ndani ya CCm kwa maana ndani ya CCM wapo walio na moyo wa Dhati na Nchi hii lakini wamebanwa.
So siwezi kutamka Sitta mnafiki, sitta amesaidia kuwapa Uhuru wabunge mpaka ishu nyingi za Ufisadi zimetoka kipindi chake sio huyu bibi kidude alieyekuwepo sasa, Sitta anaitakia Heri TZ cha msingi ni kuwepa Njia sahihi yeye peke yake awezi hakuna asiyeitaka Pumzi jaman hata kama kufa kishujaa ni bora zaidi lakini Dunia ni tamu
 
K

KYALUMUKUNZA

Senior Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
145
Points
0
K

KYALUMUKUNZA

Senior Member
Joined Aug 19, 2012
145 0
6 mnafiki,alianza kupambana na gazeti la Mwana Halisi,akaanza kuishusha hadhi chadema wapambanaji wa ufisadi wa ukweli,akaanza mapambano na Dr.Slaa lakini mwisho wa siku zote yule anaepambana na chadema au Dr.Slaa uishia shimoni kama Shekh YAYA
wapo wengi tu hata kina KADINALI KALAMBWA.
 
N

Ngandema Bwila

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2010
Messages
999
Points
1,195
N

Ngandema Bwila

JF-Expert Member
Joined Sep 8, 2010
999 1,195
6 tangu alipotajwa kuwa ni miongoni mwa waasisi wa CCJ amekuwa kama kinyonga hatabiriki, amekuwa kama farasi anaenda mwendo wakasi lakini hajui anaenda wapi kama yule prof wa The commedy ya TBC1.
 
bushman

bushman

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
2,392
Points
1,250
bushman

bushman

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
2,392 1,250
samweli sitta ni kama mfugaji hadhaminiki leo ccm,kesho ccj keshokutwaa,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,!!!!!!!!!!!!!!!
 
MARCKO

MARCKO

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Messages
2,262
Points
0
MARCKO

MARCKO

JF-Expert Member
Joined Jun 10, 2011
2,262 0
6 akianza kumsakama Dr. Slaa , hutadhani ndio huyu anaehitaji huruma kama Kinda la ndege!
 
sifongo

sifongo

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2011
Messages
4,801
Points
2,000
sifongo

sifongo

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2011
4,801 2,000
huyu mzee 6 anazeeka vibaya ukiona mtu kadiri umri unavyoenda anakuwa manafiki na porojo nyingi kama yupo na wajukuu zake wake anawasimulia hadithi wakati anajua anaongelea hatima ya maisha ya watu ujue mwisho umefika

makaburi ya hawa watu yakuja kuchapwa sana viboko
Mkuu sio viboko tu, unakojolea kabisa juu ili liwe linanuka muda wote.
 
sifongo

sifongo

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2011
Messages
4,801
Points
2,000
sifongo

sifongo

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2011
4,801 2,000
Mr 6 alipata nafasi nzuri sana ya kuwamaliza mafisadi alipokuwa spika akajifanya anaremba sasa jua linamuwakia atakoma, lakini ni kheri kwetu wananchi wa kawaida tunapata nafasi ya kujua unafiki wao.......kama si makundi ndani ya chama mengi tusingeyajua.
 

Forum statistics

Threads 1,296,008
Members 498,495
Posts 31,230,509
Top