CCM si baba yangu wala mama yangu - Sitta

CCM si baba yangu wala mama yangu - Sitta

Kama kiongozi wa kuiondoa CCM madarakani atatoka ndani ya CCM basi ufisadi hautakufa ni donda ndugu. Sipendi kabisa kusikia mtu anajifanya anauchungu na Watanzania wakati huko aliko kunavunda kwa rushwa. Zitto kapata wapi amjina ya hawa wenye mabilioni huko Uswiss wakati watuhumiwa wenyewe ni wenzenu huko CCM, kama kweli mnauchungu na sisi wananchi basi saidieni kumpa Bw Mkuchika majina ya wahusika. Mbona mnanyamaza kwa zamu mkisubiri Zitto eti awataje halafu mjifanye kupiga kelele kana kwamba nyie ndiye mliyegundua hayo.
Zitto pekee namuona kuwa kweli kijana anauchungu na maisha duni ya sisi wananchi wakati kuna wachache wamejilimbikizia mabilioni yetu nje ya nchi tena kwa siri. Kwa hili ndiyo maana sipendi kabisa URAIA WA NCHI MBILI.
 
Naukumbuka wimbo mzuri wa Kihehe,
"Nige nene ngwalala, nige nene ngwalala, nige nene ngwalala ngwalala baba singumuwona x2
Ngwenda bee, Ee ngwenda ndimuwonage X2

MAANA YA WIMBO KIMAELEZO:

Jamaa analia kwa kufiwa na baba yake anasema "hakika mimi namtafuta baba yangu kwasababu napenda niwe namuona muda wote lakini, simuoni"

Mytake:
Watanzania wengi sasa hivi tunamkumbuka Baba wa Taifa, hata hao wanaotudanganya na kupaa mabegani mwetu kisha wanaanza kuchuma utajiri wetu na kuupeleka nje ya nchi wanajitahidi sana kutumia jina la Baba wa Taifa kupata kura zetu. Tuanze sasa kuwaogopa hawa jamaa kama ukoma. Wamekuwa wakijiita ni matajiri wa watu na kamwe hawawezi kufilisika hii ni kutukejeli sisi masikini. Tafisri ya kauli ya Lowassa kuwa yeye si tajiri wa fedha bali watu ni kwamba katufanya sisi ni rasilimali kwa ajili yake binafsi. Kwa maana nyingine kwa tafsiri ya kiingereza anasema "We are his property thus he will never get poor, our existence is his wealth our disappearence is poverty and of course never shall we see his povery for we are dead."
 
wakuu huyu waziri wa af.mashariki amekua hasikiki hata ktk kazi zake za uwaziri,licha kutajwa ktk makundi ya wasaka urais wa ccm 2015.naomba mwenye kujua aliko huyu mheshimiwa atujuze..
 
nimemuona itv akiongolea ujenzi wa Reli ya EAC,utazani alikuwa amejaza makande mdomoni.
 
Alifanya kazi nzuri saana akiwa Spika ila kwa sasa kadri siku zinavyoenda heshima yake inazidi kushuka anaweza kuwa yupo vizuri kidogo ila msafara alionao ndio unamchafua
 
Back
Top Bottom