Elections 2010 CCM sasa yadai JK hakukataa kura za wafanyakazi

lazima kieleweke, tunahitaji maelezo ya kina, maana tambwe hujatuconvince bado-jaribu tena, mimi ckubaliani na wewe
 
Ile event imesikitisha watu wengi, sana sana

Sio imesikitisha imewaudhi wengi sana. Kwanza wafanyakazi ndio wanaoendesha nchi. Pili kusema kuwa serikali haina uwezo wakati mafile wanayapitisha kwa wafanyakazi wa chini wanaona kila kitu ndio mzaha kwani ni sawa na kumwambia mfanyakazi wa benki kuwa benki haina hela wakati anasimamia hela. Tatu kutwambia kuwa kama hahitaji kura zetu ni dharau kana kwamba wafanyakazi wanajipendekeza kwa bwana mkubwa. Anasahau muheshimiwa rais wafanyakazi wa serikalini au private ndio wanamuwezesha kutawala kwa ufanisi na amani.
 
Ukirejea kauli ya JK utagundua wengi hawajamwelewa..nasema hivyo coz kuna tofauti kati ya kusema "Sitaki kura zenu" na "niko radhi kuzikosa kura zenu...kuliko kuwaahidi kitu kisichotelekezeka". nadhani kuna mapungufu makubwa kwenye kutafsiri kauli hizi hasa zinapotolewa na kiongozi wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi hivyo kufanya wote tutafsiri na kufikiri on that perspective...tuutazame ukweli na tusiendeshwe na watu wenye nia zao kama Mgaya...kwani nionavyo mimi JK hajakataa kura ila ameonesha msimamo kuwa kama kura zitatumika kumhukumu basi sawa yuko radhi kuzikosa kuliko kuwaahidi kitu watakachomhukumu nacho wakimchagua kwa kuwa aliwaahidi..
so let see this on that perspective na tusihukumu kwa itikadi za kisiasa kwani inaonekana kauli hiyo itatumika sana kujaribu kumnyima kura JK but naogopa haina mashiko sana kuweza kumshawishi mtu timamu asie na ushabiki wa kichama kuiamini kama akiichambua ila kwa kuwa tumezoea kuambiwa fanya hivi fanya vile basi hata kauli hii tutashindwa kuichambua mantiki yake na kujikuta tukipoteza muda kuijadili na kuijengea hoja kama mtaji wa kuing'oa CCM ambalo kwa mtazamo wangu si option nzuri coz hakuna mtu anaewania urais akakataa kura za kundi fulani kwa hiyo Tambwe katumwa kuuelewesha umma ila kwakuwa umma umeshalishwa majibu basi ufafanuzi wowote hautasaidia ila nadhani iko haja ya kupembua haya mambo kwa umakini kwani tumeona pale ambapo watu hudhani wamefanikiwa kudhoofisha mpinzani wake basi hurelax na kujikuta akishindwa analia kuibiwa kura na rafu kadha wa kadha.
Tuambiane ukweli kwenye hili, ushabiki hautusaidii kurekebisha mambo ila kuusema ukweli na kuacha kuwalisha wananchi wasioelewa siasa zinaendaje maneno na mifano ambayo mchambuzi makini wa mambo hawezi kushawishika nayo..
wito wangu ni kuwa wakweli na tutumie busara kwenye yale ya msingi kwani ni busara tu ndio itamfanya mtu achague kiongozi bora na si maneno ya magazeti na mitandao ambayo mengine yana unazi wa vyama fulani hivyo iko haja kuchambua kila tunalosikia na kusoma.
 
JK hajakataa kura ila ameonesha msimamo kuwa kama kura zitatumika kumhukumu basi sawa yuko radhi kuzikosa kuliko kuwaahidi kitu watakachomhukumu nacho wakimchagua kwa kuwa aliwaahidi..

Unajua maana ya kuwa radhi kuzikosa? unasema kama kura zitatumika kumhukumu(unajua makosa yake eenh)... Atahukumiwa tu kwa udhalimu wake na serikali kiujumla!...

Usimtetee, nia na maana haswa ya kauli ni kuwa ahitaji kura za wafanyakazi sababu serikali yake yenye MASHANGINGI na MAFEDHULI wala rushwa HAINA PESA za kuwalipa wafanyakazi wanaohangaika kila siku kulisogeza gurudumu la maendeleo...!! Usiweke ushabiki hapa
 
Tambwe Hiza CV yako ya SIASA hii hapa...Kugumbea ubunge
1995-NCCR MAGEUZI(Looser to Kihiyo)
1996-NCCR MAGEUZI(Cowardice by allowing Mrema to run)
2000-TLP(Looser to Hadija Kusaga)
2005-CUF(Looser to Zubeir Mtemvu)
2010-CCM(Looser to Zubeir Mtemvu again...damn in primaries!!!With your very uncle Makamba looking...argh)
2015-JAIL TERM FOR ADVOCATING FOR FISADIS!!!!!!!

lost to Kihiyo.....a fraud guy? that is funny.
Lost to Mtemvu in CUF primairies
and again to the same guy in CCM, what was he thinking before running, didn't he know the outcome?
 
Hii inaonyesha ile hotuba Tambwe alishiriki kuiandika...

Wala si kwamba alishiriki, ni kujikomba huko si unajuwa tena kitumbua kitamu. Ingekuwa Kiranja alitumia lugha ya ishara kungekua na fursa ya kila mmoja kutafsiri lakini yalitumika maneno ya kiswahili ambayo yanaeleweka na kila mtanzania.
 
Its amasing !!! .....

Rais na serekali yake wamekaa kimya kama kawaida .... ikimaanisha wankubaliana kabisa na walichofanya ...

LAKINI

mtu mwingine ana bwabwajika kumpinga Rais wake mtukufu na Serekali yake ambayo for sure haizihitaji hizo kura za wafanyakazi ...

Tambwe ..work up!!

Heshemu wakubwa wako na serekali yako vinginevyo utatimuliwa kazi!!
 
Back
Top Bottom