Ndugu wanaJF, kwa hali inavyojionesha CCM inahaha sana mbunge au diwani wake akijiuzuru au akifa maana hakuna uhakika tena wa kuchaguliwa mbunge au diwani wa chama hicho. Hebu angalia nguvu iliyotumika huko Igunga - kupeleka rais mstaafu, mawaziri... Ni wazi watu wamekichoka chama hiki tawala na wanataka chama kingine kiingie madarakani. Chadema kinaonekana kuwavutia wengi na bila shaka mwisho wa CCM unakaribia ili kije chama kitakacholeta mabadiliko ya kweli katika maisha ya Watanzania. Chama tawala kimeleta mapinduzi kutoka chama cha wakulima na wafanyakazi kuwa chama cha matajiri na mafisadi kwa kutumia ujinga na umaskini wa Watanzania walio wengi. Ndiyo maana sehemu nyingi ambazo wananchi wameelimika au kupata mwanga zaidi, CCM haina nguvu tena, nguvu yao imebakia kule ambako wananachi ni rahisi kuwadanganya na wakadanyika na kuwatumia tu kisiasa.