CCM sasa inahaha mbuge au diwani wake akijiuzuru au akifa!

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,619
2,567
Ndugu wanaJF, kwa hali inavyojionesha CCM inahaha sana mbunge au diwani wake akijiuzuru au akifa maana hakuna uhakika tena wa kuchaguliwa mbunge au diwani wa chama hicho. Hebu angalia nguvu iliyotumika huko Igunga - kupeleka rais mstaafu, mawaziri... Ni wazi watu wamekichoka chama hiki tawala na wanataka chama kingine kiingie madarakani. Chadema kinaonekana kuwavutia wengi na bila shaka mwisho wa CCM unakaribia ili kije chama kitakacholeta mabadiliko ya kweli katika maisha ya Watanzania. Chama tawala kimeleta mapinduzi kutoka chama cha wakulima na wafanyakazi kuwa chama cha matajiri na mafisadi kwa kutumia ujinga na umaskini wa Watanzania walio wengi. Ndiyo maana sehemu nyingi ambazo wananchi wameelimika au kupata mwanga zaidi, CCM haina nguvu tena, nguvu yao imebakia kule ambako wananachi ni rahisi kuwadanganya na wakadanyika na kuwatumia tu kisiasa.
 
Aisee nikweli kabisa, CCM inazidi kuchoka, kwani ikitokea majimbo zaidi ya mawili yakihitaji uchanguzi kwa wakati mmoja sijui nini kitatokea, kwani wastaafu wote hawatopatikana kwa pamoja ati. CDM pigeni bao mambo mazuri yaja.
 
Sasa akijiuzuru mwingine ndio CDM inafilisika kabisa, hakuna cha helikopta tena, mtapanda punda kama Lipumba na mlishaambiwa punda kwenye lami ni kuvunja sheria.

Au mnataka Mbowe auze nyumba?
 
itahaha vipi wakati maghala yamejaa mahindi nchi nzima? mwaga uchaguzi mwingine uone kazi.
 
Sasa akijiuzuru mwingine ndio CDM inafilisika kabisa, hakuna cha helikopta tena, mtapanda punda kama Lipumba na mlishaambiwa punda kwenye lami ni kuvunja sheria.

Au mnataka Mbowe auze nyumba?
mtatukopesha hela za Dowans mkishalipwa.
 
Sasa akijiuzuru mwingine ndio CDM inafilisika kabisa, hakuna cha helikopta tena, mtapanda punda kama Lipumba na mlishaambiwa punda kwenye lami ni kuvunja sheria.

Au mnataka Mbowe auze nyumba?

wewe kweli ni wa jikoni au chumbani .Chadema siku zote na chaguzi zote wanaruka angani wakiwa hawana wabunge na leo wanapesa na wabunge ndiyo wakose pesa ? Chadema wana own helikopta kumbuka hawakodishi au ulikuwa hujui hili ?
 
Hiyo helikopta inatumia chibuku? Kweli wewe ni punguani. Unajua kuwa moshi mzima inamdai hela Mbowe kutokana na huu uchaguzi? Huoni kama huyo dingi zimeshoti?
 
Naunga mkono hoja kw asilimia 100% Peoplessssssssssssssssssssss......power!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hicho ni kinyume. Hivi nani aliyetumia nguvu kubwa. Kulikuwa na wabunge wangapi wa CDM na kila kiongozi wa magwanda alikuwa huko Igunga. Kutembeza kichapo na vitendo lukuki vya ukatili na uhalifu.
 
Sio tu walimtumia Rais Mstaafu bali hata Katibu Mkuu Mstaafu waliyekuwa wamemweka kando kabisa! Walitumia mbinu za kijinga kma udini na yule Mama asiye na aibu aliyejifanya Mwislamu. Wakasingizia CDM wana fujo na wakawachokoza kila kukicha. Ingekuwa aibu kuu kama CCM wangeshindwa! Wana-Igunga waliwaonea aibu wakawapa ushindi kiduchu! Lakini sitarajia huruma kama hii tena mahali pengine.
 
Sasa akijiuzuru mwingine ndio CDM inafilisika kabisa, hakuna cha helikopta tena, mtapanda punda kama Lipumba na mlishaambiwa punda kwenye lami ni kuvunja sheria.

Au mnataka Mbowe auze nyumba?

cdm wanamiliki helkopta ccm wanakodi wa kufilisika na ccm.cdm wao ni kujaza mafuta 2
 
Hicho ni kinyume. Hivi nani aliyetumia nguvu kubwa. Kulikuwa na wabunge wangapi wa CDM na kila kiongozi wa magwanda alikuwa huko Igunga. Kutembeza kichapo na vitendo lukuki vya ukatili na uhalifu.

Kwa maoni yangu CCM A na B walitumia nguvu zaidi na kusaidiwa na Bakwata na magazeti yanayojiita "Sauti ya Waislamu". CCM B walidai Chadema haijakomaa kisiasa na baada ya kusma hivyo wameangukia pua!
 
cdm wanamiliki helkopta ccm wanakodi wa kufilisika na ccm.cdm wao ni kujaza mafuta 2

kama wanamiliki helkopta ni vizuri ila nawashauri wajenge na ofisi dar na huko mikoani maana ni aibu. ushauri tu
 
Vyama vyote vimetumia nguvu nyingi, tusidanganyane na kupeana matumaini yasiyo na maana.
Kwa wananchi hawa hata wabunge wote wa ccm wakijiuzulu, bado ccm watatetea viti vyao.
Tusifanye imagnation kama za Igunga.
 
Kwa mjibu wa NAPE mafisadi wote lazima wajivue Magamba ndani ya CCM hivyo tunasubiri Uchaguzi wa Monduli, Bariadi etc Vyama vya upinzani viendelee kujipanga
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom