Kampeni za kuing'oa CCM hata 2025 zipo pale pale, ipo siku watang'oka tu!

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,930
3,803
Mifano ni mingi sana kutoka sehemu mbalimbali za dunia, wangapi walivuma na kujiona ndio wao tu, mbona wameondoka tena wengine kwa aibu. Mimi sio mtu wa siasa wala sina kadi ya chama chochote ni mpenda mpira na kuangalia mechi katika medani ya siasa.

Nipo huru kifikra kwa hio naweza kushangiria chama chochote,mtu au kiongozi yeyote,sema huwaga sipendi kuwa upande wa chama tawala,yaani CCM ikianguka leo mimi nitakuwa upande wao kwa hali na mali. Ndio natamani ishindwe ili nijiunge nayo.

Ni kuanzia sasa Chama kikuu cha upinzani kianzishe harakati za kudai Tume mpya ya uchaguzi isiyofungamana na upande wowote, tena madai haya yawe ndani ya nchi na pia yakuzwe kimataifa.

Tunahitaji uwanja wa kupata Chama tawala uwepo huru, hizi tabia za kuiba matokeo, kuyabadilisha kuuwana kisa kupata nafasi iwe ya mbunge, udiwani uraisi au uchama sio hulka zetu waTanzania wala sio tabia zetu ni mambo mabaya tuliyoyaiga. Kubwa ni kule kufanya ubunge, udiwani uraisi kuwa biashara, ukiukwaa ubunge inakuwa umetoka kimaisha,pale bungeni ukigonga meza tu inatosha na kuunga mkono liwe baya au zuri halikuhusu just kila kikao unapokea donge nono na posho kedekede.

Ikipatikana tume huru hata wananchi watakuwa na faida na kura yake anajuwa mbunge au diwani akiwa mzinguaji wanaweza kumuondosha au kuchagua chama kingine, lakini leo hii kura ya mwananchi haina faida hata chembe, ipo ipo tu.

Yaani kila mtu sasa ajipange kuiondoa CCM hapo 2025. ila mtu tuone kama haitaondoka.
 
Bila Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi.,hayo yoote uliyoyaandika ni sawa na kuandika sifuri juu ya maji ndugu
 
kwa kampeni za ki chadema za kigaidi gaidi, hamtafanikiwa kabisa.Watanzania wamewashtukia sasa chama cha upinzani cha kizalendo ni ACT Wazalendo
 
Nadhani utakuwa unaishi sayari nyingine umevamia tu hii sayari ya dunia earth
 
Siamini kama CCM ni tatizo, naamini watu ndo tatizo.
 
Je! Tukiwa na tume huru na bado CCM ikashinda itakuwaje? Maana ninavyo ona Tanzania tunaelekea kuwa kama China! Yaani CCM inakuwa na nguvu na utajiri sana kiasi vyama vingine vinadhoofika. Vinadhoofishwa na umasikini wa pesa, hivyo vitabaki nyuma hata tume ikiwa huru. Tume huru haigawii vyama hela!
 
Je! Tukiwa na tume huru na bado CCM ikashinda itakuwaje? Maana ninavyo ona Tanzania tunaelekea kuwa kama China! Yaani CCM inakuwa na nguvu na utajiri sana kiasi vyama vingine vinadhoofika. Vinadhoofishwa na umasikini wa pesa, hivyo vitabaki nyuma hata tume ikiwa huru. Tume huru haigawii vyama hela!
nani alikuwa tajiri kuliko Gadafi ,mwanafunzi unaenda kusoma majuu unanunuliwa na gari huko huko shule,wangapi wameanguka itakuwa CCM,zidi kufikiria kwa kina ,unajua ikifika wakati hakutakuwa na wakurudi nyuma si viongozi ndani ya ccm,si viongozi ndani ya jeshi si viongozi ndani ya polisi ,.

Muhimu ni kuwepo kwa tume huru tu kila mmoja akaridhika nayo,si unaziona mechi za mpia wanaridhika na refa hata kama atapatiwa chauchau lakini kuna upeo kuwa mechi ilikuwa huru na matokeo hayana upingwaji.

Tupate tume huru tuijenge Tanzania kwa pamoja kuliko hivi sasa huyu ccm yule chadema huko kwenye maendeleo hawaendi hivyo.

Nina wasi wasi hata Zanzibar watatushinda na kutuacha njiani,tunaona wanavyokabiliana na mawimbi na dhoruba lakini hawajakata tamaa wamo ndani tena.

Huku Tanganyika bado tunaona ukiiba ndio unakuwa shujaa ,wakati unajua siku za mwizi ni arubaini. Waungwana jitahidini tupate tume iliyo huru tuijenge Tanganyika yetu.

Roho inaniuma sana pale waZanzibari wanaposema tuijenge Zanzibar yetu.
 
Je! Tukiwa na tume huru na bado CCM ikashinda itakuwaje? Maana ninavyo ona Tanzania tunaelekea kuwa kama China! Yaani CCM inakuwa na nguvu na utajiri sana kiasi vyama vingine vinadhoofika. Vinadhoofishwa na umasikini wa pesa, hivyo vitabaki nyuma hata tume ikiwa huru. Tume huru haigawii vyama hela!
Haya ni mawazo ya kusubiri chakula, watu wale waondokwe.

Kwa mfumo wa kuendesha mambo wa kibinadamu, kundi au mtu yeyote aanzishae jumuia, shiirika ndio huwa anapewa upendeleo na waajiriwa na mara nyingi bila kuomba.

Kwa magwiji kama US wame shindwa kutengeneza Mahakama kuu (Supreme Court of United States ) ambayo inatakiwa isiwe na upendeleo katika maamuzi yake ya kijamii, lakini muda mwingi jamii inatambua wataamua kipi, kutegemea na u wingi wa Majaji wa Domocrats na Majaji wa republican, sembuse Tanzania.
 
Back
Top Bottom