CCM, Rage mficha ugonjwa mwisho huumbuliwa hadharani

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
rage.jpg


Vyombo vya dola, serikali na CCM walifanya jitihada za ziada kuzima kashfa ya Rage kupanda na silaha kali hadharani wakati wa kampeni huko Igunga. Kwa bahati wanaotegemea nguvu ya Mungu hulindwa pale bila Rage kujua shati lake limefunuliwaje hadi wenye uchu wa kutopitwa na taswiras za matukio kunasa picha kwa nafasi nzuri isiyo na utata.

Polisi, Maofisa wasimamizi wa kampeni na uchaguzi, serikali na CCM yenyewe kufanya jitihada zisizo za kawaida kufifisha jambo hilo kwa kuudanganya umma kwamba amepata adhabu ya kulipa faini ya Tsh 100, 000. Faini hiyo ilikuwa ni kinyume cha sheria za uchaguzi kwani jambo hilo lingefanyika na chama cha upinzani mambo yangekuwa makubwa.

Hatimaye pamoja na hoja nyingine kadhaa kati ya saba, moja ya hoja nzito ambazo Mahakama Kuu kanda ya Tabora imeegemea kumvua ubunge Dr. Kafumu ni hili la Aden Rage kupanda jukwaani na silaha kali kutishia wapiga kura.

Binafsi napongeza makama za Tanzania kuanza kufunguka na kulinda haki kwa misingi ya kufuata sheria bila kujali sura ya mtu ikoje. Kama mahakama zitazidi kufunguka hivyo itasaidia kujenga utawala wa kisheria ambao kwa sasa unapindishwa kila kukicha na wenye malengo binafsi ya kuhodhi nchi hii kama yao.
 
Rage mtu wa hovyo kabisa! Ona hata juzi suala la Yanga na usajili anaishia kupayuka tu oohhh!mtoto wa kigogo kaingilia mchakato,,anaulizwa taja,anamungúnya maneno tu!
 
Kweli asili ya mtu ni jambo lisiloweza kujificha. Unaweza kumtoa mtu porini lakini huwezi kutoa pori kichwani mwake. Huyu msomali Rage bado anadhani Tanzania ni sawa na kwao Somalia. Anadhani nchi inaendeshwa kiharamia na kibazazi kama kwao. Hata hivyo kosa si la Rage, kosa ni la watanzania kupenda kuchagua wageni wakati wenyeji wapo. Nenda Singida, Tabora, Morogoro hata Mtwara, wamechagua ma********* utadhani hawana watu wazalendo miongoni mwao. Acheni chuki miongoni mwenu.
 
Ccm bana yaani utadhani ni mambumbumbu the way wanavo deal na issues zao
 
Huyu jamaa si ni msomali huyu? Mnashangaa nini yeye kuwa na kibunduki kiunoni?
 
wameigeuza tanzania kama jalala lakini bahati mbaya wao ndi wamegeuka taka taka jalalani humo shame on them.
 
Rage anafaa zaidi Simba kuliko siasa anazojaribu kuzifanya. Kule ndio unaweza kucheza na mambo jinsi unavyotaka.
 
Kweli asili ya mtu ni jambo lisiloweza kujificha. Unaweza kumtoa mtu porini lakini huwezi kutoa pori kichwani mwake. Huyu msomali Rage bado anadhani Tanzania ni sawa na kwao Somalia. Anadhani nchi inaendeshwa kiharamia na kibazazi kama kwao. Hata hivyo kosa si la Rage, kosa ni la watanzania kupenda kuchagua wageni wakati wenyeji wapo. Nenda Singida, Tabora, Morogoro hata Mtwara, wamechagua ma********* utadhani hawana watu wazalendo miongoni mwao. Acheni chuki miongoni mwenu. Maneno makali mno japo ni hisia kutoka moyoni
 
Ukipanda bangi usitarajie utavuna maharage. Lazima uvune bangi. Nashukuru Mahakama kwa kutenda haki tena basi haki inayoonekana waziwazi.
 
icho kibastola majambazi wataanza kummendea ili wampore sasa, hujui kama kumiliki silaha ni hatari kuliko kutomiliki silaha? iyo ni dili kubwa sana kwa majambazi, wanaweza kummendea hata mwaka mzima akiingia kwenye anga zao tu wanampora.....mali kubwa hiyo na inauzwa garama sana kwa majambazi....kama kuna mtu alishawahi kuwa mpelelezi wa makosa ya jinai hapa atathibitisha hili.
 
Back
Top Bottom