CCM ni pagumu mno Profesa J wala Sugu wasingepewa nafasi CCM, FA nenda Kigamboni ACT unatoboa

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,964
3,895
Jamani utaratibu wa kupata nafasi ya kugombea CCM Ni mgumu mno kwa mtu wa kawaida na asiyemfanyabiashara mkubwa, pale ni kweli Kuna wenyewe, na fitina , kujuana, family history, rushwa vina husika sana.

Mimi naamini huyu Sugu au professor asingepata nafasi ya kugombea ubunge kupitia CCM miaka 1000.

Pia sielewi kwanini wafanyabiashara wakubwa wanakimbilia kugombea CCM na so vyama vingine ni kwanini, Kuna nini hapa.

Lastly, mtu kama mwana FA, Zamaradi waliomba ridhaa majimbo ya dar kupitia upinzani wanaweza kutoboa. CCM Ni pagumu Sana, wapinzani wengi walitoka CCM baada ya kunyimwa nafasi wakaenda kupata nafasi upinzani wengi tu,. Bulaya, moleli, etc

CCM Ina wenyewe Kama zilivyotenda za kutengeneza mabango nguo za kampeni Ni wao kwa wao wanapeana even kazi kubwa kubwa serikalini. Japo awamu hii imepungua hio.
 
Mzembe huyo Nlimwambia mapema aachane huko hakunisikia acha wamnyooshe
 
Nchi hii kila mtu anakimbilia ccm tu matokeo unakuta wenye ccm yao na mizizi iliyojikita chini zaidi, but mwafa has a bright future
Kama angekuja upinzani angepita bila ya shida sijui aliwaza nini..
 
Huyo FA, zamsrad ndy watu gani Kwani Wana nini cha ajabu? Kwanza Mfumo wa ccm tu hawaujui
Ccm inawenyewe

Ova
 
Uoga wake tu huyo Mwana FA Ila kajitahidi ukilimganisha na mastar wenzake waliokula spana za hatari za wajumbe
Kilicho mshinda kwa yule jamaa ni uzoefu katika mambo haya na jamaa anajua aingilie wapi na atokee wapi.ila kweli kajitahidi kwa kura alizopata...
 
Ila kajitahidi mwafa kapata kura 284 asikate tamaa aanze kujiandaa mapema
mkuu kwa uzoefu wangu siasa ni upepo tu ,haina mambo ya kujiandaa ipo kama bahati nasibu.Wewe unadhani wale wabunge waliokuwa viti maalumu akina Mpango, Ummy mwalimu, Ndalichako na Kabudi kwenye Majimbo waliopita kwamba kulikuwa hamna wana CCM waliojindaa kuwazidi?? la hasha ni upepo wa kisuri suri umepita maana hata ingetokea katika hayo majimbo mtu amejindaa kwa miaka 10 bado asingeshinda na hata ingetokea mtu anayegombea nao ana hela kama MO pamoja na hela zake asingeshinda.
 
Back
Top Bottom