CCM ni kinyonga

ASIWAJU

JF-Expert Member
Nov 18, 2022
1,939
1,625
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kina sifa na tabia ya kubadilika badilika kama kinyonga.

Kinyonga anabadilika rangi kutokana na mazingira aliyopo lakini kamwe mwili wa kinyonga haubadiliki kuwa wa ng'ombe au mbuzi.

Kinyonga atabadili rangi lakini siku zote hataendelea kutambulika kama kinyonga.

Wafuasi, wanachama na viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani kumwamini kinyonga huyu kutokana na kujibadili rangi kutokana na mazingira ya sasa ni kujidanganya.

Wengi wameingia katika mtego huu wa huyu kinyonga na kupotea kwa kudhani kuwa amebadilika na kuwa mbuzi, huku wakisahau kuwa yeye ni kinyonga na ana tabia za kubadili rangi kutokana na mazingira aliyopo.

CUF, NCCR next CHADEMA.

KINYONGA
AcclaimedHandyCommongonolek-size_restricted.gif
 
KAULI MAARUFU

MAMA ATAWAACHIA MAJIMBO KADHAA



Swali la Msingi.. Anaegawa majimbo ni Rais au?
Wamejisalimisha kwa mtukufu malkia, future ya tume huru na katiba mpya kwao wanaona haionekani. Ili wapate chochote kitu 2024 na 2025 wameona ni vyema kutii mamlaka na kujisalimisha.
 
Hakuna lenye mwanao lisilokua na mwisho ndugu! Huko kite walifanikiwa ila kwa CDM ni ngumu sana. Na naamini huo ukinyonga wap mwisho wake unafila muda si mrefu..atageuka kwa mbuzi mazima.
 
MAONO YA KINYONGA WA KIJANI na MANJANO.

Mwona maono Fulani aliona Kinyonga akiyameza mayai yake na kupanda juu ya mti mrefu,

Nia ya kupanda juu ya mti ni kujiachia Kutoka JUU ya mti Ili kuliangukia jiwe lililo chini ya mti, tumbo lipasuke na watoto watoke wakiwa hai.

Kinyonga aliliangukia jiwe na tumbo lake likipasuka kama alivyodhamiria bt Cha kuhuzunisha ni kuwa, hakuna mtoto aliyetoka hai, sababu ni kuwa mayai hayakuwa yamekamilisha siku zake za kuanguliwa.

RANGI ya mayai ni MEUPE, bt tumbo lilipopasuka, vilionekana vipande vya maganda ya mayai RANGI Nyeupe, na Damu yenye RANGI RED kutokana na mayai kupasuka, pia Kinyonga aliaga Dunia.

Nia ya Kinyonga ilikuwa njema. Bt muda haukuwa sahihi.

CCM ni Kinyonga, anaenda kufa baada ya 2026, bt maandalizi ya mrithi Bado hayaendi vizuri.

CCM haijakiandaa chama Cha kuja kurithi CCM. Vyama vilivyopo havijawa Bado na uwezo wa kuendesha Nchi, kiitikadi, kimaadili, kimfumo nk.

Nyerere: Bila CCM imara, Nchi itayumba.

Tusubiri.
 
Vyovyote iwavyo iwe mama anania njema au kuna jambo ameficha moyoni mwake lakini hatua aliyoifikia so far so good lazima tumpongeze, hatutaki turudi kule tulipokuwa.

Shida kubwa ni hawa chawa na mafidhina.
 
Vyovyote iwavyo iwe mama anania njema au kuna jambo ameficha moyoni mwake lakini hatua aliyoifikia so far so good lazima tumpongeze, hatutaki turudi kule tulipokuwa.

Shida kubwa ni hawa chawa na mafidhina.
Hata Magu alikuwa na Nia njema kuiona Nchi aliyoiita "TANZANIA ya MAGUFULI"

Alifanikiwa kuiona Tanzania hiyo?

Tusubiri.
 
Hata Magu alikuwa na Nia njema kuiona Nchi aliyoiita "TANZANIA ya MAGUFULI"

Alifanikiwa kuiona Tanzania hiyo?

Tusubiri.
Katika maraisi wa hovyo basi Jiwe alikuwa wa hivyo sana, kifo chake kimetokana na damu za watu zilizo mwajika.
 
Kwani ccm ndio kinyonga peke yake? Cdm hawawezi kuwa kinyonga? Mbona wote wamebadilika? Huoni kama mtego wa cdm karibia unase? Huoni kama kutoka kwenye mtego ni kuharibu maridhiano?
 
Kwani ccm ndio kinyonga peke yake? Cdm hawawezi kuwa kinyonga? Mbona wote wamebadilika? Huoni kama mtego wa cdm karibia unase? Huoni kama kutoka kwenye mtego ni kuharibu maridhiano?
CCM hajaanza ukinyonga kwa vyama pinzani leo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom