Elections 2010 CCM na wasanii waliofulia....

jamani mimi huyu ndo amenisikitisha kabisa.........ni mpendwa hasa ila hapa kachemka......huwa anadai kuwapeleka watu kwa heaven kwa sir god,chaajabu leo anawasindikiza watu upotevuni......imeniuma kinoma,yaani naandika moyo unahasiraa kinomi.
Nimenotice kitu kimoja,majority wa watumbuizaji na njaa tu,kukosa uzalendo,uelewa mdogo and mostly are are after money.wote walioitwa maboya na shule ndogo.......wangemuita mpoto...........
Bora ata mdada wa b.o.t yeye alikuwa anamuimbia mumewe....heri yake!!

Kwa kweli inatia huruma sana watu wengi huwa wanafikiria kuwa kumkana yesu lazima uulizwe mara tatu kama petro kumbe inaweza kuwa mara moja tu!
 
Halafu khadijah kopa kaenda
kuimba matusi matupu..........yaani hadi aibu............
 
hivi na nyie wote sio mashabiki kweli?mlikaa kutwa njima mnaangalia huo mkutano?????????wote washabiki,msiwaseme wenzenu bwana!
 
Mimi sioni shida kwa wasanii kuipigia debe CCM, kwani wale wanaishi kwa sanaa.CCM wana hela za kifisadi hivyo wacha vijana wazitumbue, swali hapa ni kwanini CCM imeamua kukodi zaidi ya vikundi 30 vya sanaa kuinadi? Jibu ni kuwa kuwa CCM imefulia kimvuto, ndiyo maana inakodi wasanni ili kurudisha mvuto kwa walala hoi wa nchi, kwani wengi wa wabongo hawana uwezo wa kuwaona wasanii hao kwa kulipa viingilio basi watajipeleka kwenye mikutano ya CCM. Hivyo siyo wasanii waliofulia bali CCM ndiyo imefulia. Labda kwa Flora Mbasha ambaye nilikuwa najua ni mwimbaji wa INJILI, huyu kwa kuimbia CCM amefulia ki huduma, kwani INJILI ni habari njema, lakini kuitukuza CCM siyo habari njema iletyo wokovu bali habari mbaya iletayo maangamizi kwa taifa. Sote tunajua kuwa nchi yetu ni tajiri mno kwa rasilimali tulizowekewa na Mwenyezi Mungu lakini leo hii watanzania ndiyo jamii ya watu masikini mno duniani kutokana ufisadi uliomo ndani ya CCM, leo hii tukiona mtumishi wa Mungu akihimiza watu waichague CCM , tunakuwa na wasiwasi na mtumishi huyo,kwani lazima atakuwa anatumikia miungu mingine, na wala siye Mungu aliyeumba mbingu na nchi. CCM IMEFULIA NA FLORA MBASHA AMEFUKIA PIA. Naomba kutoa hoja.
 
Halafu khadijah kopa kaenda
kuimba matusi matupu..........yaani hadi aibu............

Boss, utamu wa ngoma sharti uingie...Huwezi kujua yaliyojiri bila kufanya upembuzi yakinifu...na huwezi kufanya upembuzi yakinifu bila kushiriki kama mtazamaji makini!
 
Nilishangaa kumuona dokii kwenye mkutano wa ccm,
mara flora mbasha mara marlaw........

Sijui kama ni burudani au ni kuganga njaa....
But honestly ....nimeona kama hawa wasanii wamejidhalilisha hivi....

Halafu msanii akishafulia kama dokii ukija kumuona
kwenye mkutano wa ccm ....
You just feel pity..........

Wasanii hawa nimeona kama wamejishusha hivi.....
Sijui nyinyi mnaonaje........


umekosea ndg yangu. hao ni wajanja. wapo pale kikazi wanalipwa. si unajua ccm ina hela za kumwaga?
 
Sina uhakika kama wamefulia, lakini pia kupiga mziki CCM ni mtaji. Mtu anayekwenda CCM hata kama amefulia ujue atasimama mbona wote wenye uwezo wako kule. Unashangaa hata Sabodo kawapa Chadema 100mil lakini uliza kawapa CCM ngapi utaona hiyo ni kijiko cha chai
 
Njaa ya ubongo blaza ni balaa acha..
Najitahidi nisiangukie huko..
 
Kwa CCM walichofanya ni kujidhalilisha kisiasa mbele ya dunia! Sijaona kwingineko duniani mkutano mkuu wa chama ukageuzwa jukwaa la muziki na burudani!! Walioalikwa ni wanamuziki wasiokuwa na upeo, wale ambao watafurahisha tu CCM bila kutazama kwa undani zaidi madhara ya muziki na sanaa yao kwa ujumla! Mbasha alishafulia siku nyingi, kukata mauno mbele ya mafisadi ambao alipaswa kutumia muziki kuwakosoa au dini kuwaongoza ni kuonyesha ni jinsi gani alivyopotea!! Dokii mbona kesha siku nyingi, nadhani kulikuwa na kutumika zaidi ya pale....Bushoke naye ni vichekesho vitupu...ni aibu!! Halafu nimesoma comment ya Chege Chigunda leo na hizi ni comment zake:-

"Tumemaliza perfomance na mh jakaya,na tutaendelea kuwepo dodoma kwa ajili ya chakula cha mchana na mh jakaya ikulu ndogo dodoma,safi kabisa"

"TMK wanaume famili tumekinukisha mbaya mbele ya mh jakaya kikwete kipenzi cha wa tanzania,mjini dodoma leo."...Jiulize "kukinukisha" ni nini?

Kwa ujumla, kwa CCM na wanamuziki ilikuwa ni upuuzi unafanyika pale

 
Jamani nimesoma comment ya Chegge kuhusu perfomance yao pale Dodoma kwenye mkutano mkuu maalum wa CCM! Kuna neno Chegge amecomment kwenye Facebook kuwa "wamekinukisha" mbele ya JK.....!!

Kwa kumbukumbu zangu siku ya tukio JK alikuwa so excited, alikuwa anachekelea tu mwanzo hadi mwisho, hata pale wenziwe walipoonyesha kutokufurahia....sijui ndiyo kilikuwa kimeshanukishwa?

Hebu someni hii comment ya Chegge kwenye Facebook mnisaidie, KILICHONUKISHWA MBELE YA JK NI NINI? Kilimletea madhara mheshimiwa?

"TMK wanaume famili tumekinukisha mbaya mbele ya mh jakaya kikwete kipenzi cha wa tanzania,mjini dodoma leo."....By Chegge Welcome to Facebook)
 
Njaa ni kitu kibaya sana. Usipoweza kukikonturooo unaweza kufanya mambo ya aibu. Si kweli kuwa wasanii hawa wanaipenda CCM lakini wafanyeje kama wana njaa na CCM iko tayari kutoa mkate??? Ni watu wachache sana wenye uwezo wa kukataa kufanya kitu wasichokiamini ili mradi wapate mkate wakiwa na njaa.
 
Jamani acheni kuwashambambulia wasanii hawa....HIVI PALE ASIYEGANGA NJAA NANI? KUANZIA JUKWAA KUU MPAKA UKUMBINI? NANI ASIYEGANGA NJAA katika SIASA?
mix with yours
 
Back
Top Bottom