CCM na Urais 2015: Tujadili Aina Kuu za Wagombea

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,850
9,405
Mwaka 2015 sio mbali, na kwa mara nyingine tena watanzania tutapata fursa ya kutumia haki yetu ya kikatiba kumchagua mtu mmoja ambae tunaamini kwamba ndiye atakaefaa kutuongoza kama taifa katika hiki kipindi kigumu cha uchumi kinachotuathiri kwa miaka zaidi ya 50 sasa.

Nimelenga zaidi kwenye CCM kwani ni jambo lililo dhahiri kwamba iwapo upinzani utashinda kiti cha urais mwaka 2015 basi kwa kiasi kikubwa itatokana na kutumia vyema udhaifu na mapungufu ya CCM. Vinginevyo CCM bado ina nafasi kubwa ya kurekebisha mambo kadhaa muhimu na hivyo kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kuendelea kutawala nchi mwaka 2015.

Hii ni kwa sababu CCM kama chama kimefanikiwa sana kuepuka siasa za ukabila katika ngazi ya urais tofauti na nchi kama Kenya ambako suala la ukabila ndio kigezo kikubwa, huku vigezo vingine vikija baadae. Ni mafanikio ya CCM katika kudumisha amani, utulivu na umoja ndio yanayokilinda CCM nyakazi hizi, hasa kwenye chaguzi za Rais. Bado kuna imani kubwa sana katika jamii kwamba ni sawa kwa upinzani kuchukua majimbo lakini sio ngazi ya urais.

Kama ilivyo ada, kampeni za urais uambatana na matangazo mbali mbali juu ya wasifu wa wagombea (adverts), ushindani wa hoja, na ushindani wa maneno (ambao mara nyingine huwa ni fitina). Kwa mtazamo wangu ambao nadhani pia unafanana na wa watanzania wengine wengi, katika uchaguzi wa 2015, CCM itakuwa na aina kuu saba za wagombea ambayo nitayajadili kama ifuatavyo:

1. Kundi la kwanza ni lile linaloendesha siasa za kupambana na ufisadi ndani ya CCM.

2. Kundi la pili ni lile ambao tumeshuhudia kupitia vyombo vya habari likipigwa vita na kundi la kwanza kwamba ndio linalokigharimu CCM kimvuto katika siasa za ushindani nyakati hizi. Kundi hili kinara wake mkuu ni Lowassa ingawa sio lazima yeye kugombea moja kwa moja. Kundi hili litakuwa na mgombea angalau mmoa ingawa kama ilivyokuwa kwa kundi la kwanza, ni mapema bado kubaini nani hasa atasimamsishwa na kundi hili. Kitu muhimu hapa pia ni kwamba kuna uwezekano mkubwa Lowassa akashinda vita dhidi yake ndani ya chama kwani CCM kama chama kimeshindwa kumalizia the last mile katika azma yake ya kummaliza Lowassa kisiasa na kuna hisia nyingi inayozidi kujengeka ndani ya jamii kwamba pengine kinachoendelea ni fitina na minyukano ya maslahi kuliko ukweli. Jamii bado inasubiri ukweli juu ya hili, vinginevyo kwa sasa the verdict is equally divided.

3. Kundi la tatu ni lile linalopambana kuhakikisha kwamba linampokea Rais wa sasa mwaka 2015. Kama ilivyokuwa kwa makundi mengine hapo juu, hapa pia ni mapema mno kuja na majina ya uhakika mbali ya kutaja yale yanayovumishwa na vyombo vya habari bila ushahidi wa maana.

4. Kundi la nne ni lile lenye msimamo na mtazamo wa baba wa taifa – Mwalimu Nyerere. Vinara wa kundi hili ni kina mzee Butiku, Warioba, Salim, Kitine, Kaduma n.k. Kwa vile wazee wote hawa umri wao umeshakwenda, watamsimamisha mtu wao lakini kama ilivyokuwa kwa makundi mengie hapo juu, ni mapema mno kuja na jina au majina ya watu hao.

5. Kundi la tano ni lile ambao litapendekezwa baada ya busara ya watu kama mzee mkapa, mwinyi na kinana kutumika katika kuokoa kuvunjika kwa chama. Ni vigumu kwa sasa kubaini ni kina nani ambao wanaweza kuteuliwa na ambao makundi yote yatakayokuwa yanahasimiana wakati huo yatajihisi yapo salama hivyo kumuunga mkono mgombea huyo.

6. Kundi la sita ni lile la wale walioshindwa kuingia katika tatu bora mwaka 2015. Tatu bora ya wakati ule – Mwandosya na Salim tayari wana majina makubwa hivyo uwezo wa kujitegemea ikifananisha na wagombea wengine kama Sumaye na Dr. Kigoda ambao ili kufanikiwa itakuwa ni muhimu kujenga a coalition.

7. Na kundi la mwisho ni lile litakalokuwa na mchanganyiko wa wagombea mbalimbali ambao hawatakuwa na mahusiano ya moja kwa moja na makundi mengine hapo juu na ambao hawajawahi kuwania nafasi ya urais. Wagombea hawa watajaribu bahati zao kutokana na nafasi zitakazojitokeza wakati huo, hasa kutokana na upepo wa kisiasa ndani ya CCM lakini muhimu zaidi, kutokana na nguvu ya mgombea wa Chadema mwaka 2015. Humu watakuwepo watu kama Magufuli, mawaziri wengine waandamizi katika awamu hii na awamu iliyopita ambao hawajawahi kuwania nafasi hiyo, lakini pia kina mama na vijana iwapo itatokea CCM ikahitaji mgombea wa namna hiyo. Kundi hili linaweza kutumiwa na kundi la tano (rejea hapo juu) kama nia itakuwa ni kuzuia CCM isivunjike kutokana na minyukano ambayo ni dhahiri itajitokeza.

Mara nyingi, watanzania wengi huwa na tabia ya kuchagua viongozi kwa misukumo mikuu mitatu:
1. Mazoea.
2. Mkumbo.
3. Hisia na mapenzi binafsi juu ya wagombea.

· Tukianza na mazoea; mara nyingi CCM imekuwa na utamaduni wa kumsimamisha mgombea ambae chama (sio lazima wanachama au mvuto wake kwa umma) kina amini ndiye anaefaa. Na mara nyingi mgombea wa namna hii hupitishwa na wananchi kwani wapiga kura wengi, hasa wa vijijini huchagua CCM kutokana na mazoea.

· Tukija kwenye suala la mkumbo; watanzania wengi hupigia kura mgombea urais kutokana na mkumbo; kwa mfano, kama upepo wa siasa ya wakati huo unapeperusha UJANA, basi mgombea mwenye haiba ya ujana atakuwa na nafasi kubwa ya kupigiwa kura; kama upepo wa siasa unapeperusha UWEZO WA KIFEDHA, basi wananchi wengi watampigia kura mgombea mwenye uwezo kwa imani kwamba huyo hatakuwa na tama ya kuponda mali ya umma; na kama upepo utakuwa unapeperusha bendera ya UADILIFU, basi mgombea mwadilifu atakuwa na nafasi kubwa n.k. Pamoja na haya yote, kutumia vigezo kama hivi - kijana, au mwenye uwezo kifedha au uadilifu haina maana ndiye atakuwa Rais bora kwani kuna vigezo vingine vingi na muhimu vya kutazama kama nia ni kupata Rais atakaetufaa.

· Na mwisho tukija kwenye suala la hisia na mapenzi binafsi juu ya mgombea; hili tumeliona sana katika siasa za nchi yetu. Ni kawaida watanzania wengi kujenga hoja kwamba fulani ana mvuto na mwonekano wa kuwa rais, au ana uwezo wa kujenga hoja n.k, lakini mara nyingi wanaotoa hoja hizi ni wale ambao aidha wanafanana na wagombea husika in terms of socio-economic class, au wanatoka kanda au kabila moja na mgombea na kadhalika.

Kwa kifupi, hawajengi hoja zao kwa maslahi ya taifa. Watu wa namna hii ugeuka kuwa wapambe wa wagombea husika, na kutokana na nguvu na ushawishi wao mkubwa katika jamii, wapambe hawa hufanikiwa kuaminisha umma, hasa ule jamii ambayo ambao haifanani kabisa na ‘class' ya mgombea na wapambe wake. Kazi hii ya wapambe hufanikiwa kwa urahisi hasa pale suala la mkumbo na mazoea linapojipenyeza pole pole miongoni mwa watanzania (umma), hasa wale wenye uelewa mdogo juu ya masuala ya demokrasia na maendeleo. Ndio maana kati ya masuala haya ya Mazoea, Mkumbo na Hisia/mapenzi binafsi, hili la tatu – yani hisia/mapenzi binafsi huwa ni overriding factor.

Je: Katika nyakati za sasa, hasa tunapoelekea uchaguzi mkuu wa tano wa vyama vingi, vigezo hivi vitatu vitakuwa na nafasi gani katika kutupatia mgombea kupitia tiketi ya CCM?

Ni dhahiri kwamba mchakato huu unaotumika kuaminisha watanzania kwamba fulani na fulani ndio wanaotufaa katika nafasi ya Urais, (hasa ule wa hisia/mapenzi binafsi) sio wa kuaminika (it is not a reliable process) katika kutupatia viongozi/rais bora. Ipo mifano mingi kuhusu jinsi gani mchakato huu umezaa viongozi wabovu katika taifa letu.
Kwa mtazamo wangu ambao unaweza pengine ukawa finyu, mgombea wa kweli atapatikana iwapo vigezo vikuu vitatu vitatumika katika mchakato wa kumpata mgombea ndani ya CCM:

1. Wasifu (hulka) ya mgombea – ni muhimu wahusika wakatazama morality of the person, kwa mfano, je ana any moral failings in the past? Je amewahi kuwa involved in any unethical decisions na kuna ushahidi katika hilo? Ni muhimu sana all skeletons za mgombea zikawekwa hadharani ili umma uweze ku scrutinize, na ikiwezekana, zoezi hilo lianze sasa. Lakini pia muhimu hapa ni kwa watanzania kuelewa tofauti ya ukweli na fitina katika mchakato huu.

2. Msimamo wa mgombea on issues mbalimbali – hili ni suala muhimu sana; kwa mfano, iwapo mgombea urais kupitia CCM 2015 alikuwa kambi moja na alisimamia msimamo sawa katika masuala mbalimbali ya kiuchumi, kijamii, na kisiasa, na wenzake ambao nyakati hizi wanaonekana hawafai mbele ya jamii, umma usiwaache hawa bila kuwadadisi kwa undani kwani kuna uwezekano mkubwa wakashindwa kufanya maamuzi magumu kutokana na kuwindwa na dhambi ya asili.

Pia katika suala la msimamo on issues – msimamo wa mgombea ni muhimu uwe compatible with available evidence, not just fiction or theories – kwa mfano msimamo na imani yake katika masuala mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, over and above ilani ya CCM ambayo ipo to vague.

3. Na tatu ni – Uzoefu wa mgombea katika masuala ya uongozi. Uzoefu hapa sio lazima iwe katika siasa bali katika uongozi hata kama ni kwenye NGO au private sector; kikubwa ni awe na uzoefu wa kutosha na pia track record ya mafanikio katika uongozi wake; katiba yetu ya sasa ya Tanzania inaeleza kwamba moja ya sifa ya mgombea urais ni lazima awe na sifa za kuwa mbunge; nadhani hii imepitwa na wakati na tuondokane nayo kwani kuna wabunge wa CCM ambao kwa miaka zaidi ya 20 wamekuwa bungeni wakifanya madudu ambayo yanashangaza hata watoto wadogo wa chekechea.

Nia yangu ni kupendekeza vigezo vya ku scrutinize wale wote ambao wataweka nia ya kugombea urais kupitia CCM. Inawezekana vigezo hivi vikawa havitoshi, na ndio maana ya kuwa na mjadala ili tusaidiane kuboresha mjadala huu. Tukifanikisha hilo, nina hakika kwamba kwa pamoja tutaweza kutokomeza desturi ya kuchagua rais kwa njia za mkumbo, mazoea na hisia/mapenzi binafsi, vigezo ambavyo tayari vimeshatugharimu sana kama taifa.
 
sababu hawa walioua siasa za nyerere hususan mkapa bado wako hai ccm haiwezi kupata mgombea anyekubalika na wananchi bali watapata mgombea wanayemtaka wao kwa maslahi ya wao kutoulizwa madhambi yao hususan ben mkapa
 
Mi nafikiri kuna makundi mawili au matatu Ikundi la 1, 2, makubwa huku mengine yakiwa loosely kwenye orbit ya haya makundi makubwa.

Mfano; kundi la kwanza lina ka uhusiano kidogo na kundi la 4. Na kundi la pili kupitia mfanyabiashara mmoja lina uhusiano na kundi la tano . Kundi la7 linaweza tumia na wanaotaka kumrithi Jk na kundi lao kumpenyeneza huyu mtu.

Kundi la 6 linaweza kuangukia kundi la 1 n.k
 
Tujadili wagombea uraisi kwa mtazamo wa kitaifa siyo CCM, siamini kama CCM kwa zama hizi wanaweza kutoa mgombea, sahihi, wana matatizo mengi ya ndani, the perfect candidate atatoka nje ya CCM, sisi wananchi tunatakiwa kufanya mabaliko, vinginevyo tusilamike, tukubali maumivu kwa ujinga wetu, naungana na mtoa mada hapo juu, ila mimi naenda mbele zaidi, nadhani tuanze kuweka vipaumbele vyetu kama taifa ninini!!

Kama uchumi na siasa za aina gani zinatufaa(ujamaa, ubepari, ujapari.......?), muungano wetu, umoja wa kitaifa, ulinzi na usalama wetu, mahusiano ya kimataifa nakadhalika, suala la kujadili majina lije baadaye,
 
...nadhani tuanze kuweka vipaumbele vyetu kama taifa ninini!!

Kama uchumi na siasa za aina gani zinatufaa(ujamaa,ubepari,ujapari.......?????),muungano wetu,umoja wa kitaifa, ulinzi na usalama wetu, mahusiano ya kimataifa nakadhalika, suala la kujadili majina lije baadaye,

Kama umenisoma vizuri, nilianza mjadala kwa kuelezea hali halisi ilivyo - kwamba kutatokea makundi ya wagombea mbalimbali na baadae nikaonya kwamba zama za siasa za aina hii zimeshapitwa na wakati kwani zimetugharimu sana kama taifa.

Nikapendekeza njia sahihi za ku scrutinize wagombea na nikaja na vigezo vitatu huku nikihimiza kwamba pengine vipo vingi na itakuwa vyema kama tukiviongeza na kuvijadili. Kwa mtazamo wangu, ni vigumu kwa siasa zetu za sasa kujenga a consensus juu ya vipaumbele ambavyo vitakuwa over and above party politics; Mimi nadhani njia pekee ni kuruhusu wagombea mbali mbali wajinadi kutuelezea wapi wanataka kuipeleke nchi yetu, kisha sisi tuchague kutokana na itikadi zilizopo ndani ya jamii.

Tukumbuke tu kwamba itikadi haitokani na vyama vya siasa bali jamii; siasa ni vehicle tu ya kutekeleza itikadi zilizopo tayari kwenye jamii;

Ningependa kukuuliza swali lifuatalo:

Je, katika mazingira ya sasa ambayo ushindani wa kisiasa uliopo ni CCM kung'ang'ania madaraka kwa liwalo liwe huku upinzani ukitumia kila aina ya udhaifu wa CCM kuitoa madarakani, tutawezaje kama taifa kufikia consensus juu ya vipaumbele vya taifa ambavyo ni over and above partisan politics?

Tuliweza hilo chini ya mfumo wa chama kimoja na ndio ilikuwa sababu kubwa ya kufuta vyama vya upinzani ili tuwe na umoja na mshikamano under a common vision and cause; tulifanikiwa kwa kiasi fulani kuwa na mwelekeo na dira kama taifa ingawa safari yetu haikukamilika.

Je, kufanya hivyo katika nyakati hizi italeta athari gani kwa CCM na vyama vya upinzani katika mazingira ya sasa ambayo yametawaliwa na siasa za kuviziana kuliko za kujenga nchi?
 
Haya makundi ndugu Mchambuzi yana maono yoyote kuhusu maendeleo ama ni makundi ya mbwa-mwitu wanaogombea kitoweo?

Naungana na hoja naweza kujenga kuwa Siamini kama ndani ya CCM kuna mpambanaji (kwa muktadha wa Kamusi) dhidi ya Rushwa na Ufisadi hapa nchini, maana najua huwezi kuusukuma gari ukiwa ndani ya gari lile lile utasukuma uzito wako mwenyewe!
 
Yawezekanaje MWALIMU aue vyama vya upinzani akiwa Rais halafu awe advocate wa upinzani akiwa MSTAAFU?Hii huitwa kurudia matapishi au kujichanganya tu?
 
Mi nafikiri kuna makundi mawili au matatu Ikundi la 1, 2, makubwa huku mengine yakiwa loosely kwenye orbit ya haya makundi makubwa.

Mfano; kundi la kwanza lina ka uhusiano kidogo na kundi la 4. Na kundi la pili kupitia mfanyabiashara mmoja lina uhusiano na kundi la tano . Kundi la7 linaweza tumia na wanaotaka kumrithi Jk na kundi lao kumpenyeneza huyu mtu.

Kundi la 6 linaweza kuangukia kundi la 1 n.k
Kwa mtazamo wangu, makundi haya yote yatakuwa very active katika hatua za mwanzo huku kila kundi likijaribu kufanikisha azma yake, lakini dakika za mwisho kundi la tano ndilo litakalotoa mgombea wa CCM kama njia ya kuepusha chama kusarambatika;

Naungana na wewe kwamba kundi namba tano na namba mbili at some point yatakuwa na uhusiano wa karibu sana lakini mimi nadhani uhusiano huo hautadumu kwa muda mrefu kutokana na uhalisia wa mambo ambao utahitaji wazee wenye busara na wanaoheshimika ndani ya chama kuja na mgombea ambae atakubalika na pande zote;

Ni hapa ambapo mimi nadhani mgombea kutoka kundi namba saba ataweza kupenya kwa urahisi.
 
Yawezekanaje MWALIMU aue vyama vya upinzani akiwa Rais halafu awe advocate wa upinzani akiwa MSTAAFU?Hii huitwa kurudia matapishi au kujichanganya tu?

Mkuu,
kwa hili umeniacha kidogo, naomba ufafanue zaidi kidogo;

Swali lako kuhusu iwapo katika makundi yote haya kuna yeyote ambae ana dira na maono kwa maslahi ya taifa letu, nadhani ni mapema mno kubaini hilo, lakini so far ni dhahiri kwamba hakuna yoyote hadi sasa ambae amegusia vipaumbele vyake vya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu katika mazingira ya a political strategy inayoeleweka;

Pengine ni mapema mno lakini sina matumaini makubwa sana katika hili, na kuna kila dalili kwamba tofauti kubwa itakayojengeka itakuwa baina ya wasafi na wachafu;
 
Nafikiri NYERERE NI KICHWA kati ya vichwa vichache vinavyoelewa logic ya Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wa haraka haraka bila Referendum kati ya Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 na Muungano wa TANU na ASP MWAKA 1977( NJE YA BOKSI LA YALIYOANDIKWA na kulishwa waalimu na wanafunzi wa Tanzania)

Unakumbuka kuwa yasemekana kwamba 80% YA WATANZANIA walipendekeza Chama kimoja dhidi ya 20% waliopendekeza vyama vingi, lakini Nyerere akaweza kushawishi wana CCM kuvikubali vyama vingi?

Sasa wakati huu alikuwa ashang'atuka kwa namna alivyokuita kustaafu!Sasa jibu swali langu kuhusu kubadilika kwa muumini wa chama kimoja kuwa muumini wa vyama vingi ili nione kama hili la ugombea uraisi ndani ya CCM kweli unalielewa.

Pia ufafanue kwa nini busara za Mkapa, Mwinyi na Kinana ni muhimu wala siyo SALIM AHMED SALIM,JAJI WARIOBA, wala JOSEFU BUTIKU wote kutoka CCM?
 
Nafikiri NYERERE NI KICHWA kati ya vichwa vichache vinavyoelewa logic ya Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wa haraka haraka bila Referendum kati ya Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 na Muungano wa TANU na ASP MWAKA 1977( NJE YA BOKSI LA YALIYOANDIKWA na kulishwa waalimu na wanafunzi wa Tanzania)

Unakumbuka kuwa yasemekana kwamba 80% YA WATANZANIA walipendekeza Chama kimoja dhidi ya 20% waliopendekeza vyama vingi, lakini Nyerere akaweza kushawishi wana CCM kuvikubali vyama vingi?

Kuhusu nyerere na mfumo wa vyama vingi - ni yeye aliyefuta mfumo wa vyama vingi mwaka 1965 na kufanya nchi yetu iwe chini ya chama kimoja kwa miaka karibia 24, na nia yake ilikuwa ni nzuri tu.

Tulihitaji kuwa na umoja na mshikamano ili kufanikisha self determination yetu kama taifa kwani uwepo wa mfumo wa vyama vingi ungetoa mianya ya siasa zetu kuingiliwa na mataifa makubwa ya nje kupitia vibaraka wao ambao hata leo wapo miongoni mwetu; sasa kuhusu tume ya nyalali kukusabya 80% ya maoni yaliyotaka nchi iendelee kuwa chini ya mfumo wa chama kimoja.

Walimu alishaona tatizo lililopo kwani tofauti na watanzania wengi ambao hawakuwa na uelewa juu ya mageuzi yaliyokuwa yanatokea Eastern europe na urusi, Nyerere alikuwa anayafuatilia hatua kwa hatua na aligundua athari zitazakozikumba CCM iwapo mageuzi ya vyama vingi yangekuja kwa nguvu ya umma kwani hata kama Nyerere angeamua nchi ifuate maoni ya tume ya nyalali, that was to be very short-lived; uamuzi wa kuruhusu vyama vingi unawapumbaza baadhi ya watanzania kwamba CCM ilifanya kwa hiyari, na ni imani hii ndio inachangia kwa kiasi fulani watanzania wengi hasa waliopo vijijini wasiviamini vyama vya upinzani; This is a fallacy;

Kuhusu busara za Mkapa vis a vis Salim, Warioba, Butiku - nadhani kama unafuatilia siasa za nchi hii, kambi ya wazee wetu hawa bado ina maslahi katika kinyang'anyiro cha urais hivyo haitakuwa jambo la busara kuwapa jukumu hili; Mkapa, Mwinyi, Kinana, hawa wote ni viongozi ambao wana uwezo wa kusikilizwa na kambi zote kwani hawana maslahi ya moja kwa moja tena na kiti cha urais; ndio maana mtu kama kinana alikuwa maneja wa kampeni wa Mkapa 1995 na pia kikwete baada ya mkapa kumaliza muda wake;
 
Kuhusu nyerere na mfumo wa vyama vingi - ni yeye aliyefuta mfumo wa vyama vingi mwaka 1965 na kufanya nchi yetu iwe chini ya chama kimoja kwa miaka karibia 24, na nia yake ilikuwa ni nzuri tu - tulihitaji kuwa na umoja na mshikamano ili kufanikisha self determination yetu kama taifa kwani uwepo wa mfumo wa vyama vingi ungetoa mianya ya siasa zetu kuingiliwa na mataifa makubwa ya nje kupitia vibaraka wao ambao hata leo wapo miongoni mwetu;...
Mchambuzi ukiangalia hali halisi ya sasa naweza kusema kutakuwa na kundi moja tu la wagombea, kundi hilo ni lile linalosukumwa na maslahi binafsi, sioni kama kutakuwa na tofauti yoyote na hali ya 2005. Uzuri wa 2015 ni kuwa JK factor ambayo ilikuwa tishio 2015 haitakuwepo, na hata kama ikiwepo basi haitakuwa tishio kama 2005. Lakini ndani ya CCM mgombea yeyote ataongozwa na maslahi binafsi, hata kama kutakuwa na makundi itakuwa ni sababu ya maslahi binafsi ya makundi, na sio ya nchi.

Umezungumzia maslahi ya CCM wazee aka CCM asilia, no doubt kuwa watakuwa na influence fulani, lakini ususahau pia kuwa CCM mtandao watakuwa na nguvu pia, may be RA factor itakuwa at work tena kulinda maslahi. Lakini je ni maslahi gani, ya taifa? ya chama? au binafsi?

Ukiangalia Mkapa alikuwa na maslahi yake kwa JK, kwa kuwa JK amemlinda, kwa hiyo angependa kuwa atakayeingia baada ya JK amlinde pia, so as Kinana na kashfa ya meli ya vipusa Taiwan, so as many politicians wa hapa nyumbani. Kwa hiyo ukiangalia kwa undani maslahi binafsi ndio yatakayotawala, watasema wanaamini hiki au hiki, wataimba sera zile au hizi, lakini in the end wataongozwa na maslahi binafsi.

Na wakiingia madarakani they will be no different na wa sasa, unless mungu atuone. Ukisikia mtu anamuunga mkono mgombea A si kwa sababu anaamini kuwa mgombea A anafaa kuliongoza taifa, au kuwa kwake madarakani kuna maslahi kwa taifa, au kwa kuwa mgombea B hafai, hapana, ni kuwa kuwa ana maslahi binafsi anayopata kutokana na A kuwa madarakani.

katika wote wanaotaka urais, wanaosema hadharani na wanaosema pembeni, hakuna ambaye anaonekana kweli kuwa concerned na miasha ya mtanzania, muungano, uchumi na Tanzania. Hakuna anayeoenekana kujua kuwa umoja, usalama wa Tanzania sasa upo mashakani sana, kila mtu anaangalia maslahi binafsi, kwa hiyo bado naona maslahi binafsi ndio yataoangoza, and people will spend big kuutaka urais. None of them is on issues Tanzania is facing now.

Tukiangalia JK aliyosema 2005 na aliyorudia 2010, tunaona wazi kabisa kuwa hakuna alilotekeleza, hata kama lipo not significant. Hakuingia madarakani kwa lengo la kutekeleza yale aliyosema, bali aliyasema ili aweze kuingia madarakani. Nadhani malengo yake halisi ya kuutaka urais ameyatekeleza, kama yamebaki ni machache tu, still ana muda wa kuyakamilisha.

Lakini lile la ari mpya,kasi mpya, nguvu mpya na maisha bora kwa mtanzania kwa sasa haliwezi kusemwa, kwa kuwa tuko hatua kadhaa nyuma ikilinagnishwa na alivyopokea nchi kutoka kwa Mkapa. Angalia ahadi zote alizotoa na uone kama kweli zinaweza kutekelezwa kabla ya 2015, ukweli ni kwamba haiwezekani, so it is clear kuwa aliingia kwa melongo binafsi.

Lakini tusiomwangalie JK as individual tuangalie chama pia, yale yaliyomo kwenye manifesto, itikadi zake, sera na hata misngi ya chama haifuatwi kabisa, ipo tu kwenye makaratasi. Chama kinatumiwa tu kama daraja la watu kutimiza maslahi yao binafsi, au chama pia kina maslahi yake binafsi ambayo sio yale yaliyopo kwenye katiba yake, manifesto yake, sera zake na itikadi yake.

Kwa hiyo naona 2015 msingi mkubwa utakuwa maslahi binafsi kiwanza, usisahau kuwa katika miaka hii 10 JK pia amejitahidi kupalilia udini, so inawezekana kuwa kwanza maslahi binafsi, pili ya dini, tatu chama, nne, tano......... na mwisho kabisa taifa.

Only hope ipo kwa electorate, lakini kama ulivyosema ni kuwa hakuna vigezo madhubiti vya kupiga kura. Na ule aliousema Profesa Baregu, mtaji mkubwa wa CCM, yaani unyonge wa wananchi hasa kielemu still unaweza kuplay big part kwenye uchaguzi wa 2015.
 
Baada ya uchaguzi wa Taifa, ndiyo tutajua makundi haya yana nguvu gani, kwa sasa hivi ni kitendawili.

Ninavyojua mimi, CCM ni chama cha kijamaa, sasa sijui hawa marais wetu tuliwapataje.Kwa sababu wote wameenda kinyume cha katiba zote (chama na jamhuri).

Sijaona kundi linalotaka siasa ya ujamaa iendelee Tanzania. Tukimpata mgombea huyo, basi tunaweza kuchukua madaraka 2015. Bila hivyo, wote waliobaki ni wahuni tu.
 
Kwa mtazamo wangu, makundi haya yote yatakuwa very active katika hatua za mwanzo huku kila kundi likijaribu kufanikisha azma yake, lakini dakika za mwisho kundi la tano ndilo litakalotoa mgombea wa CCM kama njia ya kuepusha chama kusarambatika; naungana na wewe kwamba kundi namba tano na namba mbili at some point yatakuwa na uhusiano wa karibu sana lakini mimi nadhani uhusiano huo hautadumu kwa muda mrefu kutokana na uhalisia wa mambo ambao utahitaji wazee wenye busara na wanaoheshimika ndani ya chama kuja na mgombea ambae atakubalika na pande zote; ni hapa ambapo mimi nadhani mgombea kutoka kundi namba saba ataweza kupenya kwa urahisi.

well put. nafikiri kutakua na compromise candidate kutoka kundi la 7,huku makundi "dhaifu" kama la 4,5,6, wakimsapoti huyu mtu. hii itawafanya kundi la kwanza na la pili wakasirike lakini watakubali kumsapoti huyu mtu kwa shingo upande lakini watabaki kwenye chama.

safi sana mchambuzi.
 
Well said, Tunajadili wagombea wa ccm pamoja na mapungufu yao kwa sababu ya kukosa mbadala.

Kumbuka kule kote ambako ccm wameshindwa, vyama vya upinzani vyote wamekuwa wakishinda kwa platform ya mapungufu ya chama tawala, mgombea asiyekubalika au fitna za walioshindwa kutoka ccm yenyewe.

Bado nasubiri kundi litakaloainisha sera mbadala kuwapa watu uwanja mpana wa kuchagua uongozi.
 
So kwa mtazamo wako kundi la 4, 5 na 6 ni dhaifu hata for 2015? does it mean kundi namba moja a mbili ndio yenye nguvu? in what sense, ndani ya chama au mgombea wao kukubalika na umma? ningependa kusikia mawazo yako on that;
 
Well said, Tunajadili wagombea wa ccm pamoja na mapungufu yao kwa sababu ya kukosa mbadala.

Kumbuka kule kote ambako ccm wameshindwa, vyama vya upinzani vyote wamekuwa wakishinda kwa platform ya mapungufu ya chama tawala, mgombea asiyekubalika au fitna za walioshindwa kutoka ccm yenyewe.

Bado nasubiri kundi litakaloainisha sera mbadala kuwapa watu uwanja mpana wa kuchagua uongozi.

Well said!!! Nadhani kwa mara ya kwanza CCM 2015 itasimamisha mgombea anaekubalika na mwenye mvuto na umma, badala ya vigezo tulivyokwisha vizoea kama vile kuhonga vizuri wajumbe wa kutosha wa mkutano mkuu kuliko washindani wake, au kuteuliwa kwa maslahi ya wachache, hasa kuwalinda watu kadhaa kadhaa ambao wanajua hawakuwa waaminifu enzi zao za uongozi n.k. Tunachobakia kujiuliza ni je, kwa mfano mtu kama magufuli ambae kwa kiasi kikubwa anakubalika sana na umma, je akifanikiwa kusimamishwa atasimamia sera gani? Au upuuzi ule ule wa ilani za CCM?
 
Baada ya uchaguzi wa Taifa, ndiyo tutajua makundi haya yana nguvu gani, kwa sasa hivi ni kitendawili.

Ninavyojua mimi, CCM ni chama cha kijamaa, sasa sijui hawa marais wetu tuliwapataje.Kwa sababu wote wameenda kinyume cha katiba zote (chama na jamhuri).

Sijaona kundi linalotaka siasa ya ujamaa iendelee Tanzania. Tukimpata mgombea huyo, basi tunaweza kuchukua madaraka 2015. Bila hivyo, wote waliobaki ni wahuni tu.

nadhani una maana baada ya uchaguzi wa ndani wa CCM unaokuja hivi karibuni ndio tutajua makundi gani yana nguvu; nakubaliana na wewe lakini tujaribu kutofautisha baina ya nguvu ndani ya chama na nguvu mbele ya umma kwa maana ya kuwa na mvuto na kukubalika na watanzania from different walks of life.

Kuhusu CCM na ujamaa, huu ni udhaifu mkubwa sana ambao upinzani umeshindwa to exploit kikamilifu; isitoshe hata katiba yetu ya sasa inatamka wazi kwamba nchi yetu ni ya kijamaa; sijui kama katika kukusanya maoni ya watanzania kuna watu wanaopata wasaa wa kuhoji hili na kupendekeza nchi yetu ifuate mfumo wa namna gani;
 
Mchambuzi ukiangalia hali halisi ya sasa naweza kusema kutakuwa na kundi moja tu la wagombea, kundi hilo ni lile linalosukumwa na maslahi binafsi, sioni kama kutakuwa na tofauti yoyote na hali ya 2005. Uzuri wa 2015 ni kuwa JK factor ambayo ilikuwa tishio 2015 haitakuwepo, na hata kama ikiwepo basi haitakuwa tishio kama 2005. Lakini ndani ya CCM mgombea yeyote ataongozwa na maslahi binafsi, hata kama kutakuwa na makundi itakuwa ni sababu ya maslahi binafsi ya makundi, na sio ya nchi.

Umezungumzia maslahi ya CCM wazee aka CCM asilia, no doubt kuwa watakuwa na influence fulani, lakini ususahau pia kuwa CCM mtandao watakuwa na nguvu pia, may be RA factor itakuwa at work tena kulinda maslahi. Lakini je ni maslahi gani, ya taifa? ya chama? au binafsi?

Ukiangalia Mkapa alikuwa na maslahi yake kwa JK, kwa kuwa JK amemlinda, kwa hiyo angependa kuwa atakayeingia baada ya JK amlinde pia, so as Kinana na kashfa ya meli ya vipusa Taiwan, so as many politicians wa hapa nyumbani. Kwa hiyo ukiangalia kwa undani maslahi binafsi ndio yatakayotawala, watasema wanaamini hiki au hiki, wataimba sera zile au hizi, lakini in the end wataongozwa na maslahi binafsi.

Na wakiingia madarakani they will be no different na wa sasa, unless mungu atuone. Ukisikia mtu anamuunga mkono mgombea A si kwa sababu anaamini kuwa mgombea A anafaa kuliongoza taifa, au kuwa kwake madarakani kuna maslahi kwa taifa, au kwa kuwa mgombea B hafai, hapana, ni kuwa kuwa ana maslahi binafsi anayopata kutokana na A kuwa madarakani.

katika wote wanaotaka urais, wanaosema hadharani na wanaosema pembeni, hakuna ambaye anaonekana kweli kuwa concerned na miasha ya mtanzania, muungano, uchumi na Tanzania. Hakuna anayeoenekana kujua kuwa umoja, usalama wa Tanzania sasa upo mashakani sana, kila mtu anaangalia maslahi binafsi, kwa hiyo bado naona maslahi binafsi ndio yataoangoza, and people will spend big kuutaka urais. None of them is on issues Tanzania is facing now.

Tukiangalia JK aliyosema 2005 na aliyorudia 2010, tunaona wazi kabisa kuwa hakuna alilotekeleza, hata kama lipo not significant. Hakuingia madarakani kwa lengo la kutekeleza yale aliyosema, bali aliyasema ili aweze kuingia madarakani. Nadhani malengo yake halisi ya kuutaka urais ameyatekeleza, kama yamebaki ni machache tu, still ana muda wa kuyakamilisha.

Lakini lile la ari mpya,kasi mpya, nguvu mpya na maisha bora kwa mtanzania kwa sasa haliwezi kusemwa, kwa kuwa tuko hatua kadhaa nyuma ikilinagnishwa na alivyopokea nchi kutoka kwa Mkapa. Angalia ahadi zote alizotoa na uone kama kweli zinaweza kutekelezwa kabla ya 2015, ukweli ni kwamba haiwezekani, so it is clear kuwa aliingia kwa melongo binafsi.

Lakini tusiomwangalie JK as individual tuangalie chama pia, yale yaliyomo kwenye manifesto, itikadi zake, sera na hata misngi ya chama haifuatwi kabisa, ipo tu kwenye makaratasi. Chama kinatumiwa tu kama daraja la watu kutimiza maslahi yao binafsi, au chama pia kina maslahi yake binafsi ambayo sio yale yaliyopo kwenye katiba yake, manifesto yake, sera zake na itikadi yake.

Kwa hiyo naona 2015 msingi mkubwa utakuwa maslahi binafsi kiwanza, usisahau kuwa katika miaka hii 10 JK pia amejitahidi kupalilia udini, so inawezekana kuwa kwanza maslahi binafsi, pili ya dini, tatu chama, nne, tano......... na mwisho kabisa taifa.

Only hope ipo kwa electorate, lakini kama ulivyosema ni kuwa hakuna vigezo madhubiti vya kupiga kura. Na ule aliousema Profesa Baregu, mtaji mkubwa wa CCM, yaani unyonge wa wananchi hasa kielemu still unaweza kuplay big part kwenye uchaguzi wa 2015.

Bongolander,

Una hoja za msingi na za maana sana. Nakubaliana na wewe kwamba its all about maslahi binafsi, hakuna anayejali maskini wa nchi hii, hatuna viongozi wa namna hiyo nyakati hizi, lakini lazima tukubali kwamba hii ni kote CCM na hata upinzani, kama wapo ni wachache sana. Advantage ya upinzani sasahivi ni kwamba CCM wamekuwa madarakani kwa miaka 50 na ushee na hakuna cha maana in terms of maendeleo kwa mtanzania wa kawaida, hasa wale wa vijijini. kwahiyo CCM has become a punching bag, ngumi zinaingia kweli kweli, huku wananchi wakishangilia kutokana na kuchoshwa na utawala chini ya chama ambacho kinatumia resources kujizatiti na kwenye law and order kuliko on issues pertaining to social welfare.

Lakini kuhusu makundi, mimi nadhani yatakuwepo makundi kadhaa na ni kwa sababu hizi:
1. Wataibuka watu ambao watajiamini kwamba wao ndio mtaji wa mwisho wa CCM kabla chama hakijasambaratika. Watu wa aina hii watakuwa katika kundi zaidi ya moja;
2. Wapo wale ambao watagombea kama njia ya kujilinda - kutafuta immunity kutokana na madudu waliyoyafanya huko nyuma.
3. Wapo wale ambao watagombea kama njia ya kuzuia kundi jingine lisikamate nchi kwani ni dhahiri kwamba maadui zao wakishinda, nchi kwao itakuwa chungu.
4. Wapo watakao gombea kwa nia ya kujijenga for the future, either ndani ya CCM au baadae kutimkia upinzani bada ya kupata umaarufu watakaokuwa wanautafuta.
5. Wapo watakaogombea baada ya kushinikizwa na viongozi fulani fulani ambao kazi yao kubwa itakuwa ni kujaribu kukinusuru chama. The list goes on and on and on...
 
Yawezekanaje MWALIMU aue vyama vya upinzani akiwa Rais halafu awe advocate wa upinzani akiwa MSTAAFU?Hii huitwa kurudia matapishi au kujichanganya tu?
Ukisikiliza hotuba aliyoitoa Mwalimu Singida mwaka 1986 utagundua ni kwa nini aliamua Tanzania iingie mfumo wa vyama vingi. Katika hotuba hiyo alibainisha kuwa CCM ilikuwa kama KANU ilivyokuwa baada ya kushinda 1963, yaani haikuwa tena na input kutoka grassroots. (Unakumbuka Mwalimu aliachia uongozi mwaka mzima kuhakikisha kuwa TANU inakuwa chama cha grassroots wakati wote). Mwalimu hakurudia matapishi yake. Alikuwa ni msomi ambaye aliweza kubaini hatari za kuendelea na mfumo wa chama kimoja, ambazo sote tunazishuhudia hivi leo. CCM ilikuwa imegeuka kuwa behemoth lisiloweza kudhibitiwa. Mwaka huo huo nilikutana na Mwalimu New York, tukazungumzia hatima ya CCM. Alinishangaza aliposema kuwa bila kuwepo ushindani CCM italeta utawala wa kidikteta nchini na itakuwa vigumu kukiondoa.
 
Back
Top Bottom