Asalaam za siku nyingi wana JF.
Nilipotea kwa muda mrefu humu jamvini hii ni kutokana na shughuli za ujenzi wa taifa.
Leo napenda kuzungumzia kwa kifupi kuhusu mwenendo wa siasa zetu za hapa bongo. Hatua tuliyofikia kisiasa ni mbaya sana hatuna tofauti na wanyama, tunafanya siasa za uhasama, siasa za kulipiza kisasi, siasa za kudharau utu wetu wenyewe, imefikia hatua ya kuwatumia marehemu waliotangulia mbele za haki.
Ukweli ulio wazi, baadhi ya ndugu zetu wa CCM wamejivua utu hawawaheshimu ndugu zao waliotangulia kana kwamba wao hawaelekei huko. Juzi nilimsikia kada mmoja wa chama kipya cha ACT kupitia Star TV akisema, "ana uhakika Chacha Wangwe RIP aliuawa na Chadema", nikajiuliza polisi wako wapi na yeye alikuwa wapi kupeleka ushahidi huo mahakamani wakati wa kesi hadi kupelekea Deusi Mallya kufungwa kwa zaidi ya miaka mitatu. Leo tena nimesikia Antony Diallo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza anataka kumtumia Mallya huyo huyo aliyefungwa kwa kesi ile ile kuendelea kumtumia marehemu Wangwe.
Hizi siasa za kutumia marehemu zimetoka wapi? nani mwanzilishi wake? na zinatupeleka wapi.
Naomba kuwaasa wana CCM wanapoanza kufukua makaburi wasije kujilaumu hapo baadaye wakati makaburi ya ndugu zao yatapoanza kufufuliwa.
Niwakumbushe tu kama CCM wako tayari kutuambia nani alisababisha kifo cha Kolimba, nani alimuua Sokoine, kina nani wako nyuma ya kifo cha Imran Kombe. Kwani Karume Sr. aliuawa na nani? Tukiachilia mbali vifo vyenye utata kama vya (RIP) Malima, Prof Shaba, Dr. Mvungi, Prof. Harub Othman, Prof. Chachage, na wengine wengi, CCM wanaweza kututhibitishia baba wa taifa alikufa tarehe ngapi? Ni maswali mengi ya kujiuliza lakini ukiangalia kwa undani hayana msingi wowote. Tuache kutonesha vidonda.
CCM kama chama au mtu yeyote anayefanya siasa za marehemu aache mara moja kuwatumia marehemu ndugu zetu wapendwa kwenye siasa zao chafu. Kama kuna mtu anapenda sana kutumia marehemu basi awatumie wazazi wake au ndugu zake waliotangulia mbele ya haki. Inasikitisha.
Naomba kuwasilisha.

Katibu Mkuu wa CCM Imrani Kombe aliuliwa na Polisi kwa kupigwa risasi,miezi michache baada ya kusema CCM imepoteza Dira!!
Kumekuwepo na propaganda za kipumb@vu sana kwenye media ya kiongozi wa CCM kutumia makada waliofukuzwa CHADEMA kutumiwa na CCM inayoendesha serikali kusambaza tuhuma za mauaji ya kisiasa!!
Wachunguzi na wafuatiliaji wa kisiasa wanajua kuwa kila awamu ya CCM iliyokaa madarakani ilifanya mauaji ya mtu mmoja mmoja na hata kwa makundi ya watu!!!
Awamu iliyopo madarakani haiwezi kujinasua na mauaji,rejea kupelekwa kwa jeshi mkoani Mtwara na kufanyika uvunjifu wa haki kwa kutumia silaha za moto,ulipuaji wa mabomu kwenye mikutano ya kisiasa na sasa kwenye nyumba za Ibada,Mauaji ya Mwangosi,watesaji wa Kibanda na Mwangosi,kupigwa risasi kwa Sheikh Ponda,kupigwa na kukamatwa viongozi wa uamsho ambao kimsingi wanapinga serikali 2 na sasa wameshughulikiwa na ugaidi,"ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya"!!
Awamu ya Mkapa ilikubuhu zaidi kwa mauaji hadi kufikia hatua ya kuzalisha wakimbizi,rejea mauaji ya Zanzibar 2001,rejea mauaji ya Mwembe Chai ndani ya msikiti na nje,rejea ufukiwaji wa wachimbaji wadogo wadogo kwenye migodi kisa kupisha makaburu kutekeleza sera ya uwekezaji na ubinafsishaji,kutangazwa CUF ni Chama cha Kigaidi na IGP Omary Mahita kuratibu makontena fake ya visu na majambia ya CUF ambapo hadi sasa vinauzwa!!
CCM na vibaraka wake waache kuhatarisha amani kwa kufanya propaganda za kishenzi,
RockSpider 01:11 Today
Diallo, Mchange, Deus Malya et al wanazidi kujidhalilisha! Autopsy iliyofanyika chini ya Prof. Wangwe ilikuwaje? Kwanini Prof. Wangwe na Baadhi ya Ndugu waliwekwa sawa na CCM? Ilikuwaje Makamba Sr akakutwa na Laptop ya Marehemu 15 baada ya ajali? Ilikuwaje Sitta aliipoteza hoja ya Marehemu kuhusiana na Mgodi wa North Mara? Kwanini Sitta alichanganyikiwa sana baada ya ajali? huku akiihusisha na ile hoja yake binafsi kuhusiana na mgodi wa North Mara?
Yule Witness aliekuwepo pale Pandambili yuko wapi sasa hivi? Mkanganyiko kuwa Marehemu alikuwa anaendesha, Mara Malya ndo alikuwa anaendesha ilitatuliwa vipi? Ilikuwaje Marehemu alikuwa kwenye kiti cha nyuma? Ilikuwaje Malya akatoka clean kama bwana harusi kwenye ajali kubwa kama ile? ... Kwanini tusiamini ile theory kuwa Marehemu aliuawa mapema na alisafirishwa hadi eneo la tukio, wakaweka natisha accelerator gari likawa katika mwendokasi na kusababisha ajali ionekane halisi!!! Kuthibitisha hilo; tayari laptop ya Marehemu alikwisha kabidhiwa Katibu Mkuu wa CCM Makamba Sr!!! ...
CCM na wajinga wajinga wengine wote wajue kuwa wanatonesha vidonda vingi sana, watambue kuwa ndugu na Jamaa zetu waliowaua tunajua! Uvumilivu wetu usichukuliwe kama sisi ni Mbumbu sana hatujui kilicho wakumba akina Sokoine, Imran Kombe, Karume, Malima, Kolimba, Nyerere, Mwangosi, Mbwambo, Prof Shaba, Prof. Chachage, Prof. Harub Othman, Dr. Mvungi et al ... RIP Wapendwa wetu... Kibanda na Dr. Ulimboka ni mashuhuda wazuri sana: Mshaurini Diallo awape airtime kama kweli ana mbupuma aka balls ...