CCM na mkutano Temeke mwisho

CCM na mkutano Temeke mwisho

[h=5]Jumanne Miraji Simba
[/h][h=5]KUTANA NA MWANADADA Juliana Shonza....

NIMIONGONI MWA WANADADA WACHECHE WENYE UWEZO WA KUSEMA NA KUKEMIA..

NI MIONGONI MWA WADADA WACHECHE WENYE UWEZO WA KUTAMBA NA KUELEZA MAWAZO YAO JUKWAANI HUKU WAKISIMAMIA UKWELI WAO..

MWANADADA MSOMI NA MWENYE HAMU KUBWA SANA YA KULETA MABADILKO YA KWELI KTK TAIFA LAKE..

JAPO WAPO WATU WACHACHE WANAOTAKA KUKWAMISHA MISMAMO YA MWANASIASA HUYU KIJANA..

[/h]
 
Saumu alikuwa baramade, akawa anafagia makao makuu ya chadema. Chama kikampeleka QT na baadaye kazi ya ukarani ya kujitolea. Hakuwahi kuwa PS wa Katibu Mkuu na kazi yake ilikuwa uchapaji. Mwaka jana tarehe 27 April alimtukana matusi ya nguoni Afisa Mwandamiz Mwita Waitara kwa sabab alikuwa amelewa na hvyo kupelekea kusimamishwa kazi, akakataa kuomba msamaha na kazi akapoteza. Mbona hayo hayasemi leo? Mbulula tu
 
Mtela Mwampamba
KADA WA UKWELI(BINTI KOMANDO) AKIWA NA ALIYEKUWA SEKRETARI WA DR.SLAA (KATIBU MKUU WA CHADEMA) SAUM KISENA WA MWISHO KULIA..AMEHAMIA CCM LEO BAADA YA KUTIBUNA NA DR.SLAA KWENYE MAPENZI,DR.SLAA ALIKUWA NAMLAZIMISHA BINTI HUYU AMPE UNYUMBA

sosi....mwampamba facebook page

Halafu huyu Mwampamba atakuwa na kasoro.. Kwanza huyu binti hajaongea chochote kuhusu kutongozwa pale chadema.. Alichosema pale kwenye mkutano ni kuhusu kutolipwa "haki" zake ikiwa pamoja na nauli.. Hiyo ya kutongozwa na cijui Dr. Slaa naona walisahau kumfundisha kuisema pale..
 
Mkuu hapo mkutano ulikuwa unaendelea .. Saa 10 jioni mpaka 12..

....watu wanataka kusikiliza Mustakabali wa taifa lao si mipasho na matusi wenye akili hawawezi kwenda kuwasikiliza tena...watu wa Dar wameshashtuka.....magamba ni sumu...

Mwanzo walidai ni mkutano wa kuja kufuta uongo na umbea ulioletwa na Chadema.. Baada ya muda wakasema ni mkutano wa kuwapa wananchi mrejesho wa kazi za serikali.. Ila walichokifanya jukwaani ni kuwapandisha Juliana na Mwampamba ambao waliizungumzia Chadema.. Akampandisha Jerry Silaa ambae akaizungumza Chadema.. Akaja Naibu Meya wa kinondoni na Temeke ambao wakaizungumzia Chadema.. Akaja Zungu na naibu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge inayohusu maji akaizungumzia Chadema.. Akapanda Mtemvu akaizungumiza Chadema.. Madabida a.k.a mzee wa arv fake akaizungumzia Chadema.. Waziri Maghembe na akaizungumzia Chadema.. Mkuu wa Mkoa akaizungumzia Chadema.. Nape ndo akawa kinara wa kuizungumzia Chadema.. Mwisho wa siku wakasahau kilichowapeleka Temeke mwisho.. Wakawa wanaizungumzia Chadema na Serikali yake..
 
fyonza na mamatela waoane kabisa kwa kuwa wanafanana mpaka jinsia, semeni na njaa zenu, hayo ingekuewa vema mngesema kabla ya kufukuzwa chadema
 
fyonza na mamatela waoane kabisa kwa kuwa wanafanana mpaka jinsia, semeni na njaa zenu, hayo ingekuewa vema mngesema kabla ya kufukuzwa chadema

Nina shaka na Shonza inaweza kuwa ama chakula ya muzeee au inataka kujibananisha kwa muzeee.. Wakati wengine walikuwa na salamu za ccm oyeee yeye alimtaja muzeee oyeee...
 
Weka picha Mkuu...

hivi kwa mawazo yako picha itakayopigwa na pro chadema itaonyesha kwenye watu? mbona tunawajua siku nyingi? na chadema kama hawana watu utawaona wanapiga viongozi tu. magwanda bana!
 
picha_CCM.jpg

Bendera ya Chama Cha Mapinduzi

Mkutano huo wa Chadema ulifanyika Jumapili iliyopita, ambapo viongozi wake walitoa tuhuma mbalimbali kueleza jinsi Spika Makinda na naibu wake walivyotupa hoja za Mbunge wa Ubungo, John Mnyika na James Mbatia ambaye ni Mbunge wa Kuteuliwa.

WIKI moja baada ya Chadema kufanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Temeke Mwisho jijini Dar es Salaam na kuwashukia Spika wa Bunge, Anne Makinda na Naibu wake, Job Ndugai, CCM jana ilifanya mkutano katika viwanja hivyo, huku ikijibu hoja zilizotolewa na chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe alisema hoja ya Mnyika kuhusu uhaba wa maji katika Jiji la Dar es Salaam, ilitupwa kwa kuwa alichokuwa akikizungumza mbunge huyo, kilikuwa kikifanyiwa kazi na Serikali.

"Mnyika anatakiwa kutosherehekea mimba wakati mwenye mtoto ni CCM, Serikali ya CCM ndiyo imeweka miradi iliyopo katika Jimbo la Ubungo na inaiendeleza," alisema Maghembe.

Alifafanua kwamba Mtambo wa Maji wa Ruvu Chini utakamilika kujengwa mwishoni mwa mwezi huu na utazinduliwa na Rais Jakaya Kikwete.

"Serikali imejianda kuhakikisha kwamba Mkoa wa Dar es Salaam unakuwa na maji ya kutosha katika mpango wake wa muda mfupi na mrefu. Katika mpango wa muda mfupi mpaka kufikia Aprili 2014, maji yatakuwa ya kutosha katika jiji hili," alisema Maghembe.

Alisema kuwa hivi sasa Serikali ipo katika mpango wa kutandaza mabomba ya maji kutoka Ruvu Juu kwenda Dar es Salaam kupitia Bagamoyo, ambapo utaenda sambamba na uchimbaji wa visima 84.

Katika mkutano huo Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji, Neema Himid alisema kuwa hoja iliyowasilishwa na Mnyika bungeni ilikuwa ni; ‘Copy and Paste', (ya kamati hiyo).

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi waandamizi wa CCM akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, baadhi ya wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam.
 
hivi kumbe ni lazima angalau bomba lifike tu bagamoyo! manake la gesi ishakuwa kitendawili sasa la maji lazima. mmh!!! kaaaaazi kweri kweri, mpaka mpangaji wetu mkataba utakapoisha nyuma itakuwa ishavurugwa kinoma. mimi najiweka pembeni naepuka msongamano.
 
WIKI moja baada ya Chadema kufanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Temeke Mwisho jijini Dar es Salaam na kuwashukia Spika wa Bunge, Anne Makinda na Naibu wake, Job Ndugai, CCM jana ilifanya mkutano katika viwanja hivyo, huku ikijibu hoja zilizotolewa na chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Mkutano huo wa Chadema ulifanyika Jumapili iliyopita, ambapo viongozi wake walitoa tuhuma mbalimbali kueleza jinsi Spika Makinda na naibu wake walivyotupa hoja za Mbunge wa Ubungo, John Mnyika na James Mbatia ambaye ni Mbunge wa Kuteuliwa.

Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe alisema hoja ya Mnyika kuhusu uhaba wa maji katika Jiji la Dar es Salaam, ilitupwa kwa kuwa alichokuwa akikizungumza mbunge huyo, kilikuwa kikifanyiwa kazi na Serikali.

“Mnyika anatakiwa kutosherehekea mimba wakati mwenye mtoto ni CCM, Serikali ya CCM ndiyo imeweka miradi iliyopo katika Jimbo la Ubungo na inaiendeleza,” alisema Maghembe.

Alifafanua kwamba Mtambo wa Maji wa Ruvu Chini utakamilika kujengwa mwishoni mwa mwezi huu na utazinduliwa na Rais Jakaya Kikwete.

“Serikali imejianda kuhakikisha kwamba Mkoa wa Dar es Salaam unakuwa na maji ya kutosha katika mpango wake wa muda mfupi na mrefu. Katika mpango wa muda mfupi mpaka kufikia Aprili 2014, maji yatakuwa ya kutosha katika jiji hili,” alisema Maghembe.

Alisema kuwa hivi sasa Serikali ipo katika mpango wa kutandaza mabomba ya maji kutoka Ruvu Juu kwenda Dar es Salaam kupitia Bagamoyo, ambapo utaenda sambamba na uchimbaji wa visima 84.

Katika mkutano huo Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji, Neema Himid alisema kuwa hoja iliyowasilishwa na Mnyika bungeni ilikuwa ni; ‘Copy and Paste’, (ya kamati hiyo).

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi waandamizi wa CCM akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, baadhi ya wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam.

source: mwananchi
 
Kuhusu maji ccm inaendelea kuwahadaa wananchi. Kila mara wanasema tu kwamba kuna miradi kadhaa ya muda mfupi na muda mrefu lakini sehemu kubwa ya jiji la Dsm imeendelea kukosa maji.

Na ikifika mwaka 2014 nina uhakika huo mradi anaousema maghembe utakuwa haujakamilika na mahitaji ya maji yatakuwa makubwa zaidi kuliko sasa.
 
Kuhusu maji ccm
inaendelea kuwahadaa wananchi. Kila mara wanasema tu kwamba kuna miradi
kadhaa ya muda mfupi na muda mrefu lakini sehemu kubwa ya jiji la Dsm
imeendelea kukosa maji.

Na ikifika mwaka 2014 nina uhakika huo mradi anaousema maghembe utakuwa
haujakamilika na mahitaji ya maji yatakuwa makubwa zaidi kuliko
sasa.

hahaaaa post za rangi ya kijani humu huwa hazina mashiko maskini! kwel huwez lazimisha kupendwa ila unaweza lazimisha kupenda
 
Mbona unasahau kueleza vile vile kuwa kumbe Mnyika siyo graduate wa chuo chochote nchini.
 
Kuhusu maji ccm inaendelea kuwahadaa wananchi. Kila mara wanasema tu kwamba kuna miradi kadhaa ya muda mfupi na muda mrefu lakini sehemu kubwa ya jiji la Dsm imeendelea kukosa maji.

Na ikifika mwaka 2014 nina uhakika huo mradi anaousema maghembe utakuwa haujakamilika na mahitaji ya maji yatakuwa makubwa zaidi kuliko sasa.
Mkuu kijana wenu kumbe ni wa mwembeni!
Hoja yake imejibiwa kirahisi sana.
 
CCM HAMNAZO! Afu na mashaka na elimu ya maprofesa wengi! kwanin wizara zao zimelala!Angalia madini+nishati prof,maji prof.Nk.
 
Ukipima u-profesale wa maghembe na elimu ya kawaida ya Mnyika kwenye kuwasilisha na kujenga hoja naona tofauti kubwa sana ya maono na mantiki. Huenda hiyo phd ya AVAE ni ile watoto wa mjini wanaita pure head damage (phd).
 
Maji muhimu tuondoe siasa hapo.

Toka kwa MrArsenal

Kama nipo sahihi tuliambiwa tatizo la maji kuwa historia 2013 sasa imeshakuwa 2014!? Muda si mrefu tutaambiwa 2016, nadhani ili suala mbali ya upungufu wa maji kuna watendaji wanakwamisha kwa njia moja au nyingine.
Mimi naishi salasala ajabu maji yanapita kwenda mjini tunaambiwa eti watu wa salasala maji hayawezi kupanda, tunashindwa kuelewa yanatokaje ruvu, au ruvu ni mtelemko hadi Dar! !?, yanapandaje kwenye magorofa? tatizo huku salasala mpaka goba kuna malori kibao ya kuuza maji,nadhani wakiondoa tatizo la maji au kulipunguza,biashara ya maji itakufa na inavyoonekana inawanufaisha wengi, dawasco boko mjiandae tumechoka, maandamano ya kihonda muda si mrefu yataibukia hapo,tunasubiri mkutano wa kata tufanye maamuzi, inavyoonekana watendaji wa serikali hii wengi mpaka washinikizwe.
 
Back
Top Bottom