eden kimario
JF-Expert Member
- Jun 13, 2015
- 10,356
- 16,401
Kwanza naomba nirudie maneno ya nape nnauye kuwa ccm ilikuwa inaelekea shimoni
Na siyo shimoni tu sasa inaelekea kufa kabisa 2020 itatupa picha tu ya kule ccm ya magufuli inakoelekea
Njaa, pesa kutokuonekana kwa wajasiriamali,wenye maduka, huku kodi zikiwa zimeongezwa mara dufu sidhani kama mwananchi wa kawaida vijijini na mijini watauelewa huu utawala
Kiujumla watu wanabangaiza tu
Kazi za kufanya wanazo lakini pesa zinazotakiwa kutokana na kazi walizonazo hawazipati
Mtu alieshiba atakuelewa ila mtu ambaye shida zimemzunguka tena akijua utawala unashiriki kumkamua sifikirii kama atauelewa utawala uliopo
Ccm na magufuli ni waigizaji wazuri sana kama filamu za mambo ya utawala
Leo wanauchungu kesho hawana uchungu na taifa
Elimu bure imekuwa ni maigizo badala ya elimu bure imekuwa ni elimu bila ADA
Huku magufuli akijidai ni mzalendo kwelikweli alikutana na mtu aliemtuhumu kuwa ni mwizi wa watanzania kuhusu midhahabu yetu na akaishia kucheka na kutabasamu huku akiudanganya uma kuwa tutalipwa huku aliowaita wezi wakikanusha kutulipa
Akajidai kumwagiza ndugai mikataba ya madini irudishwe bungeni ijadiliwe kwa kina huku ndugai akiipokea kwa hati ya dharura na kutenga siku tatu tu za kuijadili
Hivi kwa akili ya kawaida tuko serious kweli na hiyo mikataba ya madini
Sasa mbwembwe zote zile za sisi ccm na magufuli ni wazalendo ndizo hizi kweli?
Ni serikali hii hii ambayo haiwezi kununua mazao ya chakula kutoka kwa wananchi ukiwauliza pesa hawana za kununua
Wananchi wameamua kuuza ndani ya nchi tu mazao yao mwisho wa siku wanaishia kukamatiwa mazao yao na serikali hii hii inataka kutaifisha mazao yaliyokamatwa bure huu hauna tofauti na wizi tena wizi wa mchana kweupe ambao Utawala huu unawaibia raia wake
Tukumbuke pesa inapatikana kwa kuuza kile ulichokipanda la sivyo utaishi maisha magumu tu
Mwisho serikali hii inayojinasibu ya viwanda uchumi unaendelea kukua kwa wenye nazo tu wananchi wa kawaida ukiwaambia uchumi unakuwa wakati pesa hana ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa ukitegemea atacheza
Kiukweli serikali hii inawakamua sana raia wake haina huruma na raia wake mpaka sasa
Serikali hii toka imeingia madarakani inapambana kurekebisha utawala tu ila ahadi kama ahadi hazitekelezeki mpaka sasa
Halafu unashangaa mtu anasimama anasema tumetekeleza ahadi zetu kwa asilimia 80
Zipi hizo mlizotekeleza?
Uchumi mbaya kwa wananchi wa kawaida kazi kutokuzaa pesa kama ilivyokuwa ni moja ya mambo ambayo yanaipeleka ccm na magufuli shimoni
Nakumbusha tu kuhusu uchaguzi uliopita ccm mlishinda kwa asilimia 58
Upinzani asilimia 40
Mtapiga wenyewe mahesabu wamezidiana kwa asilimia ngapi
Yangu macho
Na Eden kimario