Mkuu hiyo idara pia nadhani imefahamu kuwa inawalazimisha watanzania kuongozwa kwa shuruti, na sio kwa ridhaa yao. Maana 2/3 hawakujitokeza kupiga kura, maana hiyo 1/3 bado wote hawakuipa kura ccm. Nadhani saa hii wanamaliza kuhesabu kura kujua ukweli kuwa ccm sio chama cha kizazi hiki na zama zake zimepita.
Hilo la hiyo idara kuanzisha chama kingine cha siasa mbadala wa cdm liko wazi, lakini wana uwezo wa kuanzisha chama kitakacho kubalika na watu? Maana ccm imefanya Siasa yenyewe kwa miaka mitano, lakini bado imeshindwa kushawishi watu, je hicho chama chao ndio kitavutia watu? Tunajua kwenye hili bunge kibogoyo, kutafanyika drama ili kutengeneza mpasuko bandia kwa ajili ya kuleta chama mbadala, lakini watu sasa hivi ni waelewa, wanachagua watakacho na sio wanacholetewa. Mfano mrahisi ni huyo Membe, alitengeneza mpasuko fake ulioratibiwa na hiyo idara. Mbona hajapata mvuto wala kupoteza watu maboya? Ni hivi cdm imeshakuwa, uwezo wa kuia haupo tena, sana sana kutakuwa na wapiga kura wachache sana.