DSN
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 2,837
- 1,674
TUKO TAYARI
Tanganyika=Tanzania Kabla Ya Uhuru 1961
Tanzania Huru
Tanzania Baada ya Miaka 50 ya Uhuru
TUNAITAJI WIMO HUU KULUDISHA NCHI KWENYE MSTARI
1. Mungu Ibariki Afrika, (God Bless Africa)
Wabariki Viongozi Wake, (bless her leaders)
Hekima, Umoja na Amani (wisdom, unity and peace)
Hizi ni Ngao Zetu, (these are our shields)
Afrika na Watu Wake. (Africa and her people)
Ibariki, Afrika, (Bless,Africa)
Ibariki, Afrika, (Bless,Africa)
Tubariki, Watoto wa Afrika, (Bless, Children of Africa)
2. Mungu Ibariki Tanzania, (God Bless Tanzania)
Dumisha Uhuru na Umoja, (sustain independence and unity)
Wake kwa Waume na Watoto,(Women, Men and Children)
Mungu, Ibariki, (God, Bless,)
Tanzania na Watu Wake (Tanzania and her people)
Ibariki, Tanzania, (Bless,Tanzania)
Ibariki, Tanzania, (Bless,Tanzania)
Tubariki, Watoto wa Tanzania (Bless, Children of Tanzania)
Kama Taifa Huru Miaka 50 sijaona Wimbo Huu Kuonyesha Mwanga wa Uzalendo kwa Moyo wa Dhati kwa Watanzania.Wimbo huu ni kwa ajili ya sherehe za Kitaifa au Ni kwa ajili ya Maisha yetu ya kila siku na kuwa tukiusikia na kuimba popote yatupasa vinyeleo vya mwili kusisimka kwa damu ya Uzalendo wa Tanzania mbele na si vyama vya siasa mbele.
Kwenye miaka ya 1970 a 1980 kulikuwa na nyimbo za kizazi cha miaka hiyo kama wimbo huu wa kuisifu Tanzania "Tazama ramani unataona Nchi nzuri,yenye mito na mabaonde mengi ya nafaka...."
Je Serikali yetu ina mikakati gani ya kutunga wimbo wa kuhamasisha [Stimulate] vijana wa kizazi kipya [New Generation] kuwa na mwamko wa kuipenda Nchi yao pasipokujali itikadi ya kichama bali itikadi ya Kitaifa,zile nyimbo fupi zenye hisia na mwamko wa kumjenga kijana wa Tanzania kujua kuwa yuko tayari kufa kwa ajili ya Tanzania. Nimeusikia wimbo wa miaka Hamsini ukpo sawa kama wimbo tu,lakini sio wimbo ambao upo maalumu usioitaji midundo [melody] kuwa wimbo wa uzalendo ambao vijana wa leo miaka 15-35 watakapofika miaka 60-70 watakuwa na kumbukumbu ya uzalendo wa Kinchi na sio huu unaojengwa sasa wa KICCM NA KICHADEMA.
Vyama vya kisasa CCM na CDM kabla ya kuendesha mikutano yenu ya kisiasa wimbo wa Taifa unatumika vipi kuleta hisia za uzalendo pamoja na kuwa na tofauti ya kiitikadi ?