CCM NA CHADEMA Uzalendo Wa Miaka 50 Unaanzia Kwenye Wimbo Wa Taifa!!!!!!!!!!!!!!!

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674

TUKO TAYARI

baobab-tanzania.jpg
Tanganyika=Tanzania Kabla Ya Uhuru 1961

Flag_Tanzania.jpg
Tanzania Huru

3731.tanzania1.jpg
Tanzania Baada ya Miaka 50 ya Uhuru

TUNAITAJI WIMO HUU KULUDISHA NCHI KWENYE MSTARI


1.
Mungu Ibariki Afrika, (God Bless Africa)

Wabariki Viongozi Wake, (bless her leaders)
Hekima, Umoja na Amani (wisdom, unity and peace)
Hizi ni Ngao Zetu, (these are our shields)
Afrika na Watu Wake. (Africa and her people)
Ibariki, Afrika, (Bless,Africa)
Ibariki, Afrika, (Bless,Africa)
Tubariki, Watoto wa Afrika, (Bless, Children of Africa)


2. Mungu Ibariki Tanzania, (God Bless Tanzania)

Dumisha Uhuru na Umoja, (sustain independence and unity)
Wake kwa Waume na Watoto,(Women, Men and Children)
Mungu, Ibariki, (God, Bless,)
Tanzania na Watu Wake (Tanzania and her people)
Ibariki, Tanzania, (Bless,Tanzania)
Ibariki, Tanzania, (Bless,Tanzania)

Tubariki, Watoto wa Tanzania (Bless, Children of Tanzania)


Kama Taifa Huru Miaka 50 sijaona Wimbo Huu Kuonyesha Mwanga wa Uzalendo kwa Moyo wa Dhati kwa Watanzania.Wimbo huu ni kwa ajili ya sherehe za Kitaifa au Ni kwa ajili ya Maisha yetu ya kila siku na kuwa tukiusikia na kuimba popote yatupasa vinyeleo vya mwili kusisimka kwa damu ya Uzalendo wa Tanzania mbele na si vyama vya siasa mbele.

Kwenye miaka ya 1970 a 1980 kulikuwa na nyimbo za kizazi cha miaka hiyo kama wimbo huu wa kuisifu Tanzania "
Tazama ramani unataona Nchi nzuri,yenye mito na mabaonde mengi ya nafaka...."

Je Serikali yetu ina mikakati gani ya kutunga wimbo wa kuhamasisha [Stimulate] vijana wa kizazi kipya [New Generation] kuwa na mwamko wa kuipenda Nchi yao pasipokujali itikadi ya kichama bali itikadi ya Kitaifa,zile nyimbo fupi zenye hisia na mwamko wa kumjenga kijana wa Tanzania kujua kuwa yuko tayari kufa kwa ajili ya Tanzania. Nimeusikia wimbo wa miaka Hamsini ukpo sawa kama wimbo tu,lakini sio wimbo ambao upo maalumu usioitaji midundo [melody] kuwa wimbo wa uzalendo ambao vijana wa leo miaka 15-35 watakapofika miaka 60-70 watakuwa na kumbukumbu ya uzalendo wa Kinchi na sio huu unaojengwa sasa wa KICCM NA KICHADEMA.

Vyama vya kisasa CCM na CDM kabla ya kuendesha mikutano yenu ya kisiasa wimbo wa Taifa unatumika vipi kuleta hisia za uzalendo pamoja na kuwa na tofauti ya kiitikadi ?
 
Mkuu heshima. Mimi naamini hata kama tungekuwa na wimbo wa taifa mzuri na mtamu kushinda zile za Gabriel na timu yake waimbazo wakizunguka kile Kiti cha Enzi; ambazo imenenwa kwamba sauti zao ni tamu kushinda vinanda na vinubi vyote vilivyopata kuwepo; bila HESHIMA, HAKI, na KUMJALI MNYONGE, wimbo huo ni ubatili tena wafanana na sauti za waombolezao.

UZALENDO kwa taifa ni kitu ambacho hakihitaji kuchochewa kwa ghiliba kama za kutunga nyimbo mpya, kugawa vibendera, au kuvaa mavazi fulani waliyobuni watawala. Badala yake, ni kitu ambacho huja au hutoweka chenyewe kutegemea na jinsi tabaka la walio wengi linavyotendewa. Ukisikia kwa mfano vijana wanaamini ni heri kuwa mbwa Ulaya kuliko binadamu Tanzania ujue uzalendo umekwisha na uzalendo huu haurudishwi kwa kutunga nyimbo mpya.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Mkuu heshima. Mimi naamini hata kama tungekuwa na wimbo wa taifa mzuri na mtamu kushinda zile za Gabriel na timu yake waimbazo wakizunguka kile Kiti cha Enzi; ambazo imenenwa kwamba sauti zao ni tamu kushinda vinanda na vinubi vyote vilivyopata kuwepo; bila HESHIMA, HAKI, na KUMJALI MNYONGE, wimbo huo ni ubatili tena wafanana na sauti za waombolezao.

UZALENDO kwa taifa ni kitu ambacho hakihitaji kuchochewa kwa ghiliba kama za kutunga nyimbo mpya, kugawa vibendera, au kuvaa mavazi fulani waliyobuni watawala. Badala yake, ni kitu ambacho huja au hutoweka chenyewe kutegemea na jinsi tabaka la walio wengi linavyotendewa. Ukisikia kwa mfano vijana wanaamini ni heri kuwa mbwa Ulaya kuliko binadamu Tanzania ujue uzalendo umekwisha na uzalendo huu haurudishwi kwa kutunga nyimbo mpya.


Wapiganaji wakubwa [warrior] daima uwa wanapoingia kwenye mapambano utumia vichochezi vya mihemko ili kutoa na kupata nguvu kwa wapiganaji kusonga mbele katika mapambano yao.Tena siku hizi kwa mataifa makubwa kama Marekani uwa wanawapeleka wanamziki wao eneo la vita kuwapa moyo wapiganaji wao kupitia muziki.Muziki au nyimbo ni sehemu ya maisha ndio maana dunia nzima mziki au nyimbo ubeba maana moja katika maisha ya Mwanadamu.

Muziki uhamasisha [Inspire] wahusika kwa jambo la dhati na kuludisha picha muhimu ya muhusika,ndio maana makanisani kuna kwaya,na miskitini kuna kaswida nk.

Napo kama Taifa ili kuludi kwenye mstari kuona kuwa yale ya msingi ambayo kwa kiwango kikubwa tunaona siyo ya msingi,kuanza kuyazingatia na kutengeneza moyo wa uzalendo.Kwa leo hii si ajabu kuona na kusikia Wanafunzi kuanzia ngazi ya shule ya msingi mpaka chuo na kisha mitaani hawajui wimbo wa Taifa wala wimbo wa kuisifia Nchi yao.

Tumepotea,japo wakubwa wetu wanaona wako sahihi.Unawezaje kuanzisha Mkutano au shughuri yoyote ya umma wa kitaifa,Mkoa,Wilaya,Kata au Kijiji pasipo wimbo wa Taifa.Au kuendesha jambo lolote lile lianalohusu umma mkubwa bila kualika Mwamko wa wahusika kwa kuitisha wimbo wa Taifa kama kitu kinachowaunganisha wananchi toka kada na itikadi tofauti wakashiriki wote pasipo kujali itikadi yao ya kisasa.
 
Back
Top Bottom