Mimi naipongeza Jamiiforums kuweka tangazo la CCM. Huu ni uthibitisho kuwa JF ni non partisan kwenye party politicts, ni impartial na ina play neutrality which is a good move.
Tangazo kama hili lina neutralizes sentiments kuwa JF ni pro- Chadema. Wana Chadema wengi wamo humu kwa majina yao kwa vile wana feel wako free, wanaCCM kama Nape, pia waliingia kwa majina yao lakini wako kimya labda kwa hisia hizo hizo kuwa JF ni jukwaa la Chadema, tangazo kama hili ni uthibitisho tosha kuwa JF ni zaidi ya itikadi za vyama.
Nakushukuru tena kwa mwaliko huu, wife wangu ni CCM damu, mimi nitamsindikiza na nitachangia kwa moyo wote ili kulinda amani ya familia na kusocialize.
Natoa wito kwa wale wengine wasio na vyama kama mimi, kulipa 60,000/= dinner for two, Golden Tulip, is not a big deal, nitachangia kwa moyo mkunjufu sana, kwa vile siasa za Moshi, nazielewa fika, hata wakipata bilioni 100 ili kumng'oa Ndesa, watakuwa wanacheza makida makida, sio tuu CCM itaangukia pua, bali Mwenyekiti wao ataonekana kama Joti mbele ya umma wa Watanzania.
Pole Rev Kishoka kutofautiana na wewe kwenye hili, sometime ili ushinde vita sio lazima kupigana front line kwenye uwanja wa mapambano, unaweza ku-infiltrate watu wako miongoni mwao na ukaishia kuwalipua from within, hivyo kuepusha kiwango cha casuality.
Deal lote hili sio la Mama Swai, ni la kijana ambitious aliowaingiza CCM mkenge akijiaminisha Wachagga nao watauza utu wao kwa fulana na kofia pamoja na shibe ya siku moja!. Mama Swai anajua wazi Ndesa ni kisiki cha Mpingo ila kijana ni lobbyist mzuri, amemlobi mpaka Mkulu kutembeza bakuli, namhurumia watamtia aibu ya bure!.
Ila baada ya kuboronga juzi alipowahutubia Wazee wa (CCM) Darisalaam, natumaini wamesha soma dalili za nyakati, hivyo wasaidizi wake watamshauri asiende.
Kusipotokea mwana JF mwingine ambaye atakwenda, basi nitawajulisha kinachoendelea ingawa nadhani TV ya Mangi, itaonyesha live na sio TBC. Na kama itakuwa ni TBC, itabidi nishangae. Bila kusahau, MC wa CCM, ni yule yule Mtangazaji Maarufu kuliko watangazaji wote wa Redio za FM hapa jijini Dar es Salaam na nchini Tanzania kwa ujumla (naomba usibishe wala usiniulize), kwa jina maarufu la Kibonde, (ni jina tuu, sio Kibonde wa wale vibonde, shuleni alikuwa kipanga!)
Karibuni Sana.