CCM msiipoteze hii fursa tena

Kama hujui hata tozo unazolalamikia ni 'made in Jiwe' wala hata usingejipendekeza kwa mzimu!
NB: Ninachounga mkono ni kuanzishwa kwa mkoa wa Chato ili tudhibiti wahamiaji haramu kutoka nchi za wenye shari na sisi!
Unalazimisha Sana mambo .. yaani Ilimuradi tu uturudishe nyuma kwà Marehemu.

Mwache Mama afanye kazi zake kwà Uhuru.

Unataka kusema mama ana copy tu hata vitu visivyo na manufaa kwà wananchi?

Tafadhari bana. ..acha mzimu ukutese wewe na familia yako pengine na ukoo wako na kizazi chako

Sisi tunasonga mbele kwà kuangalia waliopo madarakani..
 
Marehem Kolimba alisema CCM haina dira, na ghafla macho yote ya wana CCM yakaelekezwa kwake na, ninasikia, alikufa alipopewa kipaza sauti ajieleze ati kwanini alifikiri CCM haina dira!

Pamoja na kazi za ujenzi wa miundombinu mingi zilizofanywa na serikali ya awamu ya tano, bado kuna wana CCM, na watanzania wengi nje ya chama hicho, wanaoamini kuwa maovu yaliyofanywa na rais Magufuli yamezidi uzito mema aliyotamba kulifanyia taifa hili!

Mara baada ya mazishi ya hayati Magufuli watu wengi wamekuwa wakijaribu kuongelea hitilafu kubwa za utawala wa Magufuli ikiwa ni pamoja na kukiuka matakwa ya katiba ya nchi na kupuuza haki za binaadam na utawala bora, ikienda sambamba na kutaka kuifanya Tanzania kisiwa Duniani kwa sera zake mbovu za mahusiano ya kimataifa.

Ajabu kubwa ni kwamba kuna kundi la wapuuzi na wanafiki ndani ya CCM linalofikiri kuwanyamazisha watu wanaotoa maoni yao sahihi kuhusi hatari ya kutawaliwa na watawala madikteta, kama Magufuli, ndio njia sahihi ya kulinda 'legacy' ya utawala mbovu wa Magufuli!

CCM, hii tuliyonayo ni fursa adimu sana kuwahi kutokea kwa ajili ya kuandaa kesho salama kwa ajili ya vizazi vijavyo vya Watanzania! ... ni muda muafaka sasa wa kuliita koleo koleo kama alivyofanya mwenyekiti wa CCM, Mwanza, mheshimiwa Anthony Diallo, ili nchi hii isirudie tena kuangukia mikono isiyo salama kama ya Hayati Magufuli. ... Watu wenye majibu ya haraka haraka kama mbunge wa Geita vijijini, MUSUKUMA, wanaokurupuka na kuanza kumporomoshea mvua ya matusi kila mkosoaji ni wa kuogopa kama ukoma!

Kwamba nchi ilikabidhiwa kwa mtu asiyestahili hii ni wazi hata kwa watoto wadogo, huu ulikuwa ni uzembe uliofanywa na MAJORITY, ... na hata MAJORITY ikijitetea namna gani bado ukweli unabakia kuwa nchi ilikabidhiwa kwa mtu aliyekuwa hafai TU!

Sasa CCM isiipoteze fursa hii kwa kupuuza maneno ya watu waungwana, wakweli, wanaojali kesho yetu na kukumbatia wagombea tonge na umashuhuri usio na manufaa yeyote ya muda mrefu kwa taifa letu, kina MUSUKUMA, ambao wakishiba wao wengine watajiju! ... huu ni muda wa kuitafuta dira yenu aliyowaambia Kolimba mmeipoteza mkamkodolea majicho hadi 'PRESSURE' ikampanda! ... ni wakati wa kuwakutanisha watu waliotofautiana kwa kugawanywa na utawala wa Jiwe ili mchambue mchele na chuya!

KATIBA BORA HAIEPUKIKI!

BECAUSE ... NEVER EVER AGAIN!




:cool:
Pamoja na kazi za ujenzi wa miundombinu mingi zilizofanywa na serikali ya awamu ya tano, bado kuna wana CCM, na watanzania wengi nje ya chama hicho, wanaoamini kuwa maovu yaliyofanywa na rais Magufuli yamezidi uzito mema aliyotamba kulifanyia taifa hili!
 
Mbupu kweli
... kamua!
1626497117730.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom