CCM msiipoteze hii fursa tena

Kishimbe wa Kishimbe

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
4,658
4,160
Marehem Kolimba alisema CCM haina dira, na ghafla macho yote ya wana CCM yakaelekezwa kwake na, ninasikia, alikufa alipopewa kipaza sauti ajieleze ati kwanini alifikiri CCM haina dira!

Pamoja na kazi za ujenzi wa miundombinu mingi zilizofanywa na serikali ya awamu ya tano, bado kuna wana CCM, na watanzania wengi nje ya chama hicho, wanaoamini kuwa maovu yaliyofanywa na rais Magufuli yamezidi uzito mema aliyotamba kulifanyia taifa hili!

Mara baada ya mazishi ya hayati Magufuli watu wengi wamekuwa wakijaribu kuongelea hitilafu kubwa za utawala wa Magufuli ikiwa ni pamoja na kukiuka matakwa ya katiba ya nchi na kupuuza haki za binaadam na utawala bora, ikienda sambamba na kutaka kuifanya Tanzania kisiwa Duniani kwa sera zake mbovu za mahusiano ya kimataifa.

Ajabu kubwa ni kwamba kuna kundi la wapuuzi na wanafiki ndani ya CCM linalofikiri kuwanyamazisha watu wanaotoa maoni yao sahihi kuhusi hatari ya kutawaliwa na watawala madikteta, kama Magufuli, ndio njia sahihi ya kulinda 'legacy' ya utawala mbovu wa Magufuli!

CCM, hii tuliyonayo ni fursa adimu sana kuwahi kutokea kwa ajili ya kuandaa kesho salama kwa ajili ya vizazi vijavyo vya Watanzania! ... ni muda muafaka sasa wa kuliita koleo koleo kama alivyofanya mwenyekiti wa CCM, Mwanza, mheshimiwa Anthony Diallo, ili nchi hii isirudie tena kuangukia mikono isiyo salama kama ya Hayati Magufuli. ... Watu wenye majibu ya haraka haraka kama mbunge wa Geita vijijini, MUSUKUMA, wanaokurupuka na kuanza kumporomoshea mvua ya matusi kila mkosoaji ni wa kuogopa kama ukoma!

Kwamba nchi ilikabidhiwa kwa mtu asiyestahili hii ni wazi hata kwa watoto wadogo, huu ulikuwa ni uzembe uliofanywa na MAJORITY, ... na hata MAJORITY ikijitetea namna gani bado ukweli unabakia kuwa nchi ilikabidhiwa kwa mtu aliyekuwa hafai TU!

Sasa CCM isiipoteze fursa hii kwa kupuuza maneno ya watu waungwana, wakweli, wanaojali kesho yetu na kukumbatia wagombea tonge na umashuhuri usio na manufaa yeyote ya muda mrefu kwa taifa letu, kina MUSUKUMA, ambao wakishiba wao wengine watajiju! ... huu ni muda wa kuitafuta dira yenu aliyowaambia Kolimba mmeipoteza mkamkodolea majicho hadi 'PRESSURE' ikampanda! ... ni wakati wa kuwakutanisha watu waliotofautiana kwa kugawanywa na utawala wa Jiwe ili mchambue mchele na chuya!

KATIBA BORA HAIEPUKIKI!

BECAUSE ... NEVER EVER AGAIN!

👊 :cool:✌️💥
 
Yote tisa ila kumi ni kwamba ccm muda wake wa kuliongoza hili taifa umekwisha. Ndio maana kila njia wanayoitumia ili waonekane kuwa bado zama zinawakubali zinafeli.

kama ccm mda wake umeisha chama gani kitaweza kuongoza chaggadema ni ovyo bora ccm tutarnda nayo hivyohivyo
 
mpuuzi wewe huna lolote. makufuli atakumbukwa daima
Hamuwezi kukinyamazisha kizazi kilichoamka!
1626451568610.png
 
Marehem Kolimba alisema CCM haina dira, na ghafla macho yote ya wana CCM yakaelekezwa kwake na, ninasikia, alikufa alipopewa kipaza sauti ajieleze ati kwanini alifikiri CCM haina dira!

Pamoja na kazi za ujenzi wa miundombinu mingi zilizofanywa na serikali ya awamu ya tano, bado kuna wana CCM, na watanzania wengi nje ya chama hicho, wanaoamini kuwa maovu yaliyofanywa na rais Magufuli yamezidi uzito mema aliyotamba kulifanyia taifa hili!

Mara baada ya mazishi ya hayati Magufuli watu wengi wamekuwa wakijaribu kuongelea hitilafu kubwa za utawala wa Magufuli ikiwa ni pamoja na kukiuka matakwa ya katiba ya nchi na kupuuza haki za binaadam na utawala bora, ikienda sambamba na kutaka kuifanya Tanzania kisiwa Duniani kwa sera zake mbovu za mahusiano ya kimataifa.

Ajabu kubwa ni kwamba kuna kundi la wapuuzi na wanafiki ndani ya CCM linalofikiri kuwanyamazisha watu wanaotoa maoni yao sahihi kuhusi hatari ya kutawaliwa na watawala madikteta, kama Magufuli, ndio njia sahihi ya kulinda 'legacy' ya utawala mbovu wa Magufuli!

CCM, hii tuliyonayo ni fursa adimu sana kuwahi kutokea kwa ajili ya kuandaa kesho salama kwa ajili ya vizazi vijavyo vya Watanzania! ... ni muda muafaka sasa wa kuliita koleo koleo kama alivyofanya mwenyekiti wa CCM, Mwanza, mheshimiwa Anthony Diallo, ili nchi hii isirudie tena kuangukia mikono isiyo salama kama ya Hayati Magufuli. ... Watu wenye majibu ya haraka haraka kama mbunge wa Geita vijijini, MUSUKUMA, wanaokurupuka na kuanza kumporomoshea mvua ya matusi kila mkosoaji ni wa kuogopa kama ukoma!

... kwamba nchi ilikabidhiwa kwa mtu asiyestahili hii ni wazi hata kwa watoto wadogo, huu ulikuwa ni uzembe uliofanywa na MAJORITY, ... na hata MAJORITY ikijitetea namna gani bado ukweli unabakia kuwa nchi ilikabidhiwa kwa mtu aliyekuwa hafai TU!

Sasa CCM isiipoteze fursa hii ya kupuuza maneno ya watu waungwana, wakweli, wanaojali kesho yetu na kukumbatia wagombea tonge na umashuhuri usio na manufaa yeyote ya muda mrefu kwa taifa letu, kina MUSUKUMA, ambao wakishiba wao wengine watajiju! ... huu ni muda wa kuitafuta dira yenu aliyowaambia Kolimba mmeipoteza mkamkodolea majicho hadi 'PRESSURE' ikampanda! ... ni wakati wa kuwakutanisha watu waliotofautiana kwa kugawanywa na utawala wa Jiwe ili mchambue mchele na chuya!

KATIBA BORA HAIEPUKIKI!

BECAUSE ... NEVER EVER AGAIN!

👊 :cool:✌️💥
Ili jamii ikamilike hao wana nafasi yao, kwani sayansi ya biblia inasema kufanikiwa kwa mpumbavu kutamwangamiza.
 
Yote tisa ila kumi ni kwamba ccm muda wake wa kuliongoza hili taifa umekwisha. Ndio maana kila njia wanayoitumia ili waonekane kuwa bado zama zinawakubali zinafeli.
Hili la kujua muda umeisha na kukataa kukubali ndio linszua mgogoro. Muda wa mtihani umeishs kisha unazidi kuandika msimamizi sijui!
 
We jamaa Mzimu Marehemu atakuharibia maisha.

Fanya Mambo yako.

Watu tumawaza Makato yanavyoharibu maisha yetu na namna ya kujinasua.

Wewe ukiamka ni kupambana na Marehemu tu.

Sasa hao CCM mbona wenyewe hawana mda na wewe na wanajenga Sanamu mda so mrefu
 
Na familia yako tu..unajua madeni aliyoleta kwenye Taifa..wajinga bado wanazaliwa...
... hata akiambiwa tozo zote ni 'made in Magufuli' na mamiradi ya kukurupuka, mara ndege ... mara makao makuu Dodoma ... mara standaed gauge ... muda huo huo madaraja kibao ... hujatulia Stigler's gauge, atajifanya kung'aka!
 
We jamaa Mzimu Marehemu atakuharibia maisha.

Fanya Mambo yako.

Watu tumawaza Makato yanavyoharibu maisha yetu na namna ya kujinasua.

Wewe ukiamka ni kupambana na Marehemu tu.

Sasa hao CCM mbona wenyewe hawana mda na wewe na wanajenga Sanamu mda so mrefu
Kama hujui hata tozo unazolalamikia ni 'made in Jiwe' wala hata usingejipendekeza kwa mzimu!
NB: Ninachounga mkono ni kuanzishwa kwa mkoa wa Chato ili tudhibiti wahamiaji haramu kutoka nchi za wenye shari na sisi!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom