CCM mkubali tu:- Ukweli, Haki na Uhuru lazima vitafutwe

CCM mkubali tu:- Ukweli, Haki na Uhuru lazima vitafutwe

chamilo nicolous

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2016
Posts
2,112
Reaction score
1,492
Kwa sasa nchi ipo kwenye sitofahamu, Kila kiongozi anajinasibu yuko sahihi, swali wanataka kutupeleka wapi, tuko wapi na tunaelekea wapi?
1; Nikimuuliza comrade Kikwete nani ametufikisha hapa atajibu nini??
2: Nikimuuliza Mh Samia tuko wapi na unataka kutupeleka wapi je utakuwa na jibu!!
3: Hoja za Hamfuley Kuwa tuko hapa sababu ya wanamtandao nani wa kuzikanusha?

Mwanafalsafa na profesa wa Kimarekani Noam Chomsky aliwahikutoa tafakuri zenye nguvu kuhusu jamii, historia na uhuru wa binadamu alisema:-

▪︎ “Hakuna nchi maskini, bali kuna mifumo iliyoshindwa ya usimamizi wa rasilimali.”

▪︎ “Hakuna mtu atakayekuwekea ukweli akilini mwako; ni jambo ambalo lazima ulitafute mwenyewe.”

▪︎ “Ukitaka kuwatawala watu, tengeneza adui wa kufikirika anayeonekana hatari zaidi kuliko wewe, kisha ujitokeze kama mwokozi wao.”

▪︎ “Moja ya masomo yaliyo wazi zaidi katika historia: haki hazitolewi; zinachukuliwa kwa nguvu.”

▪︎ “Kuna makusudi nyuma ya kupotosha historia ili ionekane kwamba ni watu wakubwa pekee wanaoweza kufanikisha mambo makubwa. Hii inawafundisha watu kuamini hawana nguvu na lazima wasubiri mtu mkubwa atende.”

▪︎ “Dunia ni mahali pa ajabu na penye kuchanganya. Ikiwa hutaki kuchanganyikiwa, unakuwa tu nakala ya akili ya mtu mwingine.”

▪︎ “Ili kuwadhibiti watu, wafanye waamini kwamba wao wenyewe ndio chanzo cha mateso yao, kisha ujionyeshe kama mwokozi wao.”

▪︎ “Viongozi wakubwa siku moja watajutia mawazo yao ya juujuu yanayowatenga watu na asili yao ya kwelii.”

Maneno ya Chomsky yanasalia kuwa ukumbusho kwamba ukweli, haki, na uhuru lazima vitafutwe—havipewi, viongozi CCM msiwaone wale wanaotafuta Haki na ukweli kama maadui, wasikilizeni, ila mkubali ukweli!

Ukweli itawaweka huru
 
Back
Top Bottom