CCM malipo ya DOWANS.....''NO''

CCM malipo ya DOWANS.....''NO''

PrN-kazi

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2011
Posts
2,900
Reaction score
445
CCM kupitia msemaji wake ambaye anakaribia kupoteza umaarufu wa jina la baba yake Nape Nauye akiongea na TBC1 amesema CCM hawatambui uamuzi wa mahakama kuu kwa kubariki na kuridhia Tanesco kuilipa DOWANS.
source: habari kwa ufupi TBC1 saa 10
 
Bila shaka ni habari njema,kwamba CCM nao watatusupport kwenye hayo maandamano yanayokuja kuipinga kwa nguvu zote DOWANS.Lakini bado najiuliza JK bado hajamjua mmiliki?
Acha kuwa na akili za kushikiliwa CCM ndiye nani hapa???JK+Pinda au huyo mpayukaji Nape
 
Wamesubiri kuangalia upepo unaelekea kipande ipi katika hii issue ili na wao wafuate upepo. Tunasubiri kusikia kauli ya Mwenyekiti na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM na yule Katibu Mkuu wao kama nao wanapinga malipo fisadi kwa Dowans.
 
You are damn right. Kawaida ya ccm, utawasikia hawa vibaraka....nape na uvccm wakibwatuka na kujifanya kuweka misimamo ili kuangalia umma unasemaje....wanasahau cc ya ccm ilishawahi kusema serikali iwalipe dowans.
Wamesubiri kuangalia upepo unaelekea kipande ipi katika hii issue ili na wao wafuate upepo. Tunasubiri kusikia kauli ya Mwenyekiti na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM na yule Katibu Mkuu wao kama nao wanapinga malipo fisadi kwa Dowans.
 
Ukitaka kuwawin watz 2015 ni kuwa na ela lukuki za kununua fulana na tshirt bila kusahau khanga
Na ela za Dowans ndo starting capital kwa ajili ya izo kazi
 
Kwa hiyo wana ipinga serikali ya ya CCM, kwahiyo tutakuwa wote kwenye maandamano, kumshinikiza Kikwete asijilipe mabilion ya walala njaa wa tanzania na pengine kumtaka angoke yeye pamoja na vibara wake............!?
 
vipi bado kuna mtu anaamini kauli za katibu mwenezi wa ccm? kwanza atuambie nani alimzuia kwenda igunga? kwa nini? na kama alizuiwa je ana nguvu gani ndani ya chama tawala kwa sasa?
 
Kwa hiyo wana ipinga serikali ya ya CCM, kwahiyo tutakuwa wote kwenye maandamano, kumshinikiza Kikwete asijilipe mabilion ya walala njaa wa tanzania na pengine kumtaka angoke yeye pamoja na vibara wake............!?
Yeah, CCM watakuwa kwenye maandamano kuishinikiza serikali isiilipe Dowans, kiongozi wa maandamano ni m/kiti CCM taifa Jk! Umesasau wakati wa kikao cha NEC CCM iliilalamikia serikali kwa kupandisha bei ya mafuta?
 
Rais wa kutoka CCM kakaa kimya bei ya mafuta ilipopandishwa na kusubiri hadi kikao cha chama chake kilichomuweka madarakani ndiyo wakatoe kauli ya kuipinga Serikali kupandisha bei ya mafuta...USANII MTUPU! Kwani asingeweza kutoa kauli kama Rais wa nchi kupinga kupandishwa bei ya mafuta kwa kuwa kutawaongezea Wananchi gharama za maisha!? Usanii huu wa Kikwete Watanzania tumeshaustukia.
 
CCM kupitia msemaji wake ambaye anakaribia kupoteza umaarufu wa jina la baba yake Nape Nauye akiongea na TBC1 amesema CCM hawatambui uamuzi wa mahakama kuu kwa kubariki na kuridhia Tanesco kuilipa DOWANS.
source: habari kwa ufupi TBC1 saa 10
Wanazunguka mbuyu hao, haiwezekani mazuri yawe associated na CCM halafu mabaya ya serikali yasiusianishwe na CCM. Nao saizi wanaipinga mahakama!
 
Ukitaka kuwawin watz 2015 ni kuwa na ela lukuki za kununua fulana na tshirt bila kusahau khanga
Na ela za Dowans ndo starting capital kwa ajili ya izo kazi

And that is for sure Comrade, this matter'd drugged unsettled towards 2015 while the compounded interest to settle this dispute is skyrocket high.
The departing president will intervene to support the payments.
 
huu ni usanii wa ccm, hatudanganyiki. ngoja tusubiri bakwata watasemaje na wao.
 
tunataka kauli ya mwenyekiti sio ya mwenezi kwa sababu hana nguvu hata igunga kapigwa marufuku.

Si unamjua Mwenyekiti wa Magamba alivyo msanii wa hali ya juu? Sidhani kama atatoa kauli ya kupinga haya malipo kwa Rostam hasa ukitilia maanani kwamba fisadi Rostam na mafisadi wenzie ndio waliombeba kuhakikisha anaingia Ikulu 2005.
 
Filamu ndiyo Part II imeshaanza, kama hujui hilo ni changa la macho TANESCO itashindwa makamani kila kona itabanwa halafu CCM nao watakuwa kama kenge kwenye msafara wa mamba yaani kama walivyoaanza watajitia wanapinga lakini itafika hatu watasema WANAHESHIMU MAAMUZO YA MAHAKAMA KAMA MHIMILI UNAJITEGEMEA NA DOLA hivyo wasingependa kupinga maamuzi hayo japokuwa wanajua inawaauma wananchi. Huo ndiyo mwisho wa movie kisha hazina itavunjwa kwa 111bill kulipwa kwa Dowans kiiiiiiiiii.
 
Kuna mwandishi aliwahi kusema, wakati wa uchaguzi baadhi ya watu akili wanazipeleka likizo na uchaguzi ukiisha wanazichukua tena. kuna wakati huwa najiuliza ukiwa CCM ni heri kukaa kimya kwenye baadhi ya mambo, huwa nikiangalia na kusikiliza baadhi ya hoja za viongozi wa CCM hadi nashindwa kuelewa kama ile akili ya kawaida ipo au iko likizo. Mtu kama Nape inafika mahali nahisi labda chakula anachokula kina walakini hadi uwezo wa kufikiri unapungua au anaamua kuvaa uendawazimu na kuongea kila kilichoko mbele yake. Serikali ni ya Chama chake, anakurupuka na hayo sijui bwana ni suala la wakati tu ukweli utakuja kujulikana
 
Huyu bwana mdogo anatembelea makalio, amepoteza mvuto aliokuwa nao kabla ya kuchaguliwa kuwa DC. Na kwa kumpatia usemaji wa chama msishangae akiwa ombaomba miaka mitano baadaye. Kwa nini nasema ombaomba, CCM kitakuwa kimepigwa chini na hajazoea kutafuta mali kwa jasho analojua ni kubwabwaja ili mkono uende kinywani sasa akishatumika vya kutosha watammwaga au wananchi wataimwaga CCM na hivyo kumkosesha kazi.... jiandaeni kumsaidia jamani anaganga njaa mwenzenu!
 
Back
Top Bottom