CCM kutishia watumishi wa umma kisa hawajahudhuria mikutano yao si haki!

Phillemon Mikael

JF-Expert Member
Nov 5, 2006
10,228
2,000
Nimeona Katibu wa CCM mwanza akiwa na Nape wakilalamika kitendo cha Watendaji wa serekali ...Tanroads na Tanesco kwa kukataaa kwenda kwenye mikutano Yao Kujibu Hoja za Wananchi

....Katibu ameenda Mbali kutushia kuwafukuzisha kazi.

Nimeshangaa sana Kama tunao wanasiasa ambao huwajui katika utendaji wa Vyama vingi....watumishi wa umma Kama hawa hawawajibiki kwa Katibu wa CCM na sio busara kuwatumia kisiasa .....Watofauutishe role ya mawaziri ambao wao ndio wasimamizi wa kisiasa serekalini na hawa Watendaji.

...Ni halali Kabisa kwa waziri kuwajibika kwa chama na Kijibu Hoja ......Lakini ni uwehu Kabisa kuwaonea Watendaji wa umma...kuwatumia kwenye majukwaa ya kisiasa.

Iwapo hawa Watendaji walitajwa watahamishwa au kufukuzwa kazi itaweka predecence mbaya.....na tunaomba katiba mpya iweke msisitizo juu na kuwalinda Watendaji wa umma dhidi ya wanasiasa.
 

Nsiande

JF-Expert Member
Jul 27, 2009
1,649
1,195
Wanafukuzwa kazi kwa kutotokea kikaoni ? Naomba uweke voice clip hapa if possible
 
  • Thanks
Reactions: FJM

Makala Jr

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,395
1,195
Ndugu Wanajamvi....!

Kutokana na kauli aliyoitoa katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (ccm) leo wilayani Nyamagana,Nape Nnauye ametoa kauli ya vitisho kwa watendaji wa serikali kwamba ni lazima wahudhurie vikao na mikutano ya chama ili kueleza wamewafanyia nini wananchi.

Nadhani Nape Nnauye ametumia nguvu nyingi akili kidogo kufikia maamuzi hayo. Hivi viongozi wa ccm hawawezi kuelezea utekelezaji wa ilani hadi watendaji kama mkurugenzi wa TANROADS,Mkurugenzi wa halmashauri,Afisa mtendaji wa kata au kijiji waache shughuli zao zinazowapa mwanya wa ujira waje kujieleza kwa maslahi ya ccm?

Mwajiri wa watendaji wa serikali ni nani? Je,kila mtendaji wa serikali lazima aitumikie ccm na tafsiri yake hakuna atakayepata kazi serikalini nje ya ccm? Mhe.Nape umekurupuka mno,katika kumbukumbu...uliwahi kuitisha kikao na walimu mjini Mafinga,ulifanya hivyo kama nani?

WANAJF:
Naomba kueleweshwa kama tunaongozwa na katiba ya CCM au TANZANIA?
 

Ndoa

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
1,033
1,500
Nimemsikia Nape kwenye taarifa ya habari ya ITV ya saa mbili usiku huu kuwa, CCM itawachukulia hatua watendaji wa serikali wasiotimiza wajibu. Mfano wa TANROADS na TANESCO ulitolewa.

Sasa nawauliza waungwana hiki chama ni mhimili wangapi wa dola? Kuna haja gani basi ya kusema mihimili ya dola ni serikali, bunge na mahakama? Au katiba bado inafuata siasa za chama tawala kushilka hatamu za kila kitu?
 

LE GAGNANT

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
1,243
1,195
Wamelewa madaraka hao! Wanafikiri wtakuwa watawala milele. Sijaona nchi yenye utawala wa kidemokrasia inakuwa na mambo ya kukurupuka kama hawa jamaa wa hiki chama!
 

FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,081
1,225
Sijui ni busara gani ya kugeuza 'civil service' kuwa sehemu ya Secretariat ya CCM. Hili litazua balaa muda si mrefu. Wafanyakazi wa idara za umma wameajiriwa na serikali (regardless ni serikali ya chama gani). Na hakuna sehemu yoyote kwenye job discription zao inawataka wa-report kwa chama cha siasa.

Kutishia mfanyakazi ambaye kimsingi hawajibiki kwako ni kujitakia kesi. Nape asipokuwa makini atajikuta analeta msuguano -usio wa lazima- kati ya CCM na wafanyakazi kwenye wa idara za serikali. Na pia sidhani kama makatibu wakuu au mawaziri wangetaka ma-officers wao wawe wanapelekwa kwenye mikutano ya siasa. Politising civil service si jambo jema hata kidogo. Sielewi nani katoa hii idea!
 

Chibolo

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
4,690
2,000
Nadhani magamba yamechanganyikiwa nepi kichwa chake hakiko sawa jamani angepelekwa milembe akapumzike jamani.
 

Mr.Busta

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
672
195
Hawajui watendalo.nimeckia kutendaji mmoja wa serkali amekula kona walpo mwitaji aje atoe ufafanuzi wa maendeleo ya ujenzi
 

mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
6,010
2,000
Msuguano wa chama na watendaji wa serikali utazua mtafaruku. Kina Nape waseme mapungufu kisha wawaachie waajiri kufuatilia. utaratibu wa kazi serikalini unaeleweka. kuna wakaguzi, maodita wasimamizi wa kazi, waajiri n.k sasa siasa ibaki majukwaani sio kazini
 

Cynic

JF-Expert Member
Jan 5, 2009
5,146
2,000
huyu inawezekana alipanda jukwaani akiwa amelewa au amevuta .. Maana hata wakubwa wake sijawahi sikia wakitoa kauli kama hizi
 

Nyalotsi

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
6,591
2,000
Mi mwenyewe nimesikia nikabaki macho wazi. Eti wanataka mameneja wa tanesco na tanroads waende kwenye vikao vyao. Pumbaf kabisa! Kwani wakuu wa wilaya na mikoa si ndo wenyeviti wa kamati za barabara? Wanataka wawavishe mashati ya mboga za majani? Enyi viongozi wa ccm acheni watendaji wa serikali wafanye kazi bila siasa. Hii nchi kila mtu anataka aheshimiwe, mpaka watu wa vyama!
 

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,195
Duh sipati Picha Mkurugunzi Mkuu wa EWURA Jukwaa la SIASA CCM Imeshikwa pabaya.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom