Mpaka Kieleweke
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 4,132
- 1,571
Ccm wanatafuta wa kumrushia lawama kuwa sio chama bali watendaji......l
sasa mihimili ya bunge,serikali na mhakama ina kazi gani? Kama chama tawala kinakuwa na uwezo wa kumwajibisha kila mtu. Na kama mtumishi wa serikali akikataa kuwajibishwa na chama cha siasa sheria inambana vipi kikatiba?
Na sisi watumishi wa umma ni mazuzu tu acha watuburuze wanavyotaka! Wakati wa kura ndo huwa tuko msitari wa mbele kuchakachua ili magamba waendelee! Shenzi zetu! Jamani tubadili mtazamo. Ila hiki chama kimeshikwa pabaya, kinatapatapa sana!! Jana nilimwona Joyce Masunga-Shangingi la ccm SHY miaka ile -alivyotoa maagizo kwa DC eti apeleke mapendekezo ya kuwatimua kazi meneja wa TANROADS mkoa na TANESCO mkoa. Kisa hawakwenda kwenye kikao cha CCM! NYAMB...F!
Kwa kifupi mtumishi wa serikali anayekataa kutumikia serikali iliyoundwa na chama tawala inbidi atafute ajira yake mwenyewe.sasa mihimili ya bunge,serikali na mhakama ina kazi gani? Kama chama tawala kinakuwa na uwezo wa kumwajibisha kila mtu. Na kama mtumishi wa serikali akikataa kuwajibishwa na chama cha siasa sheria inambana vipi kikatiba?
Kwa mantiki ya proposition yako naona ni ujuha zaidi kukilaumu chama tawala kwa kushindwa utekelezaji wa sera zinazoihusu TANESCO na TANROADS.Nimeona Katibu wa CCM mwanza akiwa na Nape wakilalamika kitendo cha Watendaji wa serekali ...Tanroads na Tanesco kwa kukataaa kwenda kwenye mikutano Yao Kujibu Hoja za Wananchi
....Katibu ameenda Mbali kutushia kuwafukuzisha kazi.
Nimeshangaa sana Kama tunao wanasiasa ambao huwajui katika utendaji wa Vyama vingi....watumishi wa umma Kama hawa hawawajibiki kwa Katibu wa CCM na sio busara kuwatumia kisiasa .....Watofauutishe role ya mawaziri ambao wao ndio wasimamizi wa kisiasa serekalini na hawa Watendaji.
...Ni halali Kabisa kwa waziri kuwajibika kwa chama na Kijibu Hoja ......Lakini ni uwehu Kabisa kuwaonea Watendaji wa umma...kuwatumia kwenye majukwaa ya kisiasa.
Iwapo hawa Watendaji walitajwa watahamishwa au kufukuzwa kazi itaweka predecence mbaya.....na tunaomba katiba mpya iweke msisitizo juu na kuwalinda Watendaji wa umma dhidi ya wanasiasa.
Tukiendelea hivi, masharti ya kupandishwa daraja au hata kuajiriwa itakuwa kuwa mwanachama wa CCM, subirini muone.
Kazini kwangu nimeona wiki iliyopita wafanyakazi ambao ni makada wa CCM wameanzisha umoja wao na wanafanya vikao na kuhamasisha wafanyakazi wengine kujiunga na CCM kwa ahadi za kijinga eti watatoka kimaisha. Unafikiri matokeo yake ni nini kama mtu akisema yeye siyo mwana CCM?